NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

ONGEZEKO la fedha shilingi Trilioni 10 kwenye bajeti ya Wizara ya Tamisemi imeibua matumaini kwa Wanaharakati wa masuala ya kijinsia ambapo wanatarajia itakwenda kutoa chachu ya kuinua ushiriki wa wanawake katika masuala ya uongozi na kuwaepusha na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na kuwaondolea mazingira magumu wakati wa uchaguzi.

Hayo yamesemwa leo April 17,2024 katika Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) ambazo zimekuwa zikifanyika kila Jumatano na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa Jinsia katika viwanja vya TGNP- Mtandao Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa semina, Muwasilishaji Bw.Iddi Mziray amesema wamehoji kuhusiana na urejeshwaji wa mikopo ya asilimia 10 iliyoondolewa mwaka uliopita kutokana na changamoto za marejesho endapo mifumo iliyowekwa na serikali itawasaidia kujibu changamoto za wanawake wa chini ambao ndio walengwa.

"Kulikuwa na changamoto za msimu uliopita kwa wanawake, vijana na walemavu walichukua mikopo bila elimu,je mifumo hii tuliyonayo itakwenda kutatua masuala hayo na ya vikundi hewa". Amesema Mziray.

Aidha Mziray ameeleza kuhusiana na suala la miundombinu ya shule ambapo wanatarajia ongezeko la matundu vyoo pamoja na sehemu za kubadilishia taulo za kike na fedha kwa ajili ya taulo hizo ambapo wameona bajeti haijalizungumzia suala hilo moja kwa moja na tamanio lao ni kutengwa fedha kwa ajili ya masuala hayo.

Kwa Upande wake Mdau wa masuala ya kijinsia Bw.Mophat Mapunda amelipongeza bunge kupitisha Sheria ya unyanyasaji wa kijinsia kama kosa katika uchaguzi,ambapo amedai kuwa katika kanuni za uchaguzi ambazo zinatarajiwa kupitishwa hivi karibuni hazijaonesha namna ambavyo zitampa kipaumbele mwanamke.

Aidha Mapunda ameiomba serikali kuhusiana na fedha iliyotengwa kwa lengo la kutoa elimu ya masuala ya uchaguzi,iwe inakidhi kuwezesha wanawake kushiriki katika zoezi hilo ili kuongeza usawa na kuondoa suala la mfumo dume ambalo limetawala kwa jamii kubwa.

Naye, Mwanaharakati wa Jinsia Bi.Mtumwa Nindi ambaye ni mlemavu ameiomba serikali kuwapatia elimu ili wanufaike na mikopo ya asilimia 10 ambapo ameeleza kuwa mfumo huo wa porto ambao umeundwa kwa ajili ya huduma hiyo hawatambui jinsi.ya kuutumia.

TGNP kupitia semina za Jinsia na Maendeleo imekuwa ikitoa mafunzo kwa Wanaharakati namna yakupambana ili kuwa na bajeti yenye mlengo wa kijinsia ambayo itasaidia kuunda usawa kwa jinsia zote katika masuala ya fursa za uongozi pamoja na mgawanyo wa rasilimali,na umiliki wa Mali.








Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiagana na Waziri wa Fedha, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango - Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum pamoja na viongozi wengine wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) mara baada ya kufungua Mkutano wa 10 wa Shirikisho hilo unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akionesha tuzo aliyokabidhiwa na Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) wakati wa Mkutano wa 10 wa Shirikisho hilo unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Kushoto ni Waziri wa Fedha Ofisi ya Rais Fedha-Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum na kulia ni Rais wa Chama cha Wakaguzi wa Ndani Tanzania, Dkt. Zelia Njeza.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akikabidhiwa tuzo na Rais wa Chama cha Wakaguzi wa Ndani Tanzania, Dkt. Zelia Njeza iliyotolewa na Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) wakati wa Mkutano wa 10 wa Shirikisho hilo unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Waziri wa Fedha na Mipango Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Saada Mkuya akiteta jambo na pamoja Mkaguzi Mkuu wa Ndani (IAG), Bw. Benjamini Magai na viongozi wengine wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) mara baada ya kufunguliwa kwa Mkutano wa 10 wa Shirikisho hilo unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha na Kamati ya maandalizi ya Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) Pamoja na wajumbe wengine wa mkutano.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na watoa mada pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) mara baada ya kufungua mkutano.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw. Leornad Mkude (kushoto), akisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Wizara ya Fedha, Bw. Moses Dulle (wa kwanza kiti cha pili) na Mkaguzi Mkuu wa Ndani Msaidizi Bw. Mwanika Semroki, wakisikiliza mada zilizokuwa zinatolewa wakati wa Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).


Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Fedha Bw. Lisius Mwenda, (wa kwanza kulia), akifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha)

Na Mwandishi Wetu,Rufiji

Wananchi walioathiriwa na mafuriko wilayani Rufiji wameiona thamani na umuhimu wa uwepo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA baada ya leo Aprili 16, 2024 kupokea misaada mbalimbali kutoka kwa taasisi hiyo yenye thamani ya shillingi millioni 20 ikiwemo tani 6.4 za unga wa sembe, Kilo 666 za maharage na magodoro 186.

Kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA akimkabidhi misaada hiyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakari Kunenge, Kamishna Msaidizi mwandamizi Abraham Jullu amesema TAWA imeguswa na janga la mafuriko lililowapata majirani na wadau namba moja wa uhifadhi wananchi wa Rufiji ambao wamehusika kwa kiasi kikubwa kulinda rasilimali za Hifadhi ya Selous na hivyo imelazimika kuwashika mkono.

Jullu amesema tangu changamoto hii ya mafuriko imejitokeza TAWA ilifika kwa haraka na kuongeza nguvu kwa kutoa kikosi cha Askari 24 ili kusaidia katika zoezi la uokozi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya mbinu za kujikinga na madhara yatokanayo na wanyamapori wakali na waharibifu hususani mamba na viboko kwa jamii ambapo mpaka sasa TAWA imetoa elimu hiyo kwa wananchi wapatao 4,225 na bado inaendelea na zoezi hilo.

Sanjari na hilo, TAWA imetoa boti moja lenye uwezo wa kubeba jumla ya watu 15 ili kusaidia katika shughuli za uokozi zinazoendelea wilayani humo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakari Kunenge amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupeleka misaada mbalimbali kupitia Serikali na Chama Cha Mapinduzi tangu wilaya hiyo ipate changamoto hiyo ya mafuriko.

Pia amewashukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko na Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda kwa maamuzi ya haraka waliyoyafanya kupeleka misaada hiyo kwa wananchi wa Rufiji kwa wakati.

Mkuu huyo wa Mkoa ameendelea kuishukuru TAWA kwa msaada wa boti kwa ajili ya kufanya shughuli za uokozi na ushiriki wao wa ujumla katika zoezi la uokozi kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya dola na kukiri kuwa wananchi wa Rufiji wanaona thamani na umuhimu wa uwepo wa Taasisi hiyo Mkoani Pwani.

Licha ya kuishukuru TAWA, Mkuu wa wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amesema TAWA imekuwa na mahusiano na mashirikiano mazuri kati yake na uongozi wa wilaya yake ndio maana imekuwa rahisi kwao kuitikia wito wa kutoa msaada kufuatia janga lililoikumba wilaya hiyo.
 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Abbakari  Kunenge alizungumza wakati wa kupokea msaada kutoka TAWA kwa ajili walioarhiriwa na mafuriko Rufiji na Kibiti.

 

Picha za makabidhiano ya msaada uliotolewa na TAWA.

 

Matukio ya picha mara baada ya kukabidhiana  msaada.

*Kikao cha kugushi walipeleka hazina ajili ya hiyo bajeti

Na Chalila Kibuda,Michuzi Blog

Fedha zilizobadilishwa matumizi bila kuidhinishwa na mamlaka husika na utumiaji wa nyaraka za kubadili matumizi ya udanganyifu kiasi cha Sh. bilioni 4.88

Ukaguzi ulibaini kwamba mamlaka nne za serikali za mitaa zilibadilisha matumizi ya kiasi cha Sh.bilioni 4.88bila kupata idhini kutoka kwa mamlaka husika, zikiwamo Baraza la Madiwani na Waziri wa Fedha.

