Na Karama Kenyunko Michuzi Tv

MSAJILI Mkuu wa Mahakama nchini Tanzania Eva Nkya amekabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Msajli wa Mahakama hiyo Jaji Wilbert Chuma huku mbele yake akikabiliwa na majukumu 12.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo 18 Aprili 2024, jijini Dar es Salaam katika ya Msajili Mkuu wa zamani (Chuma) na Msajili Mkuu mpya (Nkya).

Akizungumza wakati wa kumkabidhi ofisi Msajili Mkuu mpya, Jaji Chuma alimpitisha kwenye kifungu cha Sheria ya usimamizi wa Mahakama Na. 4 ya 2011.

"Kama mnavyofahamu, kwa mujibu wa kifungu 28 cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Na.4/2011 shughuli zote za kimahakama zinasimamiwa na Msajili Mkuu. Msajili Mkuu ndiye kiungo kwa masuala yote ya Sheria kati ya Mahakama ya Tanzania na Mihimili mingine ya Dola pamoja na Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na Mashirika binafsi" amesema Jaji Chuma.

Amesema kuwa majukumu ya msajili yaliyoanishwa kisheria ni pamoja na kuwezesha na kusimamia ufanisi katika uendeshaji wa mashauri Mahakamani; Kuratibu shughuli zote za uendeshaji wa mashauri, Kuwa kiunganishi kati ya Mahakama na Tume ya Utumishi wa Mahakama kwenye masuala ya uteuzi, upandishaji madaraja na masuala ya maadili kwa Maafisa Mahakama.

Ameongeza wajibu mwingine ni pamoja na Kuwasiliana na Serikali katika masuala yanahusu mambo ya kimahakama, au masuala yoyote ambayo Serikali ina maslahi nayo.

"Katika kutekeleza majukumu hayo, Msajili Mkuu anasaidiwa na Msajili wa Mahakama ya Rufani, Msajili wa Mahakama Kuu, Naibu Wasajili na Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri, Kurugenzi ya Huduma za Mahakama, Ukaguzi na usimamizi wa Maadili pamoja na Kurugenzi ya TEHAMA ambapo amesema, majukumu hayo yamefafanuliwa kwa kina kwenye taarifa ya Makabidhiano.


"Kwa ufupi, taarifa inaainisha maeneo mbalimbali ambayo yalikuwa yanaendelea kufanyiwa kazi na ofisi ya Msajili Mkuu. Miongoni mwa naeneo hayo kwa uchache ambayo pia ni mafanikio ya Mahakama kwa kipindi chote nilichohudumu"

"Kuendelea kusimamia mikakati ya kuiwezesha Mahakama kuondokana na mlundikano wa mashauri uliopungua kutoka asilimia 11, 2019 hadi asilimia tatu Machi, 2024"

Amesema majukumu aliyoendelea nayo ni kusimamia mfumo wa uratibu wa mashauri (Advanced Case Management System) , Kusimamia na kuratibu mfumo wa unukuzi na tafsiri yaani, transcription and translation system (TTs).

Jaji Chuma amesema kuwa majukumu anayotakiwa kuyavalia njuga ni pamoja na kuhakikisha maamuzi ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu yanapatikana katika mfumo wa TANZLII.

Kuongezeka kwa idadi ya vituo vya Mahakama zinazokaguliwa kutoka 75.8% mwaka 2017 hadi 98.1% mwaka 2023, na kuendelea kupunguza hatua za kuendesha mashauri kwa maana procedural steps ambazo zilipungua kutoka hatua 38 hadi hatua 21.

Amesema kuwa utekelezaji wa maoni kuhusu ripoti ya REPOA ya mwaka 2023 ambayo ilionyesha kuridhika kwa umma juu ya huduma zinazotolewa na Mahakama kutoka asilimia 61, 2015 hadi asilimia 88, 2023.

"Lakini pia ni muhimu kulinda na kuendelea kuongeza asilimia kwa kuongeza uwajibikaji. Hii ni hatua kubwa japo wapo wanaobeza juhudi hizi. Lakini nao ni wetu na wanapaswa kuhudumiwa".


"Kuendelea kulinda uhuru wa Mahakama na kusimamia nidhamu kwa maafisa wa Mahakama" amesema Jaji Chuma.


Naue, Nkya Msajili Mkuu mpya wa Mahakama akipoea majukumu ya Ofisi ya hiyo ameahidi kuwa atafanya jitihada zake zote kuhakikisha kuwa muhimli huo unazidisha kasi katika utoaji haki kwa wananchi.

Msajili Nkya amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kumuamini na kuahidi kuwa atatekeleza majukumu yake kadri ya uwezo wake wote.

Amesema kuwa amezipokea nasaha na ushauri wa Msajili Mkuu wa zamani "Nasaha zako ni nzuri zitaniimarisha ,niahidi kwamba nitatekeleza majukumu yangu kulingana na kiapo changu pia kwa uwezo ambao Mungu ameniajaalia nitafanya kazi kadri ya uwezo wangu wa mwisho".

