Na Mwandishi Wetu

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Gungu Silanga amewataka madiwani na wabunge walioko Wilaya ya Bunda mkoani Mara kutokuwa na mashaka na watu wanaopita kupiga kelele na badala yake wafanye kazi kwani wananchi wanaona utekelezaji wa Ilani unaendelea kufanywa na Serikali ya Chama hicho.

Silanga ameyasema hayo leo Aprili 15,2025 katika kikao cha ndani ya Wanachama wa CCM Wilaya ya Bunda mkoani Mara baada ya kupewa nafasi ya kusalimia wanaCCM hao waliohudhuria kikao kazi cha Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana ambaye yuko katika ziara katika wilaya hiyo akitokea Serengeti. Rorya, Tarime na Butiama.

“Wana Bunda kwanza nawapongeza kwa ushindi ambao umeupata mwaka 2020 kwa kupata madiwani na wabunge wengi.Watu wa Bunda wako timamu na sidhani kama kutakuwa na shida yoyote, wana Bunda ni wachapakazi , wapambanaji na mfumo wa Chama chetu ni kufanya kazi kwa uwazi na ukweli.

“Madiwani na viongozi wengine fanyeni kazi ya kutekeleza llani ya 20220, wanaopita na kupiga kelele achaneni nao, ukifanya kazi wananchi na wana CCM wanaona.Fanyeni kazi Chama kipo imara, Rais Samia Suluhu Hassan yuko imara na Kamati ya siasa Wilaya ya Bunda inafanya kazi,”amesema.

Pia amewahimiza wanaCCM kuendelea kushikamana kwani Chama hicho ili  kiendelee kushika dola ni pale tu ambapo kuna muungano.




Kamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilshi Zanzibar imesifu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania kwa jitihada inayofanya katika usimamizi wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania bara na Zanzibar na kupelekea kuimarika usalama wa usafiri wa anga nchini.

Wajumbe wa kamati hiyo chini ya mwenyekiti wake Mhe. Yahya Rashid Abdallah wametoa pongezi hizo wakati walipotembelea Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakiongozana na watendaji wa Mamalaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) kwa ajili ya kujifunza na kuongeza uwezo wa kusimamia anga kwa njia za kisasa zenye usalama zaidi.

Akiupokea ujumbe huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Daniel Malanga amesema hata sasa wakati taifa linatimiza miaka 60 ya muungano, Mamlaka itaendelea kusimamia sekta hii muhimu kwa kufuata misingi na miongozo yote stahiki ya kitaifa na kimataifa ili Taifa liendelee kuvutia wawekezaji wengi zaidi katika sekta hii adhimu.

Wajumbe wa Baraza wamesema usalama wa anga unatakiwa kupewa kipaumbele na kutazamwa kwa upana wake katika kuimarisha huduma za uongozaji ndege ili kuiwezesha anga kuwa salama na kuleta tija.

Aidha wajumbe hao wameisisitiza TCAA kuhakikisha wakati wote inakua mstari wa mbele katika kupokea teknolojia mpya za sekta ya anga ili kuhakikisha taifa haliachwi nyuma na mageuzi yanayotokea kwa kasi duniani.

Kamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya baraza la wawakilishi ipo Tanzania bara kwa ajili ya shughuli za kawaida za kamati hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Daniel Malanga akiwasilisha majukumu ya Mamlaka mbele ya Kamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilshi Zanzibar lipotembelea Makao Makuu ya TCAA kujionea na kujifunza shughuli za usimamizi wa sekta ya usafiri wa anga nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilshi Zanzibar Yahya Rashid Abdallah akizungumza mara baada ya kamati hiyo kupata taarifa ya kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Baadhi ya wanakamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilshi Zanzibar  wakiuliza maswali mara baada ya kupata maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) walipotembelea makao makuu wa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanakamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilshi Zanzibar, Watumishi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, watendaji wa Mamalaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa kuhusu Mamlaka hiyo.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Godlove Longole akitoa ufafanuzi kuhusu mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho kwa Kamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilshi Zanzibar waliofika chuoni hapo kwa ajili ya kujifunza na kujua kazi hasa za TCAA.
Picha ya pamoja 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, akisikiliza na kujibu maswali ya wananchi mbalimbali waliojitokeza barabarani kumsalimia wakati akiwa njiani, eneo la Mlowo, Mbozi, wakati akitokea Vwawa, Mbozi, kuelekea Mbalizi, mkoani Mbeya tayari kuanza ziara ya siku 2 mkoani humo, leo Jumanne, Aprili 16, 2024, baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili pia, mkoani Songwe. Dk. Nchimbi, ambaye ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, Oganaizesheni, Issa Haji Usi Gavu na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Gabriel Makala, yuko katika ziara ya mikoa 6 ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.