Halmashauri iliyobanika katika ripoti ya CAG kati ya hizo ni Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi ilipanga kutumia bajeti ya kiasi cha Sh.bilioni 7.06 kwa
ajili ya kulipa mishahara hata hivyo, bajeti hiyo ilibadilishwa kwa
kuongeza kiasi cha Sh.bilioni 2.07. Kati ya kiasi kiasi hicho kilichotengwa Sh.bilioni 1.61 tu ndizo zilizotumika.

Pia ukaguzi ulibaini nyaraka za mihutasari ya kikao cha kamati ya fedha, mipango na uongozi kilichofanyika tarehe 5 Juni 2023 zilighushiwa na kuwasilishwa Hazina kwa ajili yakuombakibali cha kubadili vifungu vya bajeti ya mishahara, ingawa kikaohicho hakikufanyika kama inavyoelezwa kwenye.

Hii ni kinyume na Kifungu Na.41(2) cha Sheria ya Bajeti, [Sura ya 439], ambacho kinaeleza kwamba ofisa masuuli hatabadilisha matumizi ya fedha endapo fedha hizo zinapaswa kuhamishwa kwenda kwa mtu au kwa taasisi zingineza serikali.


Maombi ya kubadilisha matumizi ya fedha yanapaswa kuambatishwa na taarifa inayoelezea kikamilifu sababu za ukosefu wa fedha zilizoidhinishwa awali. Baada ya kujadiliwa na kamati ya fedha mipango na uongozi, maombi hayo huwasilishwa kwa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kuidhinishwa.


Pia, Kifungu cha 41(1&2) cha Sheria ya Bajeti, [Sura ya 439], kinaruhusu
ofisa masuuli, kwa idhini ya waziri, kubadili matumizi kutoka kwenye
matumizi yaliyoidhinishwa.

Hata hivyo, Ofisa masuuli hatabadili matumizi ya fedha katika mazingira yafuatayo ambapo fedha zimetengwa kwa ajili ajili ya kazi maalum fedha zilizotengwa kwa ajili  ya kuhamishwa kwenda kwa mtu au taasisi zingineza serikali fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya shughuli zinazohusiana  na maendeleo fedha zilizotengwa kwa ajili ya mishahara kwenda kwenye matumizi mengine yasiyo ya mishahara na uhamishaji wa fedha mwingineo unaweza kusababisha ukiukwaji wa kanuni za kifedha.
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeahidi kusimamia na kutekeleza ipasavyo utolewaji wa elimu ya masuala ya fedha kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili taifa liweze kuwa na wataalam bobezi wa masuala ya kifedha.

Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 17, 2024 Jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga wakati akifungua warsha ya siku tatu kwa viongozi wa vyuo mbalimbali nchini ili kujadili mitaala ya elimu ya fedha kwa wanafunzi wa elimu ya juu huku ukiratibiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Amesema suala la elimu ya fedha kwa jamii ni muhimu kwa maendeleo ya nchi hivyo ni vyema elimu hiyo ikafika kwa jamii Ili watanzania waweze Kupata elimu ya masuala ya fedha.

Aidha Naibu Waziri Kipanga amesema serikali ya awamu ya sita imedhamiria kujenga uelewa wa masuala ya fedha kwa jamii.

“Wizara tutahakikisha elimu ya fedha inafundishwa katika mfumo wa elimu nchini hivyo twende kwa haraka kuhakikisha vijana ambao ni sehemu ya jamii nchini wanakuwa na uelewa wa masuala ya fedha hivyo natarajia wakuu wa vyuo mtabeba uelewa huo muhimu kwa vyuo vyetu nchini,” amesema Mhe. Kipanga.
.
Pamoja na hayo amesema kuwa BoT, itaendelea kusimama na vyuo na taasisi za elimu na Wizara ya Elimu katika kuhakikisha dhana ya elimu hiyo inakuwa endelevu na inafundishwa katika ngazi za jamii hata katika elimu zisizo rasmi.

Hata hivyo ameviagiza vyuo vikuu kushirikiana na BoT kufanya tathmini ya utekelezaji wa mpango huo ili kuboresha mbinu na nyenzo za kufikisha ujumbe huo kwa jamii.

“Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ipatiwe taarifa ya tathmnini mtakazofanya ili itusaidie katika kufanya maamuzi, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kujenga uelewa wa masuala ya fedha kwa jamii,” amesema.

