Na Mwandishi Wetu
SERIKALI ya Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) wameungana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani na kutangaza kampeni ya usambazaji wa vyandarua vilivyowekwa dawa kwa Zanzibar yote.
Kwa mujibu wa Utafiti wa Viashiria vya Malaria Tanzania wa mwaka 2022, Zanzibar bado ina kiwango cha malaria chini ya asilimia moja kwa zaidi ya muongo mmoja.
Hiyo ni kutokana na mchango mkubwa kutoka serikali ya Marekani kupitia Mpango wa Rais wa Marekani wa mapambano dhidi ya malaria na ushirikiano na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kwamba hivi karibuni idadi hii iliongozeka.
Akizungumza kuhusu Mpango huo Waziri wa Afya Zanzibar Dk.Nassor Ahmed Mazuri amesema pamoja na kupungua kwa namba ya wagonjwa wa malaria Zanzibar, amegundua hivi karibuni kuna baadhi ya wilaya zimeshuhudia ongezeko la wagonjwa wa malaria.
" Hili halikubaliki Zanzibar, naomba hatua zote zichukuliwe kudhibiti ugonjwa ya malaria kwa kushirikisha sekta zote zinazohusika” amesema Dk Mazrui.
Mwaka huu Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani yalishuhudia uzinduzi wa wa kampeni ya usambazaji wa vyandarua vilivyotiwa dawa iliyopewa jina la’ Usingizi Bul Bul.’
Kampeni hiyo inayoongozwa na Mpango wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria (PMI), itasambaza vyandarua 782,000 katika Shehia 314 Unguja na Pemba.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pia ilizindua Baraza la Kutokomeza Malaria, ambalo litaimarisha utokomezaji wa malaria kwa kuonesha umuhimu wa kuongeza rasimili zaidi.
“Marekani ina heshima kubwa kuungana na serikali ya Zanzibar katika kuanzisha kampeni ya usambazaji wa vyandarua vilivyotiwa dawa Zanzibar na kuhakikisha vinatumika ipasavyo.
" Kwa pamoja, tuna elimisha jamii kutoka kuelewa tu mpaka kutumia kwa vitendo,” amesema Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la USAID Craig Hart wakati wa hafla hiyo.
“Naipongeza serikali ya Zanzibar kwa kuzindua pia Baraza la Kutokomeza Malaria, litakaloimarisha programu za kupambana na malaria kwa kuongeza rasilimali zaidi kusaidia afua za malaria, kwa kushirikiana na sekta binafsi."
Kampeni hiyo ya usambazaji wa vyandarua vyenye dawa inawakilisha mbinu bunifu na ya kina ya kutokomeza malaria. Itatumia mfumo wa kielektroniki kufuatilia maoteo ya vyandarua, usajili wa kaya zitakazopata vyandarua, na ugawaji wa vyandarua hivi.
Itatumia jumbe fupi kufahamisha kaya siku ya kupokea vyandurua na kusambaza jumbe kuhusu matumizi sahihi ya vyandarua na utunzaji wa vyandarua. Mfumo huu umewezeshwa na kufadhiliwa na serikali ya Marekani kupitia PMI.
Ukitekelezwa na USAID na CDC, PMI ilianza kushirikiana na Tanzania mwaka 2006 na imewekeza zaidi ya dola milioni 747 nchini. Marekani bado ina dhamira ya dhati ya kuendelea kushirikiana na serikali na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, asasi za kiraia na watu wa Tanzania katika mapambano yanayoendelea ya kutokomeza malaria na kuboresha afya na ustawi wa wananchi wake.
Mkurugenzi Mkazi wa USAID Dk Crag Hart akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliozinduliwa leo
Na Mwandishi Wetu
Wakati kesho Tanzania ikisherehekea miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar (ZPPDA) zimesaini rasimu ya mkataba wa maelewano (MOU) kufanya kazi pamoja na kuimarisha muungano.
Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dodoma mbele ya wenyeviti wa bodi zote mbili za wakurugenzi na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi, wawakilishi wa wafanyakazi na makamu Mwenyekiti ZPPDA, wajumbe wa bodi wa pande zote mbili, Mkurugenzi Mkuu PPRA, Eliakim Maswi na Mkurugenzi Mtendaji ZPPDA, Othman Juma Othman na menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
Akizungumza baada ya kusaini MOU hiyo, Mkurugenzi Mkuu Mamlakaya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Eliakim Maswi, amesema wamekubaliana kushirikiana katika kujenga uzoefu kwa watendaji na kukuza maarifa ya kiutendaji kwa kubadilishana utaalamu katika kutekeleza mbinu za kimkakati na taaluma ya ununuzi.
Vilevile, kushirikiana katika kuzitambua sheria na miongozo ili kuleta tija na uwajibikaji ndani ya taasissi hizo, kuelimishana taarifa na ujuzi muhimu unaohusu ununuzi wa umma na uendeshaji mali za umma, kuhabarishana, kubadilishana uzoefu na kuhusishana katika fursa za kushiriki katika majukwaa na mikutano inayohusu ununuzi wa umma.
“Tumeamua kushirikiana kwa sababu wote tuko katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kazi tunazofanya zinafanana tumeamua kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi wetu hiyo ilikuwa ni mwaka 2022 na mwaka jana 2023 bodi yetu ya PPRA ilienda Zanzibara na kufanya kikao,” amesema Maswi na kuongeza;
“Baada ya kikao kile viongozi wetu wa pande zote mbili walitoa maelekezo kwamba tukutane na tuandae makubaliano ambayo yatatuwezesha kushirikiana na kuwezesha pande zote mbili kufanya kazi.
Wanasheria kutoka pende zote mbili wamefanya kazi kwa kushirikiana na wametuleta mapendekezo ambayo wameona yanafaa na mimi na mwenzangu tumekubaliana kwamba haya yanafaa,”
Ameongeza kwamba wamekubaliana kupeana msaada unaohitajika kupitia rasilimali walizonazo, kuimarisha, kuwajengea uwezo watendaji wa pande zote mbili na kuwaweka pamoja.
“Baada ya mkataba huu mimi nikitaka mtu kutoka Zanzibar mwenzangu atamruhusu pia akitaka nitamruhusu maana tunataka kubadilisha uzoefu, kutengeneza ushirikiano maalum katika shughuli za ufuatiliaji, ukaguzi na uchunguzi unaojumuisha uchunguzi wa uzingatiaji wa sheria na thamani ya fedha,” amesema Maswi
“Pia tutashauriana kuhusu nyenzo za kisasa za utendaji wa majukumu ikiwemo vifaa vya kielektroniki na vingine vya kazi ya uchunguzi na ufuatiliaji. Tutakuwa na shughuli za pamoja ambazo tunazifanya ikiwemo kikao cha pamoja cha bodiya Wakurugenzi, kila upande utakuwa na wajibu wa kuzingatia, kufuata na kutekeleza ratiba hiii,”
“Ni wajibu wa pamoja kuandaa dira sisi PPRA na ZPPDA na ripoti itolewe ili kubuni mikakati ya kuleta tija katika nch yetu. Tumekubaliana kufanya mafunzo ya muda mfupi ya mara kwa mara kwa watendaji wetu wa mamlaka kwenda kwa kila mamlaka kujifunza yanayohusu shughuli za usimamizi wa mali za umma na uondoaji wa mali,” amesema
Ameeleza kuwa kupitia makubaliano hayo wanaweza kufanya vikao vya pamoja vya dharura kama kuna changamoto imejitokeza ili kuimarisha Muungano, pia watakuwa wanawasiliana kupeana msaada unaohitajika kwa wakati muafaka kwa ajili ya kupeana mbinu za kutatua changamoto.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Ununuzi na uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar (ZPPDA), Othman Juma Othman amesema “tunafanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya Watanzania leo tumesaini MOU tunaishukuru idara ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar imetoa maoni yake na leo hii yametuwezesha kufika hapa.
