Bank of Africa Tanzania imeandaa warsha kwa ajili ya wajasiriamali iitwayo SME Clinic ambayo inalenga kutoa elimu ya masuala ya fedha ili kusaidia ukuaji wa biashara zao nchini kote.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo iliyofanyika jijini Dodoma, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Biashara wa Bank of Africa Tanzania, Hamza Cherkaoui, alisema sekta ya SME ina mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania, hususan katika utoaji wa ajira, kuleta ubunifu na kuboresha maisha.
“Bank of Africa Tanzania tumejikita kuhakikisha tunawapatia wajasiriamali wadogo na wa kati maarifa, nyenzo na masuluhisho ya kifedha wanayohitaji ili kustawi. Kupitia programu kama SME Clinic, tunajenga ushirikiano endelevu na wa kudumu na wateja wetu. Kwa kaulimbiu ya mwaka huu ‘Kuwezesha Ukuaji Pamoja’, tunadhihirisha dira yetu ya kuwa mshirika wa kifedha anayeaminika anayekua sambamba na wateja wake na sekta ya biashara za Tanzania,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha SME wa Bank of Africa Tanzania, Theresia Mayanie, aliwaambia washiriki kuhusu umuhimu wa SME Clinic. Alisema biashara ndogo na za kati ndizo uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania.
Alisema hata hivyo wanakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo upatikanaji wa fedha, usimamizi wa fedha na matumizi ya teknolojia za kidijitali. “Kupitia SME Clinic tunaziba pengo hili kwa kuwapatia wateja wetu maarifa, ujuzi na masuluhisho maalumu ya kifedha kidijitali kama huduma za benki za mtandao BOAWeb/Internet Banking, huduma za benki kwa simu—B-Mobile, na mtandao wa mawakala wetu,” alisisitiza.
Kaulimbiu ya mwaka huu, “Kuwezesha Ukuaji Pamoja”, inadhihirisha dhamira ya kwenda sambamba na wajasiriamali kuhakikisha si tu wanabaki sokoni, bali wanakua kwa njia endelevu na kuchangia kikamilifu maendeleo ya taifa. SME Clinic 2025 jijini Dodoma imewaleta pamoja wajasiriamali, wataalamu wa Bank of Africa Tanzania na wadau wa sekta mbalimbali kwa siku ya mafunzo, kubadilishana mawazo na kukuza ushirikiano.
Warsha hiyo hufanyika kila mwaka na inasisitiza dhamira yake ya utoaji wa elimu ya masuala ya kifedha inayolenga kuwawezesha wajasiriamali na kusaidia ukuaji wa biashara zao nchini kote.
SME Clinic ni sehemu ya Programu ya Elimu ya Fedha ya Bank of Africa Tanzania iliyoanzishwa mwaka 2021 kufuatia Kanuni za Ulinzi wa Watumiaji wa Huduma za Fedha za mwaka 2019. Kifungu cha 19 cha kanuni hizo kinahitaji kila mtoa huduma za kifedha kuandaa programu za elimu ya fedha kwa wateja wake.
Tangu ilipoanzishwa programu hii, imefanikiwa kuendesha warsha hizi (SME Clinics) katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na wilayani Kahama na tayari imeweza kuwafikia zaidi ya wateja 800.
Warsha hii pia inalenga kuboresha ujuzi katika usimamizi wa biashara kwa wateja, kuimarisha uhusiano kati ya Bank of Africa Tanzania na wateja wake, na kuhimiza matumizi ya mifumo na teknolojia za kidijitali ili kuongeza ufanisi wa biashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Biashara wa Bank of Africa Tanzania, Hamza Cherkaoui, akizungumza wakati kufungua warsha ya Elimu ya Fedha kwa wajasiriamali (SME Clinic) yenye kaulimbiu “Kuwezesha Ukuaji Pamoja,”.Dodoma hivi karibuni

Mkuu wa Kitengo cha SME wa Bank of Africa Tanzania, Theresia Mayanie, akizungumza na wajasiriamali kuhusu namna kuwasaidia wajasiriamali kupitia teknolojia na maarifa. Alisema, “Kupitia SME Clinic, Bank of Africa


Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Biashara wa Bank of Africa Tanzania ,Hamza Cherkaoui(wa tatu kushoto), akizungumza na baada ya wajasiriamali kuhusu biashara zao na changamoto wanazokutana nazo wakati wa semina ya elimu ya fedha iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji wa Biashara wa Bank of Africa Tanzania,Hamza Cherkaoui, akiwa katika picha ya pamoja baada ya kufungua warsha ya Elimu ya Fedha kwa wajasiriamali (SME Clinic) yenye kaulimbiu “Kuwezesha Ukuaji Pamoja,”.Dodoma.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...