Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi akiwasilisha hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la TCAA linalofanyika Morogoro
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la TCAA wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi akiwasilisha hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo

Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wamepongezwa kwa kuendelea kufanya Baraza la Wafanyakazi lenye tija na kuhimizwa kuendelea kuwajibika ili kuwa chachu ya maamuzi makubwa ya kuboresha uboreshwaji wa huduma za Usafiri wa Anga nchini.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la TCAA uliofanyika Aprili 23,2024 mjini Morogoro.

Pia ameongeza kuwa, kufanyika kwa vikao hivyo vya Baraza ni kuimarisha demokrasia mahala pa kazi,na kuwataka wajumbe wa Baraza hilo kurudisha mrejesho kwa watumishi wenzao ambapo pia amewahimiza watumishi wa TCAA kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kutenda kazi kwa ufanisi.

"Tunatambua umuhimu wa TCAA katika maendeleo ya nchi yetu lakini TCAA inajengwa kuianzia na wewe mtumishi mmoja, nawasihi sana mfanye kazi kwa kushirikiana kila mmoja kwa nafasi yake na inapobidi msaidie mwingine ili kuhakikisha malengo ya taasisi na serikali kwa ujumla yanafikiwa na huduma inatolewa" amesema Dkt. Possi.

Awali akizungumza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Daniel Malanga amesema Mamlaka inatekeleza Mradi wa ufungwaji wa mitambo ya Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya Sauti kati ya Rubani na Mwongoza ndege yaani VHF Radio Communication Systems ili kuboresha huduma ya Uongozaji Ndege katika Anga la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hii ikiwa na lengo la kuboresha mawasiliano katika anga la Tanzania.

“Mradi huu unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali kuu kwa fedha za kitanzania bilioni 31.5 ambapo Mamlaka iliandaa mahitaji yaani specification na kutangaza tenda shindanishi ambapo Kampuni ya Jotron AS ya Nchini Norway ilishinda zabuni na kuingia nayo mkataba na utakelezaji ulianza mara moja”

Mkurugenzi Malanga ameongeza kuwa,vingine ni kuendelea kutolewa kwa mafunzo kwa wataalam wa Usafiri wa Anga.

Na pia Bw. Malanga amezitaja baadhi ya changamoto hasa suala la upatikanaji na ucheleweshaji wa upatikanaji wa vibali vya ajira na upandaji wa madaraja kwa Watumishi wa TCAA. Kitendo ambacho kinashusha ari ya watumishi.

Baraza hilo linafanyika kwa siku mbili ambapo mbali na kujadili masuala kadhaa yanayoihusu TCAA wajumbe wamepata nafasi ya kupiga kura na kumchagua mfanyakazi bora wa Mamlaka kwa mwaka huu wa fedha.
Katibu wa Baraza Bw. Didacus Mweya (aliyesimama) akitoa salamu za utangulizi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi kwa niaba ya wajumbe wa Baraza

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Daniel Malanga akiwasilisha hotuba ya Mkurugenzi Mkuu mbele ya Mgeni Rasmi pamoja na Wajumbe wa Baraza


Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la TCAA wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Daniel Malanga
Picha ya Pamoja

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

TAASISI ya HakiElimu imependekeza kwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu kutenga Bajeti mahususi kwaajili ya kuhuisha mpango wa tatu wa Maendeleo ya Sekta ya elimu au kuandaa mpango wa nne wa Maendeleo ya Sekta ya elimu katika mwaka wa fedha mpya kwenye sera na Mtaala husika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage alisema serikali inapoelekea katika upangaji wa Bajeti ya Sekta ya elimu kwa mwaka wa fedha 2024/25 inapaswa kuzingatia mchakato wa utengenezaji wa Dira ya maendeleo ya Taifa 2025 lakini pia kuanza kwa utekelezaji wa mitaala na sera mpya ya elimu 2023.

Aidha amesema Serikali kupitia ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) imeongeza Tahasusi mpya 49 za kidato Cha Tano kutoka 16 zilizokuwepo awali hadi kufikia Tahasusi 65.