Naye, Makamu Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Ununuzi na uondoaji wa Mali za Umma (ZPPDA), Ahmed Makame Haji, amesema makubaliano hayo yameishasainiwa lakini hayatakamilika na hayatakuwa na umuhimu kama hakutakuwa na utekelezaji na suala hilo kubaki katika makaratasi.
“Kama ambavyo tumekubaliana kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisha makubaliano hayo yanatekelezwa na kujiwekea utaratibu wa kuangalia kama makubaliano hayo yanatekelezwa. Tutakuwa na suala la ufuatiliaji na kuangalia kila mwaka tumefikia wapi katika utekelezaji wa makubalaino haya na pale ambapo tutabaini kasoro tutazitatua na kuhakikisha tunafikia hayo makubaliano,” amesema Haji
Naye,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PPRA, Dkt. Leonada Mwagike, amesema “tumeishasaini mkataba kilichobaki ni utekelezaji kwa wakati ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha inapatikana katika ununuzi wa umma na kuhakikisha tunafanya tathimini ya utekelezaji wa makubaliano haya mara kwa mara ili kuhakikisha mkataba huu unatekelezeka."
Mkurugenzi Mkuu Mamlakaya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Eliakim Maswi na Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Ununuzi na uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar (ZPPDA), Othman Juma Othman wakisaini hati za makubaliano ya ushirikiano wa kiutendajiji kati ya Tanzania Bara na Zanzibar katika hafla iliyofanyika Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Kanda ya Magharibi, limewapatia elimu wanafunzi 5,000 katika shule za sekondari 20 za Manispaa ya Tabora kuhusu kazi za Baraza, taratibu na miongozo mbalimbali ya kujiunga na vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini.
Akizungumza na baadhi ya wanafunzi, Meneja wa NACTVET Kanda ya Magharibi, Bi. Faraja Makafu amesema, kampeni hiyo imelenga kuondoa changamoto wanazopata wanafunzi wakati wa kuomba kujiunga na vyuo mbalimbali vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi mara baada ya kuhitimu masomo yao ikiwemo changamoto ya kudahiliwa katika vyuo na programu zisizo na ithibati ya Baraza.
“Uzoefu wetu na maoni toka kwa wadau wetu mbali mbali umetufanya tuanzishe kampeni ya Kanda kwa kanda ili kuwasaidia wanafunzi kufanya maamuzi na machaguo sahihi wakati wa kuomba vyuo. Wanafunzi wanapaswa kuomba udahili kwa usahihi na kwa kuzingatia taratibu na miongozo iliyowekwa ili waweze kutimiza ndoto zao”, alitamatisha Bi. Faraja.
Aidha, Meneja huyo wa Kanda amewataka wanafunzi hao kusoma kwa makini kitabu cha mwongozo wa udahili ambacho kinapatikana katika tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz) kwani kina maelezo ya kina ya hatua kwa hatua hadi kukamilisha udahili wa wanafunzi katika vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
Kwa upande wao, wanafunzi hao kwa nyakati tofauti wameshukuru hatua ya NACTVET kuanzisha zoezi la kuwapatia wanafunzi Elimu hiyo muhimu kwao na kuahidi kuwa mabalozi wazuri kwa wengine kwa kuwaeleza umuhimu wa kuzingatia taratibu na miongozo pindi watakapoamua kujiunga na vyuo mbalimbali.
Kampeni ya uelimishaji wanafunzi wa shule za sekondari za Kanda ya Magharibi, mkoani Tabora imeanza tarehe 22 Aprili, 2024 na itafikia tamati mnamo tarehe 1 Mei, 2024, ambapo miongoni mwa shule zilizokwishatembelewa ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Wavulana Milambo, Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora, Shule ya Sekondari Themi Hill, Shule ya Sekondari ya wavulana Tabora, Shule ya Sekondari Ipuli, Shule ya Sekondari Cheyo, Shule ya Sekondari Isevya na Shule ya Sekondari Mihayo.
