IKIWA wikendi inaanza leo hii hapo baadae ligi mbalimbali zinatarajiwa kupigwa kuanzia kule Ujerumani mpaka Italia huku meridianbet wakikupa nafasi kubwa za kupiga maokoto ukisuka jamvi lako na kubashiri nao. Ingia sasa meridianbet ushinde pesa.

LALIGA leo itapigwa mechi moja majira ya saa 4:00 usiku ambapo Athletic Bilbao atakuwa mwenyeji wa Granada. Bilbao yupo nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi na mgeni wake yupo nafasi ya 19 mkiani kabisa. Mara ya mwisho kukutana walitoshana nguvu. Je leo hii nani ataondoka na ushindi? Mechi hii imepewa ODDS 1.22 kwa mwenyeji na 12.74 kwa mgeni. Suka jamvi hapa.

Kumbuka kucheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni ambayo inatolewa ndani ya meridianbet kama vile Poker, Roullette, Aviator, Rockertman, Keno, Sloti na mingine kibao. Ingia mchezoni na ucheze sasa.

Ligi nyingine ambayo itaendelea Ijumaa ya Leo ni SERIE A ambapo saa 1:30 kutakuw ana mtanange mzito kabisa kati ya Genoa dhidi ya Lazio ambaye yupo nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi huku mwenyeji akiwa nafasi ya 12. Tofauti ya pointi kati yao ni 10 pekee ambapo mechi ya mwisho kukutana kwenye ligi, Genoa lishinda. Mechi hii imepewa ODDS 2.99 kwa 2.50. Wewe leo hii unamdhamini nani kukupa pesa? Jisajili sasa.

Juventus chini ya Allegri baada ya kulazimishwa sare mechi iliyopita, leo hii atakuwa ugenini kupepetana dhidi ya Cagliari Calcio katika Unipol Domus huku Meridianbet wakimpa nafasi kubwa ya kushinda Juve kwa ODDS 1.76 kwa 4.90. Ikumbukwe kuwa mwenyeji hayupo nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi iliyopita kutoa sare. Je leo hii anaweza pata pointi 3 akiwa nyumbani?. Tengeneza mkeka wako hapa.

Vilevile bila kukosa utamu wa BUNDESLIGA leo hii kuna mechi ya kusisimua vilivyo ambapo Eintracht Frankfurt atamkaribisha nyumbani kwake Augsburg huku timu hizo zikiwa zinafuatan kwenye msimamo wa ligi yaani wa 6 kwa wa 7. Wamepishana pointi 3 tuu. Mara ya mwisho kukutana, Augsburg alishinda. Je Frankfurt atalipa kisasi kwa kushinda. Bashiri mechi hii ambayo ina machaguo zaidi ya 1000, ndani ya Meridianbet.

Tukimalizia na ligi kuu ya Ufaransa leo hii, LIGUE 1 napo ni mechi moja Ijumaa ya leo OGC Nice atakipiga dhidi ya FC Lorient saa 4:00 usiku huku wakitoshana nguvu mechi ya mwisho kukutana. Meridianbet wamempendelea Nice kushinda kwa ODDS 1.50 kwa 6.07. Ikumbukwe kuwa mwenyeji yupo nafasi ya 5 kwa 16. Beti sasa.

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

KAMPUNI ya Orxy Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation wamekabidhi mitungi ya gesi ya kupikia ya Orxy 50 kwa wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kati ya mitungi  1000  inayotarajiwa kukabidhiwa kwa wauguzi na madaktari katika mikoa 10 nchini .

Akizungumza wakati wakisaini makubaliano ya ushirikiano yaliyofanyika katika hospitali ya rufaa ya Mwananyama, Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite amesema makubaliano walioingia baina ys kampuni hiyo na taasisi ya Doris Mollel ni kusaidia kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa watanzania.

Aidha amesema katika kampeni hiyo ya kuwezesha watanzania kuingia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia, mpaka sasa tayari wameshatoa mitungi kwa wananchi zaidi ya elfu 32 ili kusaidia lengo la kufikia asilimia 80 ya watumiaji wa nishati safi.

Amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia inasaidia kuondoa hatari za kiafya kwa watumiaji wa kuni na mkaa kama nishati ya kupikia lakini pia hatari za kimazingira na ustawi wa jamii.

"Takribani watu 33,000 wanapoteza maisha nchini Tanzania kwa maradhi yanayotokana na kuvuta moshi unaotokana na mkaa au kuni hiyo ndio sababu ya Oryx gas kuja na suluhisho la kuwahamasisha wananchi kutumia gesi kwa matumizi ya kupikia", amesema Benoite

Ameeleza kuwa matumizi ya gesi yanaepusha wamama na watoto kuumika kubeba kuni hivyo kuepuka kujeuriwa na wanyama wakali wakiwa katika harakati za kutafuta kuni pia kuimarisha maisha ya wanawake na kuwalinda dhidi ya vitendo vya udhalilishaji.

