Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amepokelewa kwa shangwe na nderemo na wananchi wa Mbarali, wakiongozwa na vijana waendesha bodaboda, baada ya kuwasili na msafara wake katika Kata ya Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, leo Aprili 18, 2024, akitokea Mbeya Mjini.

Dk Nchimbi alisimama kuwasalimia wananchi hao wa Ubaruku, akiwa njiani kuelekea Mkoani Njombe ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya mikoa 6 ya Nyanda za Juu Kusini, ambapo ameambatana na Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndg. Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC - Oganaizesheni Ndg. Issa Haji Gavu.







NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

HOSPITALI ya Heameda imezindua Maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha.

Akizungumza April 18 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mtambo huo ambao ni lulu nchini katika taratibu za matibabu ya moyo, Mkurugenzi wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Meshack Mwandolela alisema hospitali iliamua kuitenga siku ya April 18,2024 kwa ajili ya vipimo vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza na moja wapo ya magonjwa hayo ni ugonjwa wa moyo na wameibaini watu wengi wanasumbuliwa na maradhi hayo na hawakujua kwasababu hayaoneshi dalili.

Aidha Dkt.Mwandolela alisema mtambo huo unawasaidia kuweka vifaa maalumu kusaidia wagonjwa wa moyo ambavyo ni pacemaker vinavyowekwa kwenye moyo kwa ajili ya kusaidia mambo mbalimbali.

"Mojawapo ya magonjwa yanayotibiwa kwa pacemaker ni wale wenye moyo unaoenda taratibu na wale wanaopata milipuko ya moyo bila mpangilio na Kuna wengine wanapata moyo mkubwa,na kushindwa kufanya kazi kwahiyo tunawawekea pacemaker maalumu ambayo inasaidia kupunguza saizi ya moyo,lakini pia kuongea nguvu ya moyo kusukuma damu" Mwandolela alisema

Aidha Dkt.Mwandolela alieleza kuwa tangu wameweka mtambo wa CATH LAB wamefanikiwa kufanya vipimo kwa wagonjwa zaidi ya 15 pamoja na kuweka pacemaker kwa wagonjwa takribani watatu vilevile na kwa wagonjwa watatu ambao walikua na changamoto ya kuziba kwa mishipa inayokwenda kwenye moyo.

"Tumeweza kuokoa gharama kubwa sana, kwa ajili ya matibabu haya mtu huyu ambaye alikua anatakiwa asafiri kwenda India anakuwa ameokoa pesa na muda kwa wanaomuuguza kwahiyo tunapunguzaa gharama kubwa ili watu waweze kufanya mambo yao mengine wakiwa hapa" alieleza Dkt.Mwandolela

Pamoja na hayo ametoa rai kwa wananchi kutoogopa matumizi ya teknolojia za kisasa ambazo zilichelewa kuingia nchini ,na zimekuwa zikitumika huko katika mataifa ya kigeni kwa muda mrefu ambapo imechangia kuokoa maisha na watu kuishi kwa muda mrefu.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt.Gunini Kamba, ameipongeza Hospitali ya Heameda kwa kufunga vifaa Bora ambavyo vinafanya huduma za kibingwa kwa kuzibua mishipa iliyoziba kwenye moyo.

"Mashine iliyofungwa ni ya kisasa sana ,katika nchi yetu zipo tano,na ukizingatia ina uwezo wa kuzibua mishipa ya moyo, tunashukuru tuna JKCI inafanya huduma hiyo lakini peke yake haijitoshelezi", alisema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Heameda Bi.Edwina Lupembe alionesha kujivunia timu yao ya watendaji katika hospitali hiyo kwa uadilifu wao kazini pamoja na juhudi katika shughuli zao kupambania kutoa huduma bora.

Vilevile Madaktari kutoka India walieleza kuwa watashiriki kuziba nafasi iliyokuwa wazi nchini kwa kutoa huduma za kibingwa katika matibabu ya ugonjwa wa moyo kwa wagonjwa ambao wamechelewa kupata huduma hiyo ya upasuaji wa moyo (Cardiac Surgery).

Heameda imejikita hasa katika huduma za kitabibu katika magonjwa ya moyo, saratani, pamoja na kuchuja damu kwa wagonjwa wa figo iliyofeli ambapo wamelenga kusaidia wananchi kupunguaza gharama kufata matibabu nje ya nchi.


Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Gunini Kamba akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Heameda Bi.Edwina Lupembe na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Mwandolela


Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Mwandolela akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Gunini Kamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali ya Heameda iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Heameda Bi.Edwina Lupembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.


Daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka nchini Inida akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali ya Heameda iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Mwandolela akieleza jambo kwa wadau mbalimbali walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.


Sehemu maalumu ya kuwalaza wagonjwa mara baada ya kufanyiwa matibabu katika Hospitali ya Heameda iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya madaktari bingwa pamoja na wadau mbalimbali wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Balozi wa Pakistani nchini Siraj Ahmad Khan (kushoto), Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Digit, Abdul Rehman Mahmood (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa simu maalum iitwayo Smart Kitochi+ kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa kuona na kusikia huku ikiongeza matumizi ya dijitali nchini, hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.





Ili kuimarisha ushirikishwaji na kuongeza matumizi ya huduma na bidhaa za kidijitali nchini, kampuni ya teknolojia na mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC imezindua simujanja ya kidijitali inayoitwa 'Smart Kitochi +' ambayo imeundwa ikiwa na vipengele muhimu kwa ajili ya wateja wasiosikia na wasioona.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Bi. Linda Riwa, amesema kuwa uzinduzi huu ni sehemu ya juhudi endelevu za kampuni hiyo za kukuza ushirikishwaji huku ikiunga mkono serikali katika azma yake ya kuchochea matumizi ya bidhaa na huduma za kidigitali.

"Tunafurahia mapinduzi haya ya kuleta bidhaa na huduma za kidigitali na za kibunifu kwa wateja wetu wenye mahitaji mbalimbali kote nchini. Leo, tunazindua simu ya kipekee ya kidijitali inayoitwa 'Smart Kitochi+' ambayo mbali na sifa kama kioo kikubwa na cha kugusa, uwezo mkubwa wa kuhifadhi na betri inayodumu muda mrefu, simu hii pia itawanufaisha wateja wetu wenye ulemavu wa kusikia na kuona,” anasema Linda.

“Simu hii inajumuisha teknolojia ya kugusa na sauti, ikiruhusu wateja wenye changamoto hizi kupata huduma zetu bila kutegemea msaada wa mtu mwingine. Haya ni mapinduzi muhimu katika sekta ya utoaji huduma za mawasiliano, ikizingatiwa kuwa serikali inahimiza watoa huduma kuzingatia ushirikishwaji katika utoaji wa huduma kwa wateja,” aliongeza Linda.

Uzinduzi wa simu hii ni ingizo la kipekee sokoni ukilinganisha na matoleo mengine, ikiwa na uwezo wa kuchochea ushirikishwaji katika matumizi ya huduma za mawasiliano ya kidigitali. Pia ina ubora wa hali ya juu ikiwa na kioo kikubwa na cha kugusa (2.8”), uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu kwenye 8GB na betri inayodumu muda mrefu ya 3000mAh.

Toleo hili jipya la 'Smart Kitochi+' ni sehemu ya juhudi za Vodacom kuwapeleka wateja wake kwenye matumizi ya kidigitali, ikiwa ni pamoja na mtandao wa 4G, ambao bado una watumiaji wachache ikilinganishwa na idadi ya watumiaji wa simu za mkononi nchini Tanzania.

"Tunajivunia kuwa mtandao unaoongoza nchini, tukitoa huduma za kidigitali za ubunifu kwa zaidi ya wateja milioni 21. Kuwa na idadi kubwa ya wateja pekee haitoshi; tunataka wateja wetu wanufaike na mapinduzi ya kidigitali yanayoendelea na ubunifu mkubwa tunaoingiza kwenye bidhaa zetu. Kwa kuanzisha bidhaa za kisasa kama 'Smart Kitochi+' tunaamini tutachochea wateja wengi zaidi kuhama kutoka kwenye mfumo wa 2G na kuanza kufurahia huduma mbalimbali za kidigitali zinazotolewa na mtandao wetu wa kasi wa 4G na 5G uliosambaa nchini na hatimaye kuongeza matumizi ya simujanja ambayo kwa sasa ni asilimia 32," alifafanua Bi. Linda.

Akizungumzia simu hiyo mpya, Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (TLB) Bw. Luis Benedicto aliisifia simu hiyo akikiri kuwa itakuwa mkombozi kwa watu wenye ulemavu wa kusikia na kuona.

