Na Mwandishi Wetu, Barcelona 


UBALOZI  wa Tanzania nchini Ufaransa ambao unawakilisha pia nchini Uhispania, kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), umeratibu na kuongoza ushiriki wa makampuni kadhaa ya utalii kutoka Tanzania katika Maonesho ya Utalii ya B-Travel yaliyoanza Machi 15 Machi, 2024, mjini Barcelona, Falme ya Uhispania.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ubalozi huo imesema kwamba maonesho hayo ya siku tatu yana lengo la kuwawezesha wenyeji wa Barcelona wenye wa asili ya Catalunya (Catalans) ambao wana desturi ya kutembelea kwa wingi maonesho hayo kutafuta maeneo ya kutembelea wakati wa majira ya kiangazi yanayokaribia kuanza. 

Wakati wa ufunguzi, Waziri wa Biasahara na Kazi Roger Torrent i Ramio alitembelea banda la Tanzania na kushukuru kwa ushiriki wa Tanzania kwa kueleza  Tanzania na Zanzibar ni maeneo yanayovutia watu wengi kuyatembelea kwa sasa na kwamba anategemea mafanikio makubwa ya Tanzania katika sekta ya utalii.

Na Mwandishi wetu, Babati


MKUU wa mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga amesema huduma za afya zimeboreshwa hivi sasa eneo hilo ndiyo sababu wagonjwa na majeruhi wa maafa yaliyotokea Hanang' walitibiwa Manyara.

Maporomoko ya tope kutoka mlima Hanang' yalitokea Desemba 3 mwaka 2023 na kusababisha vifo vya watu 89, wengine kujeruhiwa na wengine kukosa makazi.

Maafa hayo yalitokea jumapili alfajiri na kuathiri miundombinu ya mji mdogo wa Katesh na maeneo ya karibu ya Gendabi, Jorodom, Ganana, Sarijandu na Dumbeta.

Sendiga akizungumza mjini Babati kwenye kikao cha ushauri cha mkoa huo (RCC) amesema wagonjwa na majeruhi, walitibiwa Manyara kwani hawakusafirishwa ila madaktari bingwa ndiyo walikuja Manyara.

Amesema wagonjwa na majeruhi wa maafa ya Hanang' walitibiwa Manyara, kutokana na huduma bora za afya kuboreshwa ikiwemo kuwepo kwa vifaa tiba na dawa.

"Tukiwa tunaadhimisha miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa upande wetu mkoa wa Manyara, tumepiga hatua kubwa atika sekta ya afya," amesema Sendiga.

Amesema mara baada ya tukio hilo wagonjwa na majeruhi wa maafa hayo walipatiwa matibabu kwenye hospitali ya wilaya ya Hanang' (Tumaini).

Amesema wagonjwa na majeruhi wengine walipatiwa rufaa kwenye hospitali ya mkoa wa Manyara iliyopo mjini Babati hivyo hawakutoka nje ya Manyara.

"Wataalamu wa tiba tuu wakiwemo madaktari bingwa ndiyo walitoka nje ya Manyara, ila kwa upande wa dawa na vifaa tiba tupo vizuri, ndiyo sababu wagonjwa na majeruhi wote walitibiwa hapa kwetu," amesema Sendiga.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hanang' Rose Kamili amemshukuru mkuu huyo wa mkoa kwa namna alivyoshiriki ipasavyo katika maafa hayo.

"Tunakushukuru wewe na viongozi wengine wa mkoa huu na wilaya nyingine kwa namna mlivyotukumbatia mara baada ya sisi kupatwa na maafa hayo yaliyoondoka na wapendwa wetu," amesema Kamili.


Na. Mwandishi wetu, Mwanza

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuendeleza ujenzi wa kitega uchumi ambacho ni Hoteli yenye hadhi ya nyota Tano jijini Mwanza (Mwanza Tourist Hotel) ambao ulisimama kwa takribani miaka nane.

Akizungumza Machi 18, 2024 Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Fatma Toufiq, amesema ujenzi huo ukikamilika utachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla.

Awali, akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba Mwaka huu na utazalisha ajira zaidi ya 250.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema Hoteli hiyo inajengwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa na itakuwa na uwezo wa kuhudumia wageni kutoka Mataifa mbalimbali.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba ameihakikishia kamati hiyo kuendelea kusimamia ujenzi wa Hoteli hiyo ili ukamilike kwa wakati.






Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiongea na maafisa uchunguzi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika kikao kazi cha wachunguzi Kilichofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro jijini Arusha tarehe 18 Machi 2024.
Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst.) Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi akiongea na maafisa uchunguzi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika kikao kazi cha wachunguzi Kilichofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro jijini Arusha tarehe 18 Machi 2024.

..........

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Mb) ametoa wito kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Umma kutoka ofisini kwenda kwa wananchi kusikiliza malalamiko yao na kuyatafutia ufumbuzi badala ya kukaa ofisini kusubiri wananchi wachache wanaolalamikia viongozi.

“Sekretarieti ya Maadili nendeni mkawasilikize wananchi, yapo mambo wanayapigia kelele sana kuhusu tabia na mwenendo wa viongozi wao. Kelele zao zinaposikika tokeni mkawasikilize, hii itasaidia kutatua kero zao na mtawasaidia pia viongozi kujirudi na kufuata misingi ya maadii,” alisema.

”Tusichelewe sana kushughulikia malalamiko yanayotolewa na wananchi hadhalani.”

Mhe. Simbachawene alisema hayo jijini Arusha tarehe 18 Machi, 2024 wakatiakifungua kikao kazi cha Wachunguzi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadii ya Viongozi wa Umma.

“Misingi hii lazima tuilinde na hili ndilo jukumu letu. Misingi hii isipozingatiwa, wananchi wanakosa huduma na malengo ya nchi hayatafikiwa,” alisema.



Kwa mujibu wa Mhe. Waziri, lazima watumishi wa Sekretarieti ya Maadili watoe elimu kuhusu misingi ya maadli na kusikiliza changamoto zao.

Katika hatua nyingine Mhe. Simbachawene alisema jukumu la kusimamia maadili linahitaji mtumishi anayetumia mbinu, busara na weledi wa hali ya juu kutokana na kuwahusu viongozi wakubwa na ni la kikatiba.

“Maadili ni zaidi ya sheria, lazima msimamie maadili ya viongozi wote kuanzia ngazi ya chini. Twende mbali tuanzie ngazi ya chini huko serikali za mitaa kusimamia maadili. Tusihangaike na viongozi wanaojaza fomu za Tamko tu kwasababu lazima kiongozi yeyote lazima awe mwadilifu,” alisema na kuongeza kuwa, “maadili katika jamii zetu ni jambo la msingi na lilikuwepo hata wakati wa ujima.”

Awali akimkaribisha Mhe. Waziri, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Sivangilwa Mwangesi alieleza kuwa Taasisi imeona umuhimu wa wachunguzi wote kuwa na kikao cha pamoja kujadili mustakabali wa majukumu yao.

“Hii ni mara yetu ya kwanza tangu Taasisi ilipoanzishwa mwaka 1996 kuwa na kikao kama hiki kwa lengo la kuwakutanisha wachunguzi wote ndani ya Taasisi kujadili kwa kina mambo mbalimbali yanayohusu utendaji wa kazi na mafanikio kwa mujibu wa matakwa ya Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,” alisema.

Kwa mujibu wa kifungu cha 19(2) cha Sheria ya Maadili ya Viongizo wa Umma Na. 13 ya 1995, majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ni kupokea malalamiko ya ukiukwaji wa maadili, kufanya uchunguzi, kupokea matamko, kufanya uhakiki na kutoa elimu ya maadili.

Majukumu mengine ni kufanya utafiti wa hali ya uadilifu nchini, kutoa ushauri katika mambo ya uadilifu na kubuni mikakti ya ukuzaji maadili.

Mhe. Sivangilwa alizitaja mada zitakazo wasilishwa kuwa ni; Utendaji katika Ofisi za Kanda, Viambata vya Makosa ya Maadili, Utaratibu wa zoezi la Uhakiki, Mikakati ya utendaji kazi pamoja na Changamoto na utatuzi wake katika kushughulikia malalamiko na uchunguzi.



Na Benny Mwaipaja, Dodoma

WAZIRI wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameishukuru Denmark kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mheshimiwa Mette Dissing-Spandet, Ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo walijadili masuala kadhaa ya ushirikiano.

Alisema kuwa uhusiano wa Tanzania na Denmark umetimiza miaka 60 na katika kipindi hicho nchi hizo mbili zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na kiuchumi ambapo hivi karibuni nchi hizo zilikuwa zikitekeleza miradi ambayo Denmark iliipatia Tanzania msaada wa takriban Denish Krone bilioni 2, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 646.

