Na WILLIUM PAUL, MOSHI.

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amekabidhi magari matatu kwa ajili ya wakuu wa wilaya za Rombo, Mwanga na Same ili kuongeza ufanisi wa utendaji na kuleta maendeleo ya mkoa yenye thamani ya zaidi ya milioni 200.

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo nje ya viwanja wa ofisi za mkuu wa mkoa, Babu amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameanza kutekeleza maombi mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro ya kuwapatia Wakuu wa wilaya vitendea kazi.

Babu alisema kuwa, Wabunge wamekuwa wakilalamika Bungeni kuhusiana na wakuu wa wilaya kukosa magari ambapo mkoa ulipanga kuhakikisha bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 mpaka ifikapo mwezi Juni mwaka huu wawe wameshanunua magari matatu ya wakuu wa wilaya.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa, magari hayo yatatumika kwa ajili ya shughuli za kiserikali na kuwataka kwenda kuyatunza magari hayo kwani yamenunuliwa kwa gharama.

Aidha Babu amewataka Wakuu wa wilaya kuwaachia Madereva wafanye kazi zao kwani ndio waliyosomea kuendesha gari na kuachana na kumwambia kuvunja sheria ili kuwahi kule unapoenda ili kuepuka ajali zisizo na ulazima.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Rombo, Raymond Mangwala alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wasaidizi wake na kuwapa vitendea kazi na kuahidi kutumia gari hilo kufanya kazi iliyokusudiwa ikiwemo kuhakikisha miradi inaenda kukamilika.

Naye mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni alisema kupatikana kwa vitendea kazi kutachangia kuwafikia wananchi na kutatua kero zao .




Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi akipunga mkono kuwaaga mamia ya wananchi, walioongozwa na viongozi wa chama na Serikali Mkoa wa Ruvuma, waliofika Uwanja wa Ndege wa Songea, kumuaga kiongozi huyo baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani humo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 13 iliyomfikisha katika mikoa sita, akianzia Katavi, kisha Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Balozi Nchimbi, ambaye katika ziara hiyo aliambatana na Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Oganaizesheni na Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, akiwa ziarani kwenye maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo, amekagua na kuhamasisha uhai na ujenzi wa chama.

Aidha, katika ziara hiyo pia, Balozi Nchimbi ametoa maelekezo mbalimbali kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa wizara yaliyolenga kuboresha na kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020 - 2025, hasa maeneo ya miradi ya maendeleo ya wananchi na kuwatumikia watu.

Kupitia ziara hiyo, CCM katika ngazi ya taifa, hasa kupitia kwa Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, imeendeleza utaratibu wake wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea maelekezo kwa ajili ya kuzitatua, huku Gavu akiendelea kuhamasisha wanachama na viongozi kuendelea kukiimarisha CCM na kujiandaa kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (2024) na Uchaguzi Mkuu (2025).








Na Khadija Kalili,Michuzi TV
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani imefanya uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji wa mapato yatokanayo na machinjio ya Mtakuja iliyopo Halmashauri ya Mji Kibaha .

"Uchambuzi huu umefanywa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba kuna miaya ya rushwa katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na ushuru katika machinjio hayo,hali inayodababisha upotevu wa mapato na Halmashauri hiyo hivyo kushindwa kufikia lengo la

ukusanyaji waliyojiwekea kutoka kwenye chanzo hiki" amesema Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Pwani Ally Sadiki alipozungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari ambao umefanyika leo Aprili 24.

"Uchambuzi huu umebaini kwamba, pamoja na kuwepo kwa mashine za kieletroniki za POS katika machinjio kumekua na taarifa zinazokinzana ,kuwepo kwa tatizo la miundombinu na ucheleshaji wa kuweka fedha benki zinazo kisanywa.

TAKUKURU imebaini pia kuna uzembe katika kusimamia idadi ya ng'ombe wanao chinjwa kwa siku husika na hakuna ukaguzi kuhusu idadi ya ng'ombe waliopo eneo la kusibiri kuchinjwa.

"TAKUKURU imebaini kuwa idadi ndogo ya watumishi walioajiriwa eneo husika ndiyo chanzo cha kushindwa kutekeleza majukumu ipasavyo"amesema Kaimu Kamanda TAKUKURU Sadiki.

