--Wahamasisha jamii kuacha vitendo vya uvamizi wa Mgodi wa Barrick North Mara
WANAFUNZI
wa Shule ya Sekondari Julius Kambarage Nyerere, iliyopo kijiji cha
Nyamwaga wilayani Tarime, wameushukuru Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North
Mara kwa kuwajengea shule hiyo ambayo inachukua wanafunzi kuanzia
kidato cha kwanza hadi cha sita wanaosoma masomo ya michepuo mbalimbali.
Aidha,
wameishukuru Kampuni ya Barrick inayoendesha mgodi huo kwa ubia na
Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals, kwa jinsi
ambavyo imeendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya shule hiyo sambamba
na kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha sekta ya elimu
nchini.Katika kudumisha ubia na Serikali karibuni Barrick imetoa dola
milioni 40 kwenye mpango wa ujenzi wa barabara na dola milioni 30 zaidi
katika uboreshaji wa suhula za elimu ya juu nchini.
Walitoa
shukrani hizo kupitia risala yao wakati Mahafali ya Saba ya Kidato cha
Nne ya shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo na kuhudhuriwa na viongozi
mbambali wa kijamii, na Serikali akiwemo Diwani wa Kata ya Nyamwaga,
Mwita Marwa Magige.
“Tunatoa shukrani za dhati kwa Mgodi wa
Barrick North Mara kwani wamekuwa wadau wakubwa wa shule yetu, pia
jitihada zinazofanywa na kampuni kuunga mkono Serikali kuboresha sekta
ya elimu kupitia kuimarisha miundombinu ya shule na vifaa vya
kufundishia kwa lengo la kuwezesha wanafunzi wengi zaidi kupata elimu
bora,” walisema katika sehemu ya risala yao wakati wa hafla hiyo.
Walifafanua
katika risala hiyo kuwa mgodi wa Barrick North Mara uligharimia ujenzi
wa shule hiyo mwaka 2014, ambapo mwaka 2017 ilitoa wahitimu wa kwanza wa
kidato cha nne.
Wanafunzi hao waliongeza kuwa baadaye shule hiyo
ambayo imepewa jina la Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Tanzania,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ilisajiliwa kwa ajili ya wanafunzi wa
kidato cha tano na sita, ambapo mpaka sasa imepokea wa kidato cha tano
wa awamu ya nne.
“Tunashukuru Mungu kwamba wanafunzi wote
waliomaliza kidato cha sita katika shule yetu mwaka huu walifaulu na
kuchaguliwa kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali na pia inaendelea kuwa na
ufaulu mzuri wa wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne kila mwaka.
“Tangu
shule hii ianzishwe ufaulu wa kidato cha nne umekuwa ukiongezeka mwaka
hadi mwaka. Elimu hii ya kidato cha nne inawajengewa wanafunzi msingi
mzuri wa kujiunga na elimu ya juu. Pia imetujengea uwezo mzuri wa
kujitambua na kufikiri,” risala hiyo iliongeza.
Wanafunzi katika
risala yao pia walisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya
huduma ya maji na kuomba Serikali na wadau wengine wa maendeleo kuitupia
macho kwa hatua za utatuzi, ili kulinda usalama wa afya za wanafunzi,
walimu na wafanyakazi wa shule hiyo.
Jumla ya wanafunzi 111
(wavulana 58 na wasichana 53) wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Taifa wa
kuhitimu kidato cha nne Novemba mwaka huu.
Wakati huo huo,
wanafunzi hao kupitia igizo lao maalumu waliwataka vijana kujiepusha na
vitendo vya uhalifu, ukiwemo uvamizi katika mgodi wa Barrick North Mara
kwani vinaweza kukatisha ndoto zao kielimu,kuhatarisha maisha yao
sambamba na kufifisha jitihada za uwekezaji nchini.
Sehemu ya wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari JK Nyerere iliyopo Tarime iliyojengwa na Barrick North Mara wakicheza na kuimba kwa furaha wakati wa mahafali yao shuleni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...