WAANDISHI wa habari wameaswa kutumia taaluma zao kwa kadri wanavyoweza katika kupambana na usugu wa vimelea vya magonjwa.
Msangi amesema usugu wa vimelea vya magonjwa hutokea pale ambapo virusi vya vimelea hivyo kushindwa kutibika hususani kwa dawa maalumu na kusababisha kuongeza kasi kwa magonjwa na makali ya ugonjwa na kupelekea vifo vingi kwa watu.
Amesisitiza kuwa usugu huo wa vimelea vya magonjwa unahitaji wataalamu katika sekta mbalimbali kuweza kufanya kazi kwa pamoja ili kushughulikia kwa kasi suala hilo kwani kumekuwa na kasumba duniani juu ya suala hilo ambalo husababisha vifo katika mataifa mbalimbali duniani.
“ Siyo Tanzania tu ambao tunashughulika na Kupambana na suala la usugu wa vimelea bali duniani kwa ujumla lakini pia tunaona juhudi za Taasisi mbalimbali katika kuweka mchango wao kuhakikisha wanaendelea Kupambana na usugu huo pia FAO nao hawako nyuma katika kuendelea kutoa semina za elimu ya mapambano ya usugu wa vimelea vya magonjwa," Amesema Msangi.
Aidha amewataka wadau wa mazingira kuhakikisha wanaendelea kuchukua taadhari juu ya suala hilo kwani vimelea vingi hutoka kwa mifugo inayofugwa majumbani na kuwadhuru binadamu, pia alisisitiza hususani suala la tabia nchi ambapo kwa nchi ya Tanzania na zinginezo barani Afrika ambazo zina ukanda wa joto (Tropic) huwa ni kitovu kikubwa cha milipuko ya magonjwa mbalimbali.
“Magonjwa kama Ebola, mafua ya ndege na mengineyo hulipuka kutokea katika nyanda zenye tabia nchi ya joto na wenyewe tumekuwa mashahidi kwenye hilo hivyo wote kwa ujumla tunawajibu wa Kupambana katika suala hili," Amesema Msangi.
Kwa upande wake Mratibu Taifa Dawati la Afya Moja, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, amesema kufuatia nchi ya Tanzania kuwa imepiga hatua katika uratibu wa masuala yaAfya moja, ambayo ni dhana inayo jumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo, kilimo na mazingira kushirikiana kwa pamoja katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu.
Amesisitiza kuwa kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limeanza kutumia dhana hiyo kwakuwa linapunguza gharama katika kushughulikia athari za usugu wa vimelea vya magonjwa ambavyo ni hali ya dawa kushindwa kudhibiti vimelea hivyo kwa kushindwa kabisa kuviua au kuzuia ukuaji wake.
“Moja ya mkakati ulioibuliwa Kitaifa na Kimataifa ni kujiandaa kwa kuwa fundisha wataalam wa sekta za afya na wadau wa Afya moja jinsi ya kuwa na kufanya tathmini ya hatari ya vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa kwa ushirikiano.” Alisema Chinyuka
Ofisi ya Waziri Mkuu iliunda Dawati la Uratibu la Afya moja , likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini, Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya Uratibu Maafa Ofisiya Waziri Mkuu, kupitia Dawati hilo kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) waliandaa na kuratibu mafunzo hayo
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuu idara ya Menejimenti ya Maafa, Charles Msangi, akifungua semina ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu yaliyoandaliwa na FAO kuhusu usugu wa vimelea


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...