Aidha amesema kuwa baada ya TAKUKURU kuingilia kati makusanyo yameongezeka tofauti na ilivyokua katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kati ya Oktoba na Desemba 2023 ambapo Oktoba hadi Desemba makusanyo yalikua Mil.7,418,000 na sasa makusanyo yameongezeka na kufikia kiasi cha Mil.9,615,000.

"Katika hatua ingine Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibaha Mji ameongeza watumishi eneo hilo la machinjio ya Mtakuja kuimarisha ufuatiliaji na ukaguzi hivi sasa unafanyika kila mara ili kuondoa fedha za makusanyo ya kila siku na kuhakikisha fedha zinapelekwa benki kila siku.

Kaimu Kamanda wa TAKUKURU amesema kuwa kwa kipindi tajwa wamefanya chambuzi nyingine za mifumo tano katika sekta ya Ardhi,Elimu, AMCOS na ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya serikali ili kupata tija ya mifumo imara usiyokwamisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Ameongeza kwa kusema kuwq TAKUKURU Mkoa wa Pwani wamefuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo 23 yenye thamani ya Bilioni6.3 katika sekta za Elimu, Maji,Afya na Ujenzi (Barabara),ambapo kati ya miradi hiyo mradi mmoja umeonekana kuwa na upungufu ufuatiliaji u aendelea ii kurekebisha kasoro hizo.

Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Pwani Sadiki amesema kuwa katika kipindi hicho cha miezi mitayu wameweza kutoa elimu kwa umma kwa kufanya semina 19,mikutano yahadhara21,

vipindi vya redio 9 kuimarisha klabu za wapinga rushwa 54 uandishi makala 4 na TAKUKURU Rafiki6.

Aidha TAKUKURU Mkoa wa Pwani imefungua kesi mpya mbili Mahakamani ambapo kesi sita zimeamuliwa huku kesinne watuhumiwa wametiwa hatiani na jumla kesi sita zinaendelea Mahakamani.

Ameongeza kwa kusema kuwa mikakati waliyojiwekea ni kwamba wamejipanga kuendelea kufanya udhibiti wa mapato ya serikali na usimamizi wa rasilimali za umma ikiwa ji pamoja na udhibiti wa fedh zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze, April 24
NAIBU Waziri wa Utumishi na Utawala Bora ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete amewataka wanafunzi na vijana kuacha matumizi mabaya ya mitandao, mambo yaliyo nje ya tamaduni za kitanzania na badala Yake watumie mitandao hiyo kujifunza na kujipa uelewa zaidi katika masuala ya masomo na elimu.

Aidha amewaasa kusoma kwa bidii kwani elimu ndio nguzo ya maisha yao.

Ridhiwani alitoa rai hiyo alipokuwa akihutubia wahutimu wa kidato cha sita shule ya sekondari ya Lugoba , Halmashauri ya Chalinze, mkoani Pwani.

Aliwaasa wahitimu hao kuhakikisha wanafaulu ili waache deni la kufuatwa na wadogo zao wanaowafuata kwa upande mmoja, wawape heshima walimu na wazazi kwa kufaulu vizuri.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ,Abdallah Sakasa aliishukuru serikali kwa kuendelea kupeleka pesa za elimu bure , vifaa na kuongezeka kwa madarasa na walimu shuleni hapo .

Alimuomba mbunge kuendelea kuikumbuka shule hiyo kwa kuisaidia vifaa na kuongeza mabweni ya wanafunzi.





RAIS Samia Suluhu Hassan Atunuku Nishani Viongozi Mbalimbali katika shamrashamra za miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Tatu Mhe. Fredrick kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Gharib Bilal kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Samwel Malecela kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Janeth Magufuli Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024. Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hutunukiwa kwa Wakuu wa Nchi Wastaafu (hai au marehemu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioingia madarakani kwa njia ya kikatiba na wameendelea kuonesha Maadili mema yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Salma Kikwete Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024. Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hutunukiwa kwa Wakuu wa Nchi Wastaafu (hai au marehemu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioingia madarakani kwa njia ya kikatiba na wameendelea kuonesha Maadili mema yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.

