Kocha Mkuu wa Timu ya Tabora United Denis Laurence amesema kuwa katika kipindi cha siku saba tangu alipojiunga na timu anaridhishwa na viwango vya wachezaji kutokana na kujituma kwao kwenye mazoezi uwanjani.
Kocha Laurence amesema kuwa ameshangwaza kuona wachezaji kwa kipindi kifupi tangu alipojiunga na Timu hiyo yenye Makazi yake Mkoani Tabora wanamuonesha ushirikiano wakutosha nakusikiliza kila anachowaelekeza kwenye uwanja wa mazoezi na kwamba hajapata changamoto yoyote hadi sasa.
Ameongeza kuwa ushirikiano ambao wachezaji wanampa unatoa taswira njema kuelekea kwenye michezo tisa ya Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara pamoja na michuano ya Kombe la Azam Sport Federation dhidi ya Singida Fountain Gate kufanya vizuri kwani ndio mkakati uliopo kwa sasa kama Timu.
“Nafurahi kuona wachezaji wananisikiliza vizuri, tunakwenda sawa ,tunazungumza Lugha moja , kwa huumuda mfupi ambao nimekuwa nao hapa kwangu ni maajabu, wanafuata ninachowaambia lakini pia wanafanyia kazi, hii kwangu ni kubwa sana kama kocha, muhimu nazidi kuwasisitiza kila mmoja ananafasi kwenye kikosi changu cha kwanza” amesema Kocha Laurence.
Ukiangalia kila mmoja anauwezo mkubwa, nahii ni kawaida kwa wachezaji wa Afrika, muhimu ninachokifanya ni kuwaweka kwa pamoja wacheze kitimu ili tuweze kushinda, morali na hari zao zipo juu hivyo ninafurahia sana kuwepo na wachezaji wangu mazoezini na mazingira yote kwa ujumla.
Aidha katika hatua nyingine Kocha Laurence amesema kuwa hadi sasa tayari ameshapata kikosi chake cha kwanza lakini akasisitiza sio ndio kitadumu milele hapana kwani mfumo wake ni kuhitaji kila mmoja aweze kucheza kweye michezo hii iliyosalia kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2023/2024.
Tabora United itakuwa ugenini siku ya Aprili Nne katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza ikiwakabili Singida Fountain Gate kwenye mchezo wa ASFC na badae Aprili 14 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi hapa Mjini Tabora.
Imetolewa leo Machi 28
Na Christina Mwagala
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Tabora United
Na MWANDISHI WETU
WAWEKEZAJI kutoka China wamekutana na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kujadiliana kuhusu uwekezaji hususan katika uzalishaji wa Nishati safi ya kupikia kwa lengo la kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati ya kupikia.
Wawekezaji hao waliongozwa na Shen Don kutoka Jimbo la Shangzhou ambapo wakiwa nchini wlikutana na wadau mbalimbali kutazama fursa za uwekezaji.
Kundi hilo la wawekezaji wameridhia kufanya uwekezaji wa zaidi ya dola za Marekani milioni 312 (zaidi ya sh. bilioni 800) katika maeneo ya nishati, afya, ujenzi, kilimo na vifaa vya uchakataji viwandani
Kutokana na hatua hiyo, UWT inaamini hiyo itakuwa fursa nzuri kwao kuwafikia na kuwawezesha wanawake kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lumumba jijini Das res Salaam, jana, Katibu Mkuu wa UWT, Jokate Mwegelo alisema wawekezaji hao ambao ujio wao umeratibiwa na Kampuni Canopus Energy Solution, wameonyesha utayari wa kushirikiana katika eneo la uzalishaji wa Nishati mbadala na maeneo mengine ya kimkakati.
“Chama Cha Mapinduzi kinachoongozwa na Mwenyekiti wetu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kilizielekeza jumuiya zote Chama kutazama na kujiendeleza kupitia fursa mbalimbali, hii kwetu ni fursa tumejipanga kuzalisha nishati mbadala kupitia makaa yam awe.
