Halotel ikiwa ni kampuni ya mawasiliano Tanzania, ikitoa huduma mbalimbali za mawasiliano na ikiendelea kukidhi mahitaji ya wateja wao. Kwa kuzingatia usalama na uaminifu Halotel inaendelea kutoa huduma bora na kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya mawasiliano na jamii kiujumla.
Akiongea katika tukio hilo Mkurugenzi wa Halotel tawi la Mtwara Bwana Emmanuel Monyo “Halotel inaendelea kusimama imara katika kufanikisha malengo yake ya kukuza usawa na ujumuishaji katika pande zote za jamii.
Afisa uhusiano na mawasiliano wa Halotel, Roxana Kadio ambae aliwasilisha msaada huo alisema Halotel inaedelea kujenga ujumuishaji ambao kila mtu bila kujali uwezo wao anaweza kushiriki kikamilifu katika jamii, aliendelea kusema kuwa Halotel iliamua kuwaunga mkono wanawake wa Mtwara baada ya kujifunza kuwa wanapitia changamoto za chakula na vifaa vya nyumbani na kama kampuni inayokua nia yetu kutoa mkono wa msaada kwa jamii ya kitanzania.
“Mahitaji yaliyotolewa na Halotel ni pamoja na Chakula kama Mchele, Sukari na Mafuta ya kupikia lakini pia kutoa msaada wa magodoro na vifaa vingine vya nyumbani. Vyote hivi ni katika kuwahudumia wanawake hawa na kuwaonesha kuwa hawako peke yao katika changamoto wanazozipita” Roxana alisema.
Halotel itaendelea kutoa ushirikiano kwa majukwaa ambayo yanajikita katika kuwainua wanawake. Lakini pia Halotel itaendelea kutia chachu ya maendeleo kwa wateja wake na jamii kiujumla.
Halotel wakikabidhi msaada wa Vifaa vya nyumbani na Chakula katika taasisi ya Jukwaa la Wanawake walemavu Mtwara. Kushoto akiwa Mkurugenzi wa Tawi la Halotel Mtwara Bw. Emmanuel Monyo, Kati ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Jukwaa la Wanawake walemavu Mtwara Bi. Fatuma Mohamed Mkondomoka, Kulia Afisa uhusiano na Mawasiliano makao makuu Halotel Bi. Roxana Kadio.
KILINGE Salama (Safe Space) kilichoandaliwa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Chamwibua Diwani, Farida Abdallah ambaye ni Diwani wa wilaya ya Mtwara ambapo ameeleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wanawake viongozi ikiwemwo kukatishwa tamaa ili wasiweze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Akizungumza leo Machi 28, 2024 wakati wa kilinge salama kilichofanyika katika ukumbi wa TGNP jijini Dar es Salaam, Diwani huyo ambaye aliishia kidato cha pili na kupata ujauzito huku akimpote Mama yake mzazi amewaasa wanawake kutokukata tamaa pale yanapojitokeza maneno ya kukatisha tamaa pale yanapojitokeza wakati wa harakati za kutafuta nafasi za uongozi.
“Wakati nawania nafasi ya uongozi watu walikuja kunikatisha tamaa ili ni sigombee….. hata kwenda kumshawishi Mme wangu ili anikatishe tamaa lakini hawakufanikiwa….” Amesema Farida.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi akizungumza wakati wa kufungua Kilinge salama ambapo ni mazingira ambayo ni rasmi au yasiyo rasmi ambayo wanawake na wasichana wanapata nafasi ya kujadili kwa uhuru masuala yao, amesema kuwa Katika mwezi Machi wa wanawake, TGNP imekuwa ikiandaa vilinge hivyo ili kuhamasisha wanawake kuingia katika nafasi za uongozi.
“Mategemeo yangu ni kwamba mwisho wa siku ya leo tutaungana kwa pamoja kuendelea kusimamia Agenda ya mwanamke na uongozi katika mkoa wetu wa Dar es Salaam.”
Pia Mkurugenzi Mtendaji Lilian ameweka bayana takwimu za Wenyeviti wa vijiji kuwa ni asilimia 2.1, Wenyeviti vitongoji ni asilimia 6.7 na Wenyeviti mitaa ni asilimia 12.6.
Kwa upande wa Wabunge wa kuchaguliwa, wanawake ni 25 ya Wabunge 264 ambayo ni sawa na asilimia 9.5 tu ya Wabunge wote, idadi ya Wabunge wanawake wa Viti Maalumu ni 113 ambayo ni sawa na asilimia 29 ya Wabunge wote. Jumla ya Wabunge Wanawake ni 142 sawa na asilimia 37 ya idadi ya Wabunge wote ambao ni 393 ambapo ili kufikia 50 kwa 50 ya uongozi wa Wanawake Viongozi lazima ifikiwe kwa kutoa elimu kwa wanawake na wasichana waweze kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
Lilia pia ameeleza kuwa malengo ya Kilinge salama kwa Wasichana na Wanawake ni kukaa pamoja na viongozi wanawake wanaochipukia na viongozi wanawake wenye uzoefu, kuandika na kusambazi kestoria za safari za uongozi za wanawake viongozi mahiri ili kuonesha michango waliyonayo katika maendeleo ya nchi.