Kwa upande wake Naibu Gavana Benki Kuu ya Tanzania Bi. Sauda Msemo amebainisha kuwa lengo la kutoa elimu ya fedha kwa Vijana wa kitanzania wanaosoma elimu ya juu ni kuwawezesha kupata ujuzi na uzoefu wa matumizi ya fedha.

Amesema takwimu ya Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022 inaonesha takribani watu asilimia 34.5 ni vijana walio na umri kati ya miaka 15-35 hivyo ili kuleta tija na ufanisi katika masuala ya uchumi ujuzi na uzoefu wa masuala ya fedha ni moja ya sifa muhimu kufikia azma hiyo.

Ameeleza kuwa elimu ya fedha kwa Watanzania kutachochea maendeleo kwa kuongeza utumiaji rasmi wa huduma za fedha na kuwawezesha watu wengi kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kuendesha shughuli zao kwa ufanisi kukuza uchumi kwa ujumla.

Bi. Sauda mesema elimu kwa vijana wa vyuo vikuu itawasaidia kuweka akiba, kupanga bajeti na kufanya uamuzi wa masuala ya fedha kwa kuzingatia viashiria hatarishi na kuelewa taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za fedha ili kufanya maamuzi sahihi ya fedha ili waitawale.

” Tunatarajia kujenga ‘displine’ ya fedha kupitia elimu ya fedha kwani watakuwa na uwezo wa kutawala fedha sio fedha kuwatawala vijana hao,” amesema.

Pia amesema BoT kwa kushirikiana na wadau wengine wa Baraza la Huduma Jumuishi za Fedha, imetoa muongozo na mtaala wa elimu ya fedha kwa wakufunzi ambao utatumika na taasisi za elimu ya juu kwa kuwafundisha watoa huduma za elimu ya fedha kuwafikia wananchi wote walio nje mfumo wa elimu.

“Tayari tumeingia makubaliano na baadhi ya taasisi zaa elimu katika mtaala huo wa kufunzi wa fedha na tulioingia nao makubaliano ni Chuo Kikuu cha Iringa, Zanzibar, Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha(IFM) na Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania ,” ameseama.

Katika warsha hiyo imebainishwa kuwa elimu ya fedha inapaswa kumfikia kila mmoja ili aweze kuwa na nidhamu katika matumizi ya pesa lakini kuepuka kuingia kwenye sitofahamu ambayo inawakuta wengi hasa wanapokwenda kwenye taasisi za mikopo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga akizungumza wakati akifungua warsha ya siku tatu kwa viongozi wa vyuo mbalimbali nchini ili kujadili mitaala ya elimu ya fedha kwa wanafunzi wa elimu ya juu huku ukiratibiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 17, 2024 katika ukumbi wa BoT Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga akifungua warsha ya siku tatu kwa viongozi wa vyuo mbalimbali nchini ili kujadili mitaala ya elimu ya fedha kwa wanafunzi wa elimu ya juu huku ukiratibiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 17, 2024 katika ukumbi wa BoT Jijini Dar es Salaam.


 Naibu Gavana Benki Kuu ya Tanzania Bi. Sauda Msemo akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu kwa viongozi wa vyuo mbalimbali nchini ili kujadili mitaala ya elimu ya fedha kwa wanafunzi wa elimu ya juu huku ukiratibiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 17, 2024 katika ukumbi wa BoT Jijini Dar es Salaam.


Viongozi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini wakiwa kwenye ufunguzi wa warsha ya siku tatu kwa viongozi wa vyuo mbalimbali nchini ili kujadili mitaala ya elimu ya fedha kwa wanafunzi wa elimu ya juu huku ukiratibiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 17, 2024 katika ukumbi wa BoT Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
MBUNGE wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota,akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI 2024/25 bungeni jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

MBUNGE wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota amempongeza Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha kongani ya viwanda vya kubangua korosho mkoani Mtwara.

Alitoa pongezi hizo jana bungeni jijini hapa wakati wa mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI 2024/25, alisema kongani hiyo itasaidia uzalishaji wa ajira kwa wakazi wa mkoa huo.

“Tunamshukuru Rais kwa mradi wa umwagiliaji wa Arusha chini, ujenzi wa viyuo vya afya vitatu, mradi wa TACTIC, ujenzi wa stendi mpya ya mabasi na ujenzi wa barabara ya lami kilomita tano,” alisema Chikota.