“Wenzetu hawa wameonyesha utayari, tumefanya mazungumzo ya awali na wametualika kwenda China katika maeneo yao ya uzalishaji wa huduma na bidhaa mbalimbali kujionea namna walivyo tayari kutokana na maendeleo ya teknolojia,” alisema.
Alieleza kuwa UWT ina dhamana kubwa ya kuwaendeleza wanawake wa Tanzania kupitia fursa mbalimbali, hivyo imejipanga kuunga mkono juhudi za kumtua mama kuni kichwani kwa kutengeneza mkaa mbadala ambao ni salama kwa afya za binadamu.Kwa mujibu wa Jokate mbali na nishati mbadala, pia wanatazama uwezekano wa wa kushirikiana na wadau hao katika sekta ya madini lakini hilo litafanyika baada ya hatua mbalimbali kutekelezwa ili kuwa na ushirikiano wenye tija.
Jokate alisisitiza kwamba UWT imejipanga kutengeneza fursa ambazo zitawanufaisha wanawake katika sekta mbalimbali hususan uchumi ambao utawainua na kimaisha.
"Fursa yoyote tunayoitengeneza lengo letu ni kuona wanufaika wa kwanza wanakuwa wanawake wa Tanzania,” alisema.
Kwa upande wake Mhandisi Anna Nyangasi kutoka Kampuni ya Canopus Energy Solution, alisema ujio wa ujumbe huo ni fursa kwa uwekezaji katika sekta mbalimbali.
Anna alieleza kuwa wawekezaji hao waliongozwa na Shen Don kutoka Jimbo la Shangzhou ambapo ukiwa nchini ulikutana na wadau mbalimbali kabla ya jana kukamilisha ziara yao kwa kukutana na UWT ambapo wanaamini kuna kundi kubwa la wanawake ambalo linahitaji kuwa sehemu ya mabadiliko kutokana na uwekezaji unaoweza kufanywa na wawekezaji hao.
Kwa mujibu wa Anna, wawekezaji hao wameridhia kufanya uwekezaji wa zaidi ya dola za Marekani milioni 312 (zaidi ya sh. bilioni 800) katika maeneo ya nishati, afya, ujenzi, kilimo na vifaa vya uchakataji.
Pia, alisema ujumbe huo umeonesha nia kushirikiana na kutafuta wawekezaji katika maeneo takribani manane ambayo ni viwanda vya kuunganisha zana za kilimo (pawatila), kuzalisha vifaa vya trekta, majenereta, pampu za maji, vifaa tiba, viwanda vya bidhaa za umeme na ‘paneli’ za kuhifadhi baridi.
Mhandisi Anna alisema ujumbe huo wa watu 11 unahusisha wafanyabiashara, wawakilishi kutoka serikalini pamoja na ujumbe wa CCP, uliwasili nchini kwa mwaliko wa Canopus Energy Solution kwa kushirikiana na Kampuni ya Amec Group.Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Jokate Mwegelo (kushoto) akisalimiana na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China waliongozwa na Shen Don kutoka Jimbo la Shangzhou (wa pili kulia) baada ya kufika katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi(CCM) zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam
Na. Vero Ignatus, Arusha
Katibu Mkuu mtendaji wa Smaujata amewataka Viongozi kusimamia vyema nafasi walizonazo sambamba na kuwa barua njema kwa kila anayewasoma
Ameyasema hayo katika kikao cha Viongozi wa Smaujata mkoa kilichofanyika Jijini Arusha, ambapo aliwataka kutambua kuwa Uongozi ni majukumu poa ni mgumu,kwani hawawezi kupendwa na kila mtu badala yake kila mmoja wao atambue nafasi yake, waitumikie jamii kwa moyo wa huruma,kwa kusimamia haki, pamoja na kuwa na kifua cha kubeba mambo.
Aidha aliwataka Viongozi hao wajitahidi kuwa waadilifu kwenye nafasi zao, watafute namna wanaweza kutengeneza utaratibu wa kufuatilia mambo pamoja na kutoa nafasi kwa wengine, zaidi kufahamu mipaka yao ya kiutendaji.
