Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa wizara hiyo, Miriam Mmbaga(wapili kushoto) wakisikiliza ufafanuzi wa programu maalumu ya kudhibiti uhalifu wa Kimtandao kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya SOLAR,Timul Solovev wakati wa Maonesho ya Teknolojia ya Kudhibiti Uhalifu huo yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa EXPOFORUM ambapo Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama kutoka takribani nchi 20 Duniani wamekutana nchini Urusi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Na Mwandishi Wetu,URUSI

SERIKALI imedhamiria kushirikiana na nchi ya Urusi katika kudhibiti uhalifu nchini ikiwemo uhalifu wa mtandao ambao umeanza kushamiri katika maeneo mbalimbali nchini huku ikiweka wazi dhamira ya kujengewa uwezo kwa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na nchi zilizoendelea kiteknolojia katika kudhibiti uhalifu huo unaotajwa kuvuka mipaka.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama unaoendelea nchini Urusi ambao ulifunguliwa na Rais wa Shirikisho la Urusi na kuongozwa na Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Urusi, Nikolai Patrushev.

‘Katika kudhibiti masuala ya uhalifu wa kimtandao matumizi ya teknolojia hayaepukiki ndio maana serikali imeona kuna haja ya kuimarisha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika Nyanja mbalimbali ikiwemo ujuzi kwa askari wetu sasa kupitia mkutano huu tunaenda kujenga mahusiano kati ya Jeshi la Polisi la Tanzania na Jeshi la Polisi la Urusi ili tuweze kudhibiti uhalifu wa kimtandao ambao umekua ukisababisha madhara mbalimbali katika jamii ikiwemo ya kiusalama,kiuchumi na hata maadili’. Alisema Waziri Masauni

Akizungumza wakati wa Mkutano huo Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Miriam Mmbaga alisema muelekeo wa wizara katika kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ina mkakati maalumu wa kuwajengea uwezo askari waliopo katika Vyombo vya Ulinzi hasa katika masuala ya teknolojia huku akiweka wazi juu ya suala la ajira pia kuweka kipaumbele kwa watu waliosomea masuala ya teknolojia ya Habari.

