Hayo yamesemwa na Kaimu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jonas Rwegasira wakati akikabidhi Madawati 1000 kwa Shule tano za Msingi Wilaya ya Kinondoni yaliyofanyika Leo Aprili 20,2024 Shule ya Msingi Kisauke Jijini Dar es Salaam.
Rwegasira amesema Wadau kama Klabu ya Rotary ni watu ambao wamekuwa wakisaidia sana Serikali katika kuboresha Mazingira rafiki kwa Wanafunzi kujisomea kwa kugawa Madawati kwani Serikali imekuwa ikitafuta Wadau mbalimbali ambao watachochea ufaulu mzuri kwa Wanafunzi hao.
"Wadau hawa Rotary wameenda Kuandika historia nyingine ndani ya mioyo ya watoto hawa pamoja na Shule hizi tano ikiwemo Shule ya Msingi Mtakuja, Kisauke,Salasala,Kunduchi, pamoja na Shule ya Msingi Twiga kwani kila shule imekabidhiwa Madawati 200."
Mratibu wa mradi huo Ezra Kavana amesema Klabu hiyo ina lengo la kuboresha Mazingira mashuleni na mpango huo wa Madawati umeendelea kupewa ushirikiano na Klabu ya Rotary ya Vancouver ambapo Madawati hayo elfu 1000 yamegharimu pesa taslimu Milioni mia moja na ishirini na Saba.
Aidha ameongeza kuwa Klabu hiyo pia inalenga kupanda miti kwa wingi kwani sehemu kubwa ya Madawati hayo ni miti ambayo imekuwa ikikatawa hivyo Kuna umuhimu wa kupanda miti kwa wingi ili Madawati hayo yaendelee kuzalishwa kwa wingi.
"Kila dawati tunalolikabidhi tunahakikisha tunapanda miti miwili ambapo tayari tumeshatekeleza hilo kwa kupanda miti 2500 ."
Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kisauke Hamza Suleiman mepongeza Klabu hiyo kwa kuendelea kugawa Madawati kwa Shule za Misingi ili kuleta Ufaulu Mzuri Kwa Wilaya ya Kinondoni.
"Tunakwenda kutengeneza mazingira mazuri ya taaluma kwa watoto wetu madawati haya mia 200 yataenda kuleta chachu ya kuongeza ufaulu wa shule yetu."
Pia ameeleza kuwa bado shule hiyo inapitia changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa,ofisi za walimu pamoja na Matundu ya vyoo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapiduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesisitiza dhamira ya Chama, chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wa CCM, Dk. SAMIA Suluhu Hassan, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kukirudisha kwa wanachama, kupitia kwa mabalozi, itatekelezwa kwa vitendo.
Akizungumza na viongozi wa CCM wa ngazi mbalimbali kuanzia mashina hadi mkoa, Mkoa wa Ruvuma, kwenye mkutano wa ndani uliofanyika Ukumbi wa Parokia ya Bombambili, mjini Songea, Aprili 20, 2024, Dk Nchimbi amesema kuwa kutambua ukubwa wa nafasi ya Balozi na Shina ni kutambua dhamana kubwa waliyonayo wanachama kwa Chama chao Cha CCM.
Aidha, Dk. Nchimbi pia amewapongeza na kuwashukuru wananchi na viongozi wa mkoa wa Ruvuma kwa mapokezi nakubwa yaliyoonesha imani kubwa waliyonayo kwa Chama Cha Mapinduzi.
Mkutano huo uliojumuisha Viongozi mbalimbali wa Chama , Serikali, Dini, Wazee na Taaasisi zisizo za kiserikali, Balozi Dkt. Nchimbi amewapongeza wana Ruvuma kwa kushinda chaguzi zote zilizopita siku za hivi karibuni hali inayozidi kuonesha imani yao kwa CCM haijatetereka na kutoa pongezi kwa ushirikiano wao mkubwa wa chama na serikali.