Alimpongeza Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa na Manaibu Waziri wake kwa uchapakazi wao na kushughulikia hoja za wabunge.

Hata hivyo, alisema jimboni kwake yapo matatizo yanayohisiana na miundombinu ambapo mbali na kuupungeza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) alisema wakala huo unakabiliwa na upungufu wa Wahandisi wa barabara.

Alisema meneja wa TARURA katika jimbo lake anahudumia wilaya tau ambazo ni Masnispaa ya Mtwara, Halmashauri ya Mtwara na Halmashauri ya Mji wa Nanyamba.

Alipendekeza kuwa TAMISEMI ipewe kibali maalum cha kuajiri Wahandisi wa barabara kwaajili ya kupelekwa wilayani.

Alisema upungufu wa watumishi pia upo katika sekta ya afya ambapo katika mkoa wa Mtwara kuna upungufu wa 6.088 waliopo ni 2,153 ambao ni upungufu wa asilimia 65.

Katika sekta ya elimu alisema kuna upungufu wa walimu ambapo aliishauri TAMISEMI kuhakikisha inatoa kibali cha walimu 300 kuajiriwa katika Halmashauri ya Nanyamba.

Alisema mapato ya serikali za mitaani madogo na vyanzo vingi si vya ukakika na vichache vilivyopo havisimamiwi vizuri.

“Halmashauri nyingi zinategemea ushuru wa mazao kama chanzo muhimu cha mapato yake. Vyanzo vingi vya uhakika vipo serikali kuu,” alisema Chikota.

Alisema kwasababu wizara imetenga Zaidi ya Sh. Bilioni 190 kwaajili ya ununuzi wa magari ya viongozi basi Mkuu wa Wilaya ya Mtwara anunuliwe gari jipya kwasababu lililopo halimwezeshi kutimiza majukumu yake vizuri.

MAADHIMISHO ya Sherehe za Mei Mosi Kitaifa kwa Mwaka 2024 yanatarajiwa kufanyika Jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na Mgeni Rasmi atakuwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 17, 2024 Jijini Arusha, Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya amesema maadhimisho hayo yataenda sambamba na michezo mbalimbali ya Mei mosi itakayofunguliwa rasmi siku ya Jumamosi tarehe 20 Aprili 2024 na Wazri wa Kazi, Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Deogratious Ndejembi.

Amesema Maadhimisho hayo yameratibiwa na Vyama vyote 13 vinavyounda Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ambavyo ni; - CHODAWU, COTWU (T), CWT, DOWUTA, RAAWU, TALGWU, TAMICO, TASU, TEWUTA, TRAWU, TPAWU, TUGHE na TUICO.

"TUCTA imeshirikiana na vyama vyote vilivyo nje ya TUCTA vilivyojitokeza katika maandalizi haya ya Sherehe za Mei Mosi ambayo yatakuwa ya aina yake". Amesema

Pamoja na hayo amewahimiza Wafanyakazi wote waliopo Mkoa wa Arusha na Mikoa ya Jirani kujumika kwa pamoja siku ya kilele cha maadhimisho ya Mei mosi Kitaifa ili kusherekea kwa pamoja na kuienzi siku hiyo muhimu kwa wafanyakazi Duniani.







Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imezindua mashine mpya ya kisasa (Senographe Pristine 3D Mammography suite) Yenye uwezo mkubwa wa kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti kwa njia ya kisasa zaidi.

Mashine hiyo imezinduliwa kwa kushirikiana na GE Healthcare na Chama cha Mionzi cha Amerika Kaskazini (RSNA).

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo leo Aprili 17,2024 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea amesema ufungaji wa mashine hiyo ni jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya afya.

"Kulingana na takwimu za Shirika la kimataifa la Afya (WHO), wanawake milioni 2.3 wamegunduliwa na saratani ya matiti. Ila kwa Tanzania, wanawake 42,000 wanagundulika kuwa na saratani ya matiti lakini cha kusikitisha ni kwamba asilimia 38 pekee ndio wanaopata matibabu, ikimaanisha kuwa ni wanawake 15,000 pekee wanaopata matibabu,” amesema Dkt. Nyembea .

