Na Jane Edward,Arusha
Baadhi ya wafanyabiashara wa sekta ya uvuvi wameitaka serikali kuwatambua wanawake walioko katika sekta ya uvuvi kwa kuwapatia mitaji mikubwa sambamba na kuwaboreshea miundombinu ili waweze kuondokana na changamoto mbalimbali.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la usimamizi wa mazingira na maendeleo Tanzania (EMEDO) ,Editrudith Lukanga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Lukanga amesema,wanawake katika sekta ya uvuvi wanafanya vizuri ,ila bado kuna changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo kutokuwa na mitaji ya kutosha kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.
"Kwa kweli wanawake wanafanya vizuri sana katika sekta ya uvuvi ila changamoto kubwa ni mitaji mikubwa kwa ajili ya kukuza na kuendeleza biashara zao kwani wengi wao wana uwezo mkubwa wa kufanya biashara hizo ila changamoto ni mitaji ,hivyo naomba sana serikali iweze kuangalia katika jicho la kipekee ili kusaidia wanawake hao."amesema Lukanga.
Amesema kuwa, shirika hilo limekuwa likiwasaidia wanawake waliopo katika vikundi ambapo linalenga katika kuimarisha uwezo wa jamii ili kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na hasa katika kutumia ,kulinda na kuhifadhi mazingira na maliasili kwa ajili ya kuboresha maisha.
Ameongeza kuwa, shirika hilo limejikita kuimarisha uwezo wa jamii katika kutunza mazingira na kupambana na umaskini, kupitia mafunzo,utafiti ,uchambuzi wa sera, ushawishi na utetezi,uhamasishaji ,kupeana taarifa pamoja na uhusiano wa kitaasisi na utafutaji wa rasilimali.
Hata hivyo shirika hilo la EMEDO kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilimo duniani(FAO) pamoja na wizara ya mifugo na uvuvi inatekeleza mradi unaolenga kuwawezesha wanawake katika uvuvi mdogo nchini Tanzania.
Wanawake wavuvi wakiwa katika picha ya pamoja.
Pichani ni dagaa waliotoka ziwani wakiwa katika ndoo tayari kwa kwenda kuuzwa sokoni.
Mkurugenzi wa EMEDO Editrudith Lukanga akizungumza na waandishi wa habari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...