KLABU Ya Rotary Dar yaendelea Kuweka Mikakati ya kuchangia ufaulu wa Wanafunzi wa shule za Misingi kwa kuboresha Mazingira rafiki ya Kujisomea kwa kugawa Madawati na kutoa elimu ya Teknohama kwa Walimu.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jonas Rwegasira wakati akikabidhi Madawati 1000 kwa Shule tano za Msingi Wilaya ya Kinondoni yaliyofanyika Leo Aprili 20,2024 Shule ya Msingi Kisauke Jijini Dar es Salaam.

Rwegasira amesema Wadau kama Klabu ya Rotary ni watu ambao wamekuwa wakisaidia sana Serikali katika kuboresha Mazingira rafiki kwa Wanafunzi kujisomea kwa kugawa Madawati kwani Serikali imekuwa ikitafuta Wadau mbalimbali ambao watachochea ufaulu mzuri kwa Wanafunzi hao.

"Wadau hawa Rotary wameenda Kuandika historia nyingine ndani ya mioyo ya watoto hawa pamoja na Shule hizi tano ikiwemo Shule ya Msingi Mtakuja, Kisauke,Salasala,Kunduchi, pamoja na Shule ya Msingi Twiga kwani kila shule imekabidhiwa Madawati 200."

Mratibu wa mradi huo Ezra Kavana amesema Klabu hiyo ina lengo la kuboresha Mazingira mashuleni na mpango huo wa Madawati umeendelea kupewa ushirikiano na Klabu ya Rotary ya Vancouver ambapo Madawati hayo elfu 1000 yamegharimu pesa taslimu Milioni mia moja na ishirini na Saba.

Aidha ameongeza kuwa Klabu hiyo pia inalenga kupanda miti kwa wingi kwani sehemu kubwa ya Madawati hayo ni miti ambayo imekuwa ikikatawa hivyo Kuna umuhimu wa kupanda miti kwa wingi ili Madawati hayo yaendelee kuzalishwa kwa wingi.

"Kila dawati tunalolikabidhi tunahakikisha tunapanda miti miwili ambapo tayari tumeshatekeleza hilo kwa kupanda miti 2500 ."

Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kisauke Hamza Suleiman mepongeza Klabu hiyo kwa kuendelea kugawa Madawati kwa Shule za Misingi ili kuleta Ufaulu Mzuri Kwa Wilaya ya Kinondoni.

"Tunakwenda kutengeneza mazingira mazuri ya taaluma kwa watoto wetu madawati haya mia 200 yataenda kuleta chachu ya kuongeza ufaulu wa shule yetu."

Pia ameeleza kuwa bado shule hiyo inapitia changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa,ofisi za walimu pamoja na Matundu ya vyoo.

> Awapongeza wana Ruvuma kwa kujitoa kimasomaso kwa mapenzi ya dhati kwa CCM

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapiduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesisitiza dhamira ya Chama, chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wa CCM, Dk. SAMIA Suluhu Hassan, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kukirudisha kwa wanachama, kupitia kwa mabalozi, itatekelezwa kwa vitendo.

Akizungumza na viongozi wa CCM wa ngazi mbalimbali kuanzia mashina hadi mkoa, Mkoa wa Ruvuma, kwenye mkutano wa ndani uliofanyika Ukumbi wa Parokia ya Bombambili, mjini Songea, Aprili 20, 2024, Dk Nchimbi amesema kuwa kutambua ukubwa wa nafasi ya Balozi na Shina ni kutambua dhamana kubwa waliyonayo wanachama kwa Chama chao Cha CCM.

Aidha, Dk. Nchimbi pia amewapongeza na kuwashukuru wananchi na viongozi wa mkoa wa Ruvuma kwa mapokezi nakubwa yaliyoonesha imani kubwa waliyonayo kwa Chama Cha Mapinduzi.

