Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesema kuwa ina lengo la kuboresha maisha ya wananchi wa tarafa hiyo kwa kuwaelimisha na kuwahamisha wananchi waliojiandikisha kuhama kwa hiyari kwenda Kijiji cha Msomera Handeni Mkoani Tanga na maeneo mengine nchini.
Akizungumza na wananchi wa tarafa ya Ngorongoro kwa nyakati tofauti katika zoezi la uelimishaji, uhamaishaji na uandikishaji kaimu meneja wa Uhusiano kwa Umma wa mamlaka hiyo Hamis Dambaya amesema zoezi la kuwaelimisha wananchi hao litaendelea ili kuhakikisha kila mkazi wa tarafa ya Ngorongoro anahama kwa hiyari.
Amewaeleza wananchi hao kwamba serikali haina nia mbaya kwa kuwashawishi kuhama kutoka ndani ya hifadhi kwani inatambua kuwa iwapo wananchi hao watakubali kuhama wataweza kuboresha maisha yao katika maeneo mbalimbali watakayoamua kuelekea sambamba na kulinda usalama wao kutokana na uwepo wa matukio ya wanyama wakali ndani ya hifadhi.
“Mnaishi katika mazingira magumu hasa kutokana na kukosa uhuru wa kuingia na kutoka ndani ya hifadhi, kuhofia Wanyama wakali ambao wamekuwa hatari kwa mifugo na baadhi ya wananchi, serikali imefanya uamuzi sahihi wa kuwahamasisha ili kuwa na Maisha bora na huru nje ya hifadhi,”alisema bwana Dambaya.
Bwana Dambaya amesisitiza kuwa serikali imejipanga vizuri katika kuhakikisha kila mwananchi anayekubali kuhama kwa hiyari kutoka ndani ya hifadhi anapata stahiki zake zote za kisheria ikiwemo kitita cha shilingi milioni kumi wanaohamia msomera na shilingi Milioni kumi na tano wanaohamia maeneo mengine ambapo fedha hizi zinatolewa kama motisha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Amewataka wananchi hao kuachana na propaganda za baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wasiowatakia mema kwa kuwashawishi kuendelea kubaki ndani ya hifadhi huku wao na familia zao wakiishi katika miji mbalimbali nchini na kufanya shughuli zao katika mazingira magumu.
“Msihadaike na watu wenye nia ovu wanaowashawishi mbaki ndani ya hifadhi, hameni kwa hiyari kuelekea katika Kijiji cha Msomera na maeneo mengine ambayo huduma za kijamii zimeboreshwa kwa mustakabali wenu na vizazi vyenu”,alisema bwana Dambaya.
Katika ziara hiyo ya tarafa ya Ngorongoro timu ya uhamasishaji imeweza kutembelea kaya mbalimbali katika Kijiji cha Naiyobi, Kapenjiro na endulen ambapo wananchi kadhaa walielimishwa na kukubali kuhama kwa hiyari na kuamua kujiandikisha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 66 kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa miundombinu ya barabara zilizoharibika nchini.
Fedha hizo tayari zimegawanywa kwa mameneja wa TANROADS mikoa yote iliyoathirika kwa ajili ya kufanya kazi kwa haraka usiku na mchana ili kurekebisha kadhia zilizozikumbumba barabara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Akizungumza jana Jijini Arusha mara baada ya kukagua Barabara ya Afrika Mashariki (Arusha bypass) iliyoharibiwa na mvua hizo, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mha. Mohamed Besta amesema kuwa kutokana na udharula huo tayari Rais Samia ametoa fedha za matengenezo ya miundiombinu hiyo ambazo zimeshapelekwa katika Mikoa yote Nchini.
Mhandisi Besta amesema kuwa tayari kazi inaendelea katika maeneo yote nchini na fedha hizo zinaratibiwa na vitengo maalumu vya dharula vilivyopo TANROADS pamoja na ofisi za mikoa.
Ameongeza kuwa kutokana na tathimini iliyofanyika mpaka sasa zaidi ya Shilingi Bilioni 250 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya Barabara kuu za Mikoa yote Nchini ambazo zimeharibika vibaya kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini.
Amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo kama Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu kusini mwa Nchi mvua zimeendelea kunyesha tangu mwezi Oktoba mwaka jana, na sasa unaelekea mwezi wa saba na mvua bado zinaendelea kunyesha.
