Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetoa mafunzo Wanafunzi wa Shahada na Shahada ya Uzamili wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) hii ikiwa ni mwendelezo wa kutoa elimu kwa umma hasa kwenye vyuo vinavyotoa masomo ya Ununuzi na Ugavi.

Akizungumza na Michuzi Blog, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee amesema Bodi hiyo imeendelea kuwapa mafunzo Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali wanaochukua kozi hiyo ya Ununuzi na Ugavi kuhusu shughuli zinazofanywa na Bodi, Usajili kwa njia ya mtandao pamoja na maadili na miiko ya taaluma hiyo.

Naye, Kaimu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Jonnes Lugoye ametoa shukrani kwa wafanyakazi wa PSPTB kwa kuweza kufika chuoni hapo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Bodi hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee akitoa maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi - DMI, Jonnes Lugoye akiwakaribisha wageni kutoka Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) walipofoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Bodi hiyo.
Afisa Ununuzi kutoka Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB),  Ally Yassin Mbarouk akitoa maelezo kuhusu namna ya kuongeza dhamani kwenye taaluma hiyo kwa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Afisa TEHAMA Mwandamizi kutoka PSPTB Elihuruma Eliufoo akitoa mada kuhusu namna ya mwanafunzi anavyoweza kujisajili kwenye mfumo wa Bodi (ORS) pamoja na kufanya mitihani ya Bodi wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) wakiuliza maswali kwa wafanyakazi wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) aliofika chuoni hapo kwa ajili ya kutoa elimu .
Baadhi ya wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) wakifuatilia mada kutoka kwa wafanyakazi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) waliofika chuoni hapo kwa akili ya kutoa elimu zinayohusu Bodi hiyo.
Kaimu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi - DMI, Jonnes Lugoye akiwakabidi wanafunzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) walioshinda zawadi akati wa mafunzo yaliyotolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) 
 Kaimu Mkuu wa Idara ya Sayansi na Menejimenti - DMI, Elinathan Blasius akitoa neno la shukrani kwa wafanyakazi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) waliofika chuoni hapo kwa akili ya kutoa elimu zinayohusu Bodi hiyo.


Picha za Pamoja

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Exim Bank, Stanley Kafu (wa tatu kutoka kushoto),akikabidhi seti ya vitanda kwa Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania - Moshi, SACP Ramadhani Mungi (wa tatu kutoka kulia), kama sehemu ya mchango wa Exim Bank katika jamii ikiwemo ulinzi na usalama wa Watanzania na mali zao ambapo makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 24 Aprili, 2024.


Benki ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule ya Jeshi la Polisi Tanzania iliyopo Moshi, mkoani Kilimanjaro kama sehemu ya mchango wa Exim Bank katika jamii ikiwemo ulinzi na usalama wa Watanzania na mali zao. 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Stanley Kafu alisema, “Kupitia mkakati wetu wa kurudisha kwa jamii unayojulikana kama Exim Cares na kama ishara ya mashirikiano yetu ya muda mrefu, tunayo furaha kuchangia vitanda 40 kwa Shule ya Jeshi la Polisi Tanzania ya hapa Moshi.” 

Exim bank inaamini mchango huu utasaidia kuboresha mazingira ya mafunzo kwa maafisa wa polisi ili wapate mafunzo bora yatakayochangia kuboresha jeshi la polisi katika majukumu yake ya kuwahakikishia ulinzi na usalama Watanzania wote na mali zao. 

“Ushirikiano wetu na Jeshi la Polisi haujaanza leo, mwaka jana Exim Bank tumeingia makubaliano na Jeshi la Polisi Tanzania yenye lengo la kuwezesha utoaji wa mikopo ya masharti nafuu kwa askari polisi kupitia programu yetu maalumu ijulikanayo kama ‘Wafanyakazi Loan’”, aliongeza Kafu. 

Akifafanua zaidi Kafu alisema kuwa kupitia ‘Wafanyakazi Loan’, askari polisi wanaweza kukopa kuanzia shilingi milioni moja hadi shilingi milioni 160 ambayo inaweza kurejeshwa kati ya miezi 6 hadi miezi 96 kutegemeana na ahadi ya mkopaji ambayo inaweza kutumika kutekeleza ndoto za mkopaji ikiwa ni pamoja kupata mkopo wa nyumba, kununua magari na kulipia ada ya masomo ili kujiendeleza kielimu.

