Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imekipongeza Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kwa kuanzisha program atamizi ya biashara ambayo itawatengeneza wahitimu wa chuo hicho kuwa wafanyabiashara mahiri siku za baadae.

Pongezi hizo zilitolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk Hashill Abdalah, wakati wa mahafali ya 60 ya wanafunzi wa chuo hicho alipomwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga.

Alipongeza kuanzishwa kwa program bunifu ambapo wanafunzi wenye mawazo ya biashara huyawasilisha chuoni hapo kwaajili ya kufanyiwa kazi yamekuwa na mchango mkubwa kuwafanya wanafunzi wasome biashara kwa vitendo na si nadharia.

“Hawa wanafunzi wakihitimu watakuwa wafanyabiashara wakubwa ambao watajiajiri na kutengeneza ajira kwa wenzao, na kuongeza pato la taifa, mnaomaliza leo na mnaoendelea na wale ambao hamjajiunga na CBE mfahamu kuwa ndani ya chuo kuna fursa nyingi sana zitakazowakomboa kiuchumi,” alisema

“Eendeleeni kuitumia elimu miyopata hapa CBE itawasiaidia nyinyi na taifa kwa ujumla, endeleeni kushirikiana ili kuleta maendeleo ya chuo kitaaluma, uaminifu na uzalendo ndio nguzo kuu ya mafanikio kwa hiyo wahitimu mkawe wazalendo kweli kweli kwa taifa lenu,” alisema

Aliwapongeza wahitimu wa chuo hicho kwa kusoma kwa bidii na hatimaye kuhitimu kwenye ngazi mbalimbali za elimu

Alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maboresho kwenye elimu, kwenye mitaala na sekta ya viwanda na kuanzisha ufadhili wa Samia unaofadhili wanafunzi kwenye masomo ya sayansi.

Alisema ufadhili huo umekuwa muhimu sana hasa wakati huu ambapo dunia inajielekeza kwenye matumizi ya sayansi na teknolojia mbalimbali.

Alisema Rais Samia ameongeza upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi na ameanzisha utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa astashahada jambo ambalo linahamasisha wanafunzi wengi kujiunga na vyuo kwa ngazi za shahada na stashahada.

“Mmesema kwenye hotuba yenu kuwa mwaka huu zaidi ya wanafunzi 6,000 wanahitimu kwenye kampasi zenu zote na kampasi ya Dar es Salaam pekee wanafunzi 3,500 wanahitimu, haya yote yamesabaishwa na amani na utulivu uliopo,” alisema

Alisema ni jukumu la vijana na wanafunzi wanaoendelea na masomo kulinda amani ya nchi kwani bila amani mahafali hayo yasingewezekana kufanyika hivyo kila mwanafunzi anawajibika kuilinda na kudumisha amani.

Alisema ongezeko la machapisho ya CBE ambayo yamefikia zaidi ya 150 kwa mwaka 2025 ni ushahidi kuwa chuo hicho kinafanya kazi nzuri sana.

Mkuu wa chuo hicho, Profesa Edda Lwoga alisema CBE imeendelea kutanua wigo wa ushirikiano kitaifa na kimataifa na kwamba kitaifa wanashirikiana na taasisi 10 wakati kimataifa wanashirikiana na vyuo vya Finland, China, Ujerumani, Sweden, Uturuki na Italia.

Alisema ushirikiano huo umesaidia kuboresha mitaala yao kuanzia ngazi ya shahada hadi shahada ya umahiri na kwamba tangu mwaka 2016, CBE imekuwa ikiandaa makongamano ya kimataifa katika biashara na uchumi na mwaka huu lilifanyika mwezi Novemba.

Alisema kwenye kongamano hilo jumla ya tafiti 101 ziliwasilishwa na aliongeza kuwa wanataaluma wa CBE na wanafunzi wameendelea kutoa machapisho ambayo yamepandisha hadhi ya chuo hicho miongoni mwa vyuo vikuu bora duniani.

“Utafiti uliofanywa mwaka jana na taasisi moja umekiweka chuo chetu kimewekwa kwenye nafasi ya nane kati ya vyuo 47 vya elimu ya juu kwa hiyo wahitimu wetu, wanafunzi mnaoendelea na wale wanaotarajia kuja waje tu kwasababu CBE ni sehemu sahihi ya kusoma,” alisema






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...