" Hongereni kwa uhusiano mkubwa na mzuri wa chama na serikali na huu ndio unapelekea utekelezaji wa ilani kutekelezwa kwa kasi. "
Aidha, Balozi Dkt. Nchimbi amehimiza juu ya heshima kwa mabalozi kwa kuwa ndio msingi imara wa CCM.
" Nilipokuwa mbunge wenu hakuna watu ambao niliwapa heshima kubwa kama mabalozi ssbabu najua mabalozi ndio msingu wa shina la CCM na ndio maana tumeelekeza nguvu kubwa kuhakikisha Nchi nzima viongozi wote wanatambua hakuna viongozi wakubwa zaidi ya mabalozi na kwa mantiki hiyo chama kitarudi kwa wanachama wengine na sisi tunaochaguliwa na kuteuliwa ni watumishi tu kwa hao wanachama "
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk Nchimbi, akiambatana na Katibu wa NEC ya CCM Taifa, Oganaizesheni, Ndugu Issa Haji Usi Gavu na Katibu wa NEC ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makala, ameingia Mkoa wa Ruvuma Aprili 19, 2024, kwa ajili ya ziara yake katika maeneo mbalimbali mkoani humo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara aliyoanzia mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.
KATIBU Tawala wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Upendo Wella amesema katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanikiwa kusimamia masuala ya muungano kwa ufanisi mkubwa.
Hiyo imesababisha kuimarika kwa utaifa, umoja, amani, utulivu, na hali ya maisha ya wananchi kutokana na ukuaji wa uchumi wa pande zote mbili za Muungano.
Wella ametoa kauli hiyo alipowaongoza wananchi katika upandaji miti ikiwa ni shamshara za sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Zoezi hilo lilifanyika leo katika Kata ya Kisima, wilayani Same.
Aidha,amewahimiza wananchi wa wilaya ya Same kuendeleza utamaduni wa kupanda miti sehemu mbalimbali, hasa kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha kwa wingi, ili miti iweze kustawi vyema na kuepukana na hali ya ukame.
Pia amewaomba walimu wote kuhakikisha kila mwanafunzi anapanda mti katika mazingira ya shule na kusimamia ukuaji na utunzaji wa mti huo, pamoja na kuhimiza upandaji miti majumbani, katika taasisi za serikali na zisizo za serikali, ili baadaye wilaya iwe na rutuba nzuri ya miti.
Katibu huyo pia amewaalika wananchi kushiriki katika mkesha wa kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utakaofanyika tarehe 25, ambapo kutakuwa na matangazo ya moja kwa moja ya hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia channel ya TBC.
Amesema kwamba Aprili 26 ndio itakuwa kilele cha Siku ya sherehe za Muungano, wananchi watashiriki katika majadiliano ya masuala mbalimbali yanayoweza kujenga taifa.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau na watumiaji wa bidhaa za kielekroniki wakiwemo wataalam mbalimbali wa ujenzi, wasanifu majengo, wafanyabiashara wa vifaa vya kilektroniki, taasisi mbalimbali za kiserikali na wafanyakazi wa makampuni ya GSM GROUP pamoja na Haier.
Kampuni ya Haier iliingia rasmi ubia na kampuni ya GSM GROUP mnamo mwanzoni mwa mwaka 2023. Kwa kipindi hiki chote, kampuni ya Haier ikishirikiana na GSM GROUP imekuwa ikihakikisha inaleta bidhaa ambazo zina tija sokoni. ‘Tangu uanzishwaji wa kampuni ya Haier, Tanzania, tumekuwa tukijitahidi kuangalia matakwa ya soko na kuhakikisha tunaboresha huduma na ufanisi wa bidhaa zetu kwa watumiaji’ Alisema haya meneja biashara, Bw. Ibrahim Kiongozi.