Msajili Nkya ameomba ushirikino kwa watendaji na watumishi wote wa mahakama na kusisitiza kufanya kazi kwa jitihada zote kuhakikisha muhimili wa mahakama uzidi kuwa imara.
 

Aliyekuwa msajili wa Mahakama Kuu Tanzania, Jaji Wilbert Chuma (kulia) akikata utepe kama ishara ya kukabidhi ofisi  kwa Msajili Mkuu wa Mahakama hiyo mpya nchini, Eva Nkya..anayeshuhudia nyuma ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Tanzania,  Profesa Elisante Ole Gabrieli. Hafla za makabidhiano hayo zimefanyika leo Aprili 18,2024 jijini Dar es Salaam 

Msajili Mkuu mpya wa Mahakama Kuu Tanzania,  Eva Nkya akizungumza wakati wa kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa msajili wa Mahakama hiyo nchini Jaji Wilbert Chuma (kushoto) kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Profesa Elisante Ole Gabrieli

 

Aliyekuwa msajili wa Mahakama Kuu Tanzania, Jaji Wilbert Chuma (katikati) akizungumza wakati wa kukabidhi ofisi  kwa Msajili Mkuu wa Mahakama hiyo mpya nchini, Eva Nkya (aliyeko kushoto na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Profesa Elisante Ole Gabrieli

Na Mwandishi wetu

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo viti mwendo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wa shule ya sekondari ya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Msaada huo umekabidhiwa leo Aprili 18,2024 shuleni hapo na Mkurugenzi wa Taaluma wa CBE, Dkt. Shima Banele, katika hafla fupi iliyowashirikisha wanafunzi zaidi ya 110 wa shule hiyo wenye mahitaji maalum.

Akizungumza maara baada ya kukabidhi msaada huo, Dkt.Banele amesema chuo hicho kimejenga utamaduni wa kusaidia shule hiyo kila mwaka kwani inapokea wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma elimu jumuishi.

Dkt. Banele amesema chuo hicho kitaendelea kusaidia shule hiyo ili wanafunzi wenye mahitanji maalum waweze kusoma kwa bidii na kutimiza ndoto zao siku za baadaye.

Amesema kila mwaka chuo hicho kimekuwa na utamaduni wa kuchukua sehemu ya wanachopata na kurejesha kwenye makundi mbalimbali ndani ya jamii kama sehemu ya kutambua mchango wake kwa chuo.

Aidha amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari kwani wanafunzi wengi walikuwa wanashindwa kwenda shule kutokana na kukosa ada sasa wanaweza kupata elimu yao.

Pia amepongeza hatua ya serikali kuweka elimu jumuishi ambapo wanafunzi wenye mahitaji maalum wamekuwa wakichanganywa na wale ambao hawana changamoto yoyote.

Amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao na kuachana na fikra za kujiona wanyonge kwani wakijiamini wanaweza kufaulu vyema kwenye masomo yao na kufanya vizuri kwenye elimu ya vyuo vikuu.

“Mnaweza kuwa na changamoto ya maumbile lakini ubongo wenu unafanyakazi vizuri kwa hiyo msifikirie kwamba hamuwezi, mnaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa jamii kama mtajibidisha na mkafaulu vizuri,” amesema

“Mtakapomaliza sekondari mkafaulu vizuri na kwenda vyuo vikuu mkimaliza hangaikeni kutafuta ajira kwasababu mnauwezo wa kufanyakazi kama wengine. Kila mtakapoona nafasi za ajira pelekeni wasifu wenu,” amesema.

Aidha, amewataka kuishi kwa upendo na kupeana moyo kwenye masomo yao ili waweze kufanya vizuri kwenye masomo yao na kukua kitaaluma badala ya kukandamizana kwa uchoyo na chuki.

“Mimi leo hapa namwakilisha Mkuu wa chuo cha CBE lakini kwa nafasi yangu pale ni Mkurugenzi wa taaluma sasa kama mimi nimeweza kufika nilipo kwa sasa kwanini kesho usiwe wewe. Kwa hiyo unatakiwa kuanza kufikiria kesho yako leo hii na ninaamini mtafanikiwa sana mkijituma,” amesema

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa shule hiyo, Paulina Aweda, amesema shule hiyo inawanafunzi 110 wenye mahitaji maalum na wanasoma masomo yote kama walivyo wanafunzi ambao hawana changamoto yoyote.

Amepongeza serikali kwa kuweka mazingira mazuri kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum wanasoma bila vikwazo vyovyote na kwamba wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho ya kitaifa.

Amesema wanafunzi hao wenye mahitaji maalum wamekuwa wakipatiwa chakula, malazi na mahitaji mengine yote wanapokuwa shuleni hapo hali ambayo imewawezesha kufanya vizuri kitaaluma.

“Tunabahati ya kuwa na waalimu wa kutosha waliosomea elimu maalum ya kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa hiyo serikali imewafikiria kwa kiwango kikubwa wanafunzi wenye mahitaji maalum,” amesema.
 

Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),   Dkt. Shima  Banele ambaye ni Mkugenzi wa Taaaluma wa chuo hicho akimsukuma mwanafunzi kwenye kiti mwendo (wheelchair) walipokwenda kutoa msaada wa viti hivyo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wa shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es Salama leo Aprili 18,2024.

 

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, Dar es Salaam Paulina Aweda (kulia) akionyesha tuzo ambayo amepewa leo Aprili 18,2024 na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kutambua mchango wa shule hiyo kutunza na kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum wakati walipowatembelea shuleni hapo na kuwapa zawadi mbalimbali vikiwemo viti mwendo.



Na Mwandishi wetu, Ngorongoro Kreta.
Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Ujerumani, Ufaransa na Ubelgiji wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kutangaza utalii wa Tanzania zilizopelekea kuendelea kuongeza idadi ya watalii hapa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na mabalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mhe. Jestas Nyamanga, Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani Hassan Idd Mwamweta na Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa Mhe. Ali Jabir Mwadini walitotembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuona vivutio vya utalii, uboreshaji wa huduma na kushuhudia idadi kubwa ya wageni wa nchi wanazowakilisha wakifurahia vivutio vya nchi yetu.

Kiongozi wa mabalozi hao Mhe. Jestas Nyamanga ameeleza kuwa nchi ya Ubelgiji pekee ina takribani watalii 16,000 wanaotembelea nchi ya Tanzania kila mwaka na kwamba juhudi zinaendelea kufaywa na ofisi ya ubalozi kuendelea kuongeza idadi hiyo.

“Kwa sasa ni takribani miaka miwili tangu uzinduzi wa filamu ya Royal tour uliofanywa na Mhe. Rais, filamu hii imeitangaza nchi yetu hasa katika bara la ulaya tulipo na imeongeza uelewa wa vivutio tulivyonavyo, Nchi ya ubelgiji pekee ina zaidi ya watalii 16,000 wanaotembelea Tanzania na tumeweka mikakati ya kuongeza mara dufu” ameongeza Mhe. Nyamanga.

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta ambaye pia anasimamia nchi za Poland, Switzerland, Vatican, Hungary, Romania, Bulgaria na jamhuri ya Czech ameleeza kuwa mahusiano mazuri ya diplomasia ya Uchumi yaliyofanywa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika nchi hizo yamesaidia viiongozi wa nchi hizo kutembelea Tanzania na kuendelea kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji na utajiri wa vivutio vya utalii tulivyonanvyo.

Akiwa katika bonde la Ngorongoro balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa Mhe. Ali Mwadini amekutana na watalii kutoka Ufaransa ambao wamemueleza kuwa Wameijua zaidi Tanzania kupitia filamu ya Royal tour iliyofanywa na Mhe, Rais na kushawishika kutembelea Tanzania kwa muda wa siku 8 Zanzibar na Ngorongoro na wameahidi kuwa mabalozi wazuri watakaporudi nchini kwao.

Katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro pekee kati ya Julai 2023 hadi mwezi machi, 2024 Jumla ya watalii 750,220 ambapo watalii wa ndani ni 283,460 na watalii wa nje 466,760 wametembelea hifadhi ya Ngorongoro.
Msajili Mkuu mpyw wa Mahakama Kuu Tanzania,  Eva Nkya akizungumza wakati wa kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa msajili wa Mahakama hiyo nchini Jaji Wilbert Chuma (kushoto) kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Profesa Elisante Ole Gabrieli.
Aliyekuwa msajili wa Mahakama Kuu Tanzania, Jaji Wilbert Chuma (kulia) akikata utepe kama ishara ya kukabidhi ofisi  kwa Msajili Mkuu wa Mahakama hiyo mpya nchini, Eva Nkya..anayeshuhudia nyuma ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Tanzania,  Profesa Elisante Ole Gabrieli. Hafla za makabidhiano hayo zimefanyika leo Aprili 18,2024 jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa msajili wa Mahakama Kuu Tanzania, Jaji Wilbert Chuma (katikati) akizungumza wakati wa kukabidhi ofisi  kwa Msajili Mkuu wa Mahakama hiyo mpya nchini, Eva Nkya (aliyeko kushoto na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Profesa Elisante Ole Gabrieli

MSAJILI Mkuu wa Mahakama nchini Tanzania Eva Nkya amekabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Msajili wa Mahakama hiyo Jaji Wilbert Chuma huku mbele yake yamkabili majukumu 12.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 18 Aprili 2024, jijini Dar es Salaam katika Msajili Mkuu wa zamani (Chuma) na Msajili Mkuu mpya (Nkya).

Jaji Chuma wakati anamkabidhi Ofisi kwa Msajili Mkuu alimpitisha kwenye kifungu cha Sheria ya usimamizi wa Mahakama Na. 4 ya 2011.