"Ninyi kama Mashujaa na Viongozi ni vyema kutambua kwa kupitia uzoefu wa namna moja ama nyingine mnaweza kuangalia namna gani njema ya kutatua changamoto"alisema Injinia Juliana
Akisoma ripoti ya utendaji wa kazi katika mkoa Kaimu Katibu wa Smaijata
Lussa Melembuki alisema kuwa hadi sasa wameweza kufikia jumla ya shule za msingi zaidi ya 246,shule za sekondari zaidi ya 118,Makanisa 42, wamefanya semina 12 pamoja na kushiriki zaidi ya matamasha 18 vyote hivyo ni kwaajili ya outta elimu kwa jamii dhidi ya Ukatili
Vile vile ameweza kuushukuru Uongozi wa seriali ngazi ya mkoa kwa kuwapatia ushirikiano mkubwa kwani wamekuwa sababu ya wao kufanikisha kutoa elimu katika jamii, ikiwemo kuwajuza madhara yatokanayo na Ukatili, na mahali sahihi pa Kutoa taarifa endapo wataona dalili ama jambo lolote lenye viashiria vya ukatili.
Aidha ifahamike kuwa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania ni kampeni mahususi ya Kitaifa kwaajili ya kupinga, kuibua na kutokomeza vitendo vyote vya ukatili katika Jamii zote nchini, kuelimisha Jamii kuondokana na fikra, Imani, Mila na desturi na tamaduni zinazokinzana na Maendeleo.
Baadhi ya malengo ya kampeni hiyo ni kutambua kutengeneza mtandao Jamii, sense uwezo wa kupaza Sauti kupinga nakupambanaa na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto, kuelimisha na kurahisisha utambuzi na ufanyiaji kazi viashiria vyote vya ukatili kuanzia ngazi ya Familia.
Katibu Mkuu wa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii (Smaujata)nchini Mhandisi Juliana Marko akizungumza na Viongozi wa Wilaya pamoja na wale wa mkoa alipotembelea Jijini hapo kwaajili ya shughuli za kikazi kushoto kwake ni Mwenyekiti wa mkoa wa Arusha Godfrey Zablon.
Katibu Mkuu Smaujata Taifa wa pili kutoka kushoto Juliana Marko akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Arusha mapema Marchi 27,2024
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTARADE) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Viwanda na Biashara Imeratibu Semina ya Wafanyabiashara kuhusu fursa ya kuuza bidhaa katika soko la Uingereza kupitia Mpango wa Biashara wa Uingereza na Nchi zinazoendelea (UK-DCTS)
Semina hii ya inayofanyika katika ukumbi wa JNICC ulipo Jijin Dar es salaam. Inalenga kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na nchini Uingereza ili kujenga uwezo wa taratibu na vigezo na hivyo kuwafungulia fursa za Masoko zinazopatikana nchini Uingereza.
Wakimwakilisha Mkurugenzi Mkuu TANTRADE Bi. Latifa M. Khamis, Meneja Uhusiano kwa Umma na Masoko Lucy Mbogoro pamoja na Afisa Biashara (Masoko ya Ndani na Nje ya Nchi) Bw. Deo Shayo wameshiriki Semina hii ambayo imefunguliwa rasmi na Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Ashatu Kijaji.
Bi. Petronela Mlowe afisa ukaguzi na Mazingira anayefanya kazi uingereza na pia mtaalam elekezi wa Ukaguzi bidhaa
akitoa mada kuhusu namna bidhaa za vyakula vinavyoingizwa Uingereza vinakaguliwa.
Aidha, Bi. Mlowe ametoa hamasa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuuza uingereza na kukuza uchumi
6h
Akizungumza leo Machi 28,2024 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Janury Makamba amesema kwa miaka mingi nchi hiyo inaongoza kwa teknolojia ya juu Duniani katika udhibiti wa maji ikiwemo maji taka,mafuriko na ya kunywa hivyo ushirikiano huo wa karibu utaleta tija kubwa kwa Taifa .