BENKI ya Absa Tanzania imeendeleza udhamini wake kwa mwaka wa nne mfululizo katika mbio za Absa Dar City Marathon , ikilenga  kuifanya Tanzania kuwa Taifa lenye watu wenye afya njema.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za Absa Dar City Marathon 2024, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bwana Aron Luhanga alisema afya njema ni mtaji namba moja katika maendeleo ya Taifa la Tanzania na wanaokimbia wanajenga Afya.

Alisema lengo lingine kuu la Absa Dar City Marathon ni mapato yatayakayopatikana katika mbio hizo kuelekezwa katika shughuli za kijamii Kwa kununua vifaa  vitakavyosaidia wodi ya wanawake    katika hospitali ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

“Pamoja na hayo kama kauli mbiu ya mbio hizi isemayo ‘Kata Mtaa, Ujue Jiji’ sisi kama Absa Bank, tukiwa na Matawi ya kibenki hapa jijini,  tunajisikia fahari kusapoti mbio hizi zenye lengo pia la kutangaza vivutio vya utalii vilivyomo katika jiji letu.

“Kauli yetu ya Absa inasema ‘Story Yako ina Thamani’ hivyo tunaamini kuwa ukienda kukimbia unaandika Story Yako, ukienda kusaidia jamii, unaandika Story Yako, nasi kama Absa, Story Yako Ina thamani sana kwetu”, alisema Bwana Luhanga.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa The Runners Club, Bwana Godfrey Mwangungulu alisema mbio za mwaka huu zinazofanyika chini ya udhamini mkubwa wa Benki ya Absa Tanzania zitashirikisha mbio za Kilomita, 21, 10 na Kilomita tano.

“Absa Dar City Marathon ya  mwaka huu inayotarajiwa kufanyika Mei 5 mwaka huu ikianzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, ni zaidi ya mbio, ni zaidi ya sherehe, ni kilele cha sherehe za mbio zote zinazoendelea kufanyika hapa nchini.

“Tumefanya mbio hizi kwa miaka mitatu mfululizo, mwaka huu tunataka kuzifanya Kwa mafanikio zaidi, tunatarajia zaidi ya wakimbiaji 3000 kushiriki, tunawashukuru sana wadhamini wetu wakuu, Benki ya Absa pamoja na wadhamini wengine”, alisema Bwana Mwangungulu. 

Mbali na Benki ya Absa kama mdhamini mkuu, wadhamini wengine ni Kampuni  ya Alliance Life Assurance, Hill Water, Kilimanjaro Milk na Kampuni  ya Garda Security. 
Mwisho.



Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga ( wa pili kushoto ) akionyesha fulana zitakazovaliwa siku ya mbio  za Absa Dar City Marathon wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio hizo jijini Dar es Salaam jana, zinazotarajiwa kufanyika Mei 5 mwaka huu, jijini Dar es Salaam
  Kutoka kushoto ni Ofisa Masoko wa Hill Water, Sylvia Shoo, Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Klabu ya The Runners, waandaaji wa Absa Dar City Marathon ,Godfrey Mwangungulu, Meneja wa Bima Kibenki wa Alliance Life Assurance, Juma Patrice na Meneja Bima Binafsi, Jumanne Muruga.
Mkuu wa  Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga ( wa tatu  kushoto ), Mkuu wa Kitengo cha  Mawasilino wa The Runners Club, Bwana Godfrey Mwangungulu (kushoto kwa Aron), pamoja na wawakilishi wa wadhamini wengine, wakionyesha fulana na vitu vingine vitakavyotumika wakati wa mbio za Absa Dar City Marathon, jijini Dar es Salaam Mei 5 mwaka huu, zikianzia katika Viwanja  vya Mnazi Mmoja. Hafla hiyo ilifanyika jijini humo jana.
Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji April 23


Patrick Golwike (Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum [WMJJWM]) ameridhishwa na misaada inayoelekezwa na huduma zinazoelekezwa kwa akinamama waliojifungua na watoto waliokumbwa na maafa ya mafuriko Rufiji na Kibiti mkoani Pwani.

Aidha amepongeza mkoa,maofisa ustawi wa jamii kata,wilaya na mkoa kwa namna wanavyosimamia  makundi ya Wanawake waliojifungua, wenye watoto na vijana wa kike ambao wapo kwenye ukuaji.

