SERIKALI YANUNUA MASHINE ZA MIONZI ZA BILIONI 1.74

SERIKALI YANUNUA MASHINE ZA MIONZI ZA BILIONI 1.74

Related image

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imenunua mashine za Mionzi (digital X-ray) zipatazo kumi zenye thamani ya

SUMAKU kutumika kupunguza Maumivu
Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imenunua mashine za Mionzi (digital X-ray) zipatazo kumi zenye thamani ya shilingi bilioni 1.74.
 
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akipokea mashine hizo kwenye Bohari ya Dawa(MSD)  jijini hapa.
 
Waziri Ummy amesema kuwa Serikaki inaendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwa ni lengo  la kuhakikisha huduma za afya zinawafikia watanzainia wote karibu na maeneo wanayoishi.
 
“Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali,hivyo tunaboresha na kuimarisha huduma za tiba na uchunguzi wa magonjwa katika hospitali zetu kuwa na vifaa vya kisasa zaidi na kuondokana na utaratibu wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi”.Alisema,Waziri Ummy Mwalimu.
 
Alisema mashine hizo zitapelekwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa 10 ambazo X-ray za zamani zimekwisha muda wake na zimekua zikiharibika mara kwa mara.Alizitaja hospitali hizo ni Amana, Bukoba, Katavi,Morogoro,Njombe,Ruvuma,Simiyu na Singida pamoja na hospitali  za Wilaya ya Magu na Nzega.
 
Aidha,Waziri Ummy alisema katika bajeti ya mwaka 2018/2019, Wizara yake imepanga kununua mashine za mionzi nyingine zipatazo ishirini na nne(24) zenye thamani ya shilingi bilioni 4.1 ambazo zitapelekwa kwenye hospitali za rufaa za Mikoa na Wilaya ambazo hazina au zina X-ray za kizamani au chakavu.
 
Akizungumza kwa niaba ya Waganga Wakuu wa hospitali   zinazopelekwa mashine hizo,Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Amana Dkt.Mashack Shimwela alisema ujio wa mashine hizo za kisasa zitasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa uchunguzi  za mionzi pia utunzaji wa mazingira tofauti na aina zilizokuwa zikitumika mwanzo
 
Aidha,alisema mashine hizo zina ubora wa picha  pia ina mifumo ya Tehama ambayo ni rahisi kusomwa hata nje ya hospitali husika endapo hakuna msoma picha . 
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu akionesha baadhi ya mashine za mionzi  10 zilizonunuliwa na Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 na kusambazwa kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa,pichani kushoto ni Mwakilishi wa kampuni ya Phillips Bi.Monica Joseph 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu akipewa maelezo mafupi kutoka kwa Muwakilishi wa Kampuni ya Philips Bi. Monica Joseph mara baada ya kukabidhi baadhi ya mashine za mionzi  10 zilizonunuliwa na Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 1.74 na kusambazwa kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa
 Waziri Ummy akiongea na vyombo vya habari wakati wa kupokea mashine hizo za mionzi (digital X-ray) ambazo zitaboresha huduma za afya nchini hususani za uchunguzi wa mionzi
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dkt.Mashack Shimwela,akiongea na waandishi wa habari baada ya kupokea mashine hizo(picha zote na Wizara ya Afya)
SimBanking01

COMMENTS

WORDPRESS: 0
DISQUS: 0