"Kama mnavyofahamu, kwa mujibu wa kifungu 28 cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Na.4/2011 shughuli zote za kimahakama zinasimamiwa na Msajili Mkuu. Msajili Mkuu ndiye kiungo kwa masuala yote ya Sheria kati ya Mahakama ya Tanzania na Mihimili mingine ya Dola pamoja na Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na Mashirika binafsi" amesema Jaji Chuma.

Amesema kuwa majukumu ya msajili yaliyoanishwa kisheria ni pamoja n
Kuwezesha na kusimamia ufanisi katika uendeshaji wa mashauri Mahakamani; Kuratibu shughuli zote za uendeshaji wa mashauri, Kuwa kiunganishi kati ya Mahakama na Tume ya Utumishi wa Mahakama kwenye masuala ya uteuzi, upandishaji madaraja na masuala ya maadili kwa Maafisa Mahakama.

Ameongeza wajibu mwingine ni pamoja na Kuwasiliana na Serikali katika masuala yanahusu mambo ya kimahakama, au masuala yoyote ambayo Serikali ina maslahi nayo.

"Katika kutekeleza majukumu hayo, Msajili Mkuu anasaidiwa na Msajili wa Mahakama ya Rufani, Msajili wa Mahakama Kuu, Naibu Wasajili na Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri, Kurugenzi ya Huduma za Mahakama, Ukaguzi na usimamizi wa Maadili pamoja na Kurugenzi ya TEHAMA. Majukumu haya yamefafanuliwa kwa kina kwenye taarifa ya Makabidhiano nitakayokukabidhi hivi punde."amesema Jaji Chuma.

"Kwa ufupi, taarifa inaainisha maeneo mbalimbali ambayo yalikuwa yanaendelea kufanyiwa kazi na ofisi ya Msajili Mkuu. Miongoni mwa naeneo hayo kwa uchache ambayo pia ni mafanikio ya Mahakama kwa kipindi chote nilichohudumu ni"

"Kuendelea kusimamia mikakati ya kuiwezesha Mahakama kuondokana na mlundikano wa mashauri uliopungua kutoka 11% 2019 hadi asilimia 3 Machi, 2024"

Amesema majukumu aliyeendelea nayo ni kusimamia mfumo wa uratibu wa mashauri (Advanced Case Management System);

Kusimamia na kuratibu mfumo wa unukuzi na tafsiri yaani, transcription and translation system (TTs).

Jaji Chuma amesema kuwa majukumu anayotakiwa kuyavalua njuga ni pamoja na kuhakikisha maamuzi ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu yanapatikana katika mfumo wa TANZLII. Kutoka mwaka 2018 hadi sasa jumla ya maamuzi 50,505. Hapa kuna elimu ya kutosha kwa umma kupitia maamuzi haya;

Kuongezeka kwa idadi ya vituo vya Mahakama zinazokaguliwa kutoka 75.8% mwaka 2017 hadi 98.1% mwaka 2023, Kuendelea kupunguza hatua za kuendesha mashauri kwa maana procedural steps ambazo zilipungua kutoka hatua 38 hadi hatua 21.

Amesema kuwa utekelezaji wa maoni kuhusu ripoti ya REPOA ya mwaka 2023 ambayo kuridhika kwa umma juu ya huduma zinazotolewa na Mahakama iliongezeka kutoka asilimia 61% 2015 hadi 88% 2023.

"Lakini pia ni muhimu kulinda na kuendelea kuongeza asilimia kwa kuongeza uwajibikaji. Hii ni hatua kubwa japo wapo wanaobeza juhudi hizi. Lakini nao ni wetu na wanapaswa kuhudumiwa".

"Kuendelea kulinda uhuru wa Mahakama na kusimamia nidhamu kwa maafisa wa Mahakama" amesema Jaji Chuma.

Nkya Msajili Mkuu wa Mahakama akpoea majukumu ya Ofisi ya Msajili Mkuu wa Mahakama ameahidi kuwa atafanya jitihada zake zote kuhakikisha kuwa muhimli huo unazidisha kasi katika utoaji haki kwa wananchi.

Msajili Nkya amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kumuamini na kuahidi kuwa atatekeleza majukumu yake kadri ya uwezo wake wote.

Amesema kuwa amezipokea nasaha na ushauri wa Msajili Mkuu wa zamani "Nasaha zako ni nzuri zitaniimarisha ,niahidi kwamba nitatekeleza majukumu yangu kulingana na kiapo changu pia kwa uwezo ambao ungu ameniajaaliwa nitafanya kazi kadri ya uwezo wangu wa mwisho".

Msajili Nkya ameiomba ushirikino kwa watendaji na watumishi wote wa mahakama na kusisitiza kufanya kazi kwa jitihada zote kuhakikisha muhimili wa mahakama uzidi kuwa imara.









KATIKA kuhakikisha usalama wa maisha ya watu wilayani Rufiji, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imefanya msako wa mamba wanaotajwa kutishia maisha ya watu kutokana na kusogea karibu na makazi ya watu kufuatia kusafirishwa na mikondo ya maji yaliyosababishwa na mafuriko.

Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja akizungumza na waandishi wa habari katika mji mdogo wa utete wilayani Rufiji leo Aprili 18, 2024 amesema TAWA inaendelea na msako wa mamba tishio kwa maisha ya watu wilayani humo lengo likiwa ni kulinda usalama wa wananchi wa wilaya hiyo.

" Ni wajibu wetu kuimarisha ulinzi ili yasitokee maafa ya binadamu kupotea kutokana na kuliwa na mamba wakati sisi tuko hapa" amesema Afisa habari huyo.

"Na ndiyo maana tumekuja hapa kuhakikisha tunawasaka mamba wote ambao ni tishio kwa maisha ya binadamu.

Aidha Maganja amesisitiza kuwa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Sura ya Na. 283 inaelekeza kuwadhibiti wanyamapori wakali na waharibifu endapo itaonekana wana hatarisha maisha ya binadamu, hivyo chochote wanachokifanya ni kwa mujibu wa sheria lengo likiwa ni kulinda uhai wa binadamu.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wa wilaya hiyo kuzingatia elimu wanayoendelea kupewa na Maofisa uelimishaji kutoka TAWA ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kwa kushambuliwa na mamba.

Naye Afisa Mhifadhi wa TAWA George Boniface amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mamba wengi wamesafirishwa na maji kutoka Hifadhi ya Taifa ya Mwalimu Nyerere na Hifadhi ya Selous na kufika katika maeneo ya makazi ya watu katika mji wa utete na viunga vyake wilayani Rufiji kiasi cha kutishia maisha ya binadamu.

Amesema zoezi linaloendelea eneo hilo ni kuwasaka mamba wote ambao ni tishio kwa kutega mitego na kwa kutumia boti kwa usaidizi wa wenyeji na wavuvi.

Vilevile, Hamis Moshi Ipombo ambaye ni mzaliwa na mkazi wa utete Rufiji anayejihusisha na shughuli za uvuvi amesema katika mto Lugongwe uliopo eneo la utete kumekuwepo na mamba mkali anayetishia maisha wakazi wa eneo hilo kwa kukimbiza mitumbwi wawapo katika shughuli zao, mamba anayetajwa kusakwa na Maofisa wa TAWA.

Hata hivyo ameishukuru Serikali kupitia TAWA kwa kuwapata elimu ya kuepuka madhara yatokanayo na wanyamapori wakali na waharibifu hususani mamba huku akikiri kuwa elimu hiyo imewasaidia kuendelea na shughuli zao za kiuchumi huku wakiwa salama.
HATIMAYE Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi kibao nne kupigwa kwenye viwanja mbalimbali hatua ya robo fainali kule, na wewe una nafasi ya kupiga mkwanja ukibashiri na meridianbet.

Tukianza na mechi ya Liverpool ambao wao watasafiri hadi Italia kulipa kisasi dhidi ya Atalanta ambao mechi ya kwanza waliwafunga wakiwa Anfield. Mechi hiyo itapigwa majira ya saa 4:00 usiku meridianbet wamempa nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi Klopp na vijana wake kwa ODDS 1.57 kwa 4.90. Je Gasperin anaweza kubali kupigika nyumbani huku akiwa na uongozi wa mabao 3-0?. Beti mechi hii.

Kumbuka kucheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni ambayo inatolewa ndani ya meridianbet kama vile Poker, Roullette, Aviator, Rockertman, Keno, Sloti na mingine kibao. Ingia mchezoni na ucheze sasa.

Mechi nyingine itakuwa katika dimba la London ambapo mwenyeji West Ham United chini ya David Moyes atamleta nyumbani kwake Bayer Leverkusen ambaye ndiye bingwa wa Bundesliga ambalo alilichukua wiki iliyopita. Mechi ya kwanza Alonso alishinda akiwa kwake. Je leo hii atasonga hatua ya nusu fainali? Mechi hii imepewa ODDS 4.90 kwa Wagonga Nyundo na 1.83 kwa mgeni. Jisajili hapa.

Mpambano mwingine ni huu hapa ambao unazikutanisha timu mbili kutoka Italia ambazo zinashiriki ligi moja, yaani namaanisha AS Roma dhidi ya AC Milan ambayo ipo chini ya kocha mkuu Stephano Pioli.

AS Roma ambao wametoka kumuongezea mkataba kocha wao walishinda mechi ya kwanza walipokutana kule San Siro. Je leo hii Milan wanaweza nao shind awkaiwa ugenini? Meridianbet wamempa Pioli na vijana wake anafasi kubwa ya kushinda kwa ODDS 2.28 kwa 2.99. Tengeneza jamvi lako hapa.

Vilevile mechi ya psa itakuwa ni hii hapa ya Olympique Marseille dhidi ya SL Benfica kutoka Ureno ambaye alishinda mechi ya kwanza. Marseille anataka kulipa kisasi na kushinda leo kwa ODDS ya 2.35 kwa 2.84. Wewe nani unaona atakupa pesa?. Suka jamvi lako sasa.

