Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wakiangalia album ya picha za matukio ya Ziara Rasmi aliyoifanya katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan akiongoza ujumbe wa Nchi yake kwenye mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Ziara yake Rasmi katika Ikulu Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kuweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal Atatürk katika makumbusho ya Anitkabir, Atatürk's Jijini Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima mbele ya kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal Atatürk katika makumbusho ya Anitkabir, Atatürk's Jijini Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal Atatürk katika makumbusho ya Anitkabir, Atatürk's Jijini Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na kwa upande wa Uturuki Rais wa Baraza la Elimu Profesa Dkt. Erol Ozvar wakitia saini Makubaliano ya Ushirikiano katika Nyanja ya Elimu ya Juu baina ya Tanzania na Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wakishuhudia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Lela Muhamed Mussa pamoja na Rais wa Baraza la Utalii la Jamhuri ya Uturuki Abdullah Eren wakisaini hati za makubaliano kwa ajili ya kuanzisha ufadhili kwa wanafunzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Uturuki wanaohitimu katika Elimu ya Juu tarehe 18 Aprili, 2024.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amepokelewa kwa shangwe na nderemo na wananchi wa Mbarali, wakiongozwa na vijana waendesha bodaboda, baada ya kuwasili na msafara wake katika Kata ya Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, leo Aprili 18, 2024, akitokea Mbeya Mjini.

Dk Nchimbi alisimama kuwasalimia wananchi hao wa Ubaruku, akiwa njiani kuelekea Mkoani Njombe ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya mikoa 6 ya Nyanda za Juu Kusini, ambapo ameambatana na Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndg. Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC - Oganaizesheni Ndg. Issa Haji Gavu.







NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

HOSPITALI ya Heameda imezindua Maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha.

Akizungumza April 18 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mtambo huo ambao ni lulu nchini katika taratibu za matibabu ya moyo, Mkurugenzi wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Meshack Mwandolela alisema hospitali iliamua kuitenga siku ya April 18,2024 kwa ajili ya vipimo vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza na moja wapo ya magonjwa hayo ni ugonjwa wa moyo na wameibaini watu wengi wanasumbuliwa na maradhi hayo na hawakujua kwasababu hayaoneshi dalili.

Aidha Dkt.Mwandolela alisema mtambo huo unawasaidia kuweka vifaa maalumu kusaidia wagonjwa wa moyo ambavyo ni pacemaker vinavyowekwa kwenye moyo kwa ajili ya kusaidia mambo mbalimbali.

"Mojawapo ya magonjwa yanayotibiwa kwa pacemaker ni wale wenye moyo unaoenda taratibu na wale wanaopata milipuko ya moyo bila mpangilio na Kuna wengine wanapata moyo mkubwa,na kushindwa kufanya kazi kwahiyo tunawawekea pacemaker maalumu ambayo inasaidia kupunguza saizi ya moyo,lakini pia kuongea nguvu ya moyo kusukuma damu" Mwandolela alisema

Aidha Dkt.Mwandolela alieleza kuwa tangu wameweka mtambo wa CATH LAB wamefanikiwa kufanya vipimo kwa wagonjwa zaidi ya 15 pamoja na kuweka pacemaker kwa wagonjwa takribani watatu vilevile na kwa wagonjwa watatu ambao walikua na changamoto ya kuziba kwa mishipa inayokwenda kwenye moyo.

"Tumeweza kuokoa gharama kubwa sana, kwa ajili ya matibabu haya mtu huyu ambaye alikua anatakiwa asafiri kwenda India anakuwa ameokoa pesa na muda kwa wanaomuuguza kwahiyo tunapunguzaa gharama kubwa ili watu waweze kufanya mambo yao mengine wakiwa hapa" alieleza Dkt.Mwandolela

Pamoja na hayo ametoa rai kwa wananchi kutoogopa matumizi ya teknolojia za kisasa ambazo zilichelewa kuingia nchini ,na zimekuwa zikitumika huko katika mataifa ya kigeni kwa muda mrefu ambapo imechangia kuokoa maisha na watu kuishi kwa muda mrefu.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt.Gunini Kamba, ameipongeza Hospitali ya Heameda kwa kufunga vifaa Bora ambavyo vinafanya huduma za kibingwa kwa kuzibua mishipa iliyoziba kwenye moyo.