Sambamba na hayo amesema nchi hizi mbili zimekuwa zikifanya biashara hivyo kutafanyika makongamano ya kibiashara, ziara ili fursa zilizopo zifahamike na ushirikiano huo uendelee kudumu siku hadi siku.
"Tanzania ina vivutio vingi vya utalii na Hungary ni chanzo cha watalii kwani tumeshuhudia watalii wengi kutoka nchi hiyo wakija kutalii na miaka iliyopita walikuwa 5000 mwaka jana wakifikia 11000 hivyo kuna ongezeko kubwa kutoka nchi hiyo na kwa kuona hilo tumezungumza kwa kina na kujubaliana kuwa tutasaini usafiri wa anga watalii na wafanyabiashara watatoka moja kwa moja kutoka Hungary kuja Tanzani kwa ndege"Amesema Makamba
Sanjari na hayo amebainisha kuwa Vijana wa kitanzania wamekuwa wakinufaika kwa kupata ufadhili wa kwenda kusoma Hungari pia wamekubalina kunzisha mahusiano ya kituo cha Diplomasi cha kimataifa cha Dkt Salim Ahmed Salimna na chuo cha Diplomasia ambapo itasaidia wanadiplomasia kupata fursa ya kwenda Hungari kuongeza ujuzi.
Waziri Makamba amesema nchi ya Hungary wamedhamiria kuwekeza kwenye kiwanda cha kuwekeza ndege ndogo pale Morogoro na
Aidha nchi ya Hungary imekubali kujenga Ubalozi wao nchi Tanzania uliofungwa miaka ya 1990" hiyo ni moja ya kusaidia kuongeza mashirikiano makubwa baina ya nchi hizo mbili.
Naye Waziri wa Mambo ya nje na Biashara wa Hungary Mhe Peter Szijj'art'o amesema licha ya kufungwa kwa ubalozi lakini bado ushirikiano ikuwa unaendelea hivyo habari njema ni kuwa nchi yao mwaka huu Julay inatarajiwa kuchukua Urais wa Umoja wa Ulaya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2022/23 kutoka kwa Bw. Charles Kichere Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 28 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa mwaka 2022/2023 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna wa Polisi Salum Hamduni Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 28 Machi, 2024.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo wa kukopesha simu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire, alieleza kuwa kampuni hiyo ya simu inatekeleza mipango mbalimbali ya kupunguza gharama za vifaa vya mawasiliano ili kuwawezesha wateja wake kuhama kutoka kwenye matumizi ya mtandao wa 2G na kumiliki simu zenye uwezo wa 4G na kutumia fursa hiyo ili kunufaika na faida kemkem zinazopatikana kupitia mtandao huo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alisema, “ushirikiano huu baina yetu na Vodacom ni fursa nzuri kwa Watanzania kupata huduma za kifedha na mawasiliano kwa gharama nafuu. Kwa hiyo kama wadau muhimu tunapaswa kuunga mkono juhudi za Serikali ili kuhakikisha wananchi wake wanafaidika na ukuaji na maendeleo katika sekta hizi.”
Licha ya juhudi za mamlaka nchini kusogeza huduma za mawasiliano, wananchi wengi bado wanatumia huduma za mtandao wa 2G. Hii inapunguza upatikanaji wa fursa zilizopo mtandaoni pamoja na kufurahia na kunufaika na intaneti yenye kasi zaidi kutoka Vodacom pamoja na bidhaa nyingine za kidijitali.
Matumizi ya simujanja na intaneti yana faida kwa jamii kama vile kukuza ukuaji wa kiuchumi kwa kuwezesha ujasiriamali wa kidijitali na kuchochea uvumbuzi, utafutaji masoko mitandaoni pamoja na kuongeza kipato kwa wananchi wanaoamua kujiajili kupitia dijitali.
Mwezi August 2020, Vodacom ilizindua programu ambayo inawaruhusu wateja wake kumiliki simujanja kupitia mkopo unaolipwa kwa awamu, huku kianzio kikiwa ni Shilingi 20,000 za Kitanzania kwa muda wa miezi 12.