Aidha, Dkt. Nchemba alisema kuwa Denmark kupitia Shirika ake la Maendeleo (DANIDA), imetoa zaidi ya shilingi bilioni 103 zinazotokana na mapato ya uwekezaji wake wa hisa katika Benki ya CRDB, ambazo zimetumika kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya kupitia Mfuko wa Afya.

Aidha, aliipongeza Denmark kwa kusitisha uamuzi wake wa kutaka kufunga Ubalozi wake hapa nchini na kwamba hatua hiyo itaimarisha zaidi ushirikiano kwa manufaa ya wananchi wa pande hizo mbili.

Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na Denmark kupitia mpango wake mpya wa ushirikiano baada ya kusitisha uamuzi huo wa kufunga ubalozi wake nchini ambapo nchi hiyo imepanga kuongeza kiwango cha ufadhili na kuelekeza fedha hizo kwenye maeneo yatakayokuza uchumi, ikiwemo nishati, kuboresha mifuko ya kodi, kilimo, elimu, afya, pamoja na kusaidia sekta binafsi.

Dkt. Nchemba pia alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka Denmark kuja kuwekeza mitaji yao hapa nchini ikiwemo sekta ya fedha na kunufaika na vivutio vilivyowekwa na Serikali baada ya kurekebisha sheria kadhaa, lakini pia kunufaika na soko la uhakika linalopatikana katika nchi za SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Aliiomba pia Denmark kupitia Taasisi yake inayohusika na masuala ya Bima na Dhamana (Danish Export Credit Agency), kushiriki katika ujenzi wa mradi wa SGR kwa vipande vilivyobaki kutokana na umuhimu wa mradi huo katika kukuza biashara na ustawi wa maisha ya watu watakao tumia reli hiyo pamoja na kukuza pato la Taifa.

Kwa upande wake, Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mheshimiwa Mette Dissing-Spandet alisema kuwa nchi yake inapongeza mafanikio makubwa ya kiuchumi na kijamii yanayoendelea hivi sasa na kwamba iko tayari kutoa ushirikiano unaohitajika ili kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi hizo mbili.
Mheshimiwa Spandet alisema kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika eneo la nishati jadidifu, pamoja na gesi na kusaidia kukuza sekta binafsi ili iweze kuchangia maendeleo ya nchi.

Alisema kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo Kimataifa, Mhe. Dan Jorgensen, anatarajia kufanya ziara rasmi ya kikazi hapa nchini mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu, ambapo atatumia ziara hiyo kujadiliana na Serikali maeneo ya kipaumbele ambayo nchi hizo zitajielekeza katika mpango huo mpya wa ushirikiano.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa Mkutano na Balozi wa Denmark hapa nchini, Mhe. Mette Dissing-Spandet, ambapo ameishukuru nchi hiyo kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida. Mkutano huo umefanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, Jijini Dodoma.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Mette Dissing-Spandet, akizungumza wakati wa Mkutano wake na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ambapo alisema kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika eneo la nishati jadidifu, pamoja na gesi na kusaidia kukuza sekta binafsi ili iweze kuchangia maendeleo ya nchi. Mkutano huo umefanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, Jijini Dodoma.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kulia), ukiwa katika Mkutano na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Denmark nchini, ukiongozwa na Balozi wake, Mhe. Mette Dissing-Spandet, mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akiagana na Balozi wa Denmark hapa nchini, Mhe. Mette Dissing-Spandet, baada ya Mkutano wao uliofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, Jijini Dodoma. Katika Mkutano huo Mhe. Dkt. Nchemba, aliishukuru nchi hiyo kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), akifurahia jambo na Balozi wa Denmark hapa nchini, Mhe. Mette Dissing-Spandet (kushoto) na Mkuu wa masuala ya Biashara wa Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania, Bw. Oscar Mkude, baada ya Mkutano wao uliofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) na Balozi wa Denmark hapa nchini, Mhe. Mette Dissing-Spandet (wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mkuu wa masuala ya Biashara-Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania, Bw. Oscar Mkude (wa nne kulia) baada ya kufanya mazungumzo yao, ambapo Dkt. Nchemba, ameishukuru nchi hiyo kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida. Mkutano huo umefanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, Jijini Dodoma.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, WF, Dodoma)
Na Mwandishi Wetu

WAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video ya wimbo wao mpya unaoitwa Bwana Wastahili.

Video ya wimbo huo imeachiwa leo Machi 18,2024 saa mbili usiku na imerekodiwa katika Studio ya Flying Wave Studio na kuongozwa na Director maarufu ajulikanae kama Director Joowzey.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya video hiyo kuachiwa hewani(kuzinduliwa) Mwenyekiti wa Gethsemane Group Kinondoni GGK Geoffrey Joseph amesema ni furaha kwao kuja na video ya wimbo huo ambayo imebeba ujumbe wa kumuabudu na kumtukuza Mungu.