“Tunamshukuru Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani ametupatia shilingi bilioni 66 ambazo tumezisambaza katika Mikoa yote ambapo mameneja wote wa Mikoa wamepewa kutokana na hali ya dharura ya Mkoa husika’’ ameeleza
Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha Mhandisi Regnald Massawe amesema Mkoa huo umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kazi hizo za dharura na matengenezo ya kurejesha miundombinu hiyo yanaendelea kufanyika kwa kasi.
MKUTANO wa 5 wa Harvard Kennedy School China umefanyika katika Shule ya Harvard Kennedy Usiku wa tarehe 21, Pang Xinxing, Mwenyekiti wa Startimes Group, alialikwa kuhudhuria mtandaoni.
Aidha Lengo Mkutano huo ni kujenga daraja la mawasiliano kati ya China na ulimwengu, kutoa jukwaa rafiki na wazi kwa majadiliano kati ya academia ya kimataifa, serikali, biashara, na viongozi wa jamii.
Kauli mbiu ya mkutano huu ilikuwa "Uaminifu na Ushirikiano," ukiwa na vikao tisa vinavyojadili mada kama "Mahusiano ya Marekani na China," "Uchumi wa Dunia na Uchumi wa China," "Utawala wa Dunia wa Akili Bandia," "China na Kusini Mashariki mwa Asia," "China na Mashariki ya Kati," "China na Afrika," "China na Amerika Kusini," miongoni mwa mengine.
Hafla hiyo ilialika Xie Feng, Balozi wa China nchini Marekani, Graham Allison, mwanzilishi wa Shule ya Harvard Kennedy Graham Allison, Dean Xue Lan wa Chuo Kikuu cha Tsinghua cha Schwarzman, pamoja na wawakilishi kutoka kwa sekta za kisiasa, biashara, na kitaaluma za nchi zote mbili, zaidi ya wanafunzi na wanachama 300 wa fakulteti wa Harvard, na zaidi ya wanafunzi 300 wa Kichina wanaosoma nchini Marekani.
Kupitia mawasiliano na ushirikiano, mkutano ulilenga kupata njia za pamoja za maendeleo.
Kama mwanzilishi wa kampuni inayoongoza ya televisheni ya kidigitali barani Afrika, Pang Xinxing, Mwenyekiti wa Startimes Group, alitoa hotuba mtandaoni katika kikao cha "China na Afrika: Matarajio ya Baadaye," akishiriki safari ya kuanzishwa, kukua, na maendeleo ya biashara ya Afrika ya Startimes Group na washiriki.
Tangu kuanzishwa kwake, imekuwa kikihusika sana katika uga wa utangazaji, televisheni, na vyombo vya habari vipya.
Mwenyekiti Pang Xinxing alitambulisha: "Nchini China, StarTimes imepitia mchakato mzima wa maendeleo ya televisheni ya waya ya Kichina, kutoka kutokuwepo hadi kuwepo, kutoka analogia hadi kidijitali, ikawa msanidi wa mfumo na mtoa teknolojia mwenye athari kubwa katika tasnia ya redio na televisheni ya Kichina."
Barani Afrika, kuanzia kupata leseni ya kwanza ya uendeshaji wa televisheni ya kidigitali nchini Rwanda mwaka 2007, baada ya miaka karibu ishirini ya uendeshaji na maendeleo, "StarTimes imesimamisha jukwaa la usambazaji wa mtandao linalofunika nchi 45 na watu bilioni 1.2 katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Imekuwa kampuni pekee inayotoa huduma za video ndefu za kulipia katika mikoa inayozungumza Kiingereza, Kifaransa, na Kireno barani Afrika kwa wakati mmoja.
Imesimamisha mfumo wa uzalishaji wa yaliyomo kupitia ujumuishaji wa programu, tafsiri ya programu, na uzalishaji wa programu, sasa ikipeperusha seti 830 za vituo vya televisheni vya Kiafrika vya kimsingi, vituo vilivyoendeshwa na StarTimes, na vituo vya kimataifa kwenye jukwaa katika lugha zaidi ya kumi kwa matangazo ya 24 masaa kwa siku.
Imesimamisha mfumo kamili wa masoko na mfumo wa huduma baada ya mauzo, ikiwa ni pamoja na maduka zaidi ya 200 na maduka ya urahisi zaidi ya 30,000, na imeunda wafanyikazi wa 4,000."