"Mashine iliyofungwa ni ya kisasa sana ,katika nchi yetu zipo tano,na ukizingatia ina uwezo wa kuzibua mishipa ya moyo, tunashukuru tuna JKCI inafanya huduma hiyo lakini peke yake haijitoshelezi", alisema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Heameda Bi.Edwina Lupembe alionesha kujivunia timu yao ya watendaji katika hospitali hiyo kwa uadilifu wao kazini pamoja na juhudi katika shughuli zao kupambania kutoa huduma bora.

Vilevile Madaktari kutoka India walieleza kuwa watashiriki kuziba nafasi iliyokuwa wazi nchini kwa kutoa huduma za kibingwa katika matibabu ya ugonjwa wa moyo kwa wagonjwa ambao wamechelewa kupata huduma hiyo ya upasuaji wa moyo (Cardiac Surgery).

Heameda imejikita hasa katika huduma za kitabibu katika magonjwa ya moyo, saratani, pamoja na kuchuja damu kwa wagonjwa wa figo iliyofeli ambapo wamelenga kusaidia wananchi kupunguaza gharama kufata matibabu nje ya nchi.


Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Gunini Kamba akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Heameda Bi.Edwina Lupembe na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Mwandolela


Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Mwandolela akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Gunini Kamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali ya Heameda iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Heameda Bi.Edwina Lupembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.


Daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka nchini Inida akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali ya Heameda iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Mwandolela akieleza jambo kwa wadau mbalimbali walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.


Sehemu maalumu ya kuwalaza wagonjwa mara baada ya kufanyiwa matibabu katika Hospitali ya Heameda iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya madaktari bingwa pamoja na wadau mbalimbali wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Balozi wa Pakistani nchini Siraj Ahmad Khan (kushoto), Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Digit, Abdul Rehman Mahmood (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa simu maalum iitwayo Smart Kitochi+ kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa kuona na kusikia huku ikiongeza matumizi ya dijitali nchini, hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.





Ili kuimarisha ushirikishwaji na kuongeza matumizi ya huduma na bidhaa za kidijitali nchini, kampuni ya teknolojia na mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC imezindua simujanja ya kidijitali inayoitwa 'Smart Kitochi +' ambayo imeundwa ikiwa na vipengele muhimu kwa ajili ya wateja wasiosikia na wasioona.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Bi. Linda Riwa, amesema kuwa uzinduzi huu ni sehemu ya juhudi endelevu za kampuni hiyo za kukuza ushirikishwaji huku ikiunga mkono serikali katika azma yake ya kuchochea matumizi ya bidhaa na huduma za kidigitali.

"Tunafurahia mapinduzi haya ya kuleta bidhaa na huduma za kidigitali na za kibunifu kwa wateja wetu wenye mahitaji mbalimbali kote nchini. Leo, tunazindua simu ya kipekee ya kidijitali inayoitwa 'Smart Kitochi+' ambayo mbali na sifa kama kioo kikubwa na cha kugusa, uwezo mkubwa wa kuhifadhi na betri inayodumu muda mrefu, simu hii pia itawanufaisha wateja wetu wenye ulemavu wa kusikia na kuona,” anasema Linda.

“Simu hii inajumuisha teknolojia ya kugusa na sauti, ikiruhusu wateja wenye changamoto hizi kupata huduma zetu bila kutegemea msaada wa mtu mwingine. Haya ni mapinduzi muhimu katika sekta ya utoaji huduma za mawasiliano, ikizingatiwa kuwa serikali inahimiza watoa huduma kuzingatia ushirikishwaji katika utoaji wa huduma kwa wateja,” aliongeza Linda.

Uzinduzi wa simu hii ni ingizo la kipekee sokoni ukilinganisha na matoleo mengine, ikiwa na uwezo wa kuchochea ushirikishwaji katika matumizi ya huduma za mawasiliano ya kidigitali. Pia ina ubora wa hali ya juu ikiwa na kioo kikubwa na cha kugusa (2.8”), uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu kwenye 8GB na betri inayodumu muda mrefu ya 3000mAh.

Toleo hili jipya la 'Smart Kitochi+' ni sehemu ya juhudi za Vodacom kuwapeleka wateja wake kwenye matumizi ya kidigitali, ikiwa ni pamoja na mtandao wa 4G, ambao bado una watumiaji wachache ikilinganishwa na idadi ya watumiaji wa simu za mkononi nchini Tanzania.