Pia kutoa hamasa kwa viongozi wanawake wanaochipukia au wanawake wanaotamani kuwa viongozi.
Kilinge Salama kwa Wanawake na Wasichana pamoja na viongozi leo ni kutoka mkoa wa Dar es Salaam, halmashauri za Ilala, Kinondoni na Temeke, Mtwara, Lindi na Pwani.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameeleza hadi sasa maandalizi ya uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru yamefikia zaidi ya asilimia 90 huku akihimiza Mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha unahamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika tukio hilo la kihistoria.
Amesema hayo wakati akikagua maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Mkoani Kilimanjaro.
Aidha, Naibu Waziri Katambi amesema kuwa Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu 2024 zinaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa rasmi mwaka 1964 zikienda sanjari na Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Vile vile, Mhe. Katambi ameupongeza mkoa huo kwa utayari na maandalizi mazuri ya tukio hilo la kitaifa na kuongeza kuwa mwenge huo ni alama ya umoja, hivyo utakimbizwa katika halmashuri 195 kwa lengo la kuunganisha wananchi sambamba na kukagua viwango vya utekelezaji wa miradi ya serikali katika kuwahudumia wananchi.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Fatma Rajab amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Wizara hiyo wamekua wakishirikiana kwa karibu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo wa Kilimanjaro katika kuhakikisha maandalizi yanakamilika ndani ya muda uliopangwa.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Jackson Masaka amesema kuwa viongozi wa mkoa wamekua na utaratibu wa kukutana na makundi mbalimbali ya wananchi ikiwemo Bodaboda, Wazee, Wafanyabiashara, Wanawake kwa lengo la kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo.
Mabasi hayo ni Kampuni ya Sauli pamoja na New Force Taarifa zaidi za chanzo cha ajali hiyo na majeruhi zitatolewa baadaye leo na kamanda wa polisi.
Endelea kutufuatilia kwenye page zetu Michuzi Tv, Michuzi blog kupata taarifa zaidi
Na.Abel Paul,Jeshi la Polisi- Arusha.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Naibu kamishna wa Polisi DCP David Misime amesema Sherehe hiyo hutanguliwa na waumini wa dini hizo hukusanyika kwa wingi na kushiriki Ibada ambazo hufanyika nyakati za mchana na usiku,siku za Alhamis,Ijumaa,Jumamosi na Jumapili na Jumatatu ya Pasaka.
Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi limeendelea kujiimarisha ulinzi na kuhakikisha kwamba ibada na sherehe hizo zinafanyika katika hali ya amani, utulivu na usalama wa kutosha ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo limejipanga kufanya doria katika mitaa na barabara zote kuu ili kuzuia uhalifu au uvunjifu wowote ule wa amani.
Sambamba na hilo amesema katika barabara zote kuu, kutakuwa na doria za Askari ili kuzuia ajali za barabarani, Pamoja na kukagua watakao kiuka sheria za usalama barabarani kama vile kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi, wakiwa wamelewa pombe na kujaza abiria kupita kupita kiasi.
Msemaji wa Jeshi hilo amesema Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Viongozi wa nyumba za ibada ambao watakuwa na ibada katika kipindi hiki cha Juma Kuu wasisite kuwasiliana na Viongozi wa Polisi katika maeneo yao ili washirikiane katika kuimarisha usalama kwa kipindi chote.
Vile vile Jeshi hilo Pia linaendelea kutoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuzingatia kanuni ya kiusalama inayosema “usalama unaanza na mimi mwenyewe”
Pia Pamoja na hilo Jeshi la Polisi nchini limewataka wananchi kuchukua tahadhari na kujiepusha na marafiki wa mitandaoni na matapeli wanaojitangaza kuwa wanatoa mikopo kupitia mitandao.
Na Munir Shemweta, NZEGA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeipongeza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa utekelezaji wa mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) katika halmashauri ya Mji wa Nzega mkoa wa Tabora.
Kauli hiyo imetolewa tarehe 27 Machi 2027 wilayani Nzega na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe, Japhet Hasunga wakati wa ziara ya Kamati yake kukagua hatua iliyofikiwa katika Utekelezaji mradi wa LTIP kwenye halmashauri ya Mji wa Nzega mkoani Tabora.
Mradi wa LTIP katika Halmashauri ya Mji wa Nzega umepewa lengo la kurasimisha vipande vya ardhi 20,000 na kuongeza alama za msingi za upimaji 14.
"Niwapongeze kwa kazi hii mlioamua kuifanya tangu tupate uhuru tumekuwa na changamoto za ardhi kuanzia kutambua, kupima, kurasimisha na kadhalika, kumekuwa na shida" amesema Mhe, Hasunga.