Akiishukuru serikali ya Marekani na RSNA ameeleza kuwa mahusiano baina ya nchi hizo yamekuwa muhimu katika upatikanaji wa teknolojia ya hali ya juu inayohitajika ili kuongeza uchunguzi na utambuzi wa saratani ya matiti kwa wanawake nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa MNH, Prof.Mohammed Janabi amesema kuwa mashine hiyo mpya itawezesha utambuzi wa mapema na kuokoa maisha ya wanawake wengi nchini huku akibainisha kuwa saratani ya matiti ndiyo saratani inayowapata wanawake wengi na kwamba wanaongezeka.

“Muhimbili ni mwanga wa matumaini. Tunatarajia kwamba angalau wagonjwa 200 kwa mwaka hadi 2,400 watafaidika moja kwa moja kutokana na uchunguzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Ninaahidi kwamba mashine yetu ya uchunguzi wa saratani ya matiti (Senographe Pristina 3D) itahudumia watu wote kwa weledi wa hali ya juu na utunzaji bora,” amesema.

Amesema kuwa, mashine hiyo inatumia kiwango kidogo zaidi cha mionzi na hivyo kuifanya kuwa salama zaidi kwa watumiaji.

Aidha ametaja sifa za mashine hiyo kuwa itasaidia katika huduma za kiuchunguzi za matiti za kawaida (Core mammography functions), huduma za kiuchunguzi za kibobezi za matiti ambapo mgonjwa atachomwa sindano ya dawa ambayo wakati wa kupiga picha dawa hiyo hujikusanya zaidi kwenye maeneo yanayohisiwa kuwa na shida mathalani kwenye saratani kuonekana vizuri zaidi kwa waataalamu.

Amesema kuwa mashine hiyo ina uwezo mkubwa wa kuwaongoza wataalamu kutambua tatizo kwa usahihi wa hali ya juu na pia kutoa kinyama (sample) kwenye matiti kwa ajili ya uchunguzi pindi itakapohitajika

Kumekuwepo na uelewa mdogo katika jamii kuhusu saratani ya matiti, watu hawajui kuwa huduma za matibabu zinapatikana kwa urahisi kuanzia ngazi ya vijijini hadi ngazi ya taifa. Napenda kuwaambia wananchi kuwa huduma hizi zipo na zimeboreshwa vizuri. Ni wakati muafaka kwa wananchi kwenda kwenye vituo vya afya vilivyo karibu ili kupima afya zao na kupata ushauri wa kiafya.” ameongeza Prof. Janabi

Naye, Eyong Ebai, Meneja Mkuu wa Kanda ya Afrika mwa Jangwa la Sahara katika GE Healthcare, amesema wanasherehekea usimikaji wa hospitali ya kwanza ya umma nchini Tanzania na kuwa mwenyeji wa mfumo kamili wa mammografia wa digitali iunaotarajiwa kutoa huduma bora .

"Ni muhimu kutambua kuwa saratani ya matiti katika vidonda vinavyotiliwa shaka. Mifumo hii itawezesha utambuzi wa haraka wa saratani ya matiti ambayo itaokoa maisha".

Amesema kuwa wataendeleza mapambono hayo kwa kuwajengea watu uwezo ambao wataongoza kliniki kote Tanzania na ukanda mzima katika mapambano dhidi ya saratani ya matiti,.

“Tutapima na kutathmini viashiria vinavyoongoza ili kufuatilia maendeleo na kuhakikisha tunafanikiwa. Tutatayarisha na kutoa programu za elimu ili kujenga uwezo ili kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu. Tutatoa data na taarifa muhimu ambazo zitaendesha sera, udhibiti na ugawaji wa rasilimali kwa msingi wa ushahidi ili kuboresha matibabu ya saratani ya matiti nchini Tanzania." amesema 

Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa wa Chama cha Mionzi cha Amerika Kaskazini (RSNA) Meredith McNeil alisema pamoja na ufungaji wa mashine ya Pristina Mammography nchini Tanzania, teknolojia hiyo itasaidia kuhakikisha wanawake wanapata uelewa wa saratani ya matiti, matibabu, uchunguzi wa jumla na kinga na kuongeza kuwa. , bado kuna safari ndefu ya kupata watu wengi mafunzo na kuwavutia wanawake. "Kwa kweli hii itakuwa mfano kutoka Tanzania hadi ukanda wa Afrika juu ya kile ambacho mammografia inaweza kutoa kwa idadi ya watu, ikizingatiwa kuwa huduma ya afya ya wanawake huathiri sana familia kwa hivyo tunatarajia kuwa mfano huu unaweza kusaidia sana katika utunzaji wa kawaida na kusaidia kuokoa pesa." Amesema.