"Ujumbe mkubwa kwenye wimbo huu ni kwamba Mungu pekee ndie anastahili kuabudiwa na yeye ndiye anatosha kwa kila kitu hasa kipindi hiki ambacho baadhi ya madhehebu wapo Kwenye mfungo, tunaamini wimbo huu ni ibada na utawasogeza karibu zaidi na Mungu,"amesema Joseph

Aidha ametoa neno kwa wasikilizaji na watazamaji wa video ya wimbo huo kutambua hakuna yoyote anayestahili kuabudiwa zaidi ya Mungu pekee.


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa ukusanyaji data za wamama wajawazito leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utafiti,Machapisho na Ushauri Prof.Pendo Kasoga ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa ukusanyaji data za wamama wajawazito leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha UDOM ndaki ya TEHAMA na Elimu Angavu Dkt.Rukia Mwifunyi ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa ukusanyaji data za wamama wajawazito leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Ang'avu Dkt.Florence Rashid ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa ukusanyaji data za wamama wajawazito leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mpango wa ukusanyaji data za wamama wajawazito leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka amezindua mpango wa ukusanyaji data za wamama wajawazito ambazo zitasaidia kutengeneza moduli itakayosaidia wajawazito wengine kujua vitu hatarishi wakati wa ujauzito ili kupunguza matatizo yanayotokana na mimba kuharibika na matatizo mengine wakati wa ujauzito.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo Machi 18,2024 katika chuo hicho Prof. Kusiluka amesema mradi huo unalenga katika matumizi ya teknolojia ya akili bandia katika kutatua changamoto mbalimbali zimazoikumba sekta ya afya hasa upande wa wakina mama wakiwa wajawazito.

Amesema wataalamu kutoka UDOM kwa kushirikiana na wataalamu kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI na hospitali ya taifa Muhimbili waliandika wazo la mradi huo na kulipeleka kwenye shirika linaloitwa LACUNA la Marekani ili kuomba fedha kwaajili ya kutengeneza mfumo huo.

“Wahudumu wetu katika afya kwamaana ya madaktari, manesi na wakunga waweze kutabiri kabla ya hatari haijafika kuhusu hali ya afya ya mama mjamzito,”amesema.

Sambamba na hayo amaeongeza kuwa lengo la muda mrefu ni kuokoa maisha ya wakina mama pamoja na watoto pamoja na kuipongeza Serikali kwa jitihada zake inazozifanya kuendelea kuimarisha sekta ya afya kwa kutoa huduma bora kwa watanzania.

Amesema uanzishwaji wa mradi huo ni sehemu utekelezaji wa mpango mkakati wa chuo cha UDOM pamoja na mpango watatu wa maendeleo ya taifa ambao unatambua kuwa TEHAMA ni nyenzo muhimu katika kutatua changamoto ambazo dunia kwa ujumla inazipata.

“Akili bandia ni teknolojia ambayo imekuja huku kwetu lakini haina muda mrefu lakini imekuja kwa namna mbili kuna wengine hasa kwa elimu ya juu kuna woga kwamba tutafundishaje na tutajuaje kama wale tunaowafundisha watatumia atatumia akili bandia kweli ni wao walioelewa hiyo ni aina moja ya changamoto,"amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya utafiti, machapisho na ushauri Prof. Pendo Kasoga ameeleza kuwa 18% ya wanawake wote kati ya miaka 15 - 49 Duniani hasa nchini Tanzania wanapoteza maisha wakati wa kujifungua hususani wale walioko mbali na vituo vya Afya.

“Kwa lugha rahisi unaweza kusema ni kati ya wanawake 578 kati ya wanawake 100,000 wanakufa wakati wa kujifungua, sasa tunaweza kuona kuwa hili ni tatizo kubwa kwa wanawake hususani wale walioko mbali na hospitali,”amesema.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha UDOM ndaki ya TEHAMA na Elimu Angavu Dkt. Rukia Mwifunyi amesema mradi huo utafanyika kwa mwaka mmoja pekee ambapo taarifa zitaenda kukusanywa kwa muda wa miezi Tisa.

Amesema miradi huo umejikita katika kuandaa takwimu ambazo zitatumika kutabiri viatarishi ambavyo vinaweza kujitokeza wakati wa kijifungua baada ya kujifungua na wakati mama akiendelea na kliniki.