Aliyaeleza: "StarTimes imekuwa ikifanya uwekezaji endelevu katika tasnia ya habari ya Afrika na kutoa mchango wake katika digitalization na habari za jamii ya Kiafrika," ikiwa ni pamoja na kuvunja monopolies za tasnia, kukuza upanuzi wa televisheni ya kidigitali barani Afrika, kupunguza kwa kiasi kikubwa vikwazo vya uwekezaji na teknolojia kwa vyombo vya habari vya televisheni vya eneo hilo, kukuza utajiri na maendeleo ya vyombo vya habari vya Kiafrika vya eneo hilo, kuandaa mashindano ya kudubu lugha za Kiafrika ili kuchagua na kutoa mafunzo kwa vipaji vya kudubu vya eneo hilo, kuanzisha vituo vya kudubu katika makao makuu ya StarTimes na mahali pengine barani Afrika kukuza urithi na maendeleo ya utamaduni wa Kiafrika wa eneo hilo, na zaidi.
Leo, StarTimes imekuwa chapa inayojulikana sana barani Afrika Katika ushirikiano unaongezeka kati ya China na Afrika leo, uendeshaji wa StarTimes barani Afrika unaingia kwenye kipindi cha mavuno. Mwenyekiti Pang Xinxing alibainisha, "Kwa kina cha ushirikiano wa kiuchumi na biashara kati ya China na Afrika na kuongezeka kwa usaidizi kwa miundombinu ya nishati barani Afrika na mashirika kama Benki ya Dunia, umeme barani Afrika unazidi kuwa wa kawaida.
Kadiri inavyoendelea, muongo ujao bila shaka utakuwa muongo wa upanuzi wa vituo vya kidigitali (vya akili) vya nyumbani barani Afrika. Tuna imani kamili katika maendeleo ya uchumi wa Kiafrika!"
Mwenyekiti Pang xing xing wa StarTimes Group akitoa hotuba kwenye mkutano) Mkutano wa Harvard Kennedy School China, ulioanzishwa na Chama Kikuu cha Harvard Kennedy Greater China, unazingatia maendeleo ya uchumi, siasa, na utamaduni wa China na nchi za nje
(Washiriki wakisikiliza hotuba na kujadiliana na Mwenyekiti Pang)
Startimes Group ilianzishwa mwaka 1988 na kina historia ya miaka 35.
Matumizi ya Mfumo wa kuwezesha uratibu wa shughuli za uandaaji wa vikao mbalimbali vya bodi na menejimenti katika Halmashauri na Taasisi za Umma. (e-Board), umetajwa kurahisisha uendeshaji wa vikao na kupunguza gharama za maandalizi katika halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza.
Akizungumza kuhusu mfumo huo ofisini kwake jijini Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Bi. Ummy Mohammed Wayayu, amesema kuwa kabla ya halmashauri hiyo kuanza kutumia mfumo wa e-Board mwaka 2023, fedha nyingi zilikuwa zinatengwa katika ununuzi wa shajara,wino na vifaa vingine kwa ajili ya vikao vya madiwani na menejimenti.
“Kwa mwaka tulikuwa tunatumia takribani shilingi milioni 200 hadi 300 katika maandalizi ya uendeshaji wa vikao, lakini kwa sasa gharama hizo hatuna tena kwakuwa tunatumia mfumo huu wa e-Board, ambao umetusaidie kupeleka fedha hizo katika mambo mengine ya muhimu katika halmashauri,” alisema Bi.Ummy.
Aliongeza kuwa, mfumo wa e-Board umesaidia kupunguza gharama za kudurufu taarifa mbalimbali na badala yake zinapakiwa kwenye mfumo na madiwani wanapakuwa na kuendelea kuzifanyia kazi.
Licha ya mfumo huo kusaidia katika kupunga gharama, Mkurugenzi huyo amesema kwamba mfumo wa e-Board umesaidia katika upigaji wa kura za siri katika uchaguzi wa Wenyeviti wa Kamati pamoja na uchaguzi wa Mstahiki Meya.
“Hapo awali usiri katika chaguzi hizo ulikuwa mdogo sana, lakini kwa sasa tunatumia mfumo hivyo kura zinakuwa za siri na kila mtu ndani ya nafsi anajua amemchagua nani,” alifafanua.