Sambamba na uzinduzi huo wageni waalikwa walipata nafasi ya kujionea bidhaa hizo mpya na kupata mafunzo mafupi kwa ajili ya matumizi ya vifaa hivyo. ‘Sifa kubwa za bidhaa hizi za AC ni mfumo wake imara na wa kisasa unaosababisha matumizi kidogo ya umeme pamoja na uwezo mkubwa wa utendaji kazi katika kutoa hali ya ubaridi kwa haraka.’ Aliongezea Meneja mkuu kutoka Haier, Bw. Leon Liuchi.
Ushirikiano wa makampuni ya GSM Group na Haier unaleta tija katika ukuaji wa uchumi wa nchi kutokana na mapato na ajira mbali mbali zinazotolewa. ‘Katika kuhakikisha kwamba GSM GROUP ikishirikiana na Haier inaungana na juhudi za kukuza uchumi wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan, tunajitahidi kushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii zikiwemo udhamini wetu katika michezo kupitia timu mbali mbali za mpira wa miguu kama Young Africans Sports Club (Yanga), Coastal Union, Singida Fountain Gate na Ihefu’ Alisisitiza, Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya GSM Group, Mr. Benson Mahenya.
Vile vile katika mkutano huo, wageni waalikwa walipata fursa ya kujishindia bidhaa za jokofu (fridge) pamoja na kiyoyozi (AC).
Uongozi wa makampuni ya GSM GROUP na Haier ulitoa shukrani kwa wadau mbali mbali walioshiriki pamoja na kuahidi kuendeleza ubunifu kwa matoleo ya mbeleni ya bidhaa za kielektroniki Tanzania. Vilevile Haier imethibitisha kuongeza mpango kazi katika kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa hizo mikoa yote ya Tanzania.
Bw. Mohamed Ally, mkurugenzi wa miradi wa kampuni ya GSM Tanzania (kushoto) akimkabidhi zawadi ya Kiyoyozi mmoja wa wadau wa vifaa vya kielektroniki vya Haier
Kutoka kushoto Bw. Yang, meneja masoko Haier Africa Bw. Kevin, meneja wa bidhaa za rejareja Haier Africa Bw. Mohamed Ally, Mkurugenzi wa miradi wa kampuni ya GSM Tanzania,Mkurugenzi mkuu wa makampuni ya GSM GROUP, Bw. Benson Mahenya (katikati) Bw. Bai, meneja wa bidhaa za AC Bw. Ibrahim Kiongozi, meneja biashara wa Haier Tanzania Bw. John Nguya, mkuu wa biashara kitengo cha GSM Property.
-Yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira
Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewaonya watu wanaojenga miradi bila kupata Cheti cha Tathmini ya Mazingira EIA kwenye baraza hilo kwamba wanakabiliwa na faini ya shilingi milioni kumi.
Hayo yamesemwa leo Aprili 19,1024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na msosholojia wa Baraza hilo Suzan Chawe alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa maonyesho ya kumbukumbu ya miaka 60 ya Muungano
Maonyesho hayo yamefunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Abdulla.
Suzan amesema NEMC imekuwa ikifanya kaguzi za mara kwa mara na wale wanaokutwa wamejenga miradi bila EIA wamekuwa wakitozwa faidi inayofikia hadi shilingi milioni kumi
Amesema NEMC imekuwa ikiendesha kampeni ya elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa EIA kwa wanaojenga miradi kabla ya kufanya kaguzi na kuwatoza faini.
"Mfano unaweza kukuta mtu anajenga kituo cha mafuta kwenye makazi ya watu jambo ambalo ni hatari kama ikitokea dharura tunaweza kupoteza maisha ya watu kwa hiyo tunasisitiza umuhimu wa EIA kabla ya kuanza shughuli za ujenzi," amesema Suzan
Amesema kwa miaka 60 ya Muungano NEMC inajivunia mambo mengi ikiwemo kupigania ustawi wa mazingira kwa kuhakikisha miti mingi inapandwa na kulindwa.