Mkutano huo uliojumuisha Viongozi mbalimbali wa Chama , Serikali, Dini, Wazee na Taaasisi zisizo za kiserikali, Balozi Dkt. Nchimbi amewapongeza wana Ruvuma kwa kushinda chaguzi zote zilizopita siku za hivi karibuni hali inayozidi kuonesha imani yao kwa CCM haijatetereka na kutoa pongezi kwa ushirikiano wao mkubwa wa chama na serikali.

" Hongereni kwa uhusiano mkubwa na mzuri wa chama na serikali na huu ndio unapelekea utekelezaji wa ilani kutekelezwa kwa kasi. "

Aidha, Balozi Dkt. Nchimbi amehimiza juu ya heshima kwa mabalozi kwa kuwa ndio msingi imara wa CCM.

" Nilipokuwa mbunge wenu hakuna watu ambao niliwapa heshima kubwa kama mabalozi ssbabu najua mabalozi ndio msingu wa shina la CCM na ndio maana tumeelekeza nguvu kubwa kuhakikisha Nchi nzima viongozi wote wanatambua hakuna viongozi wakubwa zaidi ya mabalozi na kwa mantiki hiyo chama kitarudi kwa wanachama wengine na sisi tunaochaguliwa na kuteuliwa ni watumishi tu kwa hao wanachama "

Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk Nchimbi, akiambatana na Katibu wa NEC ya CCM Taifa, Oganaizesheni, Ndugu Issa Haji Usi Gavu na Katibu wa NEC ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makala, ameingia Mkoa wa Ruvuma Aprili 19, 2024, kwa ajili ya ziara yake katika maeneo mbalimbali mkoani humo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara aliyoanzia mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.













Na Mwandishi Wetu,Same

KATIBU Tawala wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Upendo Wella amesema katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanikiwa kusimamia masuala ya muungano kwa ufanisi mkubwa.

Hiyo imesababisha kuimarika kwa utaifa, umoja, amani, utulivu, na hali ya maisha ya wananchi kutokana na ukuaji wa uchumi wa pande zote mbili za Muungano.

Wella ametoa kauli hiyo alipowaongoza wananchi katika upandaji miti ikiwa ni shamshara za sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Zoezi hilo lilifanyika leo katika Kata ya Kisima, wilayani Same.

Aidha,amewahimiza wananchi wa wilaya ya Same kuendeleza utamaduni wa kupanda miti sehemu mbalimbali, hasa kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha kwa wingi, ili miti iweze kustawi vyema na kuepukana na hali ya ukame.

Pia amewaomba walimu wote kuhakikisha kila mwanafunzi anapanda mti katika mazingira ya shule na kusimamia ukuaji na utunzaji wa mti huo, pamoja na kuhimiza upandaji miti majumbani, katika taasisi za serikali na zisizo za serikali, ili baadaye wilaya iwe na rutuba nzuri ya miti.

Katibu huyo pia amewaalika wananchi kushiriki katika mkesha wa kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utakaofanyika tarehe 25, ambapo kutakuwa na matangazo ya moja kwa moja ya hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia channel ya TBC.

Amesema kwamba Aprili 26 ndio itakuwa kilele cha Siku ya sherehe za Muungano, wananchi watashiriki katika majadiliano ya masuala mbalimbali yanayoweza kujenga taifa.



Kampuni ya mabingwa wa vifaa vya kielektroniki Haier wamefanya mkutano wa uzinduzi wa bidhaa za viyoyozi (AC) katika ukumbi wa Hyatt regency, the kilimanjaro hotel, jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 19.04.2024.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau na watumiaji wa bidhaa za kielekroniki wakiwemo wataalam mbalimbali wa ujenzi, wasanifu majengo, wafanyabiashara wa vifaa vya kilektroniki, taasisi mbalimbali za kiserikali na wafanyakazi wa makampuni ya GSM GROUP pamoja na Haier.