Aidha, Bi Ummy aliongeza kuwa mfumo wa e-Board unawasaidia madiwani kushiriki katika kila kikao hata wanapokuwa nje ya halmashauri hiyo kwa kutumia vishkwambi ambavyo vimewezeshwa matumizi ya mfumo huo na kugawiwa kwa kila diwani.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo Mheshimiwa Renatus Mulunga, alisema kuwa mfumo wa e-Board umewasaidia madiwani kuendesha vikao vyao kwa ufanisi ili kuboresha huduma za wananchi wa Ilemela.
“Nina miaka 25 kwenye udiwani, huko nyuma ilikuwa lazima ujaze gari mafuta kwa ajili ya kusambaza makarabrasha, lakini kupitia mfumo wa e-Board kila diwani anapata taarifa na makabrasha yake popote alipo kupitia mfumo na kuanza kuyafanyia kazi,” alisema Bw. Mulunga.
Mhe.Mulunga alitoa rai kwa halmashauri nyingine ambazo bado hazijaanza kutumia mfumo wa e-Board, kufanya ziara halmashauri ya Manispaa ya ilemela ili zikajifunze au kuwasiliana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), ili zipate uelewa kuhusu mfumo huo.
Naye Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Halmashauri ya Ilemela Bw.Isaack Tanguye, alisema kwamba halmashauri hiyo ilianza kutumia mfumo wa e-Board baada ya kupata malalamiko kuhusu gharama kubwa za uandaaji wa vikao.
Alisema kwamba baada ya malalamiko hayo kuwa mengi, kitengo chake kiliamua kuwasiliana na e-GA kuomba mfumo wa e-Board, na baadaye walianza kuwajengea uwezo Madiwani pamoja na Menejimenti ya halmashauri hiyo ili kuanza kufanya vikao vyao kidijiti.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ndiyo halmashauri ya kwanza kuanza kutumia mfumo huu wa e-board kati ya halmashauri 184 nchini, mfumo huu umesanifiwa na kutengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).
TBL walifanya hafla ya kushirikisha wadau jana ili kupitia, kuthibitisha na kuwasilisha mapendekezo kwa Serikali ya Tanzania ili kuwezesha mipango ya kimkataba na masoko yenye umuhimu kuwezesha fedha na uwekezaji kwa wakulima na miundombinu ya kilimo na ugavi, hususani nafaka na mazao mengine. ngano, alizeti, soya, nk).
Msukumo wa ushirikiano huo ni kwamba licha ya uwezekano wa Tanzania kuwa kapu la chakula la kikanda na kuwaunganisha wakulima na viwanda vya ndani na vya kikanda vya mazao kwa ajili ya uongezaji thamani na usindikaji, changamoto za uwezo ndani na kando ya mnyororo wa ugavi zinapunguza hili kutokea.
Changamoto hizi kwa kiasi kikubwa husababishwa na upatikanaji mdogo wa fedha na mitaji kwa wakulima, hasa kwa ajili ya uzalishaji wa kilimo, na kwa ajili ya uwekezaji wa miundombinu ya kilimo ili kuongeza tija na kupunguza hasara baada ya kuvuna.
Mpangilio unaopendekezwa wa kilimo cha mkataba unaohimizwa na ushirikiano hutoa kushughulikia mtaji na upatikanaji wa vikwazo vya kifedha na kuwaingiza wakulima zaidi na wasiochukua katika mipango ya kilimo cha mkataba, kuwezesha uwekezaji wa ugavi, na kuongeza nafaka na uzalishaji mwingine wa mazao.
Mnyororo wa thamani wa shayiri nchini Tanzania unatoa jaribio la kwanza la uboreshaji wa mpango wa kilimo cha kandarasi kama ilivyowezeshwa na ushirikiano huo.
Zao hilo linakabiliwa na ukuaji mkubwa wa mahitaji kutoka kwa TBL ambayo inapanua kiwanda chake cha kutengeneza kimea mkoani Kilimanjaro ambacho kitaongeza mahitaji hadi tani 32 kwa mwaka kutoka kwa usambazaji wa sasa wa tani 3.5 kwa mwaka (ukuaji wa karibu wa 10X).