 



Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure wamefanikiwa kufanya upasuaji na kuondoa Jiwe ndani ya kibofu cha Mkojo kwa Mwanamke mwenye umri wa miaka 48.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hospitalini hapo jiwe hilo lenye uzito wa Gramu 800 lililomsumbua mhusuka kwa zaidi ya miaka mitatu.


Akizungumza leo Aprili 18, 2024 na Daktari Bingwa wa Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Dkt. Jackson Chiwaligo amesema hiyo ni mara ya kwanza kufanya upasuaji kama huo.

Dkt. Chiwaligo ameeleza kuwa mgonjwa huyo alifika Hospitali ya Sekoutoure akiwa na changamoto ya kupata maumivu makali sehemu ya chini ya  tumbo kwa zaidi ya miaka mitatu.

 “Baada ya vipimo aligundulika kuwa na uvimbe mkubwa sehemu ya kibofu cha mkojo ulisababisha  kufanyiwa upasuaji na kuondoa lenye uzito wa Gramu 800”, amebainisha Dkt. Chiwaligo

Dkt. Chiwaligo ambaye aliwaongza madakatafi wenzake amesema uwepo wa jiwe kwenye kibofu ni mkusanyiko wa madini ya chumvi ambayo hukauka na kusababisha uvimbe kutokea katika kibofu cha mkojo.
Kuhusu dalili za awali za tatizo hilo Dkt. Chiwaligo  amesema dalili mbalimbali zinazosababisha ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu, maumivu makali chini ya tumbo na kushindwa kuzuia mkojo.

“Namna ya kujikinga na ugonjwa huu ni kwenda haja ndogo kwa wakati pale unapoipata na kunywa maji ya kutosha kwa wakati ” , ameeleza Dkt. Chiwaligo

Dkt. Chiwaligo ametoa wito kwa  jamii kuwa na utaratibu wa kufika hospitalini kupata huduma za vipimo na kuwa na mtindo bora wa maisha ili kuepuka changamoto ya magonjwa kama hayo.







 

 

 

Na Mwamvua Mwinyi..


Unamilikiwa na Watanzania kwa asilimia 100

Utafiti umebaini uwepo wa mashapo ya dhahabu kiasi cha tani 21.7

Kampuni ya PMM Tanzania Limited inayomiliki mgodi wa Magambazi imeanza shughuli za uzalishaji madini ya dhahabu ambapo kuanzia Agosti 2024 mgodi huo unatarajiwa kuzalisha kilo 25 za dhahabu kwa mwezi.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa PMM Tanzania Limited, Mhandisi Ulimbakisya Spendi baada ya timu ya Wanahabari kutoka Wizara ya Madini kutembelea eneo la mgodi huo uliopo wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Aidha, Spendi alisema mgodi huo upo katika milima ya Magambazi uligunduliwa na wachimbaji wadogo mnamo mwaka 2003 .

Alifafanua, mwaka 2007 Kampuni ya Canaco iliomba leseni ya utafiti katika eneo hilo na mwaka 2009 iligundulika kwamba kuna dhahabu ambayo inaweza kuzalishwa kwa faida hivyo ikapelekea kuomba leseni ya uchimbaji wa Kati wa madini ya dhahabu.

Vilevile, Spendi anasema baada ya Serikali kuhamasisha uzalishaji katika mgodi huo, Canaco ililazimika kuuza leseni ya mgodi huo mwaka 2020 kwa Kampuni ya PMM ambayo inamilikiwa na Watanzania kwa asilimia 100.

"Mgodi huu tayari umekwishafanyiwa utafiti na kubaini uwepo wa mashapo ya dhahabu kiasi cha tani 21.7 katika eneo hilo ambapo utafiti bado unaendelea katika mgodi huo."
Pia, anaeleza mpaka sasa mgodi huo umesaidia ukarabati wa Shule ya Msingi Magambazi, ujenzi wa vyoo katika shule hiyo na unaendelea na ujenzi wa Kituo cha Afya ambayo mpaka sasa imetumia kiasi cha shilingi milioni 400, mpaka kukamilika kwake inatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 700 ikiwa ni mchango wa mgodi huo kwa Jamii inayozunguka mgodi.

Mgodi wa Magambazi una changamoto kubwa ya umeme ambapo Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limeahidi kwamba ifikapo mwezi Juni miundombinu ya umeme itakuwa imefika katika eneo la mgodi huo.










 

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Serikali ilianza rasmi kuratibu utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Mafunzo ya Uzoefu wa Kazi kwa wahitimu (internship) mwaka 2019/2020.

Aidha, tangu kuanza kwa utekelezaji wa programu hiyo jumla ya Wahitimu 21,280 wamenufaika ambapo wanaume ni 11,281, wanawake 9,999 na Miongoni mwa wanufaika hao jumla ya Wahitimu 3,772 wamepata kazi Serikalini, Sekta Binafsi na nje ya Nchi.
Mhe. Ndejembi amebainisha hayo leo Aprili 18, 2024 Bungeni Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Shally Joseph Raymond lililohoji, Wahitimu wangapi wa Vyuo wanafanya kazi ya kujitolea na wangapi wameajiriwa na kujiajiri baada ya kujitolea.






