*Yampokea bondia maarufu duniani Terence Crawford ,kumpeleka katika vivutio vya utalii

Na Said Mwishehe,Michuzi TV


MKURUGENZI wa Bodi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru amesema mkakati wa bodi hiyo ni kuendelea kuwatumia watu mashuhuri ambao wanavipaji na ushawishi mkubwa kuisemea mema Tanzania lengo likiwa kuunganisha utalii wa michezo ili kuongeza watalii nchini.

Mafuru ameyasema hayo leo Mei 24,2026 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataita wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi wa Bondia maarufu kutoka Marekani Terence Crawford ambaye hajawahi kupoteza pambano lolote na akiwa nchini atatembelea vivutio vya utalii nchini.

“Mmeshuhudia Bodi ya Utali Tanzania imeweza kumkaribisha kwa mara ya kwanza nchini Tanzania bondia maarufu kabisa duniani Terence Crawford,akiwa hapa nchini tumemuandalia ziara ya wiki nzima kutembelea vivutio vya utalii.

“Tunafanya hivyo ili kuwatumia watu mashuhuri ambao wana vipaji na ushawishi mkubwa kwa ajili ya kuisemea mema Tanzania lengo likiwa kuunganisha mazao ya utalii wa michezo ili yaongezee wageni kuja nchini kutalii.

“Mbali na utalii wa wanyamapori, utalii wa fukwe ,utalii wa mikutano, utalii wa utamaduni ,sasa Wizara ya Maliasili na Utalii imejikita kusaidia utalii wa michezo,”amesema.

Amefafanua kama ilivyoshuhudiwa kulikuwa na mchezaji bora kabisa aliyewahi kuchezea timu ya Manchester United na pia alichezea timu ya Taifa ya Uingereza Rio Ferdinand ameondoka nchini juzi leo amekuja bondia Terence Crawford ambaye hajawahi kupigwa shindano lolote ,

Mafuru amesema bodi ya utalii itampeleka bondia huyo Serengeti , Ngorongoro , Zanzibar na Tarangire sambamba na kukutana na viongozi mbalimbali.”Tunataka tumpige shule ya utalii wa Tanzania na akiondoka akaiongelee mema nchi yetu pendwa ya Tanzania.”









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...