“Kuanzia mwezi wa saba mwaka 2021 tumekuwa mstari wa mbele kuunga mkono utekelezaji wa mkakati wa serikali uliopewa nguvu na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania , Dk. Samia Suluhu Hassan kwa lengo kwamba ifikapo mwaka 2033 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia”, ameeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel amesema katika makubaliano waliosaini na oryxy watawafikia waguzi elfu moja ambapo watawapa mitungi na majiko ya gesi kama mabalozi kwa kina mama waweze kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni programu ya miaka miwili.

Amesema mitungi hiyo itakwenda kwa wauguzi walioko maeneo magumu ambapo watakuwa wanawatembelea kwenye vituo vya afya na zahanati ili kuweza kuwafikia wafanyakazi ambao ni wauguzi wanaofanya kazi kubwa ya kuokoa maisha hususani ya mama na mtoto.

Wakati huo huo Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala  Dk.Zavery Benela ameeleza kwamba hospitali hiyo  inakabiliwa na ongezeko la wagonjwa wa mifumo ya hewa.

Amefafanua kati ya wagonjwa wa nje 500 wanaofika kuonwa na madaktari bingwa asilimia 30 ya wagonjwa hao ni wa matatizo ya mfumo wa hali ya hewa unaosababishwa na hali ya hewa pamoja na mazingira ya kuandaa chakula kutokna na kuni na mkaa.

Aidha Dokta Benela amesema magonjwa ya mfumo wa hali wa hewa  yamekuwa changamoto hasa kwa watu wazima na watoto.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel akisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Kampuni ya Orxy Gas kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini na Taasisi ya Doris Mollel kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya makubalinao na Kampuni ya Orxy Gas kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel (katikati) akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya makubalinao na Kampuni ya Orxy Gas kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala mkoani Dar es Salaam  Dk.Zavery Benela
akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini na Taasisi ya Doris Mollel kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel wakionesha mkataba waliosaini  kwaajili ya kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy mmoja wa wauguzi katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini makubalino kati ya kampuni ya Orxy Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite  akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy kwa wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala katika hafla ya utiaji saini kati ya kampuni ya Orxy Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.


Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala wakifuatilia hafla ya utiaji saini kati ya kampuni ya Orxy Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


Wahitimu wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC), kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uganda (UCAA) wamekumbushwa kwamba kusoma hakuishii darasani pekee, mengine wataendelea kujifunza maofisini mwao wakati wanafanya kazi husika kwa vitendo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege TCAA Bi Flora Alphonce aliyekuwa mgeni rasmi Aprili 19, 2024 wakati wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance). Na kuongeza kuwa anaishukuru UCAA kwa kuendelea kukiamini chuo cha CATC na kuendelea kuleta watalaam wake kwa mafunzo.

Bi Flora aliwafahamisha wahitimu hao kwamba chuo cha CATC ndani ya kipindi cha miaka mitatu ijayo kitakuwa na majengo na vifaa vya kisasa ambavyo vitaongeza tija na kuleta utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza hapa na pale kufuatia Serikali ya Tanzania kutenga Shilingi bilioni 78 kwa ajili ya mradi huo.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha CATC Bw.Aristid Kanje alisema amefurahishwa na kuwapongeza wahitimu hao wote kwa kumaliza kozi zao kwa ufaulu wa juu. Na kuongeza kuwa ni vugumu kumlazimisha mtu kupata maarifa, kwani maarifa yanapatikana kwa kuwa na hamu ya kuyapokea.

Wahitimu hao watano kutoka UCAA walifanya kozi mbili kwa muda wa wiki 12, awali kabla ya mahali wahitimu hao walipatiwa semina juu ya umuhimu wa masuala ya kiafya na namna yanavyoweza kuathiri waongoza ndege katika majukumu yao kutoka kwa Daktari Concethar Mushi.