"Kama serikali inakusudia kuanza utoaji wa Tahasusi hizo zote ni muhimu kupanga na kutenga Bajeti maalum katika mwaka wa fedha 2024/25 kwaajili ya mambo mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo kazini kwa walimu waliopo, kuajiri walimu wapya wenye ujuzi na umahiri katika Tahasusi husika lakini pia kuwa na mpango maalumu wa Kuhamasisha udahili wa wanafunzi wa ualimu vyuoni ili kuendelea kutengeneza walimu wenye ujuzi kulingana na mabadiliko hayo". Amesema 

Pamoja na hayo, HakiElimu imependekeza pia Bajeti kwaajili ya uchapaji na usambazaji wa vitabu vya Kiada shuleni, ambapo wameiomba serikali katika Bajeti ya Sekta ya elimu mwaka wa fedha 2024/25 watenge Bajeti maalumu kwaajili ya uchapaji na usambazaji wa vitabu hivyo mashuleni hasa kwa kuzingatia kuwa vitabu hivyo ni vipya hivyo shule hazina akiba ya vitabu mbadala.

Pia wameiomba serikali kuweka mpango maalumu wa usambazaji wa vitabu hivyo mashuleni ukiainisha muda mahususi wa ukamilishaji wa zoezi hilo

Mbali na hayo, Hakielimu wamependekeza ujumuishi wa teknolojia katika utekelezaji wa mtaala mpya wa Elimu, ambapo imeishauri serikali kupitia Wizara za Sekta ya elimu kutenga Bajeti kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu ya shule ya msingi na sekondari ili kuziandaa na utoaji wa Elimu kwa Mtaala mpya na matumizi ya teknolojia.

Vilevile HakiElimu imependekeza Serikali itenge Bajeti kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia vya teknolojia lakini pia kuanzisha vipindi vya ujuzi wa matumizi ya mtandao ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na umahiri wa kutumia mtandao kwa usahihi, uwezo wa kutatua matatizo na uwezo wa kujifunzia.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 wakati wakitoa mapendekezo  juu ya  upangaji  na utendaji bajeti  ya sekta  ya Elimu  ya Mwaka  wa Fedha 2024/25.
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 wakati wakitoa mapendekezo  juu ya  upangaji  na utendaji bajeti  ya sekta  ya Elimu  ya Mwaka  wa Fedha 2024/25.
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 wakati wakitoa mapendekezo  juu ya  upangaji  na utendaji bajeti  ya sekta  ya Elimu  ya Mwaka  wa Fedha 2024/25.
Mkuu wa Miradi HakiElimu, Godfrey Boniventura akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 wakati wakitoa mapendekezo  juu ya  upangaji  na utendaji bajeti  ya sekta  ya Elimu  ya Mwaka  wa Fedha 2024/25.


Meneja Idara ya Utafiti, Uvumbuzi na Uchambuzi wa Sera- Hakielimu, Bw. Makumba Mwemezi akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 wakati wakitoa mapendekezo  juu ya  upangaji  na utendaji bajeti  ya sekta  ya Elimu  ya Mwaka  wa Fedha 2024/25.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


Na Mwandishi wetu, Mirerani

Viongozi wa dini, wa Serikali, wanachama na wakereketwa wa CCM wa Wilaya ya Simanjiro, Mkoani Manyara, wamefanya maombi ya kuliombea Taifa kwa kutimiza miaka 60 ya muungano wa Tanzania.

Maombi hayo yamefanyika mji mdogo wa Mirerani yakiongozwa na viongozi wa madhehebu mbalimbali huku mgeni maalum akiwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara Peter Toima.

Mwenyekiti Toima ambaye alikuwa mgeni maalum wa maombi hayo amesema wameshiriki ili kuwaombea viongozi wa Taifa waweze kuendelea kuongoza nchi kwa kumtanguliza Mungu.

"Mimi ni nani nikatae fursa ya kuwa mgeni maalum kwenye tukio hili ambalo mgeni rasmi ni Mungu mwenyewe," amesema Toima.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Fakii Lulandala amewashukuru viongozi wa dini, wa serikali, wa CCM na wananchi kwa ujumla kwa kushiriki maombi hayo ambayo kiwilaya yamefanyika mji mdogo wa Mirerani.

"Maombi haya yatafikia tamati Aprili 26 mji mdogo wa Orkesumet mbapo ndipo yalipo makao makuu ya wilaya kwa kuweka TV kubwa kwa ajili ya wananchi kusikiliza hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan," amesema Lulandala.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara, Peter Toima ambaye alikuwa mgeni maalum wa maombi hayo amesema wameshiri ili kuwaombea viongozi wa Taifa waweze kuendelea kuongoza nchi kwa kumtanguliza Mungu.

Mchungaji Kefa Simon amesema Taifa linapaswa kuwaongoza wananchi wake kwa kutenda haki kwani lisipofanya hivyo litakuwa linatenda dhambi.

