Na. Peter Haule, WF, Nairobi, Kenya

Tanzania na Marekani zimeeleza dhamira ya kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za maendeleo, ikiwemo afya, kilimo, nishati, madini, miundombinu, elimu na utalii.

Dhamira hiyo imeelezwa wakati Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu wa Hazina ya Marekani anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Bi. Erin Browne, mjini Nairobi, Kenya, kando ya Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Luswetula amezialika kampuni na wawekezaji kutoka Marekani kutumia fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana Tanzania, akitaja maeneo ya kilimo, nishati, madini, miundombinu, afya, elimu na utalii.

Aidha, Mhe. Luswetula ameishukuru Serikali ya Marekani kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania pamoja na mchango wake katika maeneo mbalimbali ya maendeleo tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mwaka 1968.

Amesema ushirikiano huo umekuwa na mchango katika juhudi za Tanzania za kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kupunguza umaskini.

Kwa upande wake, Naibu Katibu wa Hazina ya Marekani anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Bi. Erin Browne, amesema Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya maendeleo, pamoja na kuimarisha na kukuza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo.

Mazungumzo hayo yameangazia pia umuhimu wa kuendelea kujenga ushirikiano wa kiuchumi na uwekezaji kati ya Tanzania na Marekani kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb) akisalimiana na Naibu Katibu wa Hazina ya Marekani anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Bi. Erin Browne, mjini Nairobi, Kenya, kando ya Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya.



Naibu Katibu wa Hazina ya Marekani anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Bi. Erin Browne, mjini Nairobi, Kenya, akizungumza kuhusu ushirikiano wa maendeleo wakati wa mkutano na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), kando ya Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya.




Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb) (katikati), akieleza fursa za uwekezaji wakati wa mkutano na Naibu Katibu wa Hazina ya Marekani anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Bi. Erin Browne kando ya Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha Afrika, kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya, wengine ni wajumbe walioambatana nae kutoka Tanzania.




Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb) (wa pili kushoto) na Naibu Katibu wa Hazina ya Marekani anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Bi. Erin Browne (wa pili kulia) wakiwa katika mkutano kati yao, kando ya Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha Afrika, kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya.





Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb) na Naibu Katibu wa Hazina ya Marekani anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Bi. Erin Browne wakiteta jambo, kando ya Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha Afrika, kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya.



(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...