Mkurugenzi wa Miradi Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Frank Mashalo (Pili kulia) akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, kuhusu maendeleo ya Mradi wa Kusafirisha Umeme wa msongo wa kilovolti 132 kutoka Tabora hadi Katavi unaotekelezwa na Kampuni ya ETDCO ambao umefikia asilimia 96, hayo yamejiri katika ziara ya Mkuu wa Mkoa huo ya kukagua miradi ya maendeleo iliyofanyika Mei 15, 2025, Mkoani Katavi.

Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, ameridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Kusafirisha Umeme wa msongo wa kilovolti 132 kutoka Tabora hadi Katavi, unaotekelezwa na Kampuni ya ETDCO, ambao kwa sasa umefikia asilimia 96.

Akizungumza Mei 14, 2025, akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Mkoa wa Katavi, Mhe. Mrindoko amewataka wananchi wa Mkoa wa Katavi, hususan wa Wilaya ya Mlele, kujitayarisha kupokea umeme kwa kujiimarisha katika shughuli za uzalishaji ili kujiongezea kipato.

Aidha, Mhe. Mrindoko ametoa rai kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kufikiria kuwekeza katika Mkoa wa Katavi, kwani sasa utakuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Alhaji Majid Mwanga, amewataka wananchi kuilinda na kuitunza miundombinu ya umeme inayojengwa na serikali kwa gharama kubwa.

Nao wananchi wa Wilaya ya Mlele wameishukuru serikali kwa kuwaletea umeme wa Gridi ya Taifa, huku wakisema kuwa hatua hiyo itachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.

Katika ziara hiyo Mhe. Mrindoko ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Alhaji Mwanga, ambapo amekagua ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 132 kutoka Tabora, pamoja na Kituo cha Kupokea, Kupozea na Kusambaza Umeme cha Inyonga, kilichopo Wilaya ya Mlele.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...