Dodoma


Mhe. Dkt. Biteko ameyasema hayo alipokuwa akiwasha umeme kwenye Kijiji cha Ndalibo, Kata ya Mtanana Wilaya ya Kongwa sambamba na kuzindua kisima cha maji ambacho kitakuwa kikitumia umeme kwa manufaa ya wananchi wa eneo hilo.
"Ndugu zangu niwahakikishie, Mhe. Rais Dkt. Samia anapambana usiku na mchana kuhakikisha umeme unapatikana na kuinua hali za maisha ya wananchi waliopo vijijini kwani umeme sio anasa bali ni jambo la muhimu kwa sasa," alisema Dkt. Biteko.
Aidha, amewaagiza TANESCO na REA kuhakikisha Vitongoji ambavyo bado havijafikiwa na umeme kuhakikisha vinawekewa huduma hiyo muhimu kwa haraka.
Awali akizungumza kabla ya mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule aliishukuru TANESCO na REA kwa kazi kubwa inayofanywa katika mkoa huo ya kuhakikisha umeme unapatikana pamoja na usimamizi mzuri wa fedha za miradi ya wilaya hiyo zinazotolewa na Mhe. Rais Samia.
Alisema mahitaji ya umeme kwa Mkoa wa Dodoma ni makubwa na kumekuwa na ongezeko la viwanda na shughuli za kiuchumi hivyo ni vema taasisi hizi zikafanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendeleo kwa wanachi
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Mhe. Job Ndugai ameikumbusha REA kupeleka umeme kwa wakati katika maeneo mengine ambayo bado hayajafikiwa na nishati hiyo hususan vitongoji vya Chinangali, Chamwino na Manzese na kuwataka TANESCO na REA kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma hiyo ya umeme.
"Tunashukuru sana jitihada za Mhe. Rais Samia kutenga fedha kwa ajili ya masuala ya nishati, hii imekuwa na msaada mkubwa kwa wananchi wa Kongwa hususan katika kuleta maendeleo ya wananchi wetu," alisema Mhe. Ndugai.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...