Kampuni ya Haier iliingia rasmi ubia na kampuni ya GSM GROUP mnamo mwanzoni mwa mwaka 2023. Kwa kipindi hiki chote, kampuni ya Haier ikishirikiana na GSM GROUP imekuwa ikihakikisha inaleta bidhaa ambazo zina tija sokoni. ‘Tangu uanzishwaji wa kampuni ya Haier, Tanzania, tumekuwa tukijitahidi kuangalia matakwa ya soko na kuhakikisha tunaboresha huduma na ufanisi wa bidhaa zetu kwa watumiaji’ Alisema haya meneja biashara, Bw. Ibrahim Kiongozi.

Sambamba na uzinduzi huo wageni waalikwa walipata nafasi ya kujionea bidhaa hizo mpya na kupata mafunzo mafupi kwa ajili ya matumizi ya vifaa hivyo. ‘Sifa kubwa za bidhaa hizi za AC ni mfumo wake imara na wa kisasa unaosababisha matumizi kidogo ya umeme pamoja na uwezo mkubwa wa utendaji kazi katika kutoa hali ya ubaridi kwa haraka.’ Aliongezea Meneja mkuu kutoka Haier, Bw. Leon Liuchi.

Ushirikiano wa makampuni ya GSM Group na Haier unaleta tija katika ukuaji wa uchumi wa nchi kutokana na mapato na ajira mbali mbali zinazotolewa. ‘Katika kuhakikisha kwamba GSM GROUP ikishirikiana na Haier inaungana na juhudi za kukuza uchumi wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan, tunajitahidi kushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii zikiwemo udhamini wetu katika michezo kupitia timu mbali mbali za mpira wa miguu kama Young Africans Sports Club (Yanga), Coastal Union, Singida Fountain Gate na Ihefu’ Alisisitiza, Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya GSM Group, Mr. Benson Mahenya.

Vile vile katika mkutano huo, wageni waalikwa walipata fursa ya kujishindia bidhaa za jokofu (fridge) pamoja na kiyoyozi (AC).

Uongozi wa makampuni ya GSM GROUP na Haier ulitoa shukrani kwa wadau mbali mbali walioshiriki pamoja na kuahidi kuendeleza ubunifu kwa matoleo ya mbeleni ya bidhaa za kielektroniki Tanzania. Vilevile Haier imethibitisha kuongeza mpango kazi katika kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa hizo mikoa yote ya Tanzania.
Bw. Mohamed Ally, mkurugenzi wa miradi wa kampuni ya GSM Tanzania (kushoto) akimkabidhi zawadi ya Kiyoyozi mmoja wa wadau wa vifaa vya kielektroniki vya Haier



Kutoka kushoto Bw. Yang, meneja masoko Haier Africa Bw. Kevin, meneja wa bidhaa za rejareja Haier Africa Bw. Mohamed Ally, Mkurugenzi wa miradi wa kampuni ya GSM Tanzania,Mkurugenzi mkuu wa makampuni ya GSM GROUP, Bw. Benson Mahenya (katikati) Bw. Bai, meneja wa bidhaa za AC Bw. Ibrahim Kiongozi, meneja biashara wa Haier Tanzania Bw. John Nguya, mkuu wa biashara kitengo cha GSM Property.


-Yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Na Mwandishi Wetu

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewaonya watu wanaojenga miradi bila kupata Cheti cha Tathmini ya Mazingira EIA kwenye baraza hilo kwamba wanakabiliwa na faini ya shilingi milioni kumi.

Hayo yamesemwa leo Aprili 19,1024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na msosholojia wa Baraza hilo Suzan Chawe alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa maonyesho ya kumbukumbu ya miaka 60 ya Muungano

Maonyesho hayo yamefunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Abdulla.

