VIONGOZI wa Umma nchini wameaswa kujali maslahi ya Umma ambayo ndiyo msingi mkuu wa Serikali yeyote duniani.

Hayo yalisemwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji wa Rufani Sivangilwa Mwangesi alipokua akitoa mada katika kikao cha Viongozi wa umma wa Mkoa wa Tabora kilichofanyika  mwishoni mwa wiki mkoani humo.

Mhe. Mwangesi alisema kuwa kiongozi yeyote wa Umma ni kioo cha jamii husika hivyo, hana budi kujali maslahi ya Umma ikiwa ni pamoja na kuwa mzalendo kwa nchi yake, kufanya kazi kwa uaminifu, huruma, umakini, kijizuia na tamaa na kuzingatia viwango vya juu vya maadili pamoja na  kuzingatia Sheria taratibu  na miongozo mbalimbali. 

“Viongozi wanapaswa kuwa na mienendo mizuri isiyotiliwa shaka ili waweze kuaminika katika jamii inayowazunguka,” alisema na kuongeza kuwa, kiongozi yeyote anapokua muadilifu kwa watu anaowaongoza bila shaka atapata heshima anayostahili katika jamii na nchi kwa ujumla

Mhe. Mwangesi alisisitiza kuwa  “kiongozi ambaye ni muadilifu hufanya mambo mazuri  hata pale ambapo hajaambiwa afanye ama pale ambapo hakuna anayemuona  lakini kwa yule ambaye si muadilifu anaweza kufanya mambo mengi kwa kutumia nguvu na asifanikiwe hivyo nawaasa viongozi kuwa waadilifu jambo ambalo litarahisisha  utendaji kazi wenu.”

Katika hatua nyingine Jaji Mwangesi aliwakumbusha viongozi  wa umma baadhi ya misingi ya maadili ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi kwa kufuata sheria, kanuni, miongozo kwa manufaa ya umma, kujiepusha na migongano ya maslahi, kuepuka mienendo inayo aibisha utumishi wa Umma, na kuzingatia mipaka ya matumizi ya madaraka.

Awali akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani alisema kuwa Viongozi wote wa umma wanapaswa kuwa waadilifu na kuepuka mgongano wa maslahi

Mhe. Batilda alisema kuwa amefurahishwa na ziara ya Kamishna wa Maadili mkoani humo kwani ni wazi kuwa ujio wake unawakumbusha viongozi wa umma kukumbuka na kujitathmini kupitia kiapo cha Ahadi ya Uadilifu walichoapa mara tu walipoapishwa kuwa Viongozi.

Kikao hicho cha Kamishna wa Maadili na Viongozi wa Umma ni sehemu ya mikakati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutoa elimu ya Maadili kwa wadau wake.

Mkuu   wa Mkoa wa Tabora   Mhe. Balozi   Dkt.  Batilda Buriani  akitoa neno la ufunguzi katika kikao cha Viongozi wa Umma wa Mkoa wa Tabora kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni  Kamishna wa Madili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi.

Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji  Sivangilwa Mwangesi akitoa mada katika kipindi cha  Mseto cha Charles George (CG) FM redio  kilichopo Mkoani Tabora mwishoni mwa wiki
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Batilda Buriani alipomtembelea ofisini kwake (Tabora)  mwishoni mwa wiki.
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji wa Rufani Sivangilwa Mwangesi akitoa mada katika kikao cha Viongozi wa Umma wa Mkoa wa Tabora   kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...