"Tulikuwa tumetengwa na kubanwa katika matumizi ya simu za mkononi, kwani nyingi hazikuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu wa kusikia na kuona. Kuzinduliwa kwa simu hii kutatusaidia sio tu kufurahia huduma za mawasiliano kutoka Vodacom bali pia kuimarisha mwingiliano wetu na wengine na kutumia simu hizi kwa manufaa ya kijamii na kiuchumi," alielezea Bw. Benedicto.

Uzinduzi huu unakuja baada ya hivi karibuni kampuni hiyo kuanzisha dawati maalum kwa ajili ya kuhudumia wateja wasioona baada ya kuanzisha dawati kama hilo kwa ajili ya wateja wenye ulemavu wa kusikia mwaka jana.

Juhudi za kampuni hiyo katika kuzingatia na kuboresha maisha ya wateja wake ili kupunguza au kufuta kabisa utofauti uliopo wa kidigitali kwa watu wenye ulemavu zimeifanya iwe miongoni mwa watia saini wa miongozo ya GSMA kwa kuchochea ushirikishwaji wa kidigitali kwa watu wenye ulemavu. Miongozo hiyo huweka misingi ya hatua za kuchukua pamoja na kinachotakiwa kufanywa na mtoa huduma za simu za mkononi ili kupunguza pengo katika upatikanaji wa huduma pamoja na matumizi ya huduma hizo.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha.Poline Msuya akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Mamlaka za maji kuhusu mfumo wa kieletroni wa MajIs ulioboreshwa kwa ajili ya kupokea taarifa za utendaji wa sekta ya maji, kilichofanyika  EWURA Makao Makuu, Dodoma.

Na.Mwandishi Wetu_DODOMA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imefanya kikaokazi cha kutambulisha mfumo wa Majis ulioboreshwa kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira. Kikao hicho kimefanyia EWURA makao makuu Dodoma.

Akifungua kikao hicho kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mha. Poline Msuya amesema Maboresho yaliyofanyika katika mfumo yalichagizwa pia na maoni ya wadau ambao ni watumiaji wa mfumo. Pia mfumo umeboreshwa kuakisi mabadiliko na maendeleo kwenye sekta ya maji.

Aidha EWURA haitosita kuchukua hatua za kiutawala kwa mamlaka za maji ambazo hazitatekeleza uwasilishaji wa taarifa zao kwa wakati, aliongezea Mha. Poline Msuya.

Akitoa maoni yake muwakilishi wa Wizara ya Maji Mha. Epimack Oscar alisisitiza Mamlaka za Maji zitumie mfumo huo kwa ajili ya kuwa na takwimu sahihi.

Kifungu cha 29(1)(h) cha Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira Sura Namba 272 kinaitaka EWURA kukusanya taarifa za utendaji kutoka mamlaka.

Meneja wa EWURA kanda ya Magharibi Mha. Walter Christopher akiwasilisha mada kuhusu mfumo wa Majis ulioboreshwa kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwenye kikaokazi cha kutambulisha mfumo huo. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano EWURA makao makuu Dodoma.

Mhandisi Mwandamizi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA, Teophil Sanjawa akiwaelekeza washiriki wa kikaokazi namna ya kujaza taarifa kwenye mfumo wa MajIs ulioboreshwa, leo 17.4.24

Washiriki wa kikao kazi wakifuatilia kwa umakini namna ya kujaza taarifa za utendaji wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira kwenye mfumo wa MajIs ulioboreshwa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mha. Poline Msuya(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za maji za makao makuu ya mikoa na miradi ya kitaifa,wawakilishi kutoka Wizara ya maji na wafanyakazi wa EWURA idara ya Maji muda mfupi baada ya ufunguzi wa kikaokazi cha utambulisho wa mfumo wa Majis ulioboreshwa kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira,Dodoma.






Serikali kupitia Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuzuia na kudhibiti athari za michezo ya kubahatisha ili kuhakikisha jamii inakuwa salama.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mlola, Mhe. Abdallah Shangazi aliyetaka kuwajua iwapo Serikali inatambua athari hasi kwa Jamii ya Watanzania zinazotokana na ongezeko kubwa la michezo ya kubahatisha.

Mhe. Chande alisema kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 7(2)(i) cha Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, Sura 41, mamlaka ya udhibiti ina jukumu la kuhakikisha kuwa jamii inalindwa ipasavyo dhidi ya athari hasi za michezo ya kubahatisha.

“Katika kutekeleza jukumu hilo, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali ya kuzuia na kudhibiti athari hasi zitokanazo na uwepo wa michezo ya kubahatisha, mikakati hiyo ni pamoja na kuimarisha udhibiti na uratibu wa sekta kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na matumizi ya mifumo ya TEHAMA,’’alisema Mhe. Chande.

