SHULE ya Msingi ya Viziwi Buguruni imeibuka mshindi wa kwanza kitaifa katika mpango wa VIA Creative 2025, unaoendeshwa na Kampuni ya TotalEnergies kwa lengo la kuhamasisha elimu ya usalama barabarani kupitia ubunifu na sanaa kwa wanafunzi.
Washindi hao wametangazwa Novemba 13, 2025 jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, ambapo Shule ya Sekondari Ndalala na Shule ya Msingi Ubungo NHC ziliibuka washindi wa pili na wa tatu.
Kupitia ushindi huo, Shule ya Msingi ya Viziwi Buguruni itaiwakilisha Tanzania katika mashindano ya ngazi ya kanda yatakayofanyika Novemba 26, 2025, na ikiwa itafanya vizuri, itapata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa jijini Paris, Ufaransa.
TotalEnergies pia imeahidi kutekeleza mapendekezo ya wanafunzi wa shule hiyo kwa kuweka alama za barabarani zinazoonyesha uwepo wa shule ya viziwi katika eneo la Buguruni ili kuongeza usalama.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TotalEnergies Tanzania, Bw. Mamadou Ngom, amewapongeza wanafunzi kwa ubunifu na dhamira yao ya kuimarisha usalama barabarani.
“TotalEnergies inajivunia kuwa sehemu ya safari hii ya mabadiliko. Kupitia elimu na uhamasishaji, tunachangia kujenga mustakabali salama kwa watoto na jamii zetu, Idadi ya wanafunzi waliowezeshwa na VIA inaonyesha dhamira yetu ya dhati katika kulinda maisha na ustawi wa jamii zinazotuzunguka.” amesema
Ngom ameongeza kuwa kujumuishwa kwa shule ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia ni hatua muhimu ya ujumuishaji.
“Toleo la mwaka huu ni la kipekee zaidi kwani tumewashirikisha wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Viziwi Buguruni. Hii ni ishara kwamba hakuna mtoto anayepaswa kuachwa nyuma,” amesisitiza.
Aidha, amewapongeza washiriki wote Buza, Makuburi, Mnadani, Ugindoni, Ubungo NHC, Buguruni Primary Deaf na Ndalala Secondary kwa kuendeleza ubunifu na usalama kupitia sanaa.
Mpango wa VIA unatekelezwa na TotalEnergies Foundation kwa kushirikiana na Nafasi Art Space, shirika la ndani linalojihusisha na elimu ya ubunifu na ushirikishwaji wa jamii katika masuala ya usalama barabarani kwa kipindi cha miaka minne sasa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Nafasi Art Space, Bi. Lilian Hipolyte amesema tangu kuanzishwa kwake, mpango huo umehusisha moja kwa moja zaidi ya wanafunzi 4,800 na kufikia zaidi ya watu 100,000 katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Dodoma.
“Mpango wa VIA Safe Mobility unaendelea kuhamasisha mabadiliko yanayoongozwa na jamii. Unawapa wanafunzi uwezo wa kutumia ubunifu wao kukuza uelewa kuhusu usalama barabarani katika shule na jamii zao,” amesema.
Ametaja matokeo ya moja kwa moja ya toleo la mwaka uliopita, ikiwemo ujenzi wa ukuta wa uzio katika Shule ya Msingi Makuburi mshindi wa VIA 2024 hatua iliyopunguza kwa kiwango kikubwa ajali katika eneo hilo.

Tangu kukamilika kwa ukuta huo, hakuna ajali iliyoripotiwa ikilinganishwa na wastani wa ajali moja kwa mwezi kabla.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki mpango wa mwaka huu wameelezea namna VIA ilivyowasaidia kubadilisha mtazamo na kuwajengea uwezo wa kuwa mabalozi wa usalama barabarani.
Latifa Nassoro, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndalala, amesema “Sikuwahi kuelewa jinsi ya kujiepusha na ajali kabla ya kushiriki katika mpango huu. Sasa ninaweza kuwafundisha familia na marafiki zangu kuhusu usalama barabarani.”
Kwa upande wake, Farid Adam, mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Ubungo NHC, amesema ushiriki wao umeongeza mshikamano na uwezo wa kutatua changamoto.
“Tumepata maarifa mengi na tumetoa mapendekezo ya jinsi ya kupunguza ajali karibu na shule yetu. Tunatumaini serikali na waandaaji watayafanyia kazi,” amesema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...