“Kwahiyo tutaanza kukusanya taarifa za wakina mama kuanzia pale anaanza kliniki siku ya kwanza taarifa zake zitakusanywa na kila atakapokuwa anaenda kliniki na wakati anajifungua taarifa zitachukuliwa na mwezi mmoja baada ya kujifungua na taarifa hizi zitatumika kwaajili ya kutengeneza model ambayo itatumika katika kufanya maamuzi ya kujua huyu mama anastahili kupata matibabu ya aina gani”,amesema.

 Raisa Said,Tanga

Tanzania tayari imeanza kunufaika na mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 4, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Balozi Ombeni Sefue.

Akizungumza katika ziara ya Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), inayoongozwa na Mbunge wa Jimbo la Kwela, Deus Clement Sangu, Balozi Sefue alisema pamoja na utekelezaji wa mradi huo kufikia asilimia 27, ushiriki wa nchi katika mradi huo unaleta manufaa mengi yanayoonekana. .

Balozi Sefue alitaja baadhi ya faida hizo kuwa ni zaidi ya trilioni 2.4 zinazokadiriwa kupatikana kutokana na mradi huo, pamoja na ajira za Watanzania 4,968 tangu kuanzishwa kwa mradi huo mwaka 2021.

“Hii imechochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika mikoa inayohusika na mradi huo,” alibainisha. Alibainisha kuwa mradi huo umeajiri wazawa 385 katika Jiji la Tanga kati ya 539 katika eneo la ujenzi wa jengo hilo. “Kadhalika mkandarasi wa ujenzi wa tanki la mafuta amelipa gharama za huduma kiasi cha 53.15M/ Halmashauri ya Jiji la Tanga hadi sasa,” alisema Balozi Sefue.

Balozi Sefue pia alitaja faida nyingine kuwa ni pamoja na watoa huduma mbalimbali kunufaika na Dola za Kimarekani milioni 171.71 zilizotolewa kwa wakandarasi wa ndani, ambapo jumla ya Dola milioni 462 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa huduma na bidhaa mbalimbali.

Kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi huo, wajumbe wa Kamati ya PIC pia walielezwa kuwa mambo kadhaa ya mradi huo, kama vile ujenzi wa kambi na kuhifadhi mabomba yamekamilika kwa asilimia 100.

“Ujenzi wa Kiwanda cha Kupitishia Mifumo ya joto (TIS) umefikia asilimia 61, na mtambo huo uko tayari kwa majaribio,” alisema na kuongeza kuwa mabomba yenye uwezo wa kulazwa kwa umbali wa kilomita 280 yamefika katika kiwanda cha TIS, tayari kwa kufungwa. na mfumo wa kuhifadhi mafuta kabla ya kazi ya kuwekewa bomba kuanza Mei mwaka huu.

Matenki yatakayopelekwa katika kituo cha kupokea na kuhifadhi mafuta cha Chongoleani (MST) yapo katika hatua ya ujenzi, huku asilimia 32 ya kazi ikiwa imekamilika, huku gati ya kupakia mafuta ikiwa imekamilika kwa asilimia 36.

Balozi Sefue aliupongeza mradi huo kwa kuwa ni Ubia wa kweli wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) si tu Tanzania bali hata katika mataifa hayo mawili washirika, na kueleza kuwa yanadhihirisha jinsi diplomasia inavyoweza kusogeza mbele michakato.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Musa Makame, alieleza kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania tayari imepata 30 billion kutokana na mradi huo na watoa huduma wengine na inatarajia kukusanya zaidi kadri ujenzi unavyoendelea hadi kukamilika.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deus Clement Sangu, alieleza kuridhishwa na Tanzania kuwa imeanza kufaidika na mradi huo ambao umekuwa na upinzani mkubwa kimataifa.

Alieleza kuridhishwa na Tanzania kupitia TPDC, kama mwanahisa, inaendelea kushirikiana na wanahisa wengine kuhakikisha mradi huo unafikia malengo yake. Alieleza kuwa alifahamishwa kuwa hadi Machi 15, mwaka huu, TPDC ilichangia jumla ya dola za Marekani milioni 268.78, ambayo ni asilimia 87 ya Dola za Marekani milioni 308 ambazo Tanzania ilipangwa kuchangia kama mtaji.