Mkutano huo wa Kimataifa wa Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama umehudhuriwa na nchi takribani 20 huku msisitizo zaidi ukiwekwa katika kupambana na uhalifu wa kutumia teknolojia ambao umekua ni tishio katika mataifa mbalimbali.
Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Urusi, Nikolai Patrushev (wa kumi na tano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama kutoka takribani ya nchi 20 Duniani waliokutana nchini Urusi katika Jiji la St.Petersburg kujadili changamoto ya uhalifu wa kimtandao na jinsi ya kupambana nao.Tanzania pia inashiriki mkutano huo ikiwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto) akionyeshwa jinsi ndege isiyo na rubani inavyoweza kupambana na uhalifu na Afisa kutoka Kampuni ya DOMINA,Alexeen Alexander wakati wa Maonesho ya Teknolojia ya Kudhibiti Uhalifu huo yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa EXPOFORUM ambapo Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama kutoka takribani nchi 20 Duniani wamekutana nchini UrusiPicha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
aziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa wizara hiyio, Miriam Mmbaga(katikati) wakisikiliza maelezo ya kudhibiti uhalifu wa kimtandao kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Kupambana na Uhalifu wa Kimtandao(CyberED),Gadzhi Akhmedov wakati wa Maonesho ya Teknolojia ya Kudhibiti Uhalifu huo yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa EXPOFORUM ambapo Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama kutoka takribani nchi 20 Duniani wamekutana nchini Urusi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa wizara hiyo, Miriam Mmbaga(kulia) wakionyeshwa jinsi Mfumo wa Kudhibiti Uhalifu wa Kimtandao unavyofanya kazi na Mtaalumu wa Teknolojia ya Habari kutoka Kampuni ya KOMIB,Egor Bogomolov wakati wa Maonesho ya Teknolojia ya Kudhibiti Uhalifu huo yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa EXPOFORUM ambapo Maafisa wa Daraja la Juu kutoka serikalini wanaohusika na mambo ya Usalama kutoka takribani nchi 20 Duniani wamekutana nchini Urusi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiwasilimia Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)  walipowasili katika ukumbi wa mkutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kulifungua Kongamano la Wanawake na Muungano lililofanyika leo 25-4-2024.(Picha na Ikulu)
WASHIRIKI wa Kongamano la Wanawake na Muungano kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililofanyika leo 25-4-2024 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamano hilo.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa na Wake wa Viongozi wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake na Muungano kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifungua Kongamano hilo lililofanyika leo 25-4-2024 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)
WASHIRIKI wa Kongamano na Wanawake na Muungano kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakishingilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo 25-4-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimkabidhi Zawadi Maalum ya Picha iliyotolewa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan, akipokewa kwa niaba Mhe.Wanu Hafidh Ameir, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake na Muungano lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo 25-4-2024.(Picha na Ikulu)   
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi,akimkabidhi Zawadi Maalum ya Picha iliyotolewa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume Mama Fatma Karume,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake na Muungano lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo 25-4-2024.(Picha na Ikulu)  
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimkabidhiwa Zawadi Maalum ya Picha iliyotolewa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa mchango wake, akikabidhiwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake na Muungano  kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo 25-4-2024.(Picha na Ikulu)   
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake na Muungano kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,i lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo 25-4-2024.(Picha na Ikulu)
VIONGOZI Wastaafu wa UWT wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake na Muungano lililofanyika leo 25-4-2024 na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, lililofanyika katika ukumbi wa Mlomani City Jijini Dar es Salaam leo 25-4-2024.(Picha na Ikulu)
Na Khadija Kalili ,Michuzi Tv
MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge leo amepokea hundi yenye thamani ya Mil.20 kutoka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ikiwa ni katika muendelezo wa kuchangia watu wa Kibiti na Rufiji ambao wamepata changamoto ya mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea nchini kote.

Imeelezwa na Afisa Uhusiano wa TFS Johary Kachwamba kuwa msaada huo umetolewa na Kamishna wa Uhifadhi TFS ikiwa na lengo la kuwapa pole wakazi hao.

Afisa Uhusiano Kachambwa ndiye aliyemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kunenge hundi hiyo ambapo makabidhiano yamefanyika katika viwaja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pwani.

"Wakaazi wa Kibiti na Rufiji ni wenzetu kwani tunazo hifadhi za misitu zaidi ya kumi zenye Hekta 32,000 hivyo ni wajibu wetu kuwapa pole" amesema Kachwamba.

"Tunatoa pole kwa RC Kunenge

Akizungumza mara baada ya kupokea hundi hiyo RC Kunenge ametoa shukrani zake za Mkoa kwa TFS dhati kwa hundi hiyo pia kwa kuwapa eneo ambalo watahamishiwa watu ambao wamepata chagamoto ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko katika maeneo ya Kibiti na Rufiji.

"Pia namshkuru Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa misaada ya hali na mali aliyowapatia wananchi wa maneo yaliyokumbwa na changamoto ya mafuriko ndani ya Mkoa wa Pwani ,Tunawashukuru TFS kwani fedha hizi zitasaidia kutatua changamoto zilizowakumba wenzetu wa KibitinaRufiji.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge akizungumza  na Waandishi wa Habari  Ofisini kwake leo Aprili  25, 2024 hawapo pichani.

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge ametoa ratiba ya kuukimbiza Mwenye wa Uhuru ambao utaingia Mkoa wa Pwani Aprili 29 ukitokea Mkoa wa Morogoro.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano leo Aprili 25 amesema kuwa Mwenge huo wa Uhuru utakimbizwa kwa siku saba.

