Na Mwamvua Mwinyi, Mafia


WAKALA Wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA ) ,imepokea gawio la kiasi cha sh .Bilioni 78 kutoka katika fedha za mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko19 ambapo kati ya fedha hiyo mkoa wa Pwani utapata miradi 8 yenye thamani ya Bilioni 3.7.

Akielezea kuhusu fedha hiyo waliyopokea kutoka serikalini , baada ya kutembelea miradi ya maji na visima Mafia, Mkurugenzi Mkuu RUWASA, Clement Kivegalo alisema ,fedha hiyo ni nyingi hivyo wataisimamia na kutekeleza miradi lengwa kwa wakati.

Nae Meneja RUWASA Pwani, Beatrice Kasimbazi alisema, asilimia 76 ya watu wanapata maji Mkoani humo , ikiwemo mjini wanapata maji kwa asilimia 84 na Vijijini asilimia 72.

Alieleza ,bajeti ya mwaka huu wametengewa kiasi cha sh.Bilioni 21 ambapo Bilioni 3.7  Ni kutoka katika fedha za Uviko19, Bilioni 15 kutoka mfuko wa maji huku fedha iliyosalia Bilioni 2.9  ni kwa ajili ya miradi ya PBR.

"Hapo tutatekeleza miradi Kama 30 Lakini katika gawio la fedha ya Uviko19 itatekeleza miradi 8 ,Tunashukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji Vijijini, :;"Huu ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kufikisha maji Vijijini na mjini,:"alifafanua Kasimbazi.

Kasimbazi alisema ,agizo lililopo ni kuhakikisha ikifika March 2022  miradi hiyo iwe imekamilika na itoe huduma ,hivyo basi amejipanga na mameneja wa wilaya na watendaji wake kutekeleza agizo hilo kwa vitendo.

Mkuu wa wilaya ya Mafia, Mhandisi Martin Ntemo, aliishukuru RUWASA kwenda kutembelea miradi na visima vinne wanavyochimba mwaka huu ndani ya vijiji  ambavyo wanategemea kuongezwa kufikia visima 10.

Aliwaelekeza viongozi wa vijiji na wananchi kulinda miundombinu na vyanzo vya maji .

Ntemo alisema, watakaoenda kinyume na hilo kwa kuchoma Moto,kufuga mifugo , ama kufanya shughuli za kijamii ,katika vyanzo vya maji  watachukuliwa hatua za kisheria.

Meneja wa RUWASA Mafia Clement Lyoto,alibainisha kwa mwaka huu wametenga milioni 50 kwa ajili ya kutafuta vyanzo vya maji vinne .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...