Amesema, Mhe, Rais ameamua kutoa fedha nyingi za mradi wa LTIP na Bunge kuidhinisha ambapo kwa upande wa halmashauri ya Mji Nzega kiasi cha Shilingi Bilioni 1.4 kimeidhinishwa kwa ajili ya Kata tano hivyo wananchi watumie fursa ya kutambuliwa maeneo yao na hatimaye kupatiwa hati kupitia mradi huo.
Ameeleza kuwa, Kamati yake ya PAC itakwenda kupima thamani ya fedha zilizopitishwa na Bunge pale tu wananchi watakapokuwa na hati.
"Msipopata hati hii mingine yote ni michakato, sisi hatuhitaji michakato tunataka kuona watu wangapi wana hati" alisema Mhe, Hasunga.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda amesema, wizara yake ina uhakika michakato yote itakapokamilika katika mji wa Nzega hati milki za ardhi zitaenda kutolewa kwa wananchi.
Kwa mujibu wa Mhe, Pinda utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) unaenda kutoa jumla ya hati milki za ardhi 1,500,000 kwa maeneo yote yanayopotiwa na mradi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga ameweka wazi kuwa, kazi iliyofanyika kwa halmashauri ya Mji wa Nzega kwa sasa imefikia asilimia 55 na kiasi cha fedha kilichotolewa ni asilimia 39.
Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) unatekelezwa kwa mkopo wenye thamani ya Dola za Kimarekani milionin150 kutoka Benki ya Dunia kwa kupindi cha miaka 5 katika halmashauri 58 nchini. Mradi huo unalenga kuboresha utawala na usimamizi wa ardhi nchini pamoja na kuongeza usalama wa milki za ardhi kwa wananchi.Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe, Japhet Hasunga akisalimiana na waratibu wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) alipowasili na Kamati yake kukagua hatua iliyofikiwa katika Utekelezaji wa Mradi huo Katika Mji wa Nzega mkoa wa Tabora tarehe 27 Machi 2024.Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe, Japhet Hasunga akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mhandisi Anthony Sanga na Naibu Waziri Mhe, Geophrey Pinda wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ilipokwenda kukagua hatua iliyofikiwa katika Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi Katika Mji wa Nzega mkoa wa Tabora tarehe 27 Machi 2024.Sehemu ya washiriki wa ziara Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ilipokwenda kukagua hatua iliyofikiwa katika Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi Katika Mji wa Nzega mkoa wa Tabora tarehe 27 Machi 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe, Geophrey Pinda akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ilipokwenda kukagua hatua iliyofikiwa katika Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi Katika Mji wa Nzega mkoa wa Tabora tarehe 27 Machi 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
KATIBU Tawala wilaya ya Kibaha , mkoa wa Pwani, Moses Magogwa amewaasa wananchi kujiepusha na ukataji miti kiholela na badala yake wajenge tabia ya kupanda miti na kuitunza kwani ndio jawabu la kupambana na uharibifu wa mazingira.
Ameeleza hayo wakati Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ilipofanya maadhimisho ya siku ya upandaji miti kata ya Kikongo, wilayani humo.
Magogwa akimuwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo, Nickson Simon John alieleza, kampeni ya kupanda miti Tanzania zilianza tangu mwaka 1999 , ambapo ilionekana hali na kasi ya ukataji miti inaongezeka.
"Maana yake nini, kama jitihada hizi zisingewekwa mapema hali ingekua mbaya sana leo hii, na ndio maana leo tupo hapa kuendelea kuwa sehemu ya upandaji miti ili dunia yetu ibaki salama ," alisisitiza Magogwa.
Magogwa anaeleza, misitu ni ubunifu inabidi tutumie nishati mbadala ili kuachana na kuharibu mazingira.
"Mfano nikitazama mkoa wa Dar es salaam ndio Jiji linaloongoza kwa utumiaji wa mkaa huku bidhaa hizo zikitokea mkoa wa Pwani, tutaanda utaratibu maalum ikiwezekana Serikali ione haja ya kuongeza kasi kupeleka njia za mbadala mbalimbali ili maeneo mengine yasalimike katika kutunza misitu" alieleza Magogwa.
"Tunawajibu wa kupanda miti na kuifuatilia, hivyo ubunifu wetu ni kutafuta energy mbadala ili misitu yetu isiharibike, wenyeviti wote wa vijiji msiuze maeneo bila kufuata utaratibu, endeleeni kupokea maombi ila taarifa zifike ofisi ya Mkurugenzi, atume wataalamu ili kujiridhisha"
Alieleza kwa utaratibu huo utasaidia kupunguza pia matatizo ya migogoro ya ardhi na ufyekaji wa maeneo ya misitu ambayo bado haipo kwa uangalizi wa TFS.
Hata hivyo, Magogwa aliipongeza TFS kwa kazi nzuri wanayofanya na wilaya itaendelea kuwapa ushirikiano ili kuhakikisha misitu inabaki salama kwa manufaa ya nchi.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mkali Saidi Kanusu aliwataka wanaccm na wananchi kuiga mfano huo bora ambao umeonyeshwa kwa vitendo na Ofisi ya mkuu wa Wilaya pamoja na TFS.