Kwa sasa sekta hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo za uzalishaji mdogo na uwekezaji, ubora usio thabiti, uratibu hafifu baina ya wahusika, ushiriki mdogo wa wakulima, uhaba wa ardhi inayofaa, utafiti na miundombinu duni, mipangilio dhaifu ya mikataba na changamoto za uagizaji wa bidhaa nje ya nchi.
Mfumo wa kimkataba unaopendekezwa unatumika kama suluhu la sekta kama "chombo" muhimu cha kuwezesha sekta hiyo kukidhi mahitaji ya soko yanayoongezeka.
Ili kusaidia kutekeleza majaribio ya shayiri ya kimea, tukio hilo pia liliidhinisha mkakati kwa watendaji wa sekta ya shayiri ili kukidhi mahitaji ya soko la 10X kwa kutumia mfumo uliopendekezwa wa kimkataba.
Majukumu, majukumu na hatua zinazohusiana zinazokubalika zitafafanua "mkataba wa shayiri" au mpango wa utekelezaji kwa wadau wa sekta ambao utatumika kama msingi wa maendeleo zaidi na uboreshaji kupitia ushirikiano unaoendelea.
Tukio hilo ni nyongeza ya warsha ya siku nne ya kubuni iliyowakutanisha wataalam na watendaji ili kuandaa mfumo wa kuboresha kilimo cha mkataba na mkakati wa kukidhi mahitaji ya shayiri.
Timu ya kubuni suluhisho ilijumuisha wawakilishi kutoka wizara za serikali, mashirika, mamlaka za udhibiti, taasisi za fedha na vyama. Huu ni ushirikiano wa kwanza wa namna hii kuimarisha mifumo ya kilimo cha mkataba nchini Tanzania na unatoa thamani na athari kwa washirika na wadau:
Michelle Kilpin ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania, alisema, “Haja ya TBL kutafuta shayiri ndani ya nchi inaendana na maendeleo ya soko nchini Tanzania ambayo yatawezesha kuongeza uzalishaji wa tani 3,500 za shayiri hadi kufikia karibu tani 20,000 za shayiri kutoka kwa wakulima wengi iwezekanavyo.
"Hata hivyo, kuegemea kutoka kiasi cha sasa hadi kiasi kinacholengwa kutahitaji mabadiliko katika mipangilio ya uuzaji ili kuwezesha uwekezaji katika ubora na uwezo wa mnyororo wa ugavi, kwa kutumia zana za kidijitali kuongeza ufanisi na uwazi, upatikanaji wa fedha kwa wakulima na wengine katika msururu wa ugavi, na ushirikishwaji na uendelevu.”
*Ni katika kutoa vitambulisho Kwa idadi kubwa ya wananchi
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuwa katika miaka 60 Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar mamlaka imepata mafanikio ya kutoa Vitambulisho Kwa idadi kubwa.
Hayo ameyasema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Godfrey Tengeneza wakati akizungumza kuhusiana mafanikio ya mamlaka hiyo.
Tengeneza amesema kuwa hadi kufikia kutoa Vitambulisho hivyo kulitokana na kuweka mipango mikakati na kuweza kufanikisha hilo.
Aidha amesema kuwa katika utoaji vitambulisho ulihusisha vitambulisho vya Uzawa asili na vitambulisho vya wageni waliopo nchini na kukidhi vigezo vya Ukazi.
Amesema katika kufanikisha hilo ni pamoja na Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kuweka jitihada katika kuhakikisha wananchi wanapata vitambulisho wakati awali walikuwa wakitumia namba.
Tengeneza amesema katika mipango mikakati ilikuwa ni kuimarisha ofisi katika Wilaya na Mikoa ambapo ndio kumefanya matokeo chanya bila kukutana na changamoto katika mchakato wa vitambulisho.
Hata hivyo katika 60 ya Muungano Mamlaka inaendelea na kusajili kwa mujibu wa sheria na kutambua vitambulisho vinahitajika katika utambuzi mbalimbali kwa wananchi katika upatikanaji wa huduma za kijamii na biashara.
Tengeneza amesema ametoa hofu ya wananchi kuwa kupata kitambulisho cha Taifa ni haki hivyo hakuhitaji kutumia gharama na kinachohitajika ni kukamilisha nyaraka zinazohitaji kutokana na muongozo wa fumu.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)Godfrey Tengeneza akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na mafanikio katika miaka 60 ya Muungano kwa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.