Wawekezaji binafsi wanatekeleza mradi huo kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania na Uganda. TPDC na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) zinamiliki asilimia 15 kila moja, TotalEnergies ya Ufaransa inamiliki asilimia 62, na Shirika la Mafuta la China National Offshore Oil Corporation (CNOOC) linamiliki asilimia 8.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Chongoleani, Ambari Mabruki Hoza, ambaye pia ni Maalim Ashraf Mabano, aliipongeza Serikali kwa kuanzisha mradi huo ambao alieleza kuwa umeanza kutoa zawadi. Hata hivyo, ameitaka EACOP kuangalia namna ya kuwajengea wananchi vifaa vya kisasa vya uvuvi na ufugaji utakaoboresha maisha yao.

Naye Diwani wa Kata ya Chongoleani Kassim Mbega ameihimiza serikali au mradi huo kufikiria kujenga kituo cha afya kwa manufaa ya jamii na watendaji wa mradi huo. Alieleza kuwa inasikitisha kuwa tangu kuanza kwa mradi huo mamlaka husika hazijafikiria kupanua huduma ya afya ambayo leo inakabiliwa na ongezeko kubwa la watu.





 

KATIBU Mkuu wa Maji Mhandisi Mwajuma Waziri,akionyesha Muongozo wa Taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 mara baada ya kuuzindua leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Maji Mhandisi Mwajuma Waziri,akizungunmza wakati akizindua Taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hafla iliyofanyika leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Maji Mhandisi Mwajuma Waziri,akisisitiza jambo wakati akizindua Taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hafla iliyofanyika leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Prof.Mark Mwandosya,akizungunmza wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hafla iliyofanyika leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt.James Andilile,akiwasilisha Muhtasari wa Ripoti ya Utendaji wa Mamlaka za Maji kwa Mwaka 2022/23 wakati wa uzinduzi wa Ripoti hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hafla iliyofanyika leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Omar Ali Yussuf,akizungunmza wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hafla iliyofanyika leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

MKURUGENZI wa Maji na Usafi wa Mazingira-EWURA,Mhandisi Exaud Maro,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hafla iliyofanyika leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

BAADHI ya Washiriki wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Maji Mhandisi Mwajuma Waziri (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hafla iliyofanyika leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Maji Mhandisi Mwajuma Waziri,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hafla iliyofanyika leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Maji Mhandisi Mwajuma Waziri,akionyesha Muongozo wa Taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 mara baada ya kuuzindua leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Maji Mhandisi Mwajuma Waziri,akikabidhi tuzo (Vyeti na Ngao) kwa Mamlaka za Maji zilizofanya vizuri kwa mwaka 2022/23 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 iliyofanyika leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Maji Mhandisi Mwajuma Waziri,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hafla iliyofanyika leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

