Taasisi ya Victoria Foundation kwa kushirikiana na Orica Tanzania inatekeleza mradi wa hatua kwa hatua uitwao Binti Ng'ara, kwa ajili ya kumsaidia mtoto wa kike kupata taulo za kike za kumuwezesha Binti aweze kwenda shule wakati wote hasa wa siku zake za Hedhi.

Katika hafla ya Ugawaji wa Taulo hizo uliofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Nyankumbu Tarehe 18 April, Mgeni Rasmi alikua ni Afisa Elimu Sekondari Cassian Luoga akimuwakilisha katibu Tawala Mkoa wa Geita. Hafla hiyo ilihudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Orica Tanzania, Asha Mambo, Kaimu Mkurugenzi Taasisi ya Victoria Foundation Steven T. Mruma, Mkurugenzi na Mzalishaji wa Taulo za Kike za Palesa Sherie De Wity kutoka Nchini Afrika kusini, Maafisa Elimu wa ngazi mbalimbali , Muwakilishi wa Dawati la Jinsia Kutoka Jeshi la Polisi Afande Christina Katana pamoja na Walimu na Wanafunzi kutoka shule sita za Wilaya Ya Geita Mji.

Taulo hizo za kike zitawanufaisha Jumla ya wasichana 2500 kutoka Shule 25 za mkoa wa Geita kutoka katika Wilaya zote Sita ambapo box moja la taulo za kike linaweza kutumiwa na Mwanafunzi kwa muda wa miaka mitano kwakua Taulo hizo zinaweza kufuliwa na kutumika tena (Re usable), Zilizotengenezwa na kampuni ya Palesa Pads kutoka nchini Africa ya Kusini.

Akizungumza katika hafla hiyo ya ugawaji Mgeni Rasmi Cassian Luoga aliwashukuru Orica Tanzania kwa kufadhili mradi wa Binti Ng'ara chini ya Taasisi ya Victoria Foundation na kuomba wadau wengine wajitokeze kwa wingi ili kusaidia kutatua kabisa tatizo la wasichana kukosa vipindi vya Darasani kutokana na kukosa taulo za kike hasa wakati wakiwa katika hedhi.

Nae Mkurugenzi Wa Orica Tanzania Asha Mambo aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali pamoja na Taasisi zisizo za serikali kukabaliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili mabinti.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Mkurugunzi wa Victoria, 'Vicky Kamata',Maneja wa Miradi wa Taasisi hiyo Ndugu Steven T. Mruma aliwashukuru Orica Tanzania kwa Ufadhili wa Mradi, na Uongozi wa Mkoa wa Geita kwa ushirikiano mkubwa walioutoa wakati wote wa utekelezaji wa Mradi huo.






 

Na Mwandishi wetu- Morogoro


 Vikao vya baraza la Wafanyakazi vya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeelo ya Makazi havikufanyika kwa wakati kama ilivypongwa kufuatia watumishi wa Wizara hiyo kuwa wanachama wa vyama viwili vya wafanyakazi ambavyo ni TUGHE na TALGWU vyama ambavyo vimekuwa na mvutano juu ya uendeshaji vikao hivyo.

 

Akiongea mjini Morogoro leo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Lucy Kabyemera ambaye alimwakilisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa alisema sintofahamu iliyopo haileti afya njema kwa maendeleo ya watumishi wa Wizara yake.

    

‘’Kwa mujibu wa mkataba ni kwamba vikao vinapaswa kufanyika mara mbili kwa mwaka kwa masikitiko makubwa Wizara yetu imeshindwa kufanya vikao hivyo kwa wakati kutokana na changamoto iliyojitokeza ambayo ni uwepo wa Vyama vya Wafanyakazi viwili ndani ya Wizara  yetu’’.Aliongeza Lucy Kabyemera Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi.’’    

 

Naibu Katibu Mkuu Kabyemera aliongeza kuwa hali ya kuwa na Chama zaidi ya kimoja ndani ya Wizara ilitokana na uamuzi wa Serikali wa kuwahamisha watumishi wa Sekta ya Ardhi kutoka Sekretarieti za Mikoa na Serikali za Mitaa na kuwaleta Wizara ya Ardhi Mwaka 2019.

