Na Oscar Assenga,TANGA

WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Mendeleo ya Makazi Jerry Silaa anatarajiwa kuongoza Kliniki ya Ardhi kwa mkoa wa Tanga itakayofanyika kuanzia Aprili 22 mpaka 28 mwaka huu ikifanyika kwenye maeneo mawili Kijiji cha Miaka 21 Chumbageni Tanga na Korogwe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Tanga Tumaini Gwakisa alisema zoezi hilo litafanyika kwenye maeneo mawili ambapo litaanzia Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Mkoa wa Tanga eneo la Kijiji cha miaka 21 Chumbageni kuanzia Aprili 22 mpaka 25 mwaka huu.

Alisema baada ya kumaliza kwa Tanga wataelekea wilayani Korogwe ambapo litafanyika kuanzia Aprili 26 mpaka 28 mwaka hu na uendeshwaji wa program hiyo utasimaiwa na itaongozwa na Waziri wa Ardhi Jerry Silaa akiwa na wataalamu wa Wizara hiyo.

“Nichukue nafasi hii kwaalika wananchi wote wa mkoa wa Tanga kuhudhuria na kupata huduma mbalimbali za sekta ya ardhi katika maeneo ambayo kliniki hiyo itafanyika kwani kutakuwa na utatuzi wa migogoro ya ardhi ambapo Waziri atasikiliza kero mbalimbali za Migogoro hiyo”Alisema

Alisema pia kutakuwa na utolewaji wa elimu kuhusu usimamizi wa ardhi pamoja na uwepo wa kituo jumuishi kitakachotoa huduma ya kupokea maoni mbalimbali na utoaji hati miliki ,ukadiriaji wa kodi ya ardhi na ulipaji wa kodi ya ardhi.

Gwakisa aliwataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuhudhuria na kushiriki ambapo Waziri atakuwepo na wataalamu kutoka Wizarani


KILA kukicha Meridianbet inasambaza tabasamu na upendo kwa wateja wake wanaocheza michezo ya kasino ya mtandaoni au kubashiri mubashara, odds kubwa na bonasi za kasino ni sehemu ya zawadi za kila siku. Jisajili sasa uwe wa kwanza kupata tabasamu kila kukicha.

Kama wewe ni mdau wa kucheza kasino ya mtandaoni pale Meridianbet bila shaka neno Expanse sio geni kichwani mwako! Sasa mchongo uko hivi, kila unapocheza michezo ya kasino au sloti zilizotengenezwa na Expanse Studio unakuwa na nafasi ya kupata mgao wa mpaka Tsh 1,250,000/=

Shindano la Expanse na Meridianbet Kasino ya Mtandaoni.

Promosheni hii imeanza 18.04. 2024 ambapo bonasi za kasino zitagawiwa kwa washindi watakaokuwa wanatangazwa kila siku, baada ya kucheza moja kati ya michezo ya kasino ya mtandaoni iliyopo Meridianbet kutoka Expanse studio.

Promosheni ni halali kwa wachezaji waliosajiliwa kwenye APP na tovuti ya meridianbet.co.tz

Promosheni itafanyika katika mtindo wa mashindano kwa wachezaji kwenye sloti zinazotolewa na Expanse Studio. Michezo ya kasino ya mtandaoni itakayotumika wakati wa promosheni ni:
Battle of Egypt
Forest Rock
Fortune Farm
Lucky's Betting Shop
Maya's Treasure
Piggy Party
Spinning Buddha
Sticky 777
The Book of Eskimo
Veni Vidi Vici
Wild Corrida
Zombie Apocalypse
Battle for the Throne
Bounty Hunters
Capital City Derby
Casino Heist
Fairy in Wonderland
Odd One Out
Planet Power
Shaolin Crew

Wachezaji watashindana kwa mfumo wa pointi ambapo kila dau la jumla ya TZS 2,500 litatoa pointi 2. Dau la chini kwa kila mzunguko kwa promosheni hii ni TZS 400.

Kulingana na msimamo wa mwisho, wachezaji 40 watazawadiwa pesa taslimu na mizunguko ya bure kucheza kwenye kasino ya mtandaoni kama ifuatavyo:

Nafasi ya 1 – TSH 1,250,000
Nafasi ya 2 - TSH 750,000
Nafasi ya 3 – TSH 250,000
Nafasi ya 4 na 5 - TSH 125,000
Nafasi ya 6 mpaka 10 – Mizunguko 300 ya bure kwenye sloti ya PIA
Nafasi ya 11 mpaka 20 - Mizunguko 200 ya bure kwenye sloti ya PIA
Nafasi ya 21. mpaka 30 - Mizunguko 100 ya bure kwenye sloti ya PIA
Nafasi ya 31. mpaka 40 - Mizunguko 50 ya bure kwenye sloti ya PIA

Ushindi utakaotokana na Mizunguko ya bure utahitaji kuzungushwa mara 60x (kwa mfano, ukishinda TZS 10,000 kwenye Mizunguko ya bure, utahitaji kucheza TZS 600,000 kwenye mchezo uleule ili kuhamisha ushindi wako kwenye akaunti ya pesa halisi).