"Tunajivunia kuwa mtandao unaoongoza nchini, tukitoa huduma za kidigitali za ubunifu kwa zaidi ya wateja milioni 21. Kuwa na idadi kubwa ya wateja pekee haitoshi; tunataka wateja wetu wanufaike na mapinduzi ya kidigitali yanayoendelea na ubunifu mkubwa tunaoingiza kwenye bidhaa zetu. Kwa kuanzisha bidhaa za kisasa kama 'Smart Kitochi+' tunaamini tutachochea wateja wengi zaidi kuhama kutoka kwenye mfumo wa 2G na kuanza kufurahia huduma mbalimbali za kidigitali zinazotolewa na mtandao wetu wa kasi wa 4G na 5G uliosambaa nchini na hatimaye kuongeza matumizi ya simujanja ambayo kwa sasa ni asilimia 32," alifafanua Bi. Linda.

Akizungumzia simu hiyo mpya, Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (TLB) Bw. Luis Benedicto aliisifia simu hiyo akikiri kuwa itakuwa mkombozi kwa watu wenye ulemavu wa kusikia na kuona.

"Tulikuwa tumetengwa na kubanwa katika matumizi ya simu za mkononi, kwani nyingi hazikuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu wa kusikia na kuona. Kuzinduliwa kwa simu hii kutatusaidia sio tu kufurahia huduma za mawasiliano kutoka Vodacom bali pia kuimarisha mwingiliano wetu na wengine na kutumia simu hizi kwa manufaa ya kijamii na kiuchumi," alielezea Bw. Benedicto.

Uzinduzi huu unakuja baada ya hivi karibuni kampuni hiyo kuanzisha dawati maalum kwa ajili ya kuhudumia wateja wasioona baada ya kuanzisha dawati kama hilo kwa ajili ya wateja wenye ulemavu wa kusikia mwaka jana.

Juhudi za kampuni hiyo katika kuzingatia na kuboresha maisha ya wateja wake ili kupunguza au kufuta kabisa utofauti uliopo wa kidigitali kwa watu wenye ulemavu zimeifanya iwe miongoni mwa watia saini wa miongozo ya GSMA kwa kuchochea ushirikishwaji wa kidigitali kwa watu wenye ulemavu. Miongozo hiyo huweka misingi ya hatua za kuchukua pamoja na kinachotakiwa kufanywa na mtoa huduma za simu za mkononi ili kupunguza pengo katika upatikanaji wa huduma pamoja na matumizi ya huduma hizo.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha.Poline Msuya akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Mamlaka za maji kuhusu mfumo wa kieletroni wa MajIs ulioboreshwa kwa ajili ya kupokea taarifa za utendaji wa sekta ya maji, kilichofanyika  EWURA Makao Makuu, Dodoma.

Na.Mwandishi Wetu_DODOMA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imefanya kikaokazi cha kutambulisha mfumo wa Majis ulioboreshwa kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira. Kikao hicho kimefanyia EWURA makao makuu Dodoma.

Akifungua kikao hicho kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mha. Poline Msuya amesema Maboresho yaliyofanyika katika mfumo yalichagizwa pia na maoni ya wadau ambao ni watumiaji wa mfumo. Pia mfumo umeboreshwa kuakisi mabadiliko na maendeleo kwenye sekta ya maji.

Aidha EWURA haitosita kuchukua hatua za kiutawala kwa mamlaka za maji ambazo hazitatekeleza uwasilishaji wa taarifa zao kwa wakati, aliongezea Mha. Poline Msuya.

Akitoa maoni yake muwakilishi wa Wizara ya Maji Mha. Epimack Oscar alisisitiza Mamlaka za Maji zitumie mfumo huo kwa ajili ya kuwa na takwimu sahihi.

Kifungu cha 29(1)(h) cha Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira Sura Namba 272 kinaitaka EWURA kukusanya taarifa za utendaji kutoka mamlaka.

Meneja wa EWURA kanda ya Magharibi Mha. Walter Christopher akiwasilisha mada kuhusu mfumo wa Majis ulioboreshwa kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwenye kikaokazi cha kutambulisha mfumo huo. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano EWURA makao makuu Dodoma.

