Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili na Chama cha Wanasayansi wa Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu Tanzania (TNA) wameandaa kongamano la kimataifa la 14 katika wa Ukanda Kusini mwa Jangwa la Sahara ili kutoa mafunzo ya kukabiliana na magonjwa ya mishipa ya fahamu ikiwemo kiharusi, kifafa, maambukizi kwenye mishipa ya fahamu, magonjwa ya dharura ya mishipa hiyo na magonjwa mingine ambayo bado yana wataalamu wachache Barani Afrika.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa TNA na Profesa wa Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu Prof. William Matuja wakati akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa takwimu za Tanzania zinaonesha kuna wataalamu wa mishipa ya fahamu 14 tu ambapo kati yao 11 ni wa upande wa watu wazima na wa watatu ni wa upande wa watoto ikiwa ni idadi ndogo ukilinganisha na idadi ya Watanzania kwa sasa.

Ameongeza kuwa washiriki wengine watatoka nchi 20 Barani Afrika ikiwemo Angola, Benin, Burkina Faso, Congo DR, Ethiopia, Gabon, Ghana, Ivory Coast, Kenya, Madagascar, Mali, Mozambique, Niger, Nigeria, South Africa, Senegal, Togo, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Prof. Matuja amesema magonjwa ya mishipa ya fahamu na vifo vinavyoambatana nayo yanazidi kuongezeka siku hadi siku. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa kila sekunde arobaini (40) binadamu mmoja hukumbwa na ugonjwa wa kiharusi na kila sekunde tatu 3.5 kifo hutokea kutonana na ugonjwa huo.
Prof. Matuja amesema, mojawapo ya mkakati wa kukabiliana na uhaba wa wataalamu ni pamoja na kuwapatia mafunzo madaktari na wataalamu wengine ili kuweza kutambua na kutibu magonjwa ya mishipa ya fahamu hivyo juhudi hizi zitasaidia madaktari wetu ili wakirejea kwenye maeneo yao ya kazi waweze kuwapatia huduma wagonjwa wa namna hii kwa ufanisi zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...