"Nichukue fursa hii pia kuwapongeza watalaam wa Maendeleo ya Jamii wakiongozwa na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Pwani ambae ni mratibu wa Maafa Mkoa wa Pwani Roseline Kimaro ,ambao wamekuwa wakitekeleza jukumu la uratibu  wa kuhakikisha waathirika wa mafuriko katika kambi Tano zilizopo kibiti na Ruiji wanapata huduma za msingi hasa wanawake ,watoto,wazee,na wenye  mahitaji maalumu."alifafanua.

Hata hivyo kuhakikisha huduma za msingi zinatolewa kwa makundi hayo, mabinti balee kujilinda ,ulinzi wa watoto na kutoa elimu ya lishe na saikolojia  .

Nae Mratibu wa maafa Roseline Kimaro alifarijika kuona wadau ambao wanapeleka misaada muhimu hasa kwa akinamama waliojifungua , watoto na mabinti balee.

"Ninawashukuru na umoja wa wanawake Tanzania, na mkoa kwa kujitoa kwao kupeleka mahitaji muhimu ya wanawake ikiwemo pedi,pempas,mabeseni,,nguo ,vyombo na vyakula kwani ni kama walijua kwamba ni moja ya changamoto ambazo ziliainishwa kuwakabili wanawake na watoto "alibainisha Roseline.

Roseline aliomba wadau wa jamii kuendelea kuwakimbilia kundi la wanawake, watoto,vijana na akinamama wajawazito na waliojifungua ili kuwapunguzia changamoto zinazowakabili.


 

JE, umewahi kucheza mchezo wa droo wenye droo 10? Ikiwa hujawahi, sasa unapata nafasi kamili ya kufanya hivyo. Kupitia Meridianbet Kasino ya Mtandaoni kuna furaha inakusubiri kupitia droo moja tu ya ushindi.

Taarifa za Msingi
420 Blaze It ni mchezo wa kasino ya mtandaoni kutoka kwa mtoa huduma 1x2 Gaming na una droo 10. Kila droo ina safu tatu, na kila safu ina alama moja. Vivyo hivyo, kila droo moja ina mstari mmoja wa malipo. Ili kupata mafanikio yoyote, lazima uunganishe alama tatu zinazolinganisha katika mfululizo wa ushindi.

Kwenye kasino ya mtandaoni hii ushindi huzingatiwa tu kutoka kushoto kwenda kulia, ukitoka kwenye safu ya kwanza upande wa kushoto. Kwenye mstari mmoja wa malipo, unaweza kupata ushindi mmoja tu. Hakuna uwezekano wa kupata mafanikio zaidi kwenye mstari mmoja wa malipo.

Unapoucheza mchezo huu wa kasino pale Meridianbet utaona sehemu ya kuweka dau lako au Stake, utaona vitufe vya plus na minus ambavyo unaweza kutumia kurekebisha thamani ya dau kwa kila droo.

Alama za Ushindi Droo ya 420 Blaze It
Alama za mchezo huu wa kasino ya mtandaoni ziko nyingi kuna alama ya cheri huleta mafanikio madogo. Ikiwa utapata matunda ya cheri matatu kwenye mstari wa malipo, utapata mara mbili ya dau lako kwenye droo.

Pia utaona tunda jingine, ambalo ni limao. Ukiwa na malimao matatu katika mchanganyiko wa mafanikio, utapata mara tano zaidi ya dau.

Alama ya Bar zambarau huleta mafanikio madogo zaidi. Ikiwa unashikamana na alama tatu hizi katika mchanganyiko wa ushindi, utapata mara kumi zaidi ya dau lako.

Inafuata alama ya Bar ya bluu ambayo itakuletea mafanikio makubwa kidogo. Ukishikamana na alama tatu hizi katika mchanganyiko wa mafanikio, utapata mara kumi na tano zaidi ya dau.

Thamani kubwa zaidi kati ya alama za Bar ni ile ya rangi ya machungwa. Alama tatu hizi kwenye droo moja itakuletea mara ishirini zaidi ya dau.

Bila shaka, nguvu kubwa ya kulipa inaletwa na alama za Lucky 7 na utawaona katika mchezo wa msingi katika rangi tatu. Ili kupata mafanikio madogo zaidi miongoni mwao, unapaswa kupata Lucky 7 za kijani. Ikiwa utashikamana na alama tatu hizi katika mchanganyiko wa mafanikio, utapata mara ishirini na tano zaidi ya dau.

