Katika kuendelea kuunga mkono sekta ya afya nchini, Benki ya Stanbic imetoa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 27.2 kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo, hatua inayolenga kuboresha utoaji wa huduma afya kwa wananchi.
Vifaa vilivyokabidhiwa vinajumuisha infant radiant warmer moja, oxygen concentrator nne, mifuko ya biohazard mitatu pamoja na mashuka 200, ambavyo vyote vinatarajiwa kuongeza ufanisi wa huduma ndani ya hospitali hiyo.
Akikabidhi vifaa tiba hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian amewataka watumishi wa sekta ya afya kuimarisha utendaji wao wa kazi pamoja na kutumia lugha nzuri wanapowahudumia wagonjwa na ameendelea kwa kuishukuru Benki ya Stanbic kwa mchango wake katika kusaidia na kuboresha huduma za afya kwa jamii.
Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Tanga, Francis Fundikira, amesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanaboresha maisha ya kila Mtanzania kupitia uwekezaji na michango mbalimbali ya kijamii.
Aliendelea kusema “Mpango huu ni sehemu endelevu ya uwajibikaji wa kijamii wa Benki ya Stanbic unaolenga kurudisha fadhila kwa jamii, sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya kukua pamoja tangu benki hiyo ianze kutoa huduma nchini Tanzania”. alisema Fundikira.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo Tanga, Dkt. Frank Shega, ameishukuru Benki ya Stanbic kwa kuwapatia vifaa hivyo, huku akitoa wito kwa mashirika binafsi kuendelea kujitolea ili kuboresha zaidi sekta ya afya nchini.

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian (wapili kushoto) na Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Tanga, Francis Fundikira (kushoto) wakikabidhi moja kati ya vifa Tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 27. 2 walivyotoa benki ya Stanbic katika Hospitali ya Rufaa Bombo mkoani Tanga kwa Mganga mfawidhi hospitali hiyo, Dkt. Frank Shega (watatu kushoto), Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Clemence Imani (wapili kulia) na Muuguzi wa hospitali hiyo.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...