Na Munir Shemweta, MLELE

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda kilichopo halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wametakiwa kusoma kwa bidii na malengo ili wapate kile walichokusudia kukipata kwenye chuo hicho.

Kauli hiyo imetolewa tarehe 15 April 2024 na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mhe. Geophrey Pinda alipokutana na kufanya mazungumzo na wanafunzi wa chuo hicho cha Kilimo kwa lengo la kujua changamoto zinazowakabili.

Amesema, ni vyema wanafunzi wanaosoma chuo hicho Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda Katavi kuangalia malengo yaliyowapeleka chuoni hapo sambamba na yale ya wazazi wao ili kupata kile wanachohitaji kutoka chuo hapo.

"Kama umekubali kuja katika chuo cha Katavi ambacho kiko mbali na macho yaliyo wazi na umekubali kuja hapa kuwa ‘serious’ na masomo yako utapata kitu kikubwa sana" alisema Mhe. Pinda.

Wanafunzi wa chuo hicho ambacho ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Morogoro mbali na kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Kavuu mkoani Katavi kwa kuwatembelea ili kujua changamoto zinazowakabili, wamemuomba kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali chuoni hapo ikiwemo kupatiwa Mizinga ya Nyuki kwa ajili ya Masomo ya Vitendo, Mipira kwa ajili ya mpira wa Miguu na Pete pamoja na Televisheni.

Aidha, wamemuomba kusaidia upatikanaji mikopo kwa wale wanafunzi wasiopata mikopo ya elimu ya juu. Wamesema pamoja na mikopo kupatikana kwa asilimia tofauti kwa wanafunzi wa chuo hicho lakini wapo baadhi yao hawakupata kabisa jambo linalowafanya kuishi kwa shida.

"Ukiangalia mtu hana uwezo na mfano ni kwa mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo chetu wakati mwingine inatulazimu sisi wanafunzi wenzake timchangie" Wamesema wanafunzi.

"Hapa kuna wanafunzi wa mwaka wa kwanza hawajapata mikopo ya elimu ya juu na yupo mmoja ukimuangalia hana uwezo kabisa tulilazimika kumchangia fedha". Walisema.

Naibu RASI wa Ndaki Taaluma Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda Katavi Prof Anna Sikila amesema, pamoja na chuo hicho kuwa na mazingira mazuri lakini wanafunzi wamekuwa wakisoma vizuri na kujituma katika masomo yao.

Kwa mujibu wa Profesa Sikila, kujituma na kusoma kwa bidii kwa wanafunzi wa chuo hicho kumesababisha mwaka jana 2023 mwanafunzi kutoka chuo hicho kuongoza kimasoma kwa vyuo vyote viwili vya Morogoro na Katavi.