Exim Bank imedhamiria kuendelea kushirikiana na serikali na vyombo vyake vya usalama kuhakikisha ustawi unakuwepo katika sekta mbalimbali ikiwemo usalama, afya, uchumi, na kuboresha maisha ya Watanzania wote bila ubaguzi wa namna yoyote.


Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wamepongezwa kwa kuandaa vyema mkutano mkuu wa mwaka jambo linalowapa fursa ya kujadili kwa mapana taarifa mbalimbali za kiutendaji ndani ya chama na hatimaye kuandaa mapendekezo yatakayoweza kuleta tija ndani ya TCAA.

Hayo yameelezwa leo Aprili 25, 2024 na Mkurugenzi wa Sheria wa TCAA Bi. Maria Makalla wakati wa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) uliofanyikia Mkoani Morogoro.

"Nimefarijika kuona kwamba ninyi kama viongozi wa chama cha wafanyakazi mnatambua wajibu wenu kama ulivyoainishwa katika sheria ya Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 62(4), na kwamba mnafanya jitihada zote kuhakikisha mnafuata taratibu za vikao halali,mnapopitisha mambo yenu. Nawapongeza pia kwa hili,"amesema Bi. Makalla

Kiongozi huyo amepongeza uongozi na wanachama wa TUGHE kwa kuandaa vyema mkutano huu wa mwaka jambo linalowapa fursa ya kujadili kwa mapana taarifa mbalimbali za kiutendaji ndani ya chama na hatimaye kuandaa mapendekezo yatakayoleta tija ndani ya taasisi.

Pia amesema TCAA imekuwa tulivu na hakuna migogoro kwa kipindi chote hiki hii yote ni matokeo ya uwepo wa daraja zuri la kuwakilisha wafanyakazi, jukwaa la kuwasemea, kutokana na kuwepo na misingi imara.

Mbali na hayo, Bi. Makalla aliwakumbusha kuwa wao ni daraja zuri la kuwakilisha wafanyakazi na jukwaa la kuwasemea, yote haya yametokana na kuwepo na misingi imara iliyotengenezwa na TCAA.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la TCAA Jackline Ngoda, amesema lengo la kufanya kikao hicho ni kuwakumbusha watumishi wajibu wao katika utendaji ikiwa na kauli mbiu isemayo Maslahi bora ni kiunganishi na kichocheo cha ufanisi mahala pa kazi kwani kupitia kauli mbiu hiyo inakuwa kama kipimo cha cha namna gani TCAA inaweza kuleta ufanisi katika kazi baada ya mambo ya maslahi kuwa mazuri.

Kwa upande wa Katibu wa TUGHE mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaura ametoa wito kwa wanachama wa TUGHE tawi la TCAA kuwa wavumilivu pindi wanapowasilisha hoja zao na pia uvumilivu huo usiwakatishe tamaa waendelee kuwasilisha hoja zao na wasikae nazo.

Kwa upande wa Katibu wa Tughe tawi la TCAA Bw. Shukuru Mhina amesisitiza juu ya umuhimu wa mafunzo kwa viongozi wapya wa TUGHE TCAA na kuongeza kuwa kupitia mafunzo ndio viongozi wanajengwa.

Mkurugenzi wa Sheria  kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Maria Makalla akizungumza wakati wa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa cha Chama cha Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) uliofanyika Mkoani Morogoro
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bi. Jackline Ngoda akizungumza kuhusu namna wanavyoshirikiana na viongozi wa TCAA pamoja na kumkaribisha Mgeni rasmi.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula akitoa salamu za TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam  wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa cha Chama cha Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) uliofanyika Mkoani Morogoro.
Katibu wa TUGHE Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),Bw. Shukuru Mhina akifanywa utambulisho wa wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka wa TUGHE tawi la TCAA kwa Mgeni rasmi.
Mtoa mada kutoka TCAA Hamis Kisesa kuhusu masuala ya maadili kwenye mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) lililopo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma. Tarehe 25 Aprili 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye mara baada ya hafla ya Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) lililopo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma. Tarehe 25 Aprili 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,Mtendaji Mkuu wa UCSAF Justina Mashiba na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja watumishi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mara baada ya kuzindua jengo la Taasisi hiyo lililopo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma. Tarehe 25 Aprili 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) lililopo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma. Tarehe 25 Aprili 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka jiwe la msingi la Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) lililopo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma. Tarehe 25 Aprili 2024.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Msanifu Majengo Arch. Msuya Abdulkarim kuhusu Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wakati alipowasili kwaajili ya kuzindua jengo hilo lililopo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma. Tarehe 25 Aprili 2024.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa maagizo kwa Taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kuendelea kusimamia kwa karibu ujenzi wa minara ya mawasiliano na kuhakikisha vijiji ambavyo havina huduma za uhakika za mawasiliano ya simu vinapata mawasiliano.


Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo wakati wa uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) lililopo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma. Amesema ni muhimu kuhakikisha Wananchi wanapata mawasiliano ya uhakika wakati wote ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi hususan katika kipindi hiki ambapo huduma nyingi zinawezeshwa na huduma za mawasiliano.


Aidha Makamu wa Rais ameitaka UCSAF kuendelea kutekeleza miradi ya kuongeza uwezo wa minara kutoka teknolojia ya 2G kwenda 3G na 4G. Amesema huduma nyingi za jamii hivi sasa zinawezeshwa kwa kutumia intaneti ni muhimu kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma hiyo mijini na vijijini.


Vilevile Makamu wa Rais ameiagiza UCSAF kujipanga kuongeza misaada ya vifaa vya TEHAMA hususan kwenye shule za umma ili kuongeza hamasa kwa wanafunzi kupenda masomo ya TEHAMA na kukuza matumizi ya intaneti nchini. Ametoa wito kwa sekta binafsi na sekta ya umma kushirikiana na UCSAF kuongeza idadi ya shule zinazopokea huduma hiyo na vifaa vya TEHAMA ili kuwezesha watoto kujifunza kwa urahisi.


Halikadhalika ametoa wito kwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kushirikiana na wadau ikiwemo sekta binafsi kuona uwezekano wa kuiongezea UCSAF uwezo, ikiwemo fedha na rasilimali nyingine ili kuiwezesha kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo yasiyo na huduma ya televisheni na redio za hapa nchini. Amesema ni vema UCSAF iangalie uwezekano wa kuwezesha matangazo ya televisheni na redio kuwafikia wananchi kwa njia ya mtandao.


Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema kupitia UCSAF asilimia 98 ya wananchi waliopo katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mjini yasio na mvuto wa kibiashara wamenufaika na huduma za mawasiliano. Ameongeza kwamba wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini wamepata fursa ya kushiriki katika mageuzi ya kidijiti nchini kwa kuwa sehemu ya watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya mtandao.


Aidha Waziri Nape amesema sekta ya mawasiliano imeendelea kukua kwa kasi hapa nchini ambapo kufikia mwaka 2024 jumla ya laini za simu milioni 72 zimesajiliwa kulinganisha na laini za simu milioni 51 mwaka 2020. Pia amesema zaidi ya minara 600 hapa nchini inatumia huduma ya 5G.


Amesema kwa sasa ni muhimu kufanya uwekezaji wa namna ya kutengeneza vifaa vinavyotumia mtandao ikiwemo simu janja hapa nchini ili uwekezaji unaofanywa na serikali katika kuboresha mawasiliano kuendelea kuwa na tija.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji amesema kupitia UCSAF kwa kipindi kifupi jumla ya minara 47 imejengwa Zanzibar pamoja na ujenzi wa vituo 11 vya tehama Unguja na Pemba ambavyo imekua vikisaidia vijana kwa kiasi kikubwa.


Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ni Taasisi ya Serikali ambayo ina jukumu la kuhakikisha mawasiliano yanafikishwa katika maeneo ya vijijini na mjini yasio na mvuto wa kibishara. Mfuko huo hushirikiana na watoa huduma za mawasiliano katika kujenga minara inayowezesha upatikanaji wa mawasiliano ya simu pamoja na uimarishaji wa matangazo ya redio na televisheni.


Uzinduzi wa Jengo hilo ni shamrashamra kuelekea Miaka 60 ya Muungano.

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

25 Aprili 2024

Dodoma.

Top News