Mchungaji Yohana Ole Tiamongoi amesema wanawaombea viongozi wa Taifa waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuongoza vyema.

Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) Simanjiro Warda Abeid Maulid amesema maombi hayo pia yameshirikisha watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla.

"Tunawapongeza wote waliofanikisha maombi haya wakiwemo viongozi wa madhehebu ya dini, viongozi wa serikali, viongozi wa CCM na wote walioshiriki hadi mwisho," amesema DAS Warda.

Mkazi wa mji mdogo wa Mirerani, Anthony Jacob amesema tukio hilo limevuta hisia za wananchi wa eneo hilo kwani wameshiriki na kuomba kwa pamoja na viongozi.

Sheikh wa Wilaya ya Simanjiro, Ibrahim Idd amewaasa wakazi wa mkoa wa Manyara, kuwalinda watoto kwa kuwaepusha na vitendo vya ukatili kwani vimekithiri hivi sasa.

Sheikh Idd amesema wazazi na walezi wanapaswa kuwa makini na malezi ya watoto ikiwemo kutowaruhusu watoto wa kiume kulala na ndugu zao wakubwa wa kiume.

"Mambo ya mjomba kulala chumba kimoja au kitanda kimoja na mtoto wa kiume yamepitwa na wakati kwani anaweza kufanyiwa vitendo vibaya na kusababisha matatizo," amesema sheikh Idd.

 


Na Mwandishi Wetu 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) Bi Beng'i Issa amesema kuwa katika miaka sita ya Rais Dkt.SamiaSuluhu Hassan kimekuwa na mapinduzi katika uwekeaji nchini kwa wazawa.

Beng'i ameyasema hayo wakati wa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu kongamano la nne la Ushiriki wa Watanzania kwenye uchumi na Uwekezaji (Local Content) litakalofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 28 mwezi huu

Amesema kuwa Kongamano hilo hufanyika kila baada ya miaka miwili ikiwa ni pamoja kuangalia tathimini ya miaka miwili iliyopita na kuweka dira ya miaka miwili katika uwekezaji kwa wazawa.

Amesema , mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt Dotto Mashaka Biteko.

Amesema kuwa Kongamano hilo litaweka picha ya kuweza kukua Kwa uwekezaji wa wazawa.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) Bi. Beng'i Issa akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo picha) kuhusu kongamano la nne la Ushiriki wa Watanzania kwenye uchumi na Uwekezaji (Local Content) litakalofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 28 mwezi huu ambalo hufanyika  Kila baada ya miaka miwili , mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt Dotto Mashaka Biteko .

*Nchi imeruhusu uhuru wa kujieleza pamoja na
kukusanyika kwa uhuru

Mwandishi Wetu Maalum ,Marekani

Nchi ya Tanzania umetoa ujumbe wake Kwa Umoja wa Mataifa kuwa haitishi wala kukandamiza raia wake


Ujumbe huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Profesa Hamis Malebo kwenye mkutano Jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) ulionza Aprili 15 na kuhitimishwa Aprili 26 unaofanyika nchini Marekani

Prof. Malebo ameueleza mkutano huo wa Umoja wa Mataifa kuwa Tanzania nchi inayofuata misingi ya sheria katika mifumo ya kiutawala.

"Inasikitikisha kwamba kongamano hilo linatumiwa vibaya kwa kupewa taarifa potofu na zisizo na ukweli kuhusu “Watu wa Asili nchini Tanzania”. amesema Prof. Malebo

Ameongeza kuwa kuwa katika Kongamano hilo alimsikiliza Mwakilishi mmoja kutoka Shirika la Watu wa Asili akiishutumu Serikali ya Tanzania kuwa inawatisha na kuwakandamiza watu wa asili”.

Profesa Malebo katika ujumbe wake alibainisha kuwa madai hayo hayana msingi na kinachofanywa ni upotoshaji kwa vitu ambavyo nchi haifanyo na haifikirii kufanya kwa wananchi wake.

Aidha Profes Malebo aliukumbusha Mkutano huo unoarekodiwa huku akiwahimiza wajumbe wa jukwaa kupitia upya rekodi za mkutano ili kujiridhisha na ukweli kuwa Serikali ya Tanzania haijatoa kauli yoyote ya vitisho wala ukandamizaji kwa raia wake.

Hata hivyo amesisitiza pia kuwa Tanzania inashiriki na kuchangia hoja mbali mbali katika mkutano huo ambapo taarifa zote zinapatikana katika jarida la Umoja wa Mataifa.

