Dk Nchimbi, akiambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Oganaizesheni, Ndugu Issa Haji Usi Gavu na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makala, yuko mkoani Njombe kwa ziara ya siku mbili, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mikoa 6 ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.
Dk Nchimbi, akiambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Oganaizesheni, Ndugu Issa Haji Usi Gavu na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makala, yuko mkoani Njombe kwa ziara ya siku mbili, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mikoa 6 ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.
Amesisitiza kwamba pamoja na ugumu wa kukarabati bwawa hilo wakati likiwa na maji maamuzi magumu yafanyike wataalamu wa Wizara ya Maji watumie utaalamu wao kulifanikisha hiko kwani hakuna namna nyingine.
Akizungumza na mamia wa wananchi wa Kata za Lepruko, Sepeko, na Makuyuni Waziri wa maji maelekezo kwa Wataalamu wa Wizara kama ifuatavyo kwanza kutumia taaluma zao kuhakikisha Bwawa hilo linakarabatiwa kwa dharula haraka kuanzia kesho tarehe 19.04.2024 kudhibiti maji kuebdelea kupotea pili kufanya usanifu wa kina nyakati za kiangazi kusudi bwawa hilo liweze kukarabatiwa kwa uhakika zaidi.
Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh Fred Lowassa amesema Bwawa hilo ndio tegemeo la wana Monduli kwenye matumizi ya maji kwa Binadamu, mifugo na wanyamapori hivyo anaiomba Serikali ione namna ya kukarabati bwawa hilo kwa dharura.
Aidha, Wakizungumza katika nyakati tofauti madiwani wa kata zinazoguswa na bwawa hilo wameishukuru serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuwafikia kwa haraka na kutafuta suluhu ya utatuzi ya changamoto hii.
WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Mendeleo ya Makazi Jerry Silaa anatarajiwa kuongoza Kliniki ya Ardhi kwa mkoa wa Tanga itakayofanyika kuanzia Aprili 22 mpaka 28 mwaka huu ikifanyika kwenye maeneo mawili Kijiji cha Miaka 21 Chumbageni Tanga na Korogwe.
Akizungumza na waandishi wa habari leo,Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Tanga Tumaini Gwakisa alisema zoezi hilo litafanyika kwenye maeneo mawili ambapo litaanzia Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Mkoa wa Tanga eneo la Kijiji cha miaka 21 Chumbageni kuanzia Aprili 22 mpaka 25 mwaka huu.
Alisema baada ya kumaliza kwa Tanga wataelekea wilayani Korogwe ambapo litafanyika kuanzia Aprili 26 mpaka 28 mwaka hu na uendeshwaji wa program hiyo utasimaiwa na itaongozwa na Waziri wa Ardhi Jerry Silaa akiwa na wataalamu wa Wizara hiyo.
“Nichukue nafasi hii kwaalika wananchi wote wa mkoa wa Tanga kuhudhuria na kupata huduma mbalimbali za sekta ya ardhi katika maeneo ambayo kliniki hiyo itafanyika kwani kutakuwa na utatuzi wa migogoro ya ardhi ambapo Waziri atasikiliza kero mbalimbali za Migogoro hiyo”Alisema
Alisema pia kutakuwa na utolewaji wa elimu kuhusu usimamizi wa ardhi pamoja na uwepo wa kituo jumuishi kitakachotoa huduma ya kupokea maoni mbalimbali na utoaji hati miliki ,ukadiriaji wa kodi ya ardhi na ulipaji wa kodi ya ardhi.
Gwakisa aliwataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuhudhuria na kushiriki ambapo Waziri atakuwepo na wataalamu kutoka Wizarani
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuyapa kipaumbele masuala ya maendeleo ya vijana nchini.
Aidha, Mhe. Katambi amesema vijana ni nguvu kazi ya taifa, hivyo kuwezesha kundi hilo kunatoa fursa kubwa ya kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kuwafanya vijana kuwa chachu kwa maendeleo ya nchi.
Ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP)” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Vile vile, Naibu Waziri Katambi amesema serikali imeboresha mwongozo wa utoaji mikopo kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana ambapo kwa sasa mfuko huo unatoa mikopo kwa kijana mmoja mmoja, ambapo maboresho hayo yatawawezesha vijana walio katika sekta isiyo rasmi na wahitimu wa vyuo kujiajiri kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali.
Kwa upande wengine, Mhe. Katambi amesema programu ya Safeguard Young People ni fursa kwa vijana kujikwamua na changamoto za kijamii na kiuchumi, hivyo amehamasisha ushirikiano katika utekelezaji wa programu hiyo ili kufikia malengo na kuleta mabadiliko chanya kwa vijana.