Suzan amesema Baraza limefanya maboresho ya mifumo yake ya mapito ya taarifa za tathmini na kaguzi za athari kwa mazingira kwa kuimarisha miundombinu ya TEHAMA kulingana na matakwa ya mfumo wa serikali mtandao.
Amesema NEMC inasimamia miradi inayofanya tathmini ya athari kwa mazingira kwa njia ya kielektroniki kupitia usajili wa mtandaoni njia ambayo inamuwezesha mwekezaji kuanzisha mchakato wa kupata cheti cha EIA kupitia mfumo wa usimamizi wa mradi ( Project Management System).
"Kabla ya kufanya usajili wa mradi mwekezaji anatakiwa kuhakikisha mawazo ya wadau yamepatikana kuhusu utekelezaji wa mradi kwenye eneo husika" amesema Suzan.
Maofisa wa BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), wakihudumia watu waliofika leo kwenye viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam kwenye maonyesho ya miaka 60 ya ya Muungano. Maonyesho hayo yamefinguliwa leo Aprili 19,2024 na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Abdulla
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, KIGOMA
JAJI
Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma, amesema Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema lengo la vyombo vyote vya dola ni
ustawi wa wananchi.
Mhe.
Jaji Mkuu, ameyasema hayo mjini Kigoma Aprili 19, 2024, wakati akifungua Kikao Kazi kati ya Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF), Mahakama ya Tanzania na Watendaji wa Tume ya Usuluhishi na
Uamuzi (CMA) mjini Kigoma lengo kuu likiwa ni kujenga uelewa wa Sheria ya Fidia
kwa Wafanyakazi.
“WCF
ni Mfuko unaogusa ustawi wa wananchi, kwasababu unaweza kuwa unamtegemea mama,
kaka, bahati mbaya akapata ajali akafariki, hapa ustawi wa familia unaweza
kutoweka, kama hakuna Mfuko unaoweza kubeba hilo jukumu, kwa hivyo huu Mfuko ni
muhimu mno mno.” Amebainisha Mhe. Profesa Juma.
Aidha
Mhe. Profesa Juma amehimiza umakini na uadilifu katika utekelezaji wa sheria
hiyo ya Fidia kwa Wafanyakazi.
“Ukosefu
wa umakini, udanganyifu vyote vimechangia kuua mifuko ambayo ilikuwa na malengo
mazuri sana. Tusipokuwa waangalifu, mfuko huu wa WCF vile vile unaweza
kukumbana na tatizo hili. Tukielewa vizuri mantiki ya kuanzishwa mfuko huu tutaufanya
uwe endelevu na himilivu,” amesema.
Aidha
Mhe. Jaji Mkuu ameipongeza WCF kwa kupiga hatua kubwa katika matumizi ya TEHAMA
katika utekelezaji wa majukumu yake na kukumbusha umuhimu wa mifumo ya taasisi
za umma kusomana ili kurahisisha utoaji wa huduma.
“Ifike
mahala mfanyakazi anapowasilisha madai yake WCF, mfumo mzima uwe unaelewa
kwamba mfanyakazi fulani amepata ajali kazini au amefariki. Mifumo ya serikali ikiweza
kutambuana pia itasaidia sana kuziba mianya ya udanganyifu.” Alisisitiza.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw.
Emmanuel Humba, amemuhakikishia Mhe. Jaji Mkuu kwamba Mfuko unaendeshwa kwa
ufanisi mkubwa na umepata mafanikio makubwa katika kutekeleza malengo yake.
“Malipo
ya fidia kwa Wafanyakazi yameongeza kutoka TZS 3.88 bilioni Kwa mwaka 2016/2017
hadi kufikia TZS 23.58 bilioni kwa mwaka 2022/2023. Hili ni ongezeko kubwa la
malipo ya fidia kulinganisha na kiasi cha TZS 250 milioni zilizokuwa zikilipwa
na Waajiri kwa mwaka kabla ya kuanza Mfuko.” Amefafanua Bw. Humba.