RC Kunenge amesema kuwa baada ya kuupokea Mwenge wa Uhuru utaanza kukimbizwa Aprili 29 ndani ya Halmashauri ya Chalinze na Aprili 30 utakimbizwa Halmashauri ya Bagamoyo huku Mei mosi utaikimbiza Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha na Mei mbili utakimbizwa Halmashauri ya Mji Kibaha Mei tatu utakimbizwa Kisarawe, Mei 4 Mkuranga, Mei tano Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Rufiji na Mei 6 utakimbizwa Kibiti huku Mei 7 utakimbizwa Mafia na Mei nane utakabidhiwa Mkoa wa Dar es Salaam.

"Mkoa wa Pwani haturudi nyuma tutakuwa na mipango mizuri zaidi awali ya yote tumegundua changamoto ambazo zimetukabili za mvua hivyo kuna baadhi ya miradi ambayo imebidi tuighairi kutokanaa na mvua.

"Kimkoa tumejipanga vizuri na tunatarajia utakimbizwa katika Wilaya zetu zote tisa pia napenda kuchukua fursa hii kiwaomba wananchi wote wajitokeze kukimbiza Mwenge na kukahikisha tunafanikisha mbio za mwaka huu za mwaka 2024, huku tukitarajia kufumisha upendo,amani utu na heshima.

Amesema pindi mwenge ukikimbizwa Mkoa ni pwani utakua nakauli mbiu za Kuzuia na kuoambana a rushwa ni jukumu lako na langu tutimize wajibu,jamii iunge jitihada za kutokomeza uonjwa wa UKIMWI, Epuka dawa za kukevya zingatia utu boresha tiba na kinga na mwisho Lishe siyo kujaza tumbo zingatia unachokula,

Ziro Malaria inaanza na mimi chukua hatua kuotokomeza.
TANZANIA imechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa ZAMCOM katika mwaka 2024-2025 kwenye Mkutano wa 11 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (Zambezi Watercourse Commission - (ZAMCOM) unaoendelea mjiji Tete Nchini Msumbiji.

Uchaguzi huo umefanyika kufuatia Msumbiji kumaliza muda wake na kukabidhi uenyekiti kwa Namibia, Hivyo, Tanzania inategemewa kuwa Mwenyekiti wa ZAMCOM.

Katika mkutano huo, Tanzania imewakilishwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew.

Licha ya kushiriki Mkutano wa 11 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (Zambezi Watercourse Commission - ZAMCOM), Tanzania imefanya mazungumzo na wadau wa maendeleo na kuwakaribisha kuwekeza katika Sekta ya Maji nchini Tanzania.

Mhandisi Kundo ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo amekutana na kufanya mazungumo na Mwakilishi wa Shirika la Sweden, SwedFund.

Katika mazungumzo hayo, Tanzania imeikaribisha Taasisi ya SwedFund nchini ili kushirikiana katika maeneo ya maandalizi ya miradi ya miundombinu yenye ukubwa wa kati na wa juu.

Nae mwakilishi wa SwedFund ameahidi kushirikiana na Tanzania katika kufanya majadiliano kuhusu kuandaa miradi mahsusi.



Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetoa mafunzo Wanafunzi wa Shahada na Shahada ya Uzamili wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) hii ikiwa ni mwendelezo wa kutoa elimu kwa umma hasa kwenye vyuo vinavyotoa masomo ya Ununuzi na Ugavi.

Akizungumza na Michuzi Blog, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee amesema Bodi hiyo imeendelea kuwapa mafunzo Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali wanaochukua kozi hiyo ya Ununuzi na Ugavi kuhusu shughuli zinazofanywa na Bodi, Usajili kwa njia ya mtandao pamoja na maadili na miiko ya taaluma hiyo.