Inafuata alama ya Lucky 7 ya rangi ya bluu, na alama tatu hizi kwenye mstari wa kulipa huleta mara hamsini zaidi ya dau la droo.

Mkubwa zaidi katika mchezo huu wa kasino ya mtandaoni ni alama ya Lucky 7 yenye rangi nyekundu. Alama tatu za hivi kwenye droo moja itakuletea x100 ya dau lako.

Michezo ya ziada yenye Bonasi za Kasino.
Mchanganyiko wa mafanikio ya alama tatu za Lucky 7 huleta zawadi nyingine. Hufungua mizunguko ya bure kulingana na sheria zifuatazo:

Alama Tatu za kijani za bahati zinaweza kuleta mizunguko ya bure 10
Alama Tatu za bluu za bahati zinaweza kuleta mizunguko ya bure 15
Alama Tatu nyekundu za bahati zinaweza kuleta mizunguko ya bure 20

Wakati unaendelea kutumia mizunguko ya bure kwenye mchezo huu wa kasino ya mtandaoni, alama za Lucky 7 tu huonekana.

NB: Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni upate ushindi kirahisi, Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg.Ally Salum Hapi (MNEC) ametembelea na kuona treni mpya ya kisasa ya mwendokasi iliyowasili, Jijini Dodoma jana usiku ikitokea Jijini Dar Es Salaam iliyokuja na viongozi mbalimbali wa dini na serikali, wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Ndg.Masanja Kadogosa, pamoja na waandishi kwa ajili ya kuahiriki Dua Maalumu ya Kuliombea Taifa iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, leo, ambapo Mgeni Rasmi Alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Phillip Isdor Mpango.

Akizungumza baada ya kutembelea na kuona ubora, uzuri na utendaji kazi wa treni hiyo, Katibu Mkuu Wazazi, Ndg.Hapi, aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kutekeleza Ilani ya CCM ya Mwaka 2020 - 2024 kwa vitendo na kusema anastahili kuongezewa hali, morali na moyo wa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

"Kwa niaba ya viongozi, wanachama na wapenzi wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM nichukue fursa hii adhimu kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kuhakikisha mradi wa ujenzi wa reli ya mwendokasi kutoka Dar Es Salaam hadi Dodoma imekamilika kwa asilimia kubwa pamoja na majaribio ya treni ya mwendokasi na mabehewa yake kuletwa nchini na kuanza kufanyia majaribio yanayotoa matokeo chanya;

"Ama kwa hakika hii ni furaha na faraja kubwa sana kwetu sisi wamiliki wa duka kuona muuza duka wetu anaiendesha vizuri biashara yetu na matokeo chanya yanaonekana, lakini pia nitoe pongezi kwa watumishi wote wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa usimamizi bora wa fedha za mradi huu ambao ni Tshs.Bilioni 23.5 ni fedha nyingi mnoo ila ndugu zetu hawa wanastahili pongezi kwa kusimamia vyema fedha hizo" alisema Hapi.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa TRC, Ndg.Masanja Kadogosa, alitoa shukurani kwa viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi kwa kutembelea mradi huo kwa kusema kwao watumishi wa Shirika la Reli Tanzania hujisikia ufahari wa hali ya juu inapotokea nafasi ya viongozi wa CCM na Jumuiya zake wanapotembelea mradi wa ujenzi wa reli ya mwendokasi na kusifia kwa kile kilichofanyika inawatia moyo na morali wa kuendelea kutumikia shirika na serikali kwa maslahi mapana ya nchi.

Katika msafara wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi, Ndg.Hapi, aliongozana na Naibu Katibu Mkuu Wazazi Bara, Ndg.Joshua Mirumbe Chacha, viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dodoma, Wilaya pamoja na kata husika kwa kujitoa kuungana nao kutembelea na kutazama mradi huo.