Akitoa salamu za shukran kiongozi wa darasa hilo kwa niaba ya wenzake Bw. Erasmus Muhairwe aliishukuru CATC kwa ushirikiano iliyowapatia kwa muda wote wa kozi zao na kuwakumbusha wahitimu wenzake kwamba kwa kuhitimu kwao watu wana matarajio makubwa kwao hasa ya kutokufanya makosa.
Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege TCAA, Flora Alphonce akizungumza na wahitimu wa  mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akizungumza jambo pamoja kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akiwakabidhi vyeti pamoja na zawadi kwa  wahitimu wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole akizungumza na wahitimu wa  
mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC). 
Dkt. Concethar Mushi akitoa mafunzo kuhusu umuhimu wa masuala ya kiafya na namna yanavyoweza kuathiri waongoza ndege katika majukumu yao wakati wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Kiongozi wa darasa hilo kwa niaba ya wenzake Bw. Erasmus Muhairwe akishukuru CATC kwa ushirikiano iliyowapatia kwa muda wote wa kozi zao na kuwakumbusha wahitimu wenzake wakati wa 
mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Wahitimu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Uganda (UCAA) wakiwa kwenye mahafali hayo


Picha ya Pamoja
Serikali za Tanzania na Zambia zimefanikiwa kufuta kero nne kati ya kero 15 zilizokuwepo awali ili kurahisisha michakato ya biashara ya nchi hizo kutegemeana kibiashara.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar, Mhe. Omar Shaaban wakati wa kikao cha pamoja cha Mawaziri wa nchi zote mbili katika sekta hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Shaaban amesema kuwa kikao hicho ni utekelezaji wa maelekezo ya Wakuu wa nchi zote mbili Tanzania na Zambia ambao walikutana jijijni Lusaka mwezi Oktoba, 2023 ambapo miongoni mwa makubaliano ni pamoja na Mawaziri wa pande mbili wanaohusika wakae na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika nchi hizo.

“Tuliingia katika majadiliano haya tukiwaa na changamoto 15 na ndani ya siku tatu hizi tumeweza kutatua kabisa changamoto nne na katika hizo nne mbili zilikuwa upande wa Zambia na mbili zilikuwa Tanzania.Jambo la msingi wenzetu wa Zambia walikuwa wanashindwa 'ku-process' mizigo kwa haraka pale boda changamoto kubwa walikuwa hawana 'scanner', tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa 'scanner' kwa ajili yao. Na ilichukua muda mrefu kupokea lakini tunafuraha juzi wameandika barua kuwa wameipokea na wako tayari kwenda kuifunga”

Ameeleza kuwa Zambia kulikuwa na vizuizi vingi kutoka mpakani hadi kufika jijini Lusaka ambapo sasa vimepunguzwa kutoka 33 vilivyokuwepo awali mpaka 11.

“Kwa kweli ni hatua kubwa wenzetu wa Zambia wameweza kurahisisha mazingira ya biashara ndani ya nchi zetu. Kubwa lingine sio changamoto ya kibiashara ni maelekezo ya Wakuu wetu kuhakikisha tunaanzisha mchakato wa kutengeneza boda nyingine kule Kasesya ambayo itaunganisha nchi zetu hizi mbili ni hatua kubwa na kikao hiki kimethibitisha kwamba tayari timu imeshaandaliwa michakato kuanza” amebainisha.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Zambia, Mhe. Chipoka Mulenga amesema kuwa changamoto zilizotauliwa zina maslahi kwa nchi zote mbili.

“Tumetatua baadhi ya changamoto zilizokuwa hazina maslahi kwa nchi zetu zote mbili Tanzania na Zambia kurahisisha ufanyikaji wa biashara ikiwa ni kuongeza wafanyakazi, na kutoa vizuizi vingi njiani ambavyo vilikuwa vinasababisha foleni”

Tumetatua changamoto ya 'scana' ambayo kutokana na mahusiano ya kidiplomasia tumepewa kutoka Tanzania. Tunaamini changamoto zilizobaki mawaziri wetu wakikutana watatatua zaidi kwa maslahi mapana ya nchi zetu ili kurahisisha ufanyikaji wa biashara” amesisistiza.











Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wakiangalia album ya picha za matukio ya Ziara Rasmi aliyoifanya katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan akiongoza ujumbe wa Nchi yake kwenye mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Ziara yake Rasmi katika Ikulu Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kuweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal Atatürk katika makumbusho ya Anitkabir, Atatürk's Jijini Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima mbele ya kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal Atatürk katika makumbusho ya Anitkabir, Atatürk's Jijini Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal Atatürk katika makumbusho ya Anitkabir, Atatürk's Jijini Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na kwa upande wa Uturuki Rais wa Baraza la Elimu Profesa Dkt. Erol Ozvar wakitia saini Makubaliano ya Ushirikiano katika Nyanja ya Elimu ya Juu baina ya Tanzania na Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wakishuhudia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Lela Muhamed Mussa pamoja na Rais wa Baraza la Utalii la Jamhuri ya Uturuki Abdullah Eren wakisaini hati za makubaliano kwa ajili ya kuanzisha ufadhili kwa wanafunzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Uturuki wanaohitimu katika Elimu ya Juu tarehe 18 Aprili, 2024.

Top News