Nchi wanachama za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Southern African Development Community-SADC) zimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake katika usimamizi na uhifadhi wa misitu miombo hasa katika kuhama kutoka kwenye matumizi ya nishati ya kuni na mkaa kuelekea nishati safi ifikapo mwaka 2030.

Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 18,2024 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) katika Mkutano wa Kimataifa unaohusu Misitu ya Miombo jijini Washington DC nchini Marekani.

“Kikubwa nchi zimeweza kumpongeza Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akitoa maelekezo mbalimbali kwetu sisi kama Wizara na Sekta katika kuhakikisha kwamba misitu ya miombo inalindwa kwa nguvu kubwa, na kwa namna ambavyo amechukua uamuzi thabiti wa kuhakikisha kwamba inapofika mwaka 2030 zaidi ya asilimia 80 ya wananchi watakuwa wameachana na matumizi wa kuni na mkaa na watakuwa wamejielekeza katika nishati safi ya kupikia” Mhe. Kairuki amesisitiza.

Amesema kuwa misitu ya miombo nchini Tanzania na katika ukanda wa kusini imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uharibifu wa misitu ambao unasababishwa na ukataji wa miti usiozingatia sheria, taratibu na kanuni, moto, kilimo cha kuhamahama, uharibifu wa vyanzo vya maji na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha, amefafanua kuwa kupitia mkutano huo, wadau mbalimbali wameanza kuonesha nia ya kusaidia mpango wa utekelezaji wa Azimio la Maputo la mwaka 2022 kuhusu ulinzi na uendelezaji wa misitu ya miombo.

Amesema lengo la Mkutano huo ni kuona namna ya kuendeleza Azimio la Maputo katika kulinda na kuendeleza Misitu ya Miombo ambapo takribani asilimia 93 ya misitu ya Tanzania ni miombo ambayo pamoja na mambo mengine, inatunza wanyamapori , vyanzo vya maji na huduma nyingine za kijamii.

Naye, Kamishna Uhifadhi wa Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo amesema kuwa kupitia mkutano huo nchi za SADC zimekuwa na majadiliano kuhusu kutafuta namna ya kushirikiana baina ya nchi hizo na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kupata rasilimali fedha na kukuza ujuzi na utaalamu kwa ajili ya kusaidia uhifadhi wa misitu hiyo.

Ameongeza kuwa kongamano hilo limehitimishwa na hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi ambapo amesisitiza umuhimu wa nchi hizo kushirikiana katika kubadilishana taarifa , kukabiliana na masuala ya uharibifu wa mifumo ya ikolojia ya miombo hususan biashara haramu za mazao ya misitu na wanyamapori katika ukanda wa SADC.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Deusdedith Bwoyo amesema kuwa mkutano huo umekuwa ni wa kipekee na muhimu ambapo nchi 11 zimebaini kuwa umoja ni nguvu na kwamba kila nchi haiwezi kusimamia kwa ufanisi mkubwa misitu yake na hivyo, zimekutana na kujadili kwa pamoja changamoto za misitu ya miombo na namna ya kuunganisha nguvu na kutafuta rasilimali fedha katika usimamizi na uendelezaji wake kwa faida ya kizazi cha sasa na vijavyo.
Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe.Filipe Jaciton Nyusi akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo  jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akiwa na baadhi ya Mawaziri wa nchi za SADC katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo  jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024.
Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jaciton Nyusi (katikati) akifuatilia mawasilisho kuhusu misitu ya miombo kutoka kwa wawakilishi wa nchi za SADC katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo  jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi na Mazingira wa Msumbiji, Mhe.Ivete Maibaze na Balozi wa Umoja wa Afrika nchini Marekani, Mhe. Hilda Suka-Mafdze (kulia).

Baadhi ya washiriki wa mkutano kutoka nchi mbalimbali wakipiga makofi baada ya kikundi cha burudani cha ngoma za asili kutumbuiza katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo uliofanyika jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) na baadhi ya washiriki wakifuatilia Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo uliofanyika jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024.

Na Mwandishi Wetu,Dodoma

WAENDESHA bodaboda jijini Dodoma wametakiwa kuithamini kazi yao na kujijali wenyewe ili kuondoa dhana iliyojengeka kuwa kundi hilo limekuwa likivunja sheria za usalama barabarani.

Hayo yameelezwa na Polisi Kata wa Kata wa Kata ya Uhuru jijini Dodoma, alipokuwa akitoa mada katika semina ya mafunzo kwa bodaboda iliyoandaliwa na Shirika la Amend Tanzania kwa kushika na Ubalozi wa Uswisi nchini.

Mafunzo hayo ya naendelea jijini Dodoma ikiwa na awamu ya pili kutolewa katika Jiji hilo.