 

Bi. Lucy Kabyemera  aliongeza kuwa uamuzi huu ulipelekea Wizara kuwa na makundi mawili ya wanachama wa vyama vya wafanyakazi wanaotokana na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), ambacho kina wanachama 295 na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) chenye wanachama 792.

 

Aidha kutokana na uwepo wa vyama hivyo, Wizara ilikusudia kuunda baraza jumuishi la wafanyakazi ili kuwa na wawakilishi wa vyama hivyo viwili. Hata hivyo, Baraza hili limelazimika kufanyika kwa kibali cha nyongeza kwakuwa bado vyama hivyo havijafikia maridhiano ya kuwa na Baraza shirikishi.

 

 

‘’Nawasihi vyama kurejea katika meza ya majadiliano na kuchochea utendaji kazi wa Wizara ya Ardhi kwakuwa vyama vyote ni sehemu muhimu ya Wizara hii. Aidha, nimuombe Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi pamoja na Kamishna wa Kazi kusaidia katika kumaliza sintofahamu ya uhalali wa Vyama hivi ndani ya Wizara ya Ardhi, kwakuwa ninaamini vyama vyote vina lengo sawa la kusimamia haki na ustawi wa Wafanyakazi.’’Alinukuliwa akisema Bi. Lucy Kabyemera Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi.

 

 

Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo kwa niaba ya Waziri Silaa amewakumbusha wajumbe wa Baraza hilo kuhusu vipaumbele vyake tangu alipoingia katika Wizara yake aikibainisha kuwa moja ya vipaumbele ni utatuzi wa migogoro ya ardhi ambapo nilitoa siku 100 kwa kila mtendaji kutatua mgogoro kwenye ngazi yake ya utendaji.

 

Aidha, Waziri alitoa maelekezo kuhusu usimamizi wa maeneo ya wazi na maeneo ya huduma ikiwemo  kuhimiza matumizi sahihi ya ardhi na ubadilishaji holela wa matumizi ya ardhi mfano ujenzi wa vituo vya mafuta, kukamilishwa zoezi la urasimishaji na kuboresha utendaji wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya

 

Mengineyo ni maendeleo ya makazi na upimaji ardhi na utendaji kazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na kuwataka wote wanaoguswa na vipaumbele hivi kufanya kazi kwa bidii ili nitakapofanya tathmini ya kila eneo, asiwepo atakayeathirika.

 

Baraza hili linakutana kujadili kwa kina Makadirio ya Mipango na Matumizi kwa mwaka 2024/2025 na kuweka mipango ambayo inatekelezeka itakayosaidia kuleta maendeleo na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Lucy Kabyemera akiongea na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara yake leo Manispaa Morogoro.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifuatilia jambo wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi mapema leo Manispaa ya Morogoro.

 

 

 

Na Mwamvua Mwinyi, Rufiji April 19


Jeshi la Wananchi wa Tanzania limetoa magari kumi kwa ajili ya kusaidia kusafirisha vyakula kwenda kwenye makambi ya waathirika wa mafuriko walioko kwenye Wilaya za Rufiji na Kibiti Mkoa wa Pwani.

Akipokea Magari hayo April 18, 2024 Wilayani Rufiji, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amempongeza Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Majeshi kwa magari hayo.

Ameeleza kuwa wamepata misaada ya vyakula lakini kulikuwa na changamoto ya usafiri na Barabara katika kufikia walengwa.

Amesema magari hayo yatasaidia kufika kirahisi maeneo hayo yenye changamoto.

Vilevile Kunenge amepongeza Jeshi kwa kuendelea kulinda mipaka ya nchi na Amani kuendelea kuhudumia Jamii.

Kadhalika Kunenge,amekabidhi magari hayo kwa Wakuu wa Wilaya za Kibiti na Rufiji.