Taarifa kuhusu malipo ya juu kwa kila Kundi la Mizunguko ya bure, washindi watapokea taarifa ambayo itatumwa kwao si zaidi ya saa 13:00 AM tarehe 03.05.2024.
KAMPUNI bingwa kabisa ya michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet imeing’arisha kata ya Makongo jijini Dar-es-salaam baada ya kufika kwenye eneo hilo na kutoa vifaa vya usafi.

Mara kwa mara mabingwa hao wa michezo ya kubashiri wamekua wakihakikisha wanarudisha fadhila kwenye jamii yao ambayo imewazunguka, Leo imekua ni zamu ya eneo la Makongo jijini Dar-es-salaam ambao ndio wamekua wanufaika.

Meridianbet wamegawa matoroli, Mafagio, pamoja na Reflectors kwajili ya kuhakikisha wanaimarisha usafi katika eneo hilo la Makongo kata ya Mlalakua, Hili limekua zoezi endelevu kua kwa kampuni hiyo katika kuhakikisha wanaiunga mkono serikali katika juhudi za kuweka mazingira safi.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko kutoka Meridianbet Bi Nancy Ingram ndio aliyeongeza zoezi hilo zima la ugawaji wa vifaa hivo”Kwanza kabisa nishukuru kwa mapokezi yenu mazuri mliyotupatia, Lakini jambo muhimu zaidi ni kuja hapa kugawa vifaa hivi vya usafi kwajili ya kuhakikisha usafi unaimarishwa mara dufu na hii tunaungana na serikali yetu pendwa ambayo inapambana kuhakikisha mazingira yapo safi”

Suka mkeka wako kwenye michezo mikali itakayopigwa leo kwenye michuano ya Uefa Europa League na Uefa Conference League. Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Wakati huohuo wakazi wa eneo hilo wameonekana kufurahishwa na jambo ambalo limefanywa na uongozi wa Meridianbet, Huku moja ya viongozi wa eneo hilo akitoa shukrani zake za dhati kwa mabingwa hao wa kubashiri na kutoa wito wa makampuni mengine kuiga mfano wa Meridianbet.



Na; Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuyapa kipaumbele masuala ya maendeleo ya vijana nchini.

Aidha, Mhe. Katambi amesema vijana ni nguvu kazi ya taifa, hivyo kuwezesha kundi hilo kunatoa fursa kubwa ya kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kuwafanya vijana kuwa chachu kwa maendeleo ya nchi.

Ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP)” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Vile vile, Naibu Waziri Katambi amesema serikali imeboresha mwongozo wa utoaji mikopo kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana ambapo kwa sasa mfuko huo unatoa mikopo kwa kijana mmoja mmoja, ambapo maboresho hayo yatawawezesha vijana walio katika sekta isiyo rasmi na wahitimu wa vyuo kujiajiri kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali.

Kwa upande wengine, Mhe. Katambi amesema programu ya Safeguard Young People ni fursa kwa vijana kujikwamua na changamoto za kijamii na kiuchumi, hivyo amehamasisha ushirikiano katika utekelezaji wa programu hiyo ili kufikia malengo na kuleta mabadiliko chanya kwa vijana.

Naye, Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot amesema ni wakati wa kutambua mchango wa vijana katika kukuza maendeleo ya taifa. Aidha, ameongeza kuwa serikali ya Uswisi itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza programu hiyo ya SYP kwa lengo la kuwaondolea vijana changamoto za kiafya, kiuchumi, kisaikolojia na kijamii.

Akizungumza mmoja wa wanufaika amesema programu hiyo imewasaidia vijana kujitambu, kijithamini na kuwa na uthubutu katika kufanya maamuzi sahihi.

Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana “Safeguard Young People (SYP)” inalenga kuboresha huduma za afya, elimu ya afya kwa vijana, kuongeza ushirikishwaji wa vijana katika ngazi za maamuzi na pia kuwaunganisha vijana na fursa za kujipatia ujuzi na kipato.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II)” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II)” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot akieleza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II)” iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Tanzania, Mark Shreiner akieleza jambo kuhusu utekelezaji wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP)” wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (kulia) akizindua rasmi Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II)”. Wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Zanzibar, Bw. sahib Mohamed na Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot (wa pili kutoka kushoto).
Mmoja wa Kijana aliyeshiriki tukio la uzinduzi wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II), Getrude Clement akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.

Wasanii wa muziki wa kizazikipya Ben Pol, Phina na Tommy Flavor wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Programu ya Mpango wa Ulinzi wa Vijana Awamu ya Pili “Safeguard Young People (SYP II), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Tanzania, Mark Shreiner (kulia). Katikati ni Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot.

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
IKIWA wikendi inaanza leo hii hapo baadae ligi mbalimbali zinatarajiwa kupigwa kuanzia kule Ujerumani mpaka Italia huku meridianbet wakikupa nafasi kubwa za kupiga maokoto ukisuka jamvi lako na kubashiri nao. Ingia sasa meridianbet ushinde pesa.

LALIGA leo itapigwa mechi moja majira ya saa 4:00 usiku ambapo Athletic Bilbao atakuwa mwenyeji wa Granada. Bilbao yupo nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi na mgeni wake yupo nafasi ya 19 mkiani kabisa. Mara ya mwisho kukutana walitoshana nguvu. Je leo hii nani ataondoka na ushindi? Mechi hii imepewa ODDS 1.22 kwa mwenyeji na 12.74 kwa mgeni. Suka jamvi hapa.

Kumbuka kucheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni ambayo inatolewa ndani ya meridianbet kama vile Poker, Roullette, Aviator, Rockertman, Keno, Sloti na mingine kibao. Ingia mchezoni na ucheze sasa.

Ligi nyingine ambayo itaendelea Ijumaa ya Leo ni SERIE A ambapo saa 1:30 kutakuw ana mtanange mzito kabisa kati ya Genoa dhidi ya Lazio ambaye yupo nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi huku mwenyeji akiwa nafasi ya 12. Tofauti ya pointi kati yao ni 10 pekee ambapo mechi ya mwisho kukutana kwenye ligi, Genoa lishinda. Mechi hii imepewa ODDS 2.99 kwa 2.50. Wewe leo hii unamdhamini nani kukupa pesa? Jisajili sasa.

Juventus chini ya Allegri baada ya kulazimishwa sare mechi iliyopita, leo hii atakuwa ugenini kupepetana dhidi ya Cagliari Calcio katika Unipol Domus huku Meridianbet wakimpa nafasi kubwa ya kushinda Juve kwa ODDS 1.76 kwa 4.90. Ikumbukwe kuwa mwenyeji hayupo nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi iliyopita kutoa sare. Je leo hii anaweza pata pointi 3 akiwa nyumbani?. Tengeneza mkeka wako hapa.

Vilevile bila kukosa utamu wa BUNDESLIGA leo hii kuna mechi ya kusisimua vilivyo ambapo Eintracht Frankfurt atamkaribisha nyumbani kwake Augsburg huku timu hizo zikiwa zinafuatan kwenye msimamo wa ligi yaani wa 6 kwa wa 7. Wamepishana pointi 3 tuu. Mara ya mwisho kukutana, Augsburg alishinda. Je Frankfurt atalipa kisasi kwa kushinda. Bashiri mechi hii ambayo ina machaguo zaidi ya 1000, ndani ya Meridianbet.

Tukimalizia na ligi kuu ya Ufaransa leo hii, LIGUE 1 napo ni mechi moja Ijumaa ya leo OGC Nice atakipiga dhidi ya FC Lorient saa 4:00 usiku huku wakitoshana nguvu mechi ya mwisho kukutana. Meridianbet wamempendelea Nice kushinda kwa ODDS 1.50 kwa 6.07. Ikumbukwe kuwa mwenyeji yupo nafasi ya 5 kwa 16. Beti sasa.

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

KAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation wamekabidhi mitungi ya gesi ya kupikia ya Oryx 50 kwa wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kati ya mitungi  1000  inayotarajiwa kukabidhiwa kwa wauguzi na madaktari katika mikoa 10 nchini .

Akizungumza wakati wakisaini makubaliano ya ushirikiano yaliyofanyika katika hospitali ya rufaa ya Mwananyama, Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite amesema makubaliano walioingia baina ys kampuni hiyo na taasisi ya Doris Mollel ni kusaidia kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa watanzania.