NACTVET ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge, Sura ya 129 na Marekebisho Madogo Na.4 ya mwaka 2021, kwa lengo la kurekebu Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini. Fasiri ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi ina nasibishama “Elimu na Mafunzo yanayotolewa kwa wanachuo kwa misingi ya ujuzi na umahiri (CBET), ili kuwajengea uwezo wahitimu kutekeleza majukumu yao yanayohitaji kiwango cha juu cha ujuzi, maarifa, uelewa na weledi kuwawezesha kutimiza wajibu wao kwa ufanisi na tija katika maeneo ya taaluma walizosomea”.
NACTVET ina jumla ya kanda nane zilizoanzishwa kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wadau. Kanda hizo ni ni pamoja na Kanda ya Mashariki Dar es salaam, Kanda ya Kati Dodoma, Kanda ya Magharibi Tabora, Kanda ya Ziwa Mwanza, Kanda ya Kusini Mtwara, Kanda ya Kaskazini Arusha, Kanda ya Kati Dodoma pamoja na Ofisi ya Zanzibar.
Meneja wa NACTVET Kanda ya Magharibi Tabora Bi. Faraja Makafu akitoa Elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mihayo
Afisa Uthibiti wa NACTVET Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Mohamed Kaunasa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Milambo.
Meneja wa NACTVET Kanda ya Magharibi Tabora, Bi. Faraja Makafu akitoa zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kamazima.
Picha za matukio mbalimbali katika utoaji elimu wa NACTVET.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa wizara hiyo, Miriam Mmbaga(wapili kushoto) wakisikiliza ufafanuzi wa programu maalumu ya kudhibiti uhalifu wa Kimtandao kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya SOLAR,Timul Solovev wakati wa Maonesho ya Teknolojia ya Kudhibiti Uhalifu huo yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa EXPOFORUM ambapo Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama kutoka takribani nchi 20 Duniani wamekutana nchini Urusi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Mwandishi Wetu,URUSI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kazi kubwa waliyoifanya kuwaletea maendeleo wanawake na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na kuandaa mdahalo wa wanawake na Muungano.
Pia, ameupongeza umoja huo kwa kuendelea kuwa kinara katika kubuni na kutengeneza mambo mbalimbali yenye lengo la kuimarisha CCM, kikiunganisha na wananchi na kuimarisha umoja na mshikamano na wananchi.
Dkt. Mwinyi amesema hayo jijini Dar es Salaam leo Aprili 25, 2024 alipofungua mdahalo wa kitaifa wa Wanawake na Muungano uliondaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City.
Mdahalo huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wake za viongozi wakuu wastaafu, mawaziri, naibu mawaziri, wabunge, wawakilishi, wananchi na wanachama wa jumuiya hiyo na wa CCM.
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda amesema wanafanya mdahalo wa kuelekea miaka 60 ya Muungano na kujadili nafasi ya mwanamke katika kipindi cha nyuma,sasa na kijacho
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa UWT, Ndg.Zainab Shomari amesema muungano huo uliletwa na nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar zikiwa huru, haukuwa wa kuchanganya mchanga tu, bali wa kidamu kwa kuwa Zanzibar kuna watu wa makabila mbalimbali.
Uchaguzi huo umefanyika kufuatia Msumbiji kumaliza muda wake na kukabidhi uenyekiti kwa Namibia, Hivyo, Tanzania inategemewa kuwa Mwenyekiti wa ZAMCOM.
Katika mkutano huo, Tanzania imewakilishwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew.
Licha ya kushiriki Mkutano wa 11 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (Zambezi Watercourse Commission - ZAMCOM), Tanzania imefanya mazungumzo na wadau wa maendeleo na kuwakaribisha kuwekeza katika Sekta ya Maji nchini Tanzania.
Mhandisi Kundo ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo amekutana na kufanya mazungumo na Mwakilishi wa Shirika la Sweden, SwedFund.
Katika mazungumzo hayo, Tanzania imeikaribisha Taasisi ya SwedFund nchini ili kushirikiana katika maeneo ya maandalizi ya miradi ya miundombinu yenye ukubwa wa kati na wa juu.
Nae mwakilishi wa SwedFund ameahidi kushirikiana na Tanzania katika kufanya majadiliano kuhusu kuandaa miradi mahsusi.