Suzan amesema NEMC imekuwa ikifanya kaguzi za mara kwa mara na wale wanaokutwa wamejenga miradi bila EIA wamekuwa wakitozwa faidi inayofikia hadi shilingi milioni kumi

Amesema NEMC imekuwa ikiendesha kampeni ya elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa EIA kwa wanaojenga miradi kabla ya kufanya kaguzi na kuwatoza faini.

"Mfano unaweza kukuta mtu anajenga kituo cha mafuta kwenye makazi ya watu jambo ambalo ni hatari kama ikitokea dharura tunaweza kupoteza maisha ya watu kwa hiyo tunasisitiza umuhimu wa EIA kabla ya kuanza shughuli za ujenzi," amesema Suzan

Amesema kwa miaka 60 ya Muungano NEMC inajivunia mambo mengi ikiwemo kupigania ustawi wa mazingira kwa kuhakikisha miti mingi inapandwa na kulindwa.

Suzan amesema Baraza limefanya maboresho ya mifumo yake ya mapito ya taarifa za tathmini na kaguzi za athari kwa mazingira kwa kuimarisha miundombinu ya TEHAMA kulingana na matakwa ya mfumo wa serikali mtandao.

Amesema NEMC inasimamia miradi inayofanya tathmini ya athari kwa mazingira kwa njia ya kielektroniki kupitia usajili wa mtandaoni njia ambayo inamuwezesha mwekezaji kuanzisha mchakato wa kupata cheti cha EIA kupitia mfumo wa usimamizi wa mradi ( Project Management System).

"Kabla ya kufanya usajili wa mradi mwekezaji anatakiwa kuhakikisha mawazo ya wadau yamepatikana kuhusu utekelezaji wa mradi kwenye eneo husika" amesema Suzan.

 

Maofisa wa BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), wakihudumia watu waliofika leo kwenye viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam kwenye maonyesho ya miaka 60 ya ya Muungano. Maonyesho hayo yamefinguliwa leo Aprili 19,2024 na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Abdulla


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, KIGOMA

JAJI Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma, amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema lengo la vyombo vyote vya dola ni ustawi wa wananchi.

Mhe. Jaji Mkuu, ameyasema hayo mjini Kigoma Aprili 19, 2024, wakati akifungua  Kikao Kazi kati ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Mahakama ya Tanzania na Watendaji wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) mjini Kigoma lengo kuu likiwa ni kujenga uelewa wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.

“WCF ni Mfuko unaogusa ustawi wa wananchi, kwasababu unaweza kuwa unamtegemea mama, kaka, bahati mbaya akapata ajali akafariki, hapa ustawi wa familia unaweza kutoweka, kama hakuna Mfuko unaoweza kubeba hilo jukumu, kwa hivyo huu Mfuko ni muhimu mno mno.” Amebainisha Mhe. Profesa Juma.

Aidha Mhe. Profesa Juma amehimiza umakini na uadilifu katika utekelezaji wa sheria hiyo ya Fidia kwa Wafanyakazi.

“Ukosefu wa umakini, udanganyifu vyote vimechangia kuua mifuko ambayo ilikuwa na malengo mazuri sana. Tusipokuwa waangalifu, mfuko huu wa WCF vile vile unaweza kukumbana na tatizo hili. Tukielewa vizuri mantiki ya kuanzishwa mfuko huu tutaufanya uwe endelevu na himilivu,” amesema.

Aidha Mhe. Jaji Mkuu ameipongeza WCF kwa kupiga hatua kubwa katika matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu yake na kukumbusha umuhimu wa mifumo ya taasisi za umma kusomana ili kurahisisha utoaji wa huduma.

“Ifike mahala mfanyakazi anapowasilisha madai yake WCF, mfumo mzima uwe unaelewa kwamba mfanyakazi fulani amepata ajali kazini au amefariki. Mifumo ya serikali ikiweza kutambuana pia itasaidia sana kuziba mianya ya udanganyifu.” Alisisitiza.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Emmanuel Humba, amemuhakikishia Mhe. Jaji Mkuu kwamba Mfuko unaendeshwa kwa ufanisi mkubwa na umepata mafanikio makubwa katika kutekeleza malengo yake.