 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 kwa ajili ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano. Anayempokea ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme kuhusu majukumu yanayotekelezwa na Ofisi hiyo alipotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Hanifa Selengu wakati Makamu wa Pili wa Rais alipotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Hanifa Selengu wakati Makamu wa Pili wa Rais alipotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati akiondoka mara baada ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwaaga wananchi mara baada ya kufungua Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Wakiwa kwenye picha ya pamoja ni ujumbe kutoka Uganda, wakiwemo wabunge wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, wa Bunge la Uganda. Katikati ni Mhe. Gilbert Olanya, wa Jimbo la Kilak Kusini, Mwenyekiti wa Kamati; na kushoto kwakwe ni Prof. Lughano Kusiluka, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, (aliyevaa Kaunda).

.......

Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, ya Bunge la Uganda imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa uwekezaji mkubwa iliyofanya katika ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, pamoja na kusifu Amani na Utulivu mkubwa uliopo, kwa kuzingatia idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Gilbert Olanya, wa Jimbo la Kilak Kusini, Alhamisi tarehe 18 Aprili 2024, walipofanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho pamoja na kufanya mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka, kwenye ofisi yake iliyopo jengo la Benjamin Mkapa, Dodoma.

Aidha, wamevutiwa na aina ya masomo yanayofundishwa katika Ndaki, Shule Kuu na Taasisi za Chuo, pamoja na namna chuo kinavyoendelea kuwekeza katika kuanzisha programu mpya za masomo zinazoakisi mabadiliko makubwa ya kisekta yanayozingatia utoaji mafunzo wenye kutatua changamoto kubwa za ajira, na matumizi ya teknolojia katika ufundishaji.

Akiukaribisha ujumbe huo, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Kusiluka amelishukuru Bunge la Tanzania kwa kuona umuhimu wa kuwaleta wabunge hao kuja kujifunza UDOM, na kueleza ni kwa namna gani wabunge hao wana mchango mkubwa katika kuongeza hamasa ya ufundishaji wa lugha ya Kiswahili katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kutunga Sera zenye kusaidia nchi hizo kuendana na mabadiliko makubwa ya kisanyansi na teknolojia katika Sekta ya Elimu.

Aidha, amewahamasisha waganda kuja kusoma Tanzania kutokana na uwepo wa mitaala mizuri na masomo yenye kukidhi mahitaji katika soko la Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

“Tunayo fursa ya wananchi wa Uganda na nchi nyinginezo za Afrika Mashariki kuja kusoma UDOM. Niwahakikishie tunayo mazingira mazuri na thabiti ya kujifunzia kwa wana Afrika Mashariki kuja kusoma Tanzania. Mazingira yetu, tamaduni na mahitaji yetu yanafanana, kwangu mimi hii ni fursa kwetu sote” alisisitiza

Wajumbe wengine wa Kamati hiyo waliofika kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma ni pamoja na Mhe. Betty Ethel Naluyima, Mhe. Dkt. Isingoma Patrick Mwesigwa, Mhe. Rwemulikya Ibanda Gerald, Mhe. Patrick Ocan na Mhe. Lillian Obiale Paparu.



Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, wa Bunge la Uganda, wakiwa kwenye mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, ofisini kwake Dodoma.



Wakiwa kwenye picha ya pamoja ni ujumbe kutoka Uganda, wakiwemo wabunge wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, wa Bunge la Uganda. Katikati ni Mhe. Gilbert Olanya, wa Jimbo la Kilak Kusini, Mwenyekiti wa Kamati; na kushoto kwakwe ni Prof. Lughano Kusiluka, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, (aliyevaa Kaunda).



Prof. Lughano Kusiluka akikamkabidhi zawadi ya ukumbusho Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Uganda, Mhe. Gilbert Olanya. Wabunge hao walifika kutembelea chuo na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu utoaji wa Elimu ya Juu nchiniTanzania.



Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakiagana na waheshimiwa wabunge wa Uganda, baada ya kuhitimisha ziara yao chuoni hapo.
*Ampongeza Rais Dkt. Samia kwa kutenga sh. trilioni 8.18 sekta ya nishati

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutenga fedha za kutekeleza miradi ya nishati ambapo katika kipindi cha miaka mitatu zaidi ya shilingi trilioni 8.18 zilitolewa.

“Maono na maelekezo yake kuhusu usimamizi wa sekta hii yamekuwa na mchango mkubwa katika ufanisi wa shughuli za sekta, katika hili, ninampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuweka kipaumbele kikubwa katika utekelezaji wa miradi ya nishati.”

“Katika kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa umeme nchini, tayari nchi yetu imeanza kutumia umeme wa bwawa la Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP). Huu ni ushindi na kielelezo tosha kwamba Mama yupo kazini.”

Ametoa pongezi hizo leo jioni (Ijumaa, Aprili 19, 2024) wakati akifunga Maonesho ya Wiki ya Nishati yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amelipongeza Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kwa kuweza kuzalisha umeme zaidi ya mahitaji yaliyopo sasa. “Leo tarehe 19 Aprili, 2024 uzalishaji wa umeme ni mkubwa. Shirika letu la TAMESCO limemudu kuzalisha umeme zaidi ya mahitaji tuliyonayo na bwawa la Julius Nyerere Hydropower Project limeanza kazi na tayari megawati 235 ziko kwenye mfumo.”

Ameitaka Wizara hiyo iweke mkakati wa kuhakikisha maonesho hayo yanakuwa endelevu ili Waheshimiwa Wabunge waweze kupata fursa ya kuwasilisha hoja zao mahsusi na kutatua kero za wananchi wanaowawakilisha.

Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya washiriki wa maonesho hayo ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita, Waziri Mkuu ameitaka Wizara hiyo ione uwezekano wa kuandaa maonesho kama hayo katika ngazi ya Mikoa na Halmashauri. “Wakurugenzi wa Kanda na Mameneja wa Mikoa na Wilaya mko hapa. Nendeni mkae na muangalie jinsi ya kutekeleza jambo hilo,” amesisitiza.

Ameitaka Wizara hiyo iweke mkakati wa kuhakikisha wananchi wote wanapata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu fursa zinazopatikana kutokana na miradi inayotekelezwa na sekta ya nishati. “Pamoja na kuyaleta maonesho hapa Bungeni, kuna haja ya kupeleka maonesha kama haya kwenye maeneo ya katiati ya mji ili muweze kuwafikia wananchi wengi zaidi na kujibu hoja zao,” amesema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wadau mbalimbali walioshiriki maonesho hayo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameipongeza TANESCO kwa kuendelea kufanya kazi nzuri ya kuhakikisha wananchi wanapata nishati ya umeme.

Naye, Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema sekta ya nishati ni kati ya sekta mtambuka kwa sababu inalisha sekta nyingine nyingi na ikitikisika, inatikisa na maeneo mengine pia.

Amesema pamoja na utoshelevu wa umeme kwenye gridi ya Taifa, ili kuwe na maendeleo bado nchi inahitaji umeme wa kutosha na hasa kwenye viwanda na siyo kuwasha taa za majumbani.

Ameitaka Serikali itafute njia ya kutumia vizuri maji yanayotoka kwenye bwa la JNHPP ili yaweze kuwanufaisha wananchi wanaoishi maeneo ya jirani na bwawa hilo. “Bwawa limejaa kwa hiyo Serikali ihakikishe maeneo ya jirani yanapata maji ya kutumia. Tuanzishe gridi ya maji kama ilivyo kwenye gridi ya umeme. Kule chini tutengeneze njia ya kutunza maji kwa ajili ya matumizi ya umwagiliaji na mifugo,” amesema.

Naye, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema ushiriki wa mwaka huu umevunja rekodi kwani watu zaidi ya 480 walitembelea maonesho hayo ambapo 267 walikuwa ni Waheshimiwa Wabunge.

Ameyataja maeneo ambayo washiriki walikuwa wakiulizia zaidi ni umeme, nishati ya jua, nishati jadidifu, nishati safi ya kupikia, mafuta na gesi.

