Na Pamela Mollel Arusha

Bodi ya Wakurugenzi wa TANAPA Investment Ltd imezinduliwa rasmi Novemba 10, 2025, jijini Arusha, kwa lengo la kusimamia uwekezaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA.

Uzinduzi huo umefanywa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhimini wa TANAPA, Meja Jenerali Mstaafu George Waitara, alisisitiza uongozi wenye uwazi na uwajibikaji.

Jenerali Waitara amepongeza wajumbe wapya kwa kuteuliwa na kuwataka kuwa wabunifu, waadilifu na kushirikiana na TANAPA katika kusimamia miradi ya maendeleo itakayoongeza tija kwa taifa.

Amesema bodi hiyo inalenga kujenga taswira chanya ya kampuni, kuimarisha uwekezaji wenye tija na kutekeleza miradi inayoendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Kwa upande wake, Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, CPA Mussa Nasoro Kuji, amesema shirika linaendelea kuthamini juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuweka mazingira bora ya uwekezaji na uchumi wa kijani.

Mtendaji Mkuu wa TIL, Mhandisi Dkt. Richard Matolo, amesema kampuni hiyo imejipanga kutumia teknolojia za kisasa na utaalamu wa hali ya juu ili kuboresha sekta ya ukandarasi na utoaji huduma bora.

TANAPA Investment Ltd ni kampuni tanzu ya TANAPA iliyoanzishwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ndani na nje ya nchi, ikilenga kuongeza mapato, kukuza uchumi na kuimarisha uhifadhi endelevu wa taifa.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...