*Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Utalii awashukuru wadau sekta ya utalii kuipigia kura Tanzania




Na Said Mwishehe,Michuzi TV

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema ushindi wa tuzo tano za utalii ikiwemo tuzo kubwa kuliko zote ambayo ni tuzo ya utalii wa safari ambapo tuzo hiyo inathibitisha Tanzania inavivutio vinavyokubalika duniani.

Akizungumza leo Desemba 8,2025 baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,Dar es Salaam akitoa katika Tuzo za Dunia za Utalii 2025-Bahrain, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Hassan Abbas amesema ushindi huo unaithibutisha dunia Tanzania kuwa na vivutio bora vya utalii hivyo ni wakati wa watalii kuja nchini kujivichari kwa utalii wa kıla aina.

“Kwa mwaka wa pili mfululizo Tanzania inashinda tuzo ya Dunia katika eneo
la utalii wa safari.Hii ndio tuzo kubwa kuliko zote duniani kama ambavyo kwa wenzetu wa filamu wana tuzo za Oscars na kwa wenzetu wa muziki wana tuzo za Grammy.

“Tunaishukuru Serikali yetu chini ya mama yetu Rais Dk.Samia Suluhu Hasssan na marais wengine wote waliopita kwa namna ambavyo waliweka nguvu zao katika kuhifadhi na kuuendeleza utalii.

“Tunafahamu Rais Dk.Samia ameshiriki mpaka kutengeneza filamu ya The Royal Tour baadae akashiriki filamu nyingine ya kuitangaza nchi yetu inaitwa Amazing Tanzania.Kwahiyo tuzo hii ni matokeo ya mambo mawili,moja ni Uhifadhi.

“Kama tusingekuwa tumehufadhi vivutio vyetu leo tusingeshinda lakini la pili ni kuendeleza utalii kwahiyo haya mawili ndio siri ya ushindi wetu na dunia yote sasa inatuangalia Tanzania kwa tuzo hii inazidi kutuona ni watu wenye vivutio vizuri sana na tunaamini kupitia tuzo hizi nchi imetangazika lakini watalii wengi wataendelea kuja Tanzania.”

Akieleza zaidi Dk.Abbas amesema kutokana na kushinda tuzo hiyo Tanzania imepewa nafasi ya kuwa wenyeji wa kuandaa hizi tuzo za dunia mwaka 2026 .“Mwakani Dunia itakuja Tanzania kwa maana ya wadau wa sekta ya Utalii yakiwemo mashirika wa utalii,kampuni kubwa sasa wao watazifuata tuzo zao Tanzania.”

Kuhusu sekta ya utalii amesema iko vizuri kwani hivi sasa idadi ya watalii wa nje wamefikia milioni 2.1 na ukichanyanya na watalii wa ndani inafanya kwa sasa kuwa na kumla ya watalii Milioni 5.3

Ameongeza Tanzania inahifadhi za Taifa 21 ,mapori ya akiba na mapori tengefu zaidi ya 50 na misitu 462 .Hiyo maana yake ni kuwa Tanzania imetumia muda mwingi kuhifadhi na kuendeleza hifadhi zake.

“Ndio maana leo tunafurahia matunda ya utalii wetu ,nchi nyingi zinategemea utalii wa ufukweni , nchi nyingine zinategemea utalii wa utamaduni lakini sisi kitu cha kwanza pamoja na kwamba tuna beach na kila kitu kingine sehemu kubwa ya utalii wetu ni wanyamapori.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) Ephraim Mafuru kutokana na Tanzania kushinda tuzo hizo ametoa shukrani kwa wadau wa sekta ya utalii kwani mchakato wa tuzo hizo unahusisha kupigiwa kura.

“Sasa wanaopigiwa kura ni wadau wa sekta ya utalii sio tu watalii peke yake kwani kuna wao wameiona Tanzania na vivutio vyake vya utalii hasa utalii huu wa safari kama kituo bora kabisa duniani.

“Kwahiyo dunia imeiamini Tanzania ,dunia imeiamini Serengeti na hifadhi nyingine zote na ndio maaha tukapigiwa kura na tukashinda tuzo hizi .Sasa wengi mtajiuliza tunaelekea wapi baada ya hapa , nidhahiri tumejipanga kuidhihirishia dunia ya kwamba Tanzania ni kituo cha vivutio vya utalii na wageni wengi waendelee kuja kuviona vivutio hivi .

“Tuzo tulizoshinda ni tano kwa mwaka huu na hii ya utalii wa safari ndio tuzo kubwa kuliko zote ,ni tuzo ambayo Tanzania imekuwa nchi bora ya utalii wa safari duniani ,Tanzania pia imeshinda tuzo ya hifadhi bora kabisa duniani ya Serengeti .

“Nimeseme Tanzania tunavivutio vingi ,Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ,mwaka jana Serikali imejenga barabara za kilometa 2808 katika maeneo ya hifadhi na hivyo hifadhi zetu zinafikika.Amani ipo na dunia imetuchagua sisi.”









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...