Na Khadija Kalili, Pwani
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge,amelazimika kuchukua hatua ya kuwakutanisha wadau mbalimbali wa ardhi wakiwemo wakulima na wafugaji kwa ajili ya kujadili namna ya kupata njia sahihi zitakazosaidia kukomesha migogoro inayotokana na ardhi.

RC Kunenge,ameitisha kikao hicho katika ofisi zake zilizopo Kibaha Mkoani Pwani ambapo baadhi ya wadau walioshiriki mkutano huo ni pamoja na wakulima na wafugaji, taasisi zinazojihusisha na ardhi,wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wote wa Pwani.

Katika kikao hicho RC Kunenge ,aliwaeleza wadau hao kuwa amechoshwa na migogoro ya ardhi inayotokea mara kwa mara Mkoani kwake huku akisema kikao hicho ameitisha ili kupata njia sahihi ya kukomesha migogoro hiyo.

Alisema kuwa,jambo pekee linalompa changamoto ni suala la migogoro ya ardhi ambapo alisema kwasasa lazima ifike mwisho na majibu ya utatuzi wa jambo hilo yapatikane.

Alisema kuwa , haiwezekani kuona kila siku inazuka migogoro ya ardhi ambayo inaathiri hali za wananchi kwa kusababisha mapigano yanayoleta vifo,watu kujeruhiwa na wengine kukwamishwa kiuchumi halafu viongozi wakalichekea.

"Mimi nataka migogoro ya ardhi Pwani iwe historia na nitafanyakazi bila kumuogopa mtu ,kwahiyo lazima wakulima ,wafugaji na sisi wote tuliokuwa humu tutoe michango yetu ambayo itasaidia kumaliza migogoro ya ardhi,"alisema Kunenge

RC Kunenge,alisema kuwa watu wanapoteza maisha kwa kuchomana visu,kukatana mapanga,kupigana mikuki halafu viongozi hawajali jambo hilo halifai kuchekewa kwa sababu lina usalama na mali za wananchi.

"Leo nataka wote mtoe Solusheni ya migogoro ya ardhi na kama wewe umekuja hapa kunisikiliza mimi na hauna solusheni yoyote ni bora uondoke maana utakuwa hujasaidia kitu,"alisema RC Kunenge

Kunenge ,ameongeza kwa kusema kuwa kama kuna mambo ambayo hatuwezi kubembelezana ni hili na sababu wananchi wanapoteza maisha kwa mambo hayo,uchumi unashuka kwahiyo umefika wakati wa kupambana nalo.

Alisema kuwa,wale wote ambao wamesababisha migogoro hiyo watafutwe na ikiwezekana kama wapo na wao waondoke maana ndiyo waliosababisha tatizo hili kufika hapa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Chama Cha Wafugaji inayoshughulikia migogoro ya ardhi George Kifuko,alisema jambo lililofikiwa na mkuu wa Mkoa ni zuri na litasaidia kupunguza migogoro hiyo.

Hatahivyo,alisema jambo kubwa litakalosaidia kupunguza migogoro hiyo ni pamoja na kuweka mipango bora ya matumizi ya ardhi kwa kuhakikisha wafugaji wanatengewa maeneo yao bila kuingiliana na wakulima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...