Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wananchi
mkoani Njombe wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya UVIKO 19
inayotolewa kwenye vituo mbalimbali vya afya vilivyoainishwa kwakua
haina madhara yeyote.
Kauli
hiyo imetolewa na mwenyekiti wa umoja wa wanawake chama cha mapinduizi
UWT mkoa wa Njombe Scolastika Klistiani Kevela baada ya yeye mwenyewe
kuchanja katika kituo cha afya kibena.
"Mhe,Rais
ametuambia kwamba kuchanjwa ni muhimu kwa ajili ya afya zetu na ni
hiari mimi nimejitokeza leo kuchanja kuonyesha kwamba chanjo ni muhimu
kwa ajili ya afya zetu"alisema Scolastika Kevela
aliongeza
kuwa "Mtu aliyechanja na asiyechanja tofauti yake ni kwamba wewe ambaye
hujachanja Covid 19 ikikukuta ni rahisi kukuchukua,mimi niliyechanja
nakuwa na asilimia ndigo ya kuathirika"
Katika
hatua nyingine mwenyekiti huyo amewataka wananchi kupuuza baadhi ya
maneno ya watu ambao wanazusha kuhusu chanjo bali wamuunge mkono
Mh,Raisi Samia Suluhu Hassani kwakua nae ameshachanja.
"Ninawaambia
wananchi wa mkoa wa Njombe na wakina mama wajitokeze kwa wingi kupata
hizi chanjo kwa ajili ya usalama wa maisha na familia zao"aliongeza
Scola
Nao baadhi ya
wananchi waliopatiwa chanjo akiwemo bwana Bunduki na Mwalongo maarufu
kwa jina la kakuku wamesema wanajisikia furaha kuchanja na hawajapata
changamoto yeyote kiafya.
"Nilipofika
hapa haikuchukua hata dakika 10 kwenye kituo nikawa nimeshachanja kwa
kuwa watu ni wachache na ni bora watu wakapata chanjo kuliko homa
ikakuzidia"alisema Kakuku.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...