Na Amiri Kilagalila,Njombe
Ikiwa siku chache zimepita tangu Rais Samia afanye uzinduzi kitaifa wa anuani za makazi jijini Dodoma na kisha kufungua milango kwa mikoa mingine kuendelea na zoezi hilo,Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya ametoa siku 60 kwa halmashauri zote 6 za mkoa huo kukamilisha zoezi hilo.
Aidha Rubirya ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwasababu usajiri wa makazi utakuza biashara ya mtandaoni ambayo inashika kasi ulimwenguni.
Awali katika uzinduzi kimkoa Marwa Rubirya ambaye ni mkuu wa mkoa wa Njombe amesema kulingana na umuhimu wa zoezi hilo ambalo litasaidia serikali kuweka mipango ya maendeleo na kutoa huduma za kijamii kwa urahisi serikali imejipa muda wa kuhitimisha utekelezaji wa zoezi hilo ambalo litaleta matokeo chanya kihuduma na biashara.
“Zama hizi ambazo mambo mengi yanakwenda kwa tehama hatuwezi kuachana na mfumo huu,ni mfumo ambao ni lazima sasa twende kuufanyia kazi tukiwa na anuani hizi inakuwa ni shughuli ndogo kufika mahali popote”alisema Rubirya
Nae Katibu tawala mkoa Judica Omary na Kissa Gwakisa Kasongwa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Njombe wanasema wataifanya kazi hiyo kwa ufanisi na kwa haraka zaidi huku ikielezwa mataifa yaliyoendelea yalianza usajiri wa anuani za makazi na postcodes miaka zaidi ya 150 iliyopita.
“Tutafanya zoezi hili kwa ufanisi na tutakamilisha kwa wakati”aliahidi Kissa Kasongwa mkuu wa wilaya ya Njombe
“Hili ni jambo muhimu sana nchi nyingine zoezi lilitekelezwa miaka mingi sana iliyopita”alisema Judica Omary Katibu tawala mkoa wa Njombe
Nao wakazi wa mji wa Njombe wamekuwa na maoni chanya juu ya utekelezaji wa mpango huo huku Shukuru Milinga mkazi wa Njombe mjini akiipongeza serikali kwa mpango huo.
“zoezi hili litatuletea maendeleo kwa haraka hata mgeni akisema anakwenda mtaa wa Anne Makinda atafikishwa kwa haraka”alisema Milinga.
Mkuu wa mkoa wa Njombe barabara ya mtaa uliopewa jina la spika wa bunge mstaafu Anna MakindaMkuu wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya akizungumza na wananchi wa mji wa Njombe wakati wa zoezi rasmi la uzinduzi wa utambuzi wa anuani za makazi mkoa wa Njombe lililofanyika mjini Njombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...