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda kinatoa kozi tatu za Shahada ya Sayansi ya Usimamizi wa Rasilimali Nyuki, Stashahada ya Uzalishaji na Usimamizi wa Mazao pamoja na Astashahada ya Uongozaji Watalii na Uwindaji wa Kitalii.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati wa kikao chake na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokione cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda tarehe 15 April 2024 wilayani Mlele mkoa wa Katavi. Kulia ni Naibu RASI wa Ndaki Taaluma Profesa Anna Sikila na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano Debora Magesa.
Naibu RASI wa Ndaki Taaluma Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda Prof Anna Sikila akizungumza wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri wa Ardhi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe. Geophrey Pinda (Kushoto) na wanafunzi wa chuo hicho tarehe 15 April 2024 wilayani Mlele mkoa wa katavi. Kulia ni Rais wa Serikali ya wanafunzi William Bulongo.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda mkoa wa Katavi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Geophrey Pinda (Hayupo pichani) wakati wa kikao chao kilichofanyika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 15 April 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe. Geophrey Pinda (wa tatu kulia), Naibu RASI wa Ndaki  Taaluma Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda Prof. Anna Sikila (wa kwanza kulia), Rais wa Serikali ya Wanafunzi William Bulongo pamoja na Wakuu wa idara wa chuo hicho wakiondoka mara baada ya kikao chao kilichofanyika chuoni hapo tarehe 15 April 2024 wilayani Mlele mkoa wa Katavi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe. Geophrey Pinda (wa tatu kulia) pamoja na RASI wa Ndaki Taaluma Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda Prof Anna Sikila (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo hicho mara baada ya kuzungumza nao tarehe 15 April 2024 wilayani Mlele mkoa wa Katavi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe. Geophrey Pinda (wa pili kulia) akizungumza na Naibu RASI wa Ndaki Taaluma Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda Prof Anna Sikila (kulia) mara baada ya kikao chake na wanafunzi kilichofanyika chuoni hapo katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 15 April 2024. Wengine pichani ni wakuu wa Idara za ICT na Usimamizi Rasilimali Nyuki.

HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo miwili ya UEFA hatua ya robo fainali mechi ya marudiano kupigwa kule Hispania na Ujerumani na meridianbet wanakwambia pesa ipo huku.

Mechi kali itakuwa ya mwenyeji Barcelona dhidi ya PSG ambapo mechi ya kwanza Xavi aliondoka na ushindi pale Parc des Princes mbele ya mashabiki wao na kocha wao Enrique. Barca ameshachukua Kombe hili la ligi ya Mabingwa mara tano huku Paris akiwa hajachukua kombe hili.

PSG mara ya mwisho aliingia fainali ya Kombe hili msimu wa 2019/2020 ambapo alipoteza mbele ya Bayern kwa bao moja kwa bila, huku Barcelona mara ya mwisho kucheza fainali ilikuwa 2015. Leo ni mechi ya kuamua nani kwenda Nusu Fainali na nani abaki. Je Mbappe anaweza kuivusha Paris kwenda hatua inayofuata?

Meridianbet wamempa mwenyeji nafasi kubwa ya kushinda kwa ODDS 2.16 kwa 2.94. Je wewe beti yako unaiweka wapi kwenye hizi mechi mbili?. Je ni Luis Enrique au Xavi Alonso kutinga Nusu Fainali?. Jisajili hapa.

Kumbuka kucheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni ambayo inatolewa ndani ya meridianbet kama vile Poker, Roullette, Aviator, Rockertman, Keno, Sloti na mingine kibao. Ingia mchezoni na ucheze sasa.

Mechi nyingine ambayo itakuwa na mpambano mkali ni hii hapa ambayo inawakutanisha kati ya Borussia Dortmund kutoka Ujerumani dhidi ya Atletico Madrid ambao wanatoka Hispania.

Dortmund ndiye ambaye atakuwa nyumbani leo hii, baada ya kupoteza mechi ya kwanza akiwa ugenini kwa mabao mawili kwa moja. Pia alishawahi kuchukua kombe hili huku Atletico akiwa hajawahi kuchukua ndoo hii.

Diego Simeone na vijana wake wanaingia uwanjani wakiwa na faida ya ushindi hivyo leo wanahitaji kucheza kwa akili sana kwani faida ya goli moja sio kubwa lolote linaweza kutokea. Lakini je naye Terzic atafanya nini pale Signal Iduna Park kuingia Nusu Fainali ya UEFA?