“Malipo ya fidia kwa Wafanyakazi yameongeza kutoka TZS 3.88 bilioni Kwa mwaka 2016/2017 hadi kufikia TZS 23.58 bilioni kwa mwaka 2022/2023. Hili ni ongezeko kubwa la malipo ya fidia kulinganisha na kiasi cha TZS 250 milioni zilizokuwa zikilipwa na Waajiri kwa mwaka kabla ya kuanza Mfuko.” Amefafanua Bw. Humba.

Aidha, michango ya Waajiri iliyokusanywa imeongezeka kutoka TZS 68.40 bilioni Kwa mwaka 2015/2016 hadi kufikia TZS 86. 48 bilioni kwa mwaka 2022/2023, amesema Bw. Humba.

“Faida inayotokana na uwekezaji ya fedha zilizobaki baada ya kulipa mafao imeongezeka kutoka TZS 1.60 bilioni Kwa mwaka 2015/2016 hadi kufikia TZS 102.43 bilioni kwa mwaka 2022/2023, lakini pia   thamani ya Mfuko imeongezeka kutoka TZS 65.68 bilioni Kwa mwaka 2015/2016 hadi kufikia TZS 602.78 bilioni kwa mwaka 2022/2023.” Amefafanua.

Kuhusu ustahamilivu wa Mfuko katika kutekeleza majukumu yake, Mwenyekiti huyo wa Bodi amesema kuwa tathmnini ya uhai na uendelevu wa Mfuko iliofanywa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) inaonesha kwamba Mfuko unauhimilivu (Sustainability) kwa kipindi cha miaka 30 kuanzia mwaka wa tathmini 2022/2023.

Akizungumzia kuhusu nia ya kikao kazi hicho, Bw. Humba alibainisha kuwa pamoja na kwamba jukumu la kulipa fidia limekasimiwa kwenye Mfuko, Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi imeweka utaratibu na vyombo vya kushughulikia madai ya wanufaika pale wanapokuwa hawajaridhika na fidia iliyolipwa au maamuzi ya Mfuko yanayokinzana na matarajio yao.

Akifafanua zaisdi alisema, Sheria inamtambua Waziri Mwenye dhamana ya masuala ya kazi kuwa ni Mamlaka ya kwanza ya rufaa dhidi ya uamuzi wa Mfuko na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kuwa Mamlaka ya mwisho ya rufaa.

“Kutokana na hitaji hili muhimu la kisheria, Bodi ya Wadhamini ya WCF, Menejimenti ya Mfuko pamoja na Watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi waliona kuna hitaji la kufanya vikao kazi kwa lengo la kubadilisha uzoefu, kujenga uelewa wa pamoja na kubainisha maeneo ya sheria yanayohitaji maboresho kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kutekeleza Sheria hiyo.” Alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma ameeleza kuwa ushirikiano baina ya Mfuko na Mahakama ni muhimu kwa vile kuna maeneo mengi ambayo Mfuko unakutana na Mahakama katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Sisi kama WCF shughuli zetu hazikamiliki bila ya uwepo wa shughuli za Mahakama. Kwa mfano katika kushughulikia masuala yanayohusu mirathi, Mfuko hutegemea maamuzi ya Mahakama.” Alisema Dkt. Mduma.

Awali, akizungumza kabla ya kumkaribisha Jaji Mkuu kufungua Kikao Kazi hicho, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambia alisema kuwa kumekuwa na vikao kazi vitano ambavyo vimefanyika baina ya Mahakama, WCF na Watendaji wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) huko Bagamoyo, Mwanza, Arusha, Songea na Kigoma.

Alibainisha kuwa jumla ya Viongozi na watumishi 290 wameshiriki katika Vikao Kazi hivyo, wakiwemo Majaji 70, Naibu Wasajili 33, Watendaji 11, Wadau 48, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi 32 na zaidi ya watumishi wa Mahakama 96.