Alifafanua kuwa Bodi inaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu athari za michezo ya kubahatisha, kufanya mapitio ya mara kwa mara ya mifumo ya usimamizi wa michezo ya kubahatisha pamoja na kufanya kazi ya udhibiti kwa kushirikisha wadau na mamlaka nyingine kama vile Jeshi la Polisi, TCRA na TRA.

Mhe. Chande alisema pamoja na faida za kiuchumi na kijamii zinazotokana na michezo ya kubahatisha, Serikali inatambua athari zake katika jamii endapo haitaendeshwa kwa weledi ikiwemo uraibu na kugeuza michezo ya kubahatisha kuwa mbadala wa ajira, ushiriki wa watoto katika michezo ya kubahatisha na uwepo wa michezo haramu isiyo na usajili wa mamlaka ya udhibiti.


In Ankara's halls, under academic gaze,
Ankara University honors a Tanzanian blaze.
Samia Suluhu Hassan, a leader so rare,
In economics, an honorary doctorate she did bear.

From India's Nehru to Zanzibar's shore,
Her accolades in leadership roar.
Dar es Salaam and now Ankara's acclaim,
Her achievements in Tanzania's name.

Professor Ünüvar bestows the degree,
A symbol of her transformative spree.
Diplomats and scholars, a distinguished crowd,
In honor of her, they are bowed.

Her leadership's impact, a global view,
Economic reforms and policies anew.
Tanzania's rise under her steady hand,
A symbol of progress, across the land.

A state visit to Türkiye, a momentous affair,
Samia Suluhu Hassan, expectations to declare.
With President Erdogan, dialogue will engage,
Strengthening ties, a new historic stage.

She strengthens ties, both near and far,
Elevating Tanzania as a rising star.
Türkiye, a partner in trade and more,
Their bond deepens, united at its core.

From agriculture to technology's leap,
Education's advance, in promises deep.
Trade volumes surge, opportunities vast,
A partnership that's built to last.

Coffee, coconuts, and gems so rare,
Tanzania's treasures, beyond compare.
Turkish investments, a boon for each,
Economic growth, well within reach.

As Samia Suluhu Hassan strides ahead,
Her vision and courage, widely spread.
Tanzania's future, a path so clear,
Nasimama na Samia, her leadership we cheer.

Thank you.

Written by Christopher Makwaia
Tel: +255 789 242 396


- The writer, is a University of West London graduate (formerly Thames Valley University) and an expert in Management, Leadership, International Business, Foreign Affairs, Global Marketing, Diplomacy, International Relations, Conflict Resolution, Negotiations, Security, Arms Control, Political Scientist, and a self-taught Computer Programmer and Web Developer.


Na Karama Kenyunko Michuzi Tv

MSAJILI Mkuu wa Mahakama nchini Tanzania Eva Nkya amekabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Msajli wa Mahakama hiyo Jaji Wilbert Chuma huku mbele yake akikabiliwa na majukumu 12.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo 18 Aprili 2024, jijini Dar es Salaam katika ya Msajili Mkuu wa zamani (Chuma) na Msajili Mkuu mpya (Nkya).

Akizungumza wakati wa kumkabidhi ofisi Msajili Mkuu mpya, Jaji Chuma alimpitisha kwenye kifungu cha Sheria ya usimamizi wa Mahakama Na. 4 ya 2011.

"Kama mnavyofahamu, kwa mujibu wa kifungu 28 cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Na.4/2011 shughuli zote za kimahakama zinasimamiwa na Msajili Mkuu. Msajili Mkuu ndiye kiungo kwa masuala yote ya Sheria kati ya Mahakama ya Tanzania na Mihimili mingine ya Dola pamoja na Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na Mashirika binafsi" amesema Jaji Chuma.

Amesema kuwa majukumu ya msajili yaliyoanishwa kisheria ni pamoja na kuwezesha na kusimamia ufanisi katika uendeshaji wa mashauri Mahakamani; Kuratibu shughuli zote za uendeshaji wa mashauri, Kuwa kiunganishi kati ya Mahakama na Tume ya Utumishi wa Mahakama kwenye masuala ya uteuzi, upandishaji madaraja na masuala ya maadili kwa Maafisa Mahakama.

Ameongeza wajibu mwingine ni pamoja na Kuwasiliana na Serikali katika masuala yanahusu mambo ya kimahakama, au masuala yoyote ambayo Serikali ina maslahi nayo.