Profesa Malebo ameeleza hata katika mikutano iliyotangulia, Ujumbe wa Tanzania imekuwa ukishiriki
na kujadili hoja mbali mbali kwa uwazi kwa nia ya kujenga na kuimarisha utekelezaji wa masuala mbalimbali kwa kuzingatia haki za binadamu.

Amefafanua na kusisitiza msimamo wa muda mref wa serikali ya Tanzania na kurudia kwamba, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nchi yetu haina kundi maalumu la Watu wa Asili wenye haki zaidi ya wananchi wengine wala hatuna ardhi ya mababu wala ya kimila.

Prof. Malebo ameutaka mkutano huo kutambua kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa kwa kufuata misingi ya utawala wa sheria na inaheshimu haki za binadamu.

Amesema Serikali haikubaliani na vitendo vya vitisho, ukandamizaji na unyanyasaji kwa raia wake, watetezi wa haki za binadamu na watendaji wengine wasio wa serikali wanaotekeleza majukumu yao kwa kufuata misingi ya utawala wa sheria.

Profesa Malebo amesema Serikali ya Tanzania inashiriki kwa lengo moja la kimataifa la utambuzi wa haki za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni kwa wananchi wake wote kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu za usawa na kutobaguliwa kwa wananchi wake na kuongeza kuwa Serikali imeweka vyombo vya utawala kwa ajili ya kukuza na kulinda haki za raia wake katika kila nyanja ya maisha. Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa kujieleza na hakuna vitisho wala unyanyasaji wa wananchi wanaopaza sauti zao kwa kufuata misingi ya utawala wa sheria.

Prof. Malebo amesisitiza kuwa, Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeendelea kuimarisha juhudi za kulinda haki za binadamu kwa raia wake kwa kuruhusu pamoja na mambo mengine, uhuru wa kujieleza, kukusanyika kwa uhuru na amani kwa ajili ya mikutano ya kisiasa kwa mujibu wa Katiba.


Rukwa

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeendelea kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji kwa kujenga barabara, vivuko na madaraja katika maeneo mbalimbali mkoani Rukwa ili kuinua shughuli za kijamii na kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa TARURA Mkoa wa Rukwa, Mhandisi William Lameck alisema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa katika kuimarisha miundombinu ya barabara za wilaya nchini.

Mhandisi Lameck amemshukuru Rais Samia kwa kuongeza bajeti ya TARURA Mkoa wa Rukwa kutoka Shilingi Bilioni 5.63 hadi kufikia Shilingi Bilioni 12.3 ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia kuimarisha mtandao wa barabara mkoani humo.

"Barabara kwa kiwango cha changarawe zimeongezeka kutoka Km 867.25 hadi Km 1,143.05," alibainisha.

“Tumeongeza mtandao wa barabara za lami na kufanyia matengenezo ya kawaida maeneo korofi jumla ya Km 196.66, ujenzi wa lami Km 0.8 na zege Km 1.55 zitatengenezwa katika Manispaa ya Sumbawanga na Wilaya ya Kalambo na Nkasi", alisema.

"Pia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe Km 179.5 na ujenzi wa daraja la Kavunja lenye urefu wa mita 39 linalounganisha vijiji vya Kirando, Kazovu na Korongwe wilayani Nkasi lenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.76 ambapo ujenzi wake umekamilika na daraja linatumika.

Amesisitiza daraja hilo limepunguza gharama za usafiri na usafirishaji ambapo hapo awali wananchi walikuwa wanazunguka katika vijiji vya Wilaya ya Kalambo lakini sasa wanatumia daraja hilo bila kuwa na wasiwasi juu ya mali zao na usalama wao.

Mkazi wa Nkasi Bi. Sarafina Mbalamwezi ameipongeza kwa kile inachokifanya kuhakikisha miradi ya barabara inatekelezwa na kukamilika kwa wakati na wananchi kuondokana na changamoto ya barabara.

Alisema uboreshaji wa miundombinu ya barabara umeweza kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma mbalimbali ikiwemo ya matibabu.

Mkazi wa Sopa wilayani Kalambo, Bw. Amon Kabwe amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuboresha miundombinu vijijini ili kuhakikisha wananchi wanasafiri na kusafirisha mazao yao sokoni kwa urahisi," alisema.

Alisema hapo awali kulikuwa na changamoto ya barabara kutopitika hasa kipindi cha masika lakini kwa sasa barabara hizo zinapitika muda wote na madaraja korofi yametengenezwa na yote yanatumika.