MFANYABIASHARA Marik Ngutti wa Machimbo ya Matabi wilayani Chato Mkoa wa Geita ameeleza namna ambavyo ufuatiliaji wake wa elimu ya mlipa kodi ilivyomnasua kutoka kwenye mikono ya matapeli waliojifanya maofisa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Ngutti ametoa ushuhuda huo leo Aprili 23, 2024 alipotembelea banda la TRA katika maonesho ya Wakandarasi Geita Mjini kwenye viwanja vya EPZ ambapo amesema aliwapa elimu na wafanya biashara wenzake ambao pia walishindwa kutapeliwa baada ya kupata taarifa muhimu kuhusu maofisa wa TRA.

"Kuna watu walikuja kwenye maeneo yetu ya biashara pale Machimbo ya Matabi walijitambulisha kuwa ni maofisa wa TRA niliwajengea mashaka kwa kuwa niliona hawana utambulisho wa TRA na hawakuwa wanatoa lisiti kwa wenzetu waliotangulia kupita nikawaambia wafanyabiashara wenzangu kuwa hao sio maofisa wa TRA nikawapa namba ya TRA"

Amesema kwa kuwa tayari alishawapa elimu ya mlipa kodi walivyofika wale maofisa bandia wa TRA wale wafanyabiashara waliwahoji mambo muhimu yanayohusu TRA waliposhindwa kujibu wakaondoka zao na .

Ngutti amesema kuwa ufahamu juu ya masuala muhimu ya kodi na maofisa wa TRA ameyapata kutokana na jitihada zake za kufuatilia vipindi mbalimbali vya runinga na radio na kuwasisitiza wananchi wote kujielimisha katika masula muhimu ya kodi.




Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete amewataka wanafunzi na vijana kuacha matumizi mabaya ya mitandao, mambo yaliyo nje ya tamaduni za kitanzania na badala Yake watumie mitandao hiyo kujifunza na kujipa uelewa zaidi katika masuala ya masomo na elimu.

Aidha amewaasa kusoma kwa bidii kwani elimu ndio nguzo ya maisha yao.

Ridhiwani alitoa rai hiyo alipokuwa akihutubia wahutimu wa kidato cha sita shule ya sekondari ya Lugoba , Halmashauri ya Chalinze, mkoani Pwani.

Aliwaasa wahitimu hao kuhakikisha wanafaulu ili waache deni la kufuatwa na wadogo zao wanaowafuata kwa upande mmoja, wawape heshima walimu na wazazi kwa kufaulu vizuri.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ,Abdallah Sakasa aliishukuru serikali kwa kuendelea kupeleka pesa za elimu bure , vifaa na kuongezeka kwa madarasa na walimu shuleni hapo .

Alimuomba mbunge kuendelea kuikumbuka shule hiyo kwa kuisaidia vifaa na kuongeza mabweni ya wanafunzi.









MAHAKAMA ya Rufani leo imeshindwa kuendelea na usikilizwaji wa shauri la rufaa lililokatwa na Benki ya Equity Bank Tanzania Limited na Equity Bank Kenya Limited dhidi ya kampuni ya mafuta ya State Oil, kutokana na kesi ya msingi kusikilizwa bila hati ya madai kufanyiwa marekebisho.

Benki zilikata rufaa hiyo kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara iliyoipa ushindi kampuni ya State Oil inayodaiwa kukataa kulipa mkopo iliyopewa na benki hizo wa USD 18,640,000.

Rufaa hiyo ilikuwa imepangwa kusikilizwa leo tarehe 23, 2024 mbele ya jopo la majaji Rehema Mkuye, Abraham Mwampash na Zainabu Muruke.

Lakini majaji hao kabla ya kuanza kusikiliza rufaa hiyo wakawahoji mawakili kama ni sawa kesi ya msingi kusikilizwa bila hati ya madai kufanyiwa marekebisho baada ya Equity benki ya Kenya kujiunga katika kesi hiyo.

Mawakili wanaoziwakilisha benki hizo, Mpaya Kamala na Timon Vitalis wameieleza mahakama kuwa japo kweli kanuni zinasema kuwa baada ya kuongezwa mdaiwa mwingine hati ya madai ilipaswa kufanyiwa marekebisho, lakini wao hawaoni kama kutokufanya marekebisho ni tatizo kwani kutokufanya hivyo hakukuathiri upande wowote.