Naye, Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot amesema ni wakati wa kutambua mchango wa vijana katika kukuza maendeleo ya taifa. Aidha, ameongeza kuwa serikali ya Uswisi itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza programu hiyo ya SYP kwa lengo la kuwaondolea vijana changamoto za kiafya, kiuchumi, kisaikolojia na kijamii.
Akizungumza mmoja wa wanufaika amesema programu hiyo imewasaidia vijana kujitambu, kijithamini na kuwa na uthubutu katika kufanya maamuzi sahihi.
Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana “Safeguard Young People (SYP)” inalenga kuboresha huduma za afya, elimu ya afya kwa vijana, kuongeza ushirikishwaji wa vijana katika ngazi za maamuzi na pia kuwaunganisha vijana na fursa za kujipatia ujuzi na kipato.
Wasanii wa muziki wa kizazikipya Ben Pol, Phina na Tommy Flavor wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Tanzania, Mark Shreiner (kulia). Katikati ni Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
KAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation wamekabidhi mitungi ya gesi ya kupikia ya Oryx 50 kwa wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kati ya mitungi 1000 inayotarajiwa kukabidhiwa kwa wauguzi na madaktari katika mikoa 10 nchini .
Akizungumza wakati wakisaini makubaliano ya ushirikiano yaliyofanyika katika hospitali ya rufaa ya Mwananyama, Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite amesema makubaliano walioingia baina ys kampuni hiyo na taasisi ya Doris Mollel ni kusaidia kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa watanzania.
Aidha amesema katika kampeni hiyo ya kuwezesha watanzania kuingia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia, mpaka sasa tayari wameshatoa mitungi kwa wananchi zaidi ya elfu 32 ili kusaidia lengo la kufikia asilimia 80 ya watumiaji wa nishati safi.
Amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia inasaidia kuondoa hatari za kiafya kwa watumiaji wa kuni na mkaa kama nishati ya kupikia lakini pia hatari za kimazingira na ustawi wa jamii.
"Takribani watu 33,000 wanapoteza maisha nchini Tanzania kwa maradhi yanayotokana na kuvuta moshi unaotokana na mkaa au kuni hiyo ndio sababu ya Oryx gas kuja na suluhisho la kuwahamasisha wananchi kutumia gesi kwa matumizi ya kupikia", amesema Benoite
Ameeleza kuwa matumizi ya gesi yanaepusha wamama na watoto kuumika kubeba kuni hivyo kuepuka kujeuriwa na wanyama wakali wakiwa katika harakati za kutafuta kuni pia kuimarisha maisha ya wanawake na kuwalinda dhidi ya vitendo vya udhalilishaji.
“Kuanzia mwezi wa saba mwaka 2021 tumekuwa mstari wa mbele kuunga mkono utekelezaji wa mkakati wa serikali uliopewa nguvu na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania , Dk. Samia Suluhu Hassan kwa lengo kwamba ifikapo mwaka 2033 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia”, ameeleza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel amesema katika makubaliano waliosaini na oryxy watawafikia waguzi elfu moja ambapo watawapa mitungi na majiko ya gesi kama mabalozi kwa kina mama waweze kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni programu ya miaka miwili.
Amesema mitungi hiyo itakwenda kwa wauguzi walioko maeneo magumu ambapo watakuwa wanawatembelea kwenye vituo vya afya na zahanati ili kuweza kuwafikia wafanyakazi ambao ni wauguzi wanaofanya kazi kubwa ya kuokoa maisha hususani ya mama na mtoto.
Wakati huo huo Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Dk.Zavery Benela ameeleza kwamba hospitali hiyo inakabiliwa na ongezeko la wagonjwa wa mifumo ya hewa.
Amefafanua kati ya wagonjwa wa nje 500 wanaofika kuonwa na madaktari bingwa asilimia 30 ya wagonjwa hao ni wa matatizo ya mfumo wa hali ya hewa unaosababishwa na hali ya hewa pamoja na mazingira ya kuandaa chakula kutokna na kuni na mkaa.
Aidha Dokta Benela amesema magonjwa ya mfumo wa hali wa hewa yamekuwa changamoto hasa kwa watu wazima na watoto.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel (katikati) akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya makubalinao na Kampuni ya Oryx Gas kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala wakifuatilia hafla ya utiaji saini kati ya kampuni ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.