Amesema kumekuwapo na dhana kuwa, waendesha bodaboda wengi hawazingatii sheria za usalama barabarani, hivyo kuhatarisha maisha yao, abiria wanaowabeba na usalama wa vyombo vyao.

Kwa mujibu wa polisi Kata huyo, mafunzo wanayo yatoa ni muhimu kwa kuwa yanawawezesha bodaboda kufahamu usalama wao na jinsi ya kuvimudu vyombo wanavyoviendesha wawapo barabarani.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kata ya Uhuru Fatma Amri anasema mafunzo hayo kwa kiasi kikubwa yanawasaidia vijana katika Kata yake kujitambua na kuzingatia sheria wanapoendesha vyombo vya moto.

Amewasisitiza bodaboda waliopata mafunzo hayo kuhakikisha waafanyia kazi elimu waliyopewa kwa kuzingatia na kuzitekeleza kikamilifu sheria za usalama barabarani.

Kupitia mafunzo hayo waendesha bodaboda hao walielimishwa kuhusu huduma ya kwanza na umuhimu wake, pia usalama wao katika maeneo yao ya kazi.

Mfunzo hayo ambayo yanatolewa kwa ufasdhili wa Ubalozi wa Uswisi yamefanyika kwa bodaboda kuingia darasani na kwa njia ya vitendo kwa lengo la kuwajengea uwezo maofisa usafishaji wote watakaohudhuria mafunzo hayo.



KUBWA Zaidi kutoka Meridianbet ni promosheni ya Expanse ambayo inahusu michezo ya Kasino ya Mtandaoni, kupitia shindano hili unaweza kushinda mpaka 1,250,000/= TZS ukicheza sloti na michezo ya kasino kutoka kwa mtoa huduma wa Expanse. Jisajili Meridianbet kama bado ufurahie promosheni hii yenye kukupa bonasi za kasino kibao.

Kila unapotembelea tovuti ya Meridianbet Kasino unakuwa umetimiza hatua ya kwanza ya kupata maokoto, kisha ukianza kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni bonasi za kasino kibao zinakuwasubiri na ushindi wa shindano hili la Expanse.

Fahamu Zaidi Kuhusu Promosheni ya Expanse.
Promosheni hii imeanza 18.04. 2024 ambapo bonasi za kasino zitagawiwa kwa washindi watakaokuwa wanatangazwa kila siku, baada ya kucheza moja kati ya michezo ya kasino ya mtandaoni iliyopo Meridianbet kutoka Expanse studio.

Promosheni ni halali kwa wachezaji waliosajiliwa kwenye APP na tovuti ya meridianbet.co.tz
Promosheni itafanyika katika mtindo wa mashindano kwa wachezaji kwenye sloti zinazotolewa na Expanse Studio. Michezo ya kasino ya mtandaoni itakayotumika wakati wa promosheni ni:
Battle of Egypt
Forest Rock
Fortune Farm
Lucky's Betting Shop
Maya's Treasure
Piggy Party
Spinning Buddha
Sticky 777
The Book of Eskimo
Veni Vidi Vici
Wild Corrida
Zombie Apocalypse
Battle for the Throne
Bounty Hunters
Capital City Derby
Casino Heist
Fairy in Wonderland
Odd One Out
Planet Power
Shaolin Crew

Wachezaji watashindana kwa mfumo wa pointi ambapo kila dau la jumla ya TZS 2,500 litatoa pointi 2. Dau la chini kwa kila mzunguko kwa promosheni hii ni TZS 400.

Kulingana na msimamo wa mwisho, wachezaji 40 watazawadiwa pesa taslimu na mizunguko ya bure kucheza kwenye kasino ya mtandaoni kama ifuatavyo:

Nafasi ya 1 – TSH 1,250,000
Nafasi ya 2 - TSH 750,000
Nafasi ya 3 – TSH 250,000
Nafasi ya 4 na 5 - TSH 125,000
Nafasi ya 6 mpaka 10 – Mizunguko 300 ya bure kwenye sloti ya PIA
Nafasi ya 11 mpaka 20 - Mizunguko 200 ya bure kwenye sloti ya PIA
Nafasi ya 21. mpaka 30 - Mizunguko 100 ya bure kwenye sloti ya PIA
Nafasi ya 31. mpaka 40 - Mizunguko 50 ya bure kwenye sloti ya PIA

Ushindi utakaotokana na Mizunguko ya bure utahitaji kuzungushwa mara 60x (kwa mfano, ukishinda TZS 10,000 kwenye Mizunguko ya bure, utahitaji kucheza TZS 600,000 kwenye mchezo uleule ili kuhamisha ushindi wako kwenye akaunti ya pesa halisi).

Taarifa kuhusu malipo ya juu kwa kila Kundi la Mizunguko ya bure, washindi watapokea taarifa ambayo itatumwa kwao si zaidi ya saa 13:00 AM tarehe 03.05.2024.

NB: Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni upate ushindi kirahisi, Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz

Top News