Amesema ili kujenga uelewa mpana kwa wananchi, wanapanga kuandaa kongamano maalum juu ya gesi asilia ambalo linatarjiwa kufanyika Mei, mwaka huu.




-Asisitiza uadilifu na uwajibikaji kwa mali za umma

-Apongeza Serikali Njombe mrejesho kwa wananchi, chama kwa usimamizi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, amesema kazi kubwa iliyofanywa na Serikali, chini ya uongozi wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan, ndani ya miaka mitatu, ni nyezo inayobeba ukweli wa kutosha kusambaratisha uongo unaoenezwa na baadhi ya wapinzani wa kisiasa kupitia mikusanyiko yao.

Amewataka wana-CCM wote kuendelea kujiamini na kutembea kifua mbele wanapozisema, kuzitangaza na kuikumbusha jamii kuhusu kazi za maendeleo na ustawi wa jamii, zinazofanywa na Serikali za CCM ili wananchi waendelee kuuona ukweli, wakitofautisha na uongo unaoenezwa kwa propaganda nyepesi za kisiasa.

Balozi Nchimbi amesema hayo leo, Aprili 19, 2024, alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wanaCCM wa Mkoa wa Njombe, kupitia Mkutano Maalum wa Mkoa, uliofanyika mjini Njombe.

“Mambo yaliyofanywa na Serikali ndani ya hii miaka mitatu, unaweza kuona kama ni miujiza. Kazi kubwa sana inafanyika. Ni wajibu wetu kuitumia nyenzo yenye ukweli kupambana,” amesema.

Kupitia mkutano huo, ambao Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Antony Mtaka aliwasilisha taarifa ya mrejesho wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020 - 2025, iliyohusisha miradi mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa wananchi, Balozi Nchimbi pia amerudia kusisitiza kwa watendaji wa Chama na Serikali ulazima na umuhimu wa kuwa waadilifu wakati wote kwenye masuala yanayohusu rasilimali za umma, kwa kupiga vita rushwa na ubadhirifu.






Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, akiwa kwenye Kikao cha Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Njombe, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Njombe, Njombe Mjini, kabla ya kuelekea kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Mkoa wa Njombe, leo asubuhi, Aprili 19, 2024.

Dk Nchimbi, akiambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Oganaizesheni, Ndugu Issa Haji Usi Gavu na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makala, yuko mkoani Njombe kwa ziara ya siku mbili, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mikoa 6 ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.








Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso (MB) amefika Wilaya ya Monduli kunusuru Bwawa la Nanja ambalo ni Tegemeo la Vijiji 30 katika chanzo Maji pekee baada ya kumeguka kingo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Amesisitiza kwamba pamoja na ugumu wa kukarabati bwawa hilo wakati likiwa na maji maamuzi magumu yafanyike wataalamu wa Wizara ya Maji watumie utaalamu wao kulifanikisha hiko kwani hakuna namna nyingine.

Akizungumza na mamia wa wananchi wa Kata za Lepruko, Sepeko, na Makuyuni Waziri wa maji maelekezo kwa Wataalamu wa Wizara kama ifuatavyo kwanza kutumia taaluma zao kuhakikisha Bwawa hilo linakarabatiwa kwa dharula haraka kuanzia kesho tarehe 19.04.2024 kudhibiti maji kuebdelea kupotea pili kufanya usanifu wa kina nyakati za kiangazi kusudi bwawa hilo liweze kukarabatiwa kwa uhakika zaidi.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh Fred Lowassa amesema Bwawa hilo ndio tegemeo la wana Monduli kwenye matumizi ya maji kwa Binadamu, mifugo na wanyamapori hivyo anaiomba Serikali ione namna ya kukarabati bwawa hilo kwa dharura.

Aidha, Wakizungumza katika nyakati tofauti madiwani wa kata zinazoguswa na bwawa hilo wameishukuru serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuwafikia kwa haraka na kutafuta suluhu ya utatuzi ya changamoto hii.




Top News