Aidha amesema katika kampeni hiyo ya kuwezesha watanzania kuingia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia, mpaka sasa tayari wameshatoa mitungi kwa wananchi zaidi ya elfu 32 ili kusaidia lengo la kufikia asilimia 80 ya watumiaji wa nishati safi.

Amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia inasaidia kuondoa hatari za kiafya kwa watumiaji wa kuni na mkaa kama nishati ya kupikia lakini pia hatari za kimazingira na ustawi wa jamii.

"Takribani watu 33,000 wanapoteza maisha nchini Tanzania kwa maradhi yanayotokana na kuvuta moshi unaotokana na mkaa au kuni hiyo ndio sababu ya Oryx gas kuja na suluhisho la kuwahamasisha wananchi kutumia gesi kwa matumizi ya kupikia", amesema Benoite

Ameeleza kuwa matumizi ya gesi yanaepusha wamama na watoto kuumika kubeba kuni hivyo kuepuka kujeuriwa na wanyama wakali wakiwa katika harakati za kutafuta kuni pia kuimarisha maisha ya wanawake na kuwalinda dhidi ya vitendo vya udhalilishaji.

“Kuanzia mwezi wa saba mwaka 2021 tumekuwa mstari wa mbele kuunga mkono utekelezaji wa mkakati wa serikali uliopewa nguvu na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania , Dk. Samia Suluhu Hassan kwa lengo kwamba ifikapo mwaka 2033 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia”, ameeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel amesema katika makubaliano waliosaini na oryxy watawafikia waguzi elfu moja ambapo watawapa mitungi na majiko ya gesi kama mabalozi kwa kina mama waweze kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni programu ya miaka miwili.

Amesema mitungi hiyo itakwenda kwa wauguzi walioko maeneo magumu ambapo watakuwa wanawatembelea kwenye vituo vya afya na zahanati ili kuweza kuwafikia wafanyakazi ambao ni wauguzi wanaofanya kazi kubwa ya kuokoa maisha hususani ya mama na mtoto.

Wakati huo huo Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala  Dk.Zavery Benela ameeleza kwamba hospitali hiyo  inakabiliwa na ongezeko la wagonjwa wa mifumo ya hewa.

Amefafanua kati ya wagonjwa wa nje 500 wanaofika kuonwa na madaktari bingwa asilimia 30 ya wagonjwa hao ni wa matatizo ya mfumo wa hali ya hewa unaosababishwa na hali ya hewa pamoja na mazingira ya kuandaa chakula kutokna na kuni na mkaa.

Aidha Dokta Benela amesema magonjwa ya mfumo wa hali wa hewa  yamekuwa changamoto hasa kwa watu wazima na watoto.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel akisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Kampuni ya Oryx Gas kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini na Taasisi ya Doris Mollel kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya makubalinao na Kampuni ya Oryx Gas kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel (katikati) akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya makubalinao na Kampuni ya Oryx Gas kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala mkoani Dar es Salaam  Dk.Zavery Benela akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini na Taasisi ya Doris Mollel kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel wakionesha mkataba waliosaini  kwaajili ya kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Oryx mmoja wa wauguzi katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini makubalino kati ya kampuni ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite  akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mtungi wa kupikia wa gesi ya Oryx kwa wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala katika hafla ya utiaji saini kati ya kampuni ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.


Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala wakifuatilia hafla ya utiaji saini kati ya kampuni ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


Wahitimu wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC), kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uganda (UCAA) wamekumbushwa kwamba kusoma hakuishii darasani pekee, mengine wataendelea kujifunza maofisini mwao wakati wanafanya kazi husika kwa vitendo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege TCAA Bi Flora Alphonce aliyekuwa mgeni rasmi Aprili 19, 2024 wakati wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance). Na kuongeza kuwa anaishukuru UCAA kwa kuendelea kukiamini chuo cha CATC na kuendelea kuleta watalaam wake kwa mafunzo.

Bi Flora aliwafahamisha wahitimu hao kwamba chuo cha CATC ndani ya kipindi cha miaka mitatu ijayo kitakuwa na majengo na vifaa vya kisasa ambavyo vitaongeza tija na kuleta utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza hapa na pale kufuatia Serikali ya Tanzania kutenga Shilingi bilioni 78 kwa ajili ya mradi huo.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha CATC Bw.Aristid Kanje alisema amefurahishwa na kuwapongeza wahitimu hao wote kwa kumaliza kozi zao kwa ufaulu wa juu. Na kuongeza kuwa ni vugumu kumlazimisha mtu kupata maarifa, kwani maarifa yanapatikana kwa kuwa na hamu ya kuyapokea.