Na.Mwandishi Wetu-DODOMA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amezindua ripoti ya 15 ya utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Akizungumza leo Machi 18,2024 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi huo Mhandisi Mwajuma amewaagiza wakurugenzi wa Mamlaka za majisafi nchini kuhakikisha kuwa wanatatua tatizo la upotevu wa maji nchini kwani kiasi kinachotakiwa ni asilimia 20 lakini kuna baadhi ya mamlaka zinapoteza asilimia 37.2 za maji yanayozalishwa.
Amesema kiasi hicho ni kikubwa na kinaathiri upatikanaji wa huduma za majisafi kwa wananchi hivyo hatua za mapema zichukuliwe ili kupunguza kiwango hicho cha upotevu wa maji.
"Nazitaka mamlaka hizo kutoa elimu kwa jinsi ya kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya matumizi wakati wa ukame kwani maji mengi ya mvua huwa yanapotea na kusababisha madhara kwenye miundombinu ambayo yakivunwa yatasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa maji nchini."amesema Mhandisi Waziri
Aidha amesema kuwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya mwaka 2030 na hususan Lengo Namba 6 linaeleza umuhimu wa Majisafi na Usafi wa Mazingira.
Amesema kuwa lengo hilo linasisitiza kuhakikisha uwepo na usimamizi endelevu wa maji na usafi wa mazingira kwa wote ikiwa ni pamoja na watu wote kuwa na uhakika wa upatikanaji wa majisafi na salama ya kunywa kwa bei nafuu ifikapo mwaka 2030.
“ EWURA inategemewa katika utekelezaji wa lengo hili ukiacha wadau wengine kwani ndiyo iliyopewa dhamana ya udhibiti wa sekta hii nyeti. Tumeshuhudia tangu EWURA ianze kuzisimamia mamlaka za maji nchini, kumekuwa na maboresho ya utendaji wa mamlaka hizi. Ni kwa msingi huu, naendelea kuipongeza EWURA na kuitaka iendelee kufanya kazi ya udhibiti kwa uwazi, ufanisi, weledi na tija kama ilivyoainishwa kwenye dhamira ya kuanzishwa kwake ili pia kumsaidia Mheshimiwa Rais kutekeleza Ilani,’’ amesema Mhandisi Waziri
Amesema kuwa Taarifa hiyo inaonesha kuimarika kwa baadhi ya viashiria vya utendaji kwenye Mamlaka za Maji ikilinganishwa na Mwaka wa Fedha 2021/22 na kuzipongeza mamlaka za maji kwa kuendelea kuboresha utendaji kazi wao katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Pia amezitaka Mamlaka za Maji kuzingatia miongozo mbalimbali ya kudhibiti upotevu wa maji ambayo hutolewa na EWURA kama vile Mwongozo wa kupunguza upotevu wa maji wa mwaka 2021 ambao unazitaka Mamlaka za Maji kuandaa mizania ya kupima viwango vya upotevu wa maji kwa mujibu wa mwongozo wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wataalam wa Maji (IWA).
“Pamoja na kumairika kwa baadhi ya viashiria vya utendaji wa mamlaka za maji ambavyo baadhi nimevitaja hapo awali, nimesikitishwa na kuendelea kuzorota kwa baadhi ya viashiria hivyo pamoja na kushindwa kufikiwa kwa malengo ambayo mamlaka hizo zilijiwekea,
Na kuongeza kuwa “taarifa inaonesha kuwa, upotevu wa maji dhidi ya kiwango cha maji kinachozalishwa umeongezeka kutoka asilimia 35.5 mwaka 2021/22 hadi kufikia asilimia 37.2 mwaka 2022/23. Ndugu zangu hii haikubaliki hata kidogo. Sote tunajua kiwango cha upotevu wa maji kinachokubalika ni chini ya asilimia 20. Ni lazima mamlaka za maji ziweke na kutekeleza mikakati ya kuhakikisha zinapunguza kiwango cha upotevu wa maji,” ameeleza Mhandisi Mwajuma
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt. James Andilile amesema taarifa iliyozinduliwa leo ni ya 15 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo miaka 18 iliyopita na inahusisha uchambuzi wa utendaji wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira 85 zikiwemo; mamlaka 25 za mikoa, saba (7) za miradi ya kitaifa, 47 za wilaya na Sita (6) za miji midogo.
Dkt.Andilile amesema kuwa kwa ujumla, utendaji wa mamlaka za maji na usafi wa mazingira umeendelea kuimarika ambapo kwa mwaka 2022/23, Mamlaka za Maji 78 kati ya 85 zilipata alama kuanzia wastani hadi vizuri sana katika utendaji wa ujumla ikilinganishwa na mamlaka 77 kati ya 90 kwa mwaka 2021/22.
Aidha amesema mafanikio mengine yaliyofikiwa ni kuimarika kwa uwiano wa maunganisho yaliyofungwa dira za maji kufikia asilimia 92 ikilinganishwa na asilimia 90, Kuongezeka kwa kiwango cha ubora wa maji yanayosambazwa kwa wateja kutoka asilimia 91 hadi 94 na kuongezeka kwa wateja wa maji wa majisafi kutoka 1.3 hadi 1.5 asimia 11
Pia amesema kumekuwa na ongezeko kwa wateja wa maji wa majisafi kutoka kutoka 1,385,485 hadi 1,532,362 sawa na asilimia 11 na kuongezeka kwa wateja wa mtandao wa uondoaji majitaka kutoka wateja 55,996 hadi wateja 56,899 sawa na asilimia 16.