Meredith McNeil  Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa na muwakilishi wa Jumuiya ya akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashine ya kisasa maalumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo Aprili 17,2024 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)Radiolojia ya Amerika ya Kaskazini (RSNA) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mashine ya kisasa maalumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo Aprili 17,2024 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashine ya kisasa maalumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo Aprili 17,2024 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Guillaume Fusari Meneja Mkuu wa GE Healthcare katika masuala ya afya ya wanawake na X-Ray, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashine ya kisasa maalumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo Aprili 17,2024 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).


Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Mashine ya Kisasa ya kupima Saratani ya Matiti, uzinduzi uliofanyika leo Aprili 17, 2024 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


Na Mwamvua Mwinyi
WANANCHI wa Kijiji cha Kwedikwazu , wilayani Handeni mkoa wa Tanga wameipongeza Serikali kwa hatua mbalimbali zinazoendelea kufanyika ili kuleta maendeleo ya Kudumu kupitia Sekta ya Madini.

Hayo yalibainishwa na Katibu wa Kikundi cha Wanawake cha Mwanzo Mgumu, Saumu Kisaka wakati akizungumza na timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Madini walipotembelea Mgodi wa Dolomite Mkoani humo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake, Kisaka alisema, kikundi chao ambacho kina wanachama 12 kinajishughulisha na biashara ya kokoto za mapambo, ujenzi na uuzaji wa mawe mbalimbali yakiwemo mawe ya ujenzi, biashara inayowasaidia kujipatia kipato na kuendesha maisha yao ya kila siku.

Kisaka alisema, biashara ya uuzaji madini ya Dolomite (mawe meupe) inamsaidia kuendesha maisha yake ikiwemo kusomesha watoto, kujenga nyumba ya kuishi na kukidhi mahitaji ya lazima ikiwemo gharama za matibabu, mavazi na chakula.

Katika hatua nyingine, Kisaka aliiomba Serikali kusaidia upatikanaji wa masoko ya Madini hayo ya urembo na mashine ya usagaji wa mawe ambapo kwa sasa wanatumia nyundo za mkono kugonga mawe hayo ili kuongeza kipato kwa wananchi wanaoishi katika eneo la kijiji hicho na Tanzania kwa ujumla.

Pia, Kisaka ametumia nafasi hiyo kuishukuru timu ya Habari kutoka Wizara ya Madini kwa kutembelea eneo la uzalishaji na ufanyaji biashara ya madini hayo wilayani humo.

Awali, Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Tanga, Winnifrida Mrema alielezea ,shughuli za uchimbaji madini ya viwandani aina ya Dolomite katika kijiji cha Kwedikwazu zinafanywa na wachimbaji wadogo .

Madini hayo husafirishwa kwenda kwenye viwanda katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Arusha kwa ajili ya kutengeneza wa rangi za majengo, mbolea, na viwanda vya kuchakataji kwaajili kutengeneza urembo wa majengo mbalimbali."

Aidha, Mrema alisema Mkoa wa Tanga umepata mafanikio makubwa kwa kuwepo machimbo hayo ambapo wananchi wa Kijiji hicho wamejipatia ajira ikiwemo kina mama wanaoponda na kuuza madini hayo kwa ajili ya urembo wa nyumbani na waendesha bodaboda wanaendelea kujipatia kipato kwa ubebaji wa madini hayo kutoka migodini mpaka katika eneo la barabara kwa ajili ya ufanyaji biashara pia wasafirishaji wa madini hayo kwa kutumia malori kutoka mgodini hapo mpaka viwandani.

Mrema alitoa wito kwa Wawekezaji Wakubwa na Wadogo nchini kujitokeza na kuchukua Leseni za Uchimbaji wa Madini hayo kwa ajili ya kuleta tija na maendeleo kwa jamii.

Dolomite ni aina ya madini ya viwanda yanayotumika kwa ajili ya mapambo, ujenzi, utengenezaji wa rangi, pamoja na utengenezaji wa mbolea.

Top News