Wahitimu hao watano kutoka UCAA walifanya kozi mbili kwa muda wa wiki 12, awali kabla ya mahali wahitimu hao walipatiwa semina juu ya umuhimu wa masuala ya kiafya na namna yanavyoweza kuathiri waongoza ndege katika majukumu yao kutoka kwa Daktari Concethar Mushi.

Akitoa salamu za shukran kiongozi wa darasa hilo kwa niaba ya wenzake Bw. Erasmus Muhairwe aliishukuru CATC kwa ushirikiano iliyowapatia kwa muda wote wa kozi zao na kuwakumbusha wahitimu wenzake kwamba kwa kuhitimu kwao watu wana matarajio makubwa kwao hasa ya kutokufanya makosa.
Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege TCAA, Flora Alphonce akizungumza na wahitimu wa  mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akizungumza jambo pamoja kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akiwakabidhi vyeti pamoja na zawadi kwa  wahitimu wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole akizungumza na wahitimu wa  
mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC). 
Dkt. Concethar Mushi akitoa mafunzo kuhusu umuhimu wa masuala ya kiafya na namna yanavyoweza kuathiri waongoza ndege katika majukumu yao wakati wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Kiongozi wa darasa hilo kwa niaba ya wenzake Bw. Erasmus Muhairwe akishukuru CATC kwa ushirikiano iliyowapatia kwa muda wote wa kozi zao na kuwakumbusha wahitimu wenzake wakati wa 
mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Wahitimu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Uganda (UCAA) wakiwa kwenye mahafali hayo


Picha ya Pamoja
Serikali za Tanzania na Zambia zimefanikiwa kufuta kero nne kati ya kero 15 zilizokuwepo awali ili kurahisisha michakato ya biashara ya nchi hizo kutegemeana kibiashara.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar, Mhe. Omar Shaaban wakati wa kikao cha pamoja cha Mawaziri wa nchi zote mbili katika sekta hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Shaaban amesema kuwa kikao hicho ni utekelezaji wa maelekezo ya Wakuu wa nchi zote mbili Tanzania na Zambia ambao walikutana jijijni Lusaka mwezi Oktoba, 2023 ambapo miongoni mwa makubaliano ni pamoja na Mawaziri wa pande mbili wanaohusika wakae na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika nchi hizo.

“Tuliingia katika majadiliano haya tukiwaa na changamoto 15 na ndani ya siku tatu hizi tumeweza kutatua kabisa changamoto nne na katika hizo nne mbili zilikuwa upande wa Zambia na mbili zilikuwa Tanzania.Jambo la msingi wenzetu wa Zambia walikuwa wanashindwa 'ku-process' mizigo kwa haraka pale boda changamoto kubwa walikuwa hawana 'scanner', tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa 'scanner' kwa ajili yao. Na ilichukua muda mrefu kupokea lakini tunafuraha juzi wameandika barua kuwa wameipokea na wako tayari kwenda kuifunga”

Ameeleza kuwa Zambia kulikuwa na vizuizi vingi kutoka mpakani hadi kufika jijini Lusaka ambapo sasa vimepunguzwa kutoka 33 vilivyokuwepo awali mpaka 11.

“Kwa kweli ni hatua kubwa wenzetu wa Zambia wameweza kurahisisha mazingira ya biashara ndani ya nchi zetu. Kubwa lingine sio changamoto ya kibiashara ni maelekezo ya Wakuu wetu kuhakikisha tunaanzisha mchakato wa kutengeneza boda nyingine kule Kasesya ambayo itaunganisha nchi zetu hizi mbili ni hatua kubwa na kikao hiki kimethibitisha kwamba tayari timu imeshaandaliwa michakato kuanza” amebainisha.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Zambia, Mhe. Chipoka Mulenga amesema kuwa changamoto zilizotauliwa zina maslahi kwa nchi zote mbili.

“Tumetatua baadhi ya changamoto zilizokuwa hazina maslahi kwa nchi zetu zote mbili Tanzania na Zambia kurahisisha ufanyikaji wa biashara ikiwa ni kuongeza wafanyakazi, na kutoa vizuizi vingi njiani ambavyo vilikuwa vinasababisha foleni”

Tumetatua changamoto ya 'scana' ambayo kutokana na mahusiano ya kidiplomasia tumepewa kutoka Tanzania. Tunaamini changamoto zilizobaki mawaziri wetu wakikutana watatatua zaidi kwa maslahi mapana ya nchi zetu ili kurahisisha ufanyikaji wa biashara” amesisistiza.












Top News