Huduma ya muziki wa Kiafrika imeendelea kukua katika kila robo ya mwaka kuanzia mwaka 2021
· Jumla ya watumiaji ya robo ya Mwaka 2022 yasimama kwenye Milioni 31 ikiwa ni ongezeko la milioni 20 kutoka robo ya mwisho wa mwaka 2021.
· Huduma ipo katika mwelekeo wa kufikia idadi ya watumiaji iliyojiwekea katika mwaka wa fedha 2021-22
Nairobi, Aprili 19, 2022 Huduma inayoongoza ya muziki wa Kiafrika Mdundo.com, imetangaza kurekodi idadi mpya ya watumiaji hai milioni 31 ndani ya Afrika katika robo ya Mwaka wa 2022 ikiwa inawakilisha asilimia 49% ya ongezeko kutoka mwaka uliopita. Hili linadhihirisha ukuaji wa huduma hii katika bara zima la Afrika ndani ya mwaka uliopita.
Kampuni inatambua ukuaji huu kutokana na ongezeko la uhitaji wa matumizi rahisi wa huduma za muziki wa kimtandao katika jamii ya vijana pamoja na mkakati maradufu wa Mdundo na washirika ambao makampuni makubwa ya mtandao wa simu katika bara la Afrika.
Katika robo ya mwaka huu kampuni pia imeongeza matangazo na washirika wake tofauti tofauti. Hili limechochea ukuaji huu na kuipa mdundo alama chanya zaidi. Washirika hao ni pamoja na Benki ya Standard Chartered, East Africa Breweries Ltd, Nation Media Group, Airtel, Zenith Bank pamoja na 10Bet Africa.
“Tunaendelea kushuhudia ongezeko kubwa la uhitaji rahisi wa huduma ya muziki haswa kutoka kwa vijana ambao ndio wanatengeneza soko kubwa la wasikilizaji wa muziki ndani ya Afrika. Ni hitaji hili ambalo limepelekea ukuaji huu. Tutaendelea kujiimarisha kiteknolojia, katika uvumbuzi na njia mpya za kuongea na kuwashirikisha wasikilizaji wetu.” Amesema Rachel Karanu, Mkuu Brand na Partnerships kutoka Mdundo.
“Mkakati wetu wa kushirikisha makampuni makubwa ya mawasiliano Afrika kama MTN, Vodacom na Airtel, inaendelea kutufanya sisi kutoa jukwaa la kuwafikia wateja wetu walengwa huku tukiwapatia huduma maalum iliyotengenezwa kwa ajili yao”. Aliongeza Rachel.
Nigeria na Afrika Kusini inaongoza kwa kuandikisha wasikilizaji zaidi katika kila robo ya Mwaka, ambapo Nigeria imerekodi wasikilizaji Milion 8.3 sawa na asilimia 92% na Afrika Kusini Milioni 2.2 sawa na 80%. Wasikilizaji wa Kenya wameongezeka kwa 46% kufikia watumiaji milioni 5.7 huku Tanzania ikikua kwa 10% na kufikia wasikilizaji milioni 3.8. Kumekua pia na maongezeko ya watumiaji ya maana katika nchi za Kusini mwa Sudan, Burundi, Congo, Cameroon pamoja na Côte d’Ivoire.
Ukiacha sababu kuu ya kutoa na kuwasilisha muziki bora na unaoongoza duniani, Mdundo pia huwapatia wasikilizaji wake Mixes za ma DJ tofauti ambazo zinaweza kupakuliwa bila kulipia. Sasa hivi, Mdundo inafanya mashindano tofauti ya ma DJ kutoka nchi za Tanzania na Nigeria.
“Tuna matajario mazuri na robo ya mwaka inayofuata huku tukiendelea katika mpango wa kufikia wasikilizaji wetu walengwa katika mwaka wetu wa fedha unaoishia Juni 2022. Tutaendeleza ukuaji wetu kupitia uvumbuzi wa kiteknolojia katika kuandikisha watumiaji wapya, pamoja na kutoa jukwaa maridhawa la matangazo kwa washirika wetu” Alimaliza kuelezea Bi. Karanu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...