JAJI Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi baina ya WCF, Mahakama na CMA mjini Kigoma Aprili 19, 2024
JAJI Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi baina ya WCF, Mahakama na CMA mjini Kigoma Aprili 19, 2024
Kikao kikiendelea
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Emmanuel Humba, akieleza mafanikio mbalimbali ambayo Mfuko umeyapata tangu kuanzishwa kwake
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma, akieleza jinsi Mfuko unavyotekeleza kwa vitendo Tunu (Core value) ya Ushirikiano na taasisi zingine ikiwemo Mahakama.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambia, akkeleza matokeo ya vikao kazi hivyo katika kuboresha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi hicho.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi hicho.
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, yaya aliwasilisha mada iliyoelezea mambo mbalimbali ikiwemo jinsi tathmini za ulemavu zinavyofanyika ikiwa ni seehemu ya mchakato wa kulipa fidia.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw, Anselim Peter, yeye aliyoa mada kuhusu uendeshaji wa shughuli za Mfuko, ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kuwasilisha madai.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, WCF, Bw. Abrahamu Siyovelwa, akitoa mada kuhusu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Kamishna wa Kazi, Bi. Suzan Mkangwa akiwa ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika kikao hicho.







Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito kwa wananchi wa Tanzania kuendelea kuulinda Muungano.

Hayo ameyasema leo Aprili,19,2024 jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Taasisi za kimuungano ambapo amesema kuwa huwezi kuutenganisha umoja wa Watanzania wale wa Visiwani na Bara kwa kuwa tayari watu hawa wameungana kwa damu.

"Tangu enzi za wazee wetu watu wa visiwani wanaishi bara, wameoa bara wamejukuu bara hivyo hivyo wa bara wanaishi na wale wa bara wanaishi visiwani wameona, wamejukuu watu hawa huwezi kuwatenganisha" alisema Makamu wa pili wa Rais.

Amesema kuwa amefarijika kuona maonesho yaliyoandaliwa na Taasisi za kimuungano na kuwataka wananchi kufika kwenye maonesho hayo ili kujifunza zaidi kuhusu muungano.

Amesema kuwa Muungano umeimarika zaidi husasani kwenye huduma za kijamii na uchumi "kauli mbiu ya mwaka huu tumeimarika na tumeshikamana kwa maendeleo ya taifa letu tutaendelea umoja wetu, Muungano wetu ".

Amesema kuimarika kwa mahusiano kumetoa fursa kwa wafanyabiasha wa pande zote mbili kuwekeza katika nyanja mbambali.

Ametoa wito wa kuulinda Muungano ili kuitunza Tunu hiyo muhimu iliyotimiza miaka 60 .

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis amemhakikishia Makamu wa Pili wa Rais kuw muungano upo salama.
"Sisi wanadar es Salaam tunayomengi ya kuzungumzia kuhusu Muungano na haya maendeleo yanayoonekana hapa ni zao la Muungano."

Amesema kuwa muingiliano wa biashara umekuwa mkubwa watu wanafanya shughuli zao na wanatembea kila upande wa Muungano bila kuwa na hati kusafiria "Utawaona wapo Darajani kule Zanzibar utawaona Kariakoo hapa Dar es salaam huwezi kuwatofautisha".

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypran Luhemeja
,amesema Muungano huu umetupa fursa za kibishara na za kujamii "wengine tumepata fursa ya kuchanganya damu kwa maana tumeoa Zanzibar"
Amesema kuwa uchumi umekuwa kutokana kuchagizwa na ushirikiano wa kibiashara.

Amesema kuwa tayari Serikali ya Jamhuri imeshughulikia changamoto takribani zote za muungano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akifungua Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akitoa salamu wakati wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa neno la ukaribisho wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Washiriki mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Top News