Naye, Kaimu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Jonnes Lugoye ametoa shukrani kwa wafanyakazi wa PSPTB kwa kuweza kufika chuoni hapo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Bodi hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee akitoa maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi - DMI, Jonnes Lugoye akiwakaribisha wageni kutoka Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) walipofoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Bodi hiyo.
Afisa Ununuzi kutoka Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB),  Ally Yassin Mbarouk akitoa maelezo kuhusu namna ya kuongeza dhamani kwenye taaluma hiyo kwa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Afisa TEHAMA Mwandamizi kutoka PSPTB Elihuruma Eliufoo akitoa mada kuhusu namna ya mwanafunzi anavyoweza kujisajili kwenye mfumo wa Bodi (ORS) pamoja na kufanya mitihani ya Bodi wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) wakiuliza maswali kwa wafanyakazi wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) aliofika chuoni hapo kwa ajili ya kutoa elimu .
Baadhi ya wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) wakifuatilia mada kutoka kwa wafanyakazi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) waliofika chuoni hapo kwa akili ya kutoa elimu zinayohusu Bodi hiyo.
Kaimu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi - DMI, Jonnes Lugoye akiwakabidi wanafunzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) walioshinda zawadi akati wa mafunzo yaliyotolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) 
 Kaimu Mkuu wa Idara ya Sayansi na Menejimenti - DMI, Elinathan Blasius akitoa neno la shukrani kwa wafanyakazi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) waliofika chuoni hapo kwa akili ya kutoa elimu zinayohusu Bodi hiyo.


Picha za Pamoja

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Exim Bank, Stanley Kafu (wa tatu kutoka kushoto),akikabidhi seti ya vitanda kwa Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania - Moshi, SACP Ramadhani Mungi (wa tatu kutoka kulia), kama sehemu ya mchango wa Exim Bank katika jamii ikiwemo ulinzi na usalama wa Watanzania na mali zao ambapo makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 24 Aprili, 2024.


Benki ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule ya Jeshi la Polisi Tanzania iliyopo Moshi, mkoani Kilimanjaro kama sehemu ya mchango wa Exim Bank katika jamii ikiwemo ulinzi na usalama wa Watanzania na mali zao. 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Stanley Kafu alisema, “Kupitia mkakati wetu wa kurudisha kwa jamii unayojulikana kama Exim Cares na kama ishara ya mashirikiano yetu ya muda mrefu, tunayo furaha kuchangia vitanda 40 kwa Shule ya Jeshi la Polisi Tanzania ya hapa Moshi.” 

Exim bank inaamini mchango huu utasaidia kuboresha mazingira ya mafunzo kwa maafisa wa polisi ili wapate mafunzo bora yatakayochangia kuboresha jeshi la polisi katika majukumu yake ya kuwahakikishia ulinzi na usalama Watanzania wote na mali zao. 

“Ushirikiano wetu na Jeshi la Polisi haujaanza leo, mwaka jana Exim Bank tumeingia makubaliano na Jeshi la Polisi Tanzania yenye lengo la kuwezesha utoaji wa mikopo ya masharti nafuu kwa askari polisi kupitia programu yetu maalumu ijulikanayo kama ‘Wafanyakazi Loan’”, aliongeza Kafu. 

Akifafanua zaidi Kafu alisema kuwa kupitia ‘Wafanyakazi Loan’, askari polisi wanaweza kukopa kuanzia shilingi milioni moja hadi shilingi milioni 160 ambayo inaweza kurejeshwa kati ya miezi 6 hadi miezi 96 kutegemeana na ahadi ya mkopaji ambayo inaweza kutumika kutekeleza ndoto za mkopaji ikiwa ni pamoja kupata mkopo wa nyumba, kununua magari na kulipia ada ya masomo ili kujiendeleza kielimu.

Exim Bank imedhamiria kuendelea kushirikiana na serikali na vyombo vyake vya usalama kuhakikisha ustawi unakuwepo katika sekta mbalimbali ikiwemo usalama, afya, uchumi, na kuboresha maisha ya Watanzania wote bila ubaguzi wa namna yoyote.


Top News