"Katika kutekeleza majukumu hayo, Msajili Mkuu anasaidiwa na Msajili wa Mahakama ya Rufani, Msajili wa Mahakama Kuu, Naibu Wasajili na Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri, Kurugenzi ya Huduma za Mahakama, Ukaguzi na usimamizi wa Maadili pamoja na Kurugenzi ya TEHAMA ambapo amesema, majukumu hayo yamefafanuliwa kwa kina kwenye taarifa ya Makabidhiano.


"Kwa ufupi, taarifa inaainisha maeneo mbalimbali ambayo yalikuwa yanaendelea kufanyiwa kazi na ofisi ya Msajili Mkuu. Miongoni mwa naeneo hayo kwa uchache ambayo pia ni mafanikio ya Mahakama kwa kipindi chote nilichohudumu"

"Kuendelea kusimamia mikakati ya kuiwezesha Mahakama kuondokana na mlundikano wa mashauri uliopungua kutoka asilimia 11, 2019 hadi asilimia tatu Machi, 2024"

Amesema majukumu aliyoendelea nayo ni kusimamia mfumo wa uratibu wa mashauri (Advanced Case Management System) , Kusimamia na kuratibu mfumo wa unukuzi na tafsiri yaani, transcription and translation system (TTs).

Jaji Chuma amesema kuwa majukumu anayotakiwa kuyavalia njuga ni pamoja na kuhakikisha maamuzi ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu yanapatikana katika mfumo wa TANZLII.

Kuongezeka kwa idadi ya vituo vya Mahakama zinazokaguliwa kutoka 75.8% mwaka 2017 hadi 98.1% mwaka 2023, na kuendelea kupunguza hatua za kuendesha mashauri kwa maana procedural steps ambazo zilipungua kutoka hatua 38 hadi hatua 21.

Amesema kuwa utekelezaji wa maoni kuhusu ripoti ya REPOA ya mwaka 2023 ambayo ilionyesha kuridhika kwa umma juu ya huduma zinazotolewa na Mahakama kutoka asilimia 61, 2015 hadi asilimia 88, 2023.

"Lakini pia ni muhimu kulinda na kuendelea kuongeza asilimia kwa kuongeza uwajibikaji. Hii ni hatua kubwa japo wapo wanaobeza juhudi hizi. Lakini nao ni wetu na wanapaswa kuhudumiwa".


"Kuendelea kulinda uhuru wa Mahakama na kusimamia nidhamu kwa maafisa wa Mahakama" amesema Jaji Chuma.


Naue, Nkya Msajili Mkuu mpya wa Mahakama akipoea majukumu ya Ofisi ya hiyo ameahidi kuwa atafanya jitihada zake zote kuhakikisha kuwa muhimli huo unazidisha kasi katika utoaji haki kwa wananchi.

Msajili Nkya amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kumuamini na kuahidi kuwa atatekeleza majukumu yake kadri ya uwezo wake wote.

Amesema kuwa amezipokea nasaha na ushauri wa Msajili Mkuu wa zamani "Nasaha zako ni nzuri zitaniimarisha ,niahidi kwamba nitatekeleza majukumu yangu kulingana na kiapo changu pia kwa uwezo ambao Mungu ameniajaalia nitafanya kazi kadri ya uwezo wangu wa mwisho".

Msajili Nkya ameomba ushirikino kwa watendaji na watumishi wote wa mahakama na kusisitiza kufanya kazi kwa jitihada zote kuhakikisha muhimili wa mahakama uzidi kuwa imara.
 

Aliyekuwa msajili wa Mahakama Kuu Tanzania, Jaji Wilbert Chuma (kulia) akikata utepe kama ishara ya kukabidhi ofisi  kwa Msajili Mkuu wa Mahakama hiyo mpya nchini, Eva Nkya..anayeshuhudia nyuma ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Tanzania,  Profesa Elisante Ole Gabrieli. Hafla za makabidhiano hayo zimefanyika leo Aprili 18,2024 jijini Dar es Salaam 

Msajili Mkuu mpya wa Mahakama Kuu Tanzania,  Eva Nkya akizungumza wakati wa kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa msajili wa Mahakama hiyo nchini Jaji Wilbert Chuma (kushoto) kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Profesa Elisante Ole Gabrieli

 

Aliyekuwa msajili wa Mahakama Kuu Tanzania, Jaji Wilbert Chuma (katikati) akizungumza wakati wa kukabidhi ofisi  kwa Msajili Mkuu wa Mahakama hiyo mpya nchini, Eva Nkya (aliyeko kushoto na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Profesa Elisante Ole Gabrieli

Na Mwandishi wetu

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo viti mwendo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wa shule ya sekondari ya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Msaada huo umekabidhiwa leo Aprili 18,2024 shuleni hapo na Mkurugenzi wa Taaluma wa CBE, Dkt. Shima Banele, katika hafla fupi iliyowashirikisha wanafunzi zaidi ya 110 wa shule hiyo wenye mahitaji maalum.

