Na Said Mwishehe,Michuzi TV

TUKO Vizuri kitaaluma! Ndivyo kinavyojinadi Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) ambacho kwa sasa kimeanzisha kozi mpya ya Usimamizi wa Rasilimali Nyuki ikiwa ni mkakati wa kuzalisha watalaamu waliobobea kwenye ufugaji nyuki,uzalishaji wa asali na mazao yanayotoka na nyuki.

Hivyo katika kuhakikisha Watanzania wanafahamu vema uwepo wa programu hiyo ambayo ni ya kwanza nchini Tanzania kufundishwa na SUA wameamua kupiga kambi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam yanakofanyika Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Telnolojia ambayo yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ( TCU).

Wakati SUA wakiendelea na mkakati wa kuandaa wa taalamu kupitia programu hiyo, takwimu zinaonesha kwamba licha ya Tanzania kuwa na uwezo wa kuzalisha tani 134,000 za asali  kwa mwaka,  tani zinazolishwa ni  30,400 pekee kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa utaalam kwenye uzalishaji.

Akizungunza akiwa kwenye maonesho hayo ya vyuo vikuu, Mhadhiri kutoka SUA Dk Innocent Babili amefafnua kozi(programu) hiyo inatolewa katika kampasi ya Katavi ambako pia wanafunzi wanapata fursa ya kujifunza kwa vitendo.

Ameongeza wameona ni vema wakaipeleka  program hiyo Mkoa wa Katavi kwa kuwa kuna maeneo ya kufugia nyuki na wanafunzi wataweza kujifunza kwa vitendo. "Hadi tunapozungumza hapa ukweli mwitikio umekuwa mzuri, vijana wengi wameonekana kuichangamkia na kwa mwaka mpya wa masomo tunatarajia kudahili wanafunzi 100".

 Amesisitiza kozi hiyo wameianzisha kwa lengo maalum la kutengeneza wataalam ambao watasaidia kuongeza kiasi na ubora wa asali inayozalishwa nchini ili kukidhi viwango vya kimataifa. Aidha Dk.Babili amesema kama   nchi  bado hatujatumia vizuri rasilimali za misitu na nyuki, miundombinu na uwezo tulionao ni mkubwa lakini tunazalisha kidogo yani chini ya uwezo wetu,” alisema Dk Babili

Wakati huo huo amesema sambamba na kuzalisha watalaam kampasi hiyo ya Katavi inatoa mafunzo ya muda mfupi kwa wakazi wa jirani na chuo hicho wanaojihusisha na ufugaji nyuki.Kwa upande wake Ofisa udahili wa chuo hicho Christopher Ndaga ameeleza programu hiyo inahusisha ufugaji wa nyuki, jinsi ya kuwatunza na kuweza kuzalisha asali ya kutosha na mazao mengine yanayotokana na nyuki.

 Kwa kumbukumbusha tu, iko hivi Februari mwaka huu Samia Suluhu Hassan wakati huo akiwa  Makamu wa Rais alitoa maelekezo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa na mkakati maalum unaolenga kuongeza uzalishaji wa asali yenye viwango ili kukidhi soko la bidhaa hiyo.

Alisema mkakati huo uhakikishe asali inazalishwa kwa wingi na kwa kuwa soko la uhakika la zao hilo lipo ndani na nje ya nchi huku akibainisha kuwa  mahitaji ya bidhaa yamezidi kuwa makubwa ambapo  mataifa mbalimbali ikiwemo China yakionyesha uhitaji mkubwa.Pia alielekeza watalam kuzitambua changamoto zilizopo katika mnyororo wa thamani na kuzipatia ufumbuzi sambamba na kutambua na kujua mahitaji ya soko.

Mhadhiri Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) Dk Innocent Babili akizungumza alipohojiwa na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu yaliyoandaliwa na Tume ya
Vyuo Vikuu nchini (TCU) Viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mhadhili msaidizi (SUA) Hekima Mliga (wa kwanza kulia) akizungumza na moja ya mwanafuzi aliyefika kwenye Banda la SUA kwenye mMaonesho ya Vyuo Vikuu Jijini Dar es Salaam. (wa pili kulia) ni Anitha Ngesi Afisa Udahili Ndaki ya Mizengo Pinda iliyopo Katavi Mkoani Rukwa.
Maofisa Udahili wa Chuo Kikuu cha Sokoine wakiendelea na zoezi la kuwadahili wanafunzi wapya waliojitokeza kuomba kujiunga na Chuo hicho katika mwaka wa masomo 2021/2022 kwenye maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. (wa kwanza kulia ) ni Christopher Ndaga, (katikati) Petter Msumari, na (wa kwanza kushoto) ni John Lyatuu.
 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...