Na Janeth Raphael MichuziTv - Dar es Salaam
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema matukio ya Uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 yalikuwa matukio ya kutengeneza yakidhamiria kuangusha Dola ya Tanzania.
Rais Samia ameyaeleza hayo leo Jumanne Disemba 02, 2025 wakati akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, akisema Vijana wa Kitanzania walifanywa makasuku na kuimbishwa.
"Vijana wetu walifanywa makasuku na kuimbishwa kabisa yaliyotokea Madagascar yatokee na hapa. Lakini ukimvuta kijana pembeni ebu niambie Madagascar kumetokea nini hajui, unataka hapa kitokee nini? Hajui lakini waliimbishwa wimbo huo." Amesema Rais Samia.
Rais Samia amekaririwa akisema vurugu zile ni mradi mpana wenye nia pana ya uovu ulio na wafadhili na watekelezaji, akisema katika vurugu ile wengine waliingia bila ya kujua na kufuata mikumbo huku wengine pia wakijihusisha na vurugu zile kwa hadaa za maisha mazuri, huku wengine wakilipwa fedha ili kushiriki katika vurugu zile.
Akionesha kuumizwa na madhara yaliyojitokeza wakati wa matukio hayo ya uvunjifu wa amani ya Oktoba 29, 2025, Rais Samia ametaka mjadala wa pamoha, akihoji ikiwa yale yalikuwa maandamano ama vurugu na uharibifu wa mali za umma.









Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...