Mhandisi Mwandamizi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA, Teophil Sanjawa akiwaelekeza washiriki wa kikaokazi namna ya kujaza taarifa kwenye mfumo wa MajIs ulioboreshwa, leo 17.4.24

Washiriki wa kikao kazi wakifuatilia kwa umakini namna ya kujaza taarifa za utendaji wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira kwenye mfumo wa MajIs ulioboreshwa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mha. Poline Msuya(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za maji za makao makuu ya mikoa na miradi ya kitaifa,wawakilishi kutoka Wizara ya maji na wafanyakazi wa EWURA idara ya Maji muda mfupi baada ya ufunguzi wa kikaokazi cha utambulisho wa mfumo wa Majis ulioboreshwa kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira,Dodoma.






Serikali kupitia Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuzuia na kudhibiti athari za michezo ya kubahatisha ili kuhakikisha jamii inakuwa salama.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mlola, Mhe. Abdallah Shangazi aliyetaka kuwajua iwapo Serikali inatambua athari hasi kwa Jamii ya Watanzania zinazotokana na ongezeko kubwa la michezo ya kubahatisha.

Mhe. Chande alisema kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 7(2)(i) cha Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, Sura 41, mamlaka ya udhibiti ina jukumu la kuhakikisha kuwa jamii inalindwa ipasavyo dhidi ya athari hasi za michezo ya kubahatisha.

“Katika kutekeleza jukumu hilo, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali ya kuzuia na kudhibiti athari hasi zitokanazo na uwepo wa michezo ya kubahatisha, mikakati hiyo ni pamoja na kuimarisha udhibiti na uratibu wa sekta kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na matumizi ya mifumo ya TEHAMA,’’alisema Mhe. Chande.

Alifafanua kuwa Bodi inaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu athari za michezo ya kubahatisha, kufanya mapitio ya mara kwa mara ya mifumo ya usimamizi wa michezo ya kubahatisha pamoja na kufanya kazi ya udhibiti kwa kushirikisha wadau na mamlaka nyingine kama vile Jeshi la Polisi, TCRA na TRA.

Mhe. Chande alisema pamoja na faida za kiuchumi na kijamii zinazotokana na michezo ya kubahatisha, Serikali inatambua athari zake katika jamii endapo haitaendeshwa kwa weledi ikiwemo uraibu na kugeuza michezo ya kubahatisha kuwa mbadala wa ajira, ushiriki wa watoto katika michezo ya kubahatisha na uwepo wa michezo haramu isiyo na usajili wa mamlaka ya udhibiti.


In Ankara's halls, under academic gaze,
Ankara University honors a Tanzanian blaze.
Samia Suluhu Hassan, a leader so rare,
In economics, an honorary doctorate she did bear.

From India's Nehru to Zanzibar's shore,
Her accolades in leadership roar.
Dar es Salaam and now Ankara's acclaim,
Her achievements in Tanzania's name.

Professor Ünüvar bestows the degree,
A symbol of her transformative spree.
Diplomats and scholars, a distinguished crowd,
In honor of her, they are bowed.

Her leadership's impact, a global view,
Economic reforms and policies anew.
Tanzania's rise under her steady hand,
A symbol of progress, across the land.

A state visit to Türkiye, a momentous affair,
Samia Suluhu Hassan, expectations to declare.
With President Erdogan, dialogue will engage,
Strengthening ties, a new historic stage.

She strengthens ties, both near and far,
Elevating Tanzania as a rising star.
Türkiye, a partner in trade and more,
Their bond deepens, united at its core.

From agriculture to technology's leap,
Education's advance, in promises deep.
Trade volumes surge, opportunities vast,
A partnership that's built to last.

Coffee, coconuts, and gems so rare,
Tanzania's treasures, beyond compare.
Turkish investments, a boon for each,
Economic growth, well within reach.

As Samia Suluhu Hassan strides ahead,
Her vision and courage, widely spread.
Tanzania's future, a path so clear,
Nasimama na Samia, her leadership we cheer.

Thank you.

Written by Christopher Makwaia
Tel: +255 789 242 396


- The writer, is a University of West London graduate (formerly Thames Valley University) and an expert in Management, Leadership, International Business, Foreign Affairs, Global Marketing, Diplomacy, International Relations, Conflict Resolution, Negotiations, Security, Arms Control, Political Scientist, and a self-taught Computer Programmer and Web Developer.



Top News