Muonekano wa barabara ya Malichewe yenye urefu wa Km. 1.2 katika wilaya ya Sumbawanga ambapo ujenzi wake umekamilika.


 

Samsung Electronics East Africa will next week Monday be switching off lights at their mobile experience stores and select Consumer Electronics stores for 5 minutes from 12 noon to 12:05 pm to mark the global and historic Earth Day as a symbol of their commitment to sustainability.

Earth Day was set up to be marked globally as a commitment to end plastics for the sake of human and planetary health, demanding a 60 percent reduction in the production of ALL plastics by 2040. This year’s theme, Planet vs. Plastics, advocates for widespread awareness of the health risks of plastics, rapid phase-out of all single-use plastics, the urgent push for a strong UN Treaty on Plastic Pollution, and demands an end to fast fashion.

Over the years, Samsung has remained committed to sustainability and securing the earth through the incorporation of recycled materials into all Galaxy products, purposing to eliminate plastic from product packaging by 2025, implementation of zero standby power consumption (below 0.005 watts) for all smartphone chargers by 2025, and achievement of 'Zero Waste to Landfill' Platinum Certification for all global business sites by 2025.

Through its various products and releases, Samsung has stayed true to its commitment to sustainability. For instance, the company announced a new Galaxy S24 series, unleashing a new mobile experience with Galaxy AI. Galaxy S24 | S24+ continues to scale the variety of recycled materials in Galaxy devices by applying recycled plastics, glass, and aluminum, and now for the first time, Galaxy S24 | S24+ features components made with recycled cobalt, rare earth elements, and steel. At the same time, Galaxy S24 | S24+ offers seven generations of OS upgrades and seven years of security updates to help users reliably experience the optimized performance of their Galaxy devices for even longer.

For Samsung, the sustainability promises and commitment are not in their smartphones alone but encompasses TVs and displays too. The brand has capitalized on the reduction of product energy consumption, increased use of eco-conscious materials in packaging, increased use of recycled material, accessibility consideration for persons with visual, hearing, and other physical intellectual disabilities, and accessibility consideration for situational disabilities.

With the above and many other inventions, Samsung Electronics has demonstrated a steadfast commitment to sustainability through its multifaceted strategies and initiatives. Integrating eco-friendly practices across its product lifecycle, investing in renewable energy sources, and fostering partnerships for environmental conservation, is commitment enough to drive its sustainability agenda forward.

Through innovative technologies and responsible corporate practices, Samsung sets a benchmark for the industry, showcasing that profitability and environmental stewardship can go hand in hand. As the company continues to evolve and expand its sustainability efforts, it stands as a progress pillar, inspiring others to prioritize sustainability in their operations and contribute to a greener, more sustainable future for all.



 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Leo Aprili 23, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali, linalojihusisha na Afya ya Macho Jumuishi na Watu Wenye Ulemavu, ' Christian Blind Mission' (CBM).

CBM lenye Makao yake Makuu Nchini Ujeruman, ambalo limejikita zaidi katika Mpango wa Kuwasaidia Wenye Ulemavu wa Macho, Ujumbe wake umewasili Ofisini kwa Mheshimiwa Makamu wa Kwanza, ili kueleza mafanikio na changamoto mbali mbali walizokutana nazo, katika Harakati zao.

Shirika hilo ambalo lilianza Kazi hapa Visiwani mnamo Mwaka 2022, linatarajia kukamilisha Harakati zake mwishoni mwa Mwaka huu wa 2024.

Viongozi na Waratibu mbali mbali wamehudhuria katika Kikao hicho wakiwemo; Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman; Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Dkt. Omar Dadi Shajak; Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, Dr. Salim Slim; na Mratibu wa Shirika hilo hapa Nchini, Bi. Nesia Mahenge.

Wajumbe wengine waliohudhuria hapo ni kutoka katika Mataifa ya Kenya, Ethiopia, Ujerumani, na wenyeji Tanzania.


Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Aprili 23, 2024.
















 

Mwamko mdogo wa Watanzania kuhusu bima ya afya ni mojawapo ya changamoto katika kutoa huduma bora za afya kwa wote kutokana na idadi ndogo ya Watanzania wenye bima. Takwimu za Wizara ya Afya (2022) zinaonesha kuwa asilimia 15 tu ya Watanzania, sawa na watu milioni 9.1, walikuwa na bima ya afya mwishoni mwa mwaka 2021, ikishuka kutoka asilimia 32% mwaka 2018.