Amesema pia kumekuwa na ongezeko la wateja wa mtandao wa uondoaji majitaka kutoka wateja 55,996 hadi wateja 56,899 sawa na asilimia 16 japo bado kuna uchache wa miundombinu ya kutibu majitaka na topetaka kinyesi.
“Naomba nitumie fursa hii kumpongeza na kumshukuru Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wewe Mheshimiwa Waziri kwa usimamizi wako mahiri wa sekta ya maji kwa kufanya uwekezaji mkubwa kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani na kuimarisha ustawi wa watanzania wote, kwani maji ni UHAI.,” amesema Dkt. Andilile
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Omar Ali Yussuf,amesema kuwa EWURA imekuwa ikifanya kazi kubwa ambayo inaleta heshima kwa taifa la Tanzania.
"Niseme tu wazi kwamba EWURA imekuwa ni kioo kwa nchi nyingi sana za Afrika mashariki,tumekuwa tukipata hizi katika maeneo ambayo tumekuwa tunakwenda lakini nyie wenyewe pia ni mashahidi kwa wale ambao wanakuja kujifunza kupitia kwenu nyie,"alisema.
Pia amesema kuwa suala la maji ni suala ambalo linamgusa kila kiumbe hai katika dunia pia alisema kuwa jamii yote inahitaji maji hivo suala la maji ni suala muhimu katika Nchi.
Pia Uzinduzi huo umekwenda sambamba na utoaji wa tuzo mbalimbali Kwa Mamlaka zilizofanya vizuri huku zikigawanywa katika makundi Matatu tofauti kulingana na idadi ya wateja inayowahudumia ambapo kundi la kwanza ni Mamlaka za maji zenye wateja chini ya 5000, kundi la pili ni mamlaka za maji zenye wateja chini kati ya 5000 na 20,000 na kundi la Tatu ni mamlaka za maji zenye wateja zaidi ya 20,000.
MAMLAKA AMBAZO HAZIKUFANYA VIZURI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA YA MAJISAFI KWA MWAKA 2022/23. MAMLAKA HIZO NI
SONGE iliyoshika nafasi ya 48 miongoni mwa mamlaka za maji 48 zenye wateja chini ya 5000.
“kundi la III la Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira”.
KOROGWE iliyoshika nafasi ya 18 miongoni mwa mamlaka za maji 18 zenye wateja chini kati ya 5000 na 20,000. “kundi la II la Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira”.
ROMBO iliyoshika nafasi ya 19 miongoni mwa mamlaka za maji 19 zenye wateja zaidi ya 20,000. “kundi la I la Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira”.
MAMLAKA ZA MAJI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUTOA HUDUMA
Mamlaka zilizofanya vizuri zaidi katika katika utoaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira, washindi katika Kundi la Kwanza yaani Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za zenye wateja zaidi ya 20,000. Kundi hili lina jumla ya Mamlaka za Maji 19
TANGA imekuwa mshindi wa Tatu: Imezadiwa Cheti
MOSHI imekuwa mshindi wa Pili: Imezadiwa Cheti
IRINGA imekuwa mshindi wa Kwanza: Imezadiwa Ngao na Cheti
Washindi katika Kundi la Pili yaani Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za zenye wateja zaidi kati ya 5,000 na 20,000. Kundi hili lina jumla ya Mamlaka za Maji 18
BUSEGA imekuwa mshindi wa Tatu: Imezadiwa Cheti
IGUNGA imekuwa mshindi wa Pili: Imezadiwa Cheti
NZEGA imekuwa mshindi wa Kwanza: Imezadiwa Ngao na Cheti
Washindi katika Kundi la Tatu yaani Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za zenye wateja chini ya 5,000. Kundi hili lina jumla ya Mamlaka za Maji 48
LOLIONDO imekuwa mshindi wa Tatu: Imezadiwa Cheti
MASWA imekuwa mshindi wa Pili: Imezadiwa Cheti
BIHARAMULO imekuwa mshindi wa Kwanza: Imezadiwa Ngao na Cheti
MAMLAKA ZA MAJI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUFIKIA MALENGO YA KIUTENDAJI
Mamlaka zilizofanya vizuri zaidi katika kufikia malengo ya kiutendaji (performance targets) katika utoaji wa huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira naomba uzipatie cheti.
Washindi katika kundi la Kwanza
KASHWASA imekuwa mshindi wa Tatu
BABATI imekuwa mshindi wa Pili
TABORA imekuwa mshindi wa Kwanza
Washindi katika kundi la Pili. Hawa nao wanapata Cheti
MTWARA imekuwa mshindi wa Tatu
WANGING’OMBE imekuwa mshindi wa Pili
LINDI imekuwa mshindi wa Kwanza
Washindi katika kundi la Tatu. Hawa nao wanapata Cheti
TUNDUMA imekuwa mshindi wa Tatu
BIHARAMULO imekuwa mshindi wa Pili
MBINGA imekuwa mshindi wa Kwanza
MAMLAKA ZA MAJI ZILIZOFANYA VIZURI KATIKA KUWASILISHA TOZO YA UDHIBITI
Mamlaka za Maji zilizofanya vizuri katika uwasilishaji wa tozo ya udhibiti, naomba uzipatie cheti. Mamlaka hizi ni Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira;
Babati, Loliondo, Mbeya, Makambako, Itumba-Isongole, Orkesumet, Tukuyu, Turiani, Morogoro na Ruangwa

Top News