Aidha,
michango ya Waajiri iliyokusanywa imeongezeka kutoka TZS 68.40 bilioni Kwa
mwaka 2015/2016 hadi kufikia TZS 86. 48 bilioni kwa mwaka 2022/2023, amesema
Bw. Humba.
“Faida
inayotokana na uwekezaji ya fedha zilizobaki baada ya kulipa mafao imeongezeka
kutoka TZS 1.60 bilioni Kwa mwaka 2015/2016 hadi kufikia TZS 102.43 bilioni kwa
mwaka 2022/2023, lakini pia thamani ya
Mfuko imeongezeka kutoka TZS 65.68 bilioni Kwa mwaka 2015/2016 hadi kufikia TZS
602.78 bilioni kwa mwaka 2022/2023.” Amefafanua.
Kuhusu
ustahamilivu wa Mfuko katika kutekeleza majukumu yake, Mwenyekiti huyo wa Bodi
amesema kuwa tathmnini ya uhai na uendelevu wa Mfuko iliofanywa na Shirika la
Kazi Duniani (ILO) inaonesha kwamba Mfuko unauhimilivu (Sustainability) kwa
kipindi cha miaka 30 kuanzia mwaka wa tathmini 2022/2023.
Akizungumzia
kuhusu nia ya kikao kazi hicho, Bw. Humba alibainisha kuwa pamoja na kwamba
jukumu la kulipa fidia limekasimiwa kwenye Mfuko, Sheria ya Fidia kwa
Wafanyakazi imeweka utaratibu na vyombo vya kushughulikia madai ya wanufaika
pale wanapokuwa hawajaridhika na fidia iliyolipwa au maamuzi ya Mfuko
yanayokinzana na matarajio yao.
Akifafanua
zaisdi alisema, Sheria inamtambua Waziri Mwenye dhamana ya masuala ya kazi kuwa
ni Mamlaka ya kwanza ya rufaa dhidi ya uamuzi wa Mfuko na Mahakama Kuu
Divisheni ya Kazi kuwa Mamlaka ya mwisho ya rufaa.
“Kutokana
na hitaji hili muhimu la kisheria, Bodi ya Wadhamini ya WCF, Menejimenti ya
Mfuko pamoja na Watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi waliona kuna hitaji
la kufanya vikao kazi kwa lengo la kubadilisha uzoefu, kujenga uelewa wa pamoja
na kubainisha maeneo ya sheria yanayohitaji maboresho kwa lengo la kuongeza
ufanisi katika kutekeleza Sheria hiyo.” Alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John
Mduma ameeleza kuwa ushirikiano baina ya Mfuko na Mahakama ni muhimu kwa vile
kuna maeneo mengi ambayo Mfuko unakutana na Mahakama katika utekelezaji wa
majukumu yake.
“Sisi
kama WCF shughuli zetu hazikamiliki bila ya uwepo wa shughuli za Mahakama. Kwa
mfano katika kushughulikia masuala yanayohusu mirathi, Mfuko hutegemea maamuzi
ya Mahakama.” Alisema Dkt. Mduma.
Awali,
akizungumza kabla ya kumkaribisha Jaji Mkuu kufungua Kikao Kazi hicho, Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambia
alisema kuwa kumekuwa na vikao kazi vitano ambavyo vimefanyika baina ya
Mahakama, WCF na Watendaji wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) huko Bagamoyo, Mwanza, Arusha, Songea na Kigoma.
Alibainisha
kuwa jumla ya Viongozi na watumishi 290 wameshiriki katika Vikao Kazi hivyo,
wakiwemo Majaji 70, Naibu Wasajili 33, Watendaji 11, Wadau 48, Tume ya
Usuluhishi na Uamuzi 32 na zaidi ya watumishi wa Mahakama 96.