Vodacom Tanzania PLC imeungana na Assemble Insurance na kuja na bima ya afya ya kijiditali kupitia simu ya mkononi iitwayo AfyaPass ambayo ni rahisi, nafuu, na inapatikana kwa Mtanzania popote pale alipo nchini. Bima hii inapatikana kwa bei nafuu ya Shilingi 70,000 kwa mwaka kwa mtu mmoja na vifurushi vya familia kutoka TZS 105,000 kwa watu wawili hadi TZS 385,000 kwa watu sita kwa mwaka na inapokelewa katika hospitali binafsi na za serikali. Kwa malipo kidogo ya nyongeza, mtumiaji anaweza kupata huduma za uzazi, radiolojia, mazoezi tib ana nyingine nyingi.

Unaweza kujiunga na AfyaPass kupitia M-Pesa ikiwa ni moja ya aina za bima zinazotolewa kupitia VodaBima yenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za bima kwa kila mtu bila kujali kipato chake au umbali wa eneo anapotoka nchini Tanzania.
Kamishna wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dk. Baghayo Saqware (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Assemble Insurance, Tabia Massudi (kushoto) wakiwa na vipeperushi kuashiria uzinduzi wa kampeni ya “VodaBima kidigitali, Ni Chap, ni Nafuu” inayohamasisha matumizi ya Bima Kidigitali uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia huduma zake za VODABIMA zinazopatikana kwa M-Pesa, itanufaisha wagonjwa wa kulazwa na kutwa, vyombo vya moto na bima ya maisha kwa mtu mmoja mmoja na vikundi kwa gharama nafuu.




Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge (wa pili kulia) akipokea msaada wa kibinadamu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko ya Rufiji na Kibiti wenye thamani ya takribani shilingi 250m uliotolewa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation. Msaada huo ulikabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Vyombo vya Habari wa kampuni ya Vodacom Tanzania Annette Kanora (katikati). Wengine pichani kutoka kushoto ni Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation Sandra Oswald na Meneja Mauzo wa eneo hilo Suleiman Amri na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele (kulia). Msaada huo ulikabidhiwa mwishoni mwa wiki mjini Kibiti.



Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Tree Oceans Ltd . Inayojishughulisha na uendeshaji wa mchezo wa kubashili wa VUNADEILE Naseem Allan (katikati), akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi waliojishindia kwenye mchezo wa VUNADEILE kulia ni Mratibu kutoka BBT Vumilia Zikankura hafla yakukabidhi zawadi hizo umefanyika jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Tree Oceans Ltd . Inayojishughulisha na uendeshaji wa mchezo wa kubashili wa VUNADEILE Naseem Allan (kushoto), akikabidhi zawadi ya bajaji kwa mshindi wa VUNADEILE ambapo kila wiki kunatolewa bajaji tatu wengine pichani kutoka kulia ni Mratibu kutoka BUILDING A BETTER TOMORROW (BBT) Vumilia Zikankura Pamoja na Meneja wa Leseni Michezo kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Lenganivo Maeti.



KAMPUNI ya Three Oceans Ltd. Inayojishughulisha na uendeshaji wa mchezo wa kubashili wa VUNADEILE imesema itaendelea kushirikiana na serikali katika kuwawezesha Vijana kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa kuweza kujiajiri.

Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar Salama es Salaam na Mkuu wa kitengo Cha Masoko na Mawasiliano kutoka kwenye kampuni hiyo Naseem Allan wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wanaopatikana kila siku kwenye droo ikiwemo gari mpya kabisa aina ya Toyota Ist, pikipiki, tv na simu janja aina ya Samsung na iphone 15.

Ameeleza kuwa katika kuendesha bahati nasibu hiyo kampuni inashirikiana na Mradi wa kilimo ili kuhakikisha tunawawezusha vijana-BBT ni Taasisi iliyopo chini ya wizara ya kilimo yenye lengo kuu la kutoa hamasa kwa Vijana kujikita kwenye shughuli za kilimo biashara Ili waweze kukuza uchumi wao binafsi na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mratibu kutoka BBT Vumilia Zikankura amebainisha kuwa BBT imekuwa ikiwawezesha Vijana kuingia kwenye sekta ya kilimo biashara kwa kuwawezesha mitaji na Masoko huku akiwataka Vijana kujitokeza kwenye program ya BBT na VUNA DEILE Ili waweze kujishindia Zawadi mbalimbali.



Top News