Akizungumza maara baada ya kukabidhi msaada huo, Dkt.Banele amesema chuo hicho kimejenga utamaduni wa kusaidia shule hiyo kila mwaka kwani inapokea wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma elimu jumuishi.

Dkt. Banele amesema chuo hicho kitaendelea kusaidia shule hiyo ili wanafunzi wenye mahitanji maalum waweze kusoma kwa bidii na kutimiza ndoto zao siku za baadaye.

Amesema kila mwaka chuo hicho kimekuwa na utamaduni wa kuchukua sehemu ya wanachopata na kurejesha kwenye makundi mbalimbali ndani ya jamii kama sehemu ya kutambua mchango wake kwa chuo.

Aidha amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari kwani wanafunzi wengi walikuwa wanashindwa kwenda shule kutokana na kukosa ada sasa wanaweza kupata elimu yao.

Pia amepongeza hatua ya serikali kuweka elimu jumuishi ambapo wanafunzi wenye mahitaji maalum wamekuwa wakichanganywa na wale ambao hawana changamoto yoyote.

Amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao na kuachana na fikra za kujiona wanyonge kwani wakijiamini wanaweza kufaulu vyema kwenye masomo yao na kufanya vizuri kwenye elimu ya vyuo vikuu.

“Mnaweza kuwa na changamoto ya maumbile lakini ubongo wenu unafanyakazi vizuri kwa hiyo msifikirie kwamba hamuwezi, mnaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa jamii kama mtajibidisha na mkafaulu vizuri,” amesema

“Mtakapomaliza sekondari mkafaulu vizuri na kwenda vyuo vikuu mkimaliza hangaikeni kutafuta ajira kwasababu mnauwezo wa kufanyakazi kama wengine. Kila mtakapoona nafasi za ajira pelekeni wasifu wenu,” amesema.

Aidha, amewataka kuishi kwa upendo na kupeana moyo kwenye masomo yao ili waweze kufanya vizuri kwenye masomo yao na kukua kitaaluma badala ya kukandamizana kwa uchoyo na chuki.

“Mimi leo hapa namwakilisha Mkuu wa chuo cha CBE lakini kwa nafasi yangu pale ni Mkurugenzi wa taaluma sasa kama mimi nimeweza kufika nilipo kwa sasa kwanini kesho usiwe wewe. Kwa hiyo unatakiwa kuanza kufikiria kesho yako leo hii na ninaamini mtafanikiwa sana mkijituma,” amesema

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa shule hiyo, Paulina Aweda, amesema shule hiyo inawanafunzi 110 wenye mahitaji maalum na wanasoma masomo yote kama walivyo wanafunzi ambao hawana changamoto yoyote.

Amepongeza serikali kwa kuweka mazingira mazuri kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum wanasoma bila vikwazo vyovyote na kwamba wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho ya kitaifa.

Amesema wanafunzi hao wenye mahitaji maalum wamekuwa wakipatiwa chakula, malazi na mahitaji mengine yote wanapokuwa shuleni hapo hali ambayo imewawezesha kufanya vizuri kitaaluma.

“Tunabahati ya kuwa na waalimu wa kutosha waliosomea elimu maalum ya kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa hiyo serikali imewafikiria kwa kiwango kikubwa wanafunzi wenye mahitaji maalum,” amesema.
 

Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),   Dkt. Shima  Banele ambaye ni Mkugenzi wa Taaaluma wa chuo hicho akimsukuma mwanafunzi kwenye kiti mwendo (wheelchair) walipokwenda kutoa msaada wa viti hivyo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wa shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es Salama leo Aprili 18,2024.

 

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, Dar es Salaam Paulina Aweda (kulia) akionyesha tuzo ambayo amepewa leo Aprili 18,2024 na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kutambua mchango wa shule hiyo kutunza na kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum wakati walipowatembelea shuleni hapo na kuwapa zawadi mbalimbali vikiwemo viti mwendo.


Top News