Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa vijana wa Taifa hili wasikubali hata siku moja kushawishiwa kuichoma nchi yao wenyewe na kusisitiza wasikubali kukata tawi la mti ambao wameukalia.

Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akizindua Bunge la Tanzania la 13,Rais Dk.Samia ambaye ametoa muelekeo wa masuala mbalimbali yatakayotekelezwa na Serikali ya Sita ametumia nafasi hiyo kuelezea uvunjifu wa amani uliotokea Oktoba 29 mwaka huu.

“Pamoja na kuwa uchaguzi umefanyika kumewepo na uvunjifu wa amani ambao umesababisha uharibifu wa mali na upotevu wa maisha na kuharisha usalama wa nchi.

“Tunapoenda mbele niwasihi sana watanzania tuongozwe na dhamira ya maelewano ,ushirikishwaji ,kujirekebisha na umoja.

“Kwa wanangu vijana wa Taifa hili la Tanzania nchi hii imejengwa kwenye misingi ya amani na utulivu wa kisiasa.Sisi wazazi wenu tungeshawishika kufanya mliyofanya wakati huu nchi hii isingekuwa na neema na maendeleo mnayoyaona leo.

“Nataka kurudia hilo kwa wanangu vijana wa Taifa la Tanzania sisi wazazi wenu kama tungefanya mliyoyafanya ninyi nchi hii isingekuwa na neema na maendeleo mnayoyaona .

“Hivyo niwasihi sana wanangu vijana wa Tanzania .Nchi hii ni yenu ,shida zozote zinazowakabili msikubali hata siku moja kushawishiwa kuic
homa nchi yenu wenyewe .Msikubali kukata tawi la mti ambao umekalia.”
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassanakiwahutubia Wabunge pamoja na viongozi mbalimbali kabla ya kufungua rasmi Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...