Mawakili hao kwa nyakati tofauti wamesema kuwa hata hivyo amri ya 1, Kanuni ya 10 (4) za Mwenendo wa Mashauri ya Madai (CPC) inampa jaji uhuru wa kuamua vinginevyo badala ya kuamuru hati ya madai kufanyiwa marekebisho na kwamba ndivyo jaji aliyesikiliza kesi hiyo ya msingi alivyoamuru.

“Hapa baada ya mdaiwa wa pili, Equity Kenya kuunganishwa jaji aliamuru kuwa wadaiwa wawasilishe maelezo yao ya utetezi wa maandishi. Na sisi tunaona hakukuwa na tatizo kwani hakukuathiri upande wowote”, amesema wakili Kamara.

Wakili wa kampuni ya State Oili Frank Mwalongo naye amesema kuwa anakubaliana na hoja za mawakili wenzake kuwa haikuwa muhimu kufanya marekebisho ya hati ya madai kwa kuwa kutokufanya hivyo hakujaathiri upande wowote.

“Kwa hiyo naiomba mahakama ione kwamba hoja hii haikuathiri upande wowote na Jaji alitenda kwa mujibu wa sheria na tuendelee na usikilizwaji wa rufaa.”

Baada ya mawakili hao kumaliza kutoa hoja zao kuhusu suala hilo, Jaji Mkuye ameahirisha kesi hiyo akisema kuwa mahakama itawajulisha pande zote siku ya kutoa uamuzi utakapokuwa tayari.

Kampuni ya State Oil inadaiwa kuwa ilidhaminiwa na Benki ya Equity Kenya kuchukua mkopo wa USD 18,640,000 kutoka kwa kampuni Lamar Commodity Trading DMMC ya Dubai, huku na yenyewe ikiikabidhi Benki ya Equity ya Kenya hati za mali zake mbalimbali kama dhamana ya udhamini wa mkopo huo.

Indaiwa kuwa hata hivyo haikuweza kulipa mkopo huo, hivyo Benki ya Equity Tanzania kama mdhamini wake ndio ikalipa mkopo huo kwa kampuni ya Lamar Commodity.

Benki ya Equity Kenya baada ya kuanza kuidai kampuni hiyo mkopo huo kupitia kwa Benki ya Equity Tanzania, ambayo ndio iliyopewa jukumu la kusimamia dhamana zilizowekwa na State Oil, kampuni hiyo ilikimbilia mahakamani ambako iliifungulia kesi Benki ya Equity Tanzania ikipinga kudaiwa mkopo huo.

Kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa Benki ya Equity Tanzania iliwasilisha maombi mahakamani hapo ili Benki ya Equity Kenya nayo ijumuishwe kwenye kesi hiyo na Jaji aliyeisikiliza akaikubalia akaamuru Benki ya Equity Kenya nayo ikaunganishwa kwenye kesi hiyo.

Benki hiyo ya Kenya ilipounganishwa mahakama haikutoa amri ya kufanya marekebishoa ya hati ya madai badala yake iliamuru tu benki hizo ambazo zilikuwa wadaiwa katika kesi hiyo ziwasilishe utetezi wake wa maandishi, kisha ikaendelea na usikilizwaji mpaka ikatoa hukumu.

Katika kesi hiyo kampuni hiyo iliiomba mahakama itamke kuwa ilishalipa mkopo wake wote iliokuwa inadaiwa na kwamba haina benki hizo hazina madai yoyote dhidi yake na pia ikaomba mahakama iamuru irejeshewe hati za mali zake ilizokuwa imezitoa kama dhamana ya kupata udhamini wa mkopo huo.

Benki katika utetezi wake ziliita mashahidi sita akiwemo na mwakilishi wa kampuni ya Lamar aliyetoa ushahidi jinsi alivyoikopesha State Oil fedha hizo kwa kudhaminiwa na Benki ya Equity na kwamba ilishindwa kurejesha mkopo huo na ikabidi benki hiyo iliyomdhamini ndio ikalipa mkopo huo.

Mahakama hiyo katika hukumu yake iliyotolewa Oktoba Mosi, 2021, ilikubaliana na madai na ushahidi wa State Oil kupitia kwa shahidi wake mmoja, kuwa ilikuwa imeshalipa deni lake lote na hivyo benki hizo hazikuwa na madai dhidi yake na ikaamuru State Oil irejeshewe hati zake za mali ilizoweka dhamana.

Top News