Mechi hii imepewa ODDS 2.16 kwa 3.14 kwa Atletico kushinda. Lakini pia hapa kuna machaguo zaidi ya 1000 ya kubashiri. Hivyo Suka mkeka wako hapa na ubeti.

NA EMMANUEL MBATILO, MOROGORO

WANAWAKE viongozi na vijana wanasiasa wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa tija kwa lengo la kupeana taarifa na kuondokana na matumizi mabaya yenye kuleta athari hasi kwa vijana wakike wanaotarajia kuwa viongozi wa baadae.

Wito huo umetolewa Aprili 16,2024 mkoani Morogoro na Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro Ruth John wakati akifungua mafunzo ya ulinzi wa taarifa na usalama yaliyoandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE) kwa kushirikiana na Taasisi ya YOGE pamoja na Article 19.

Alisema kuwa miaka ya sasa wanasiasa na viongozi wanawake wamekuwa wakikumbwa na ukatili na mashambulizi mitandaoni kutoka kwa watu wasio na mapenzi mema kwa nchi.

"Wanawake ni jeshi kubwa sana na ndio taswira ya taifa na mwanamke huyu anapochafuliwa katika mitandao ataathiri jeshi kubwa ambalo liko nyuma yake hasa vijana wanaochipukia kuwa viongozi hapo baadae", alisema.

Aidha alieleza kuwa mafunzo hayo yanakwenda kujenga uwezo na uelewa kwa wanawake kuhusiana na kutunza taarifa zao pamoja na namna ya kukabiliana na kudhibiti vitendo vya ukatili jambo ambalo litaweka uhakika wa kuwaweka salama wakati wote.

Pamoja na hayo Mhe.Ruth aliwaasa viongozi na wanasiasa kuwa makini na maudhui yao wanayoyaweka mitandaoni,ambapo amebainisha kuwa kukosekana kwa umakini na weledi husababisha mianya na matumizi mabaya ya maudhui ambayo yanaweza kuwaathiri wao na jamii yao.

Pamoja na hayo alitoa pongezi kwa Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE),YOGE pamoja na Article 19 kwa kuanzisha mafunzo hayo ambayo yataleta matokeo chanya kwa viongozi.

Kwa Upande wake Mwanzilishi wa Shirika la (TAMCODE) Bi.Rose Ngunangwa alisema wameamua kuanzisha mafunzo hayo baada ya kugundua kuwa kuna changamoto kwa wanawake kushambuliwa hasa kipindi cha uchaguzi unapokaribia jambo ambalo linadhoofisha nguvu zao katika kuwania nafasi za uongozi.

"Wanawake bado hawajapata ujuzi wa kutosha kwenye matumizi ya mitandao katika kujiwezesha kiuchumi ndio maana sisi TAMCODE,YOGE pamoja na Article 19 tumeona tuanze kuwajengea uwezo wanawake madiwani kwa ukanda wa pwani ili kuwawezesha wanapoelekea katika uchaguzi watumie mitandao kunadi sera zao", alieleza.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Youth Environmental Justice and Gender equality Bi.Philomena Mwalongo alisema mafunzo hayo yamelenga kuwainua wanawake na vijana katika nyanja ya kiuchumi,Siasa pamoja na Teknolojia.

"Tulifanya tafiti tukagundua kuna ombwe kubwa katika ushiriki wa Wanawake viongozi na wanasiasa katika kutambua matumizi salama ya mitandao,na sio tu kujinufaisha wanawake binafsi waliohudhuria hapa Ila kuwagusa wanawake wengine ambao hawapo hapa", alisema

Vilevile Diwani wa kata ya Mji Mpya,Manispaa ya Morogoro Bi.Emmy Kiula ametoa shuhuda ya kuchafuliwa mtandoni ambapo ameeleza kuwa jambo hilo halipendezi kwani linaondoa imani kwa wananchi ambao wamempa dhamana ya uongozi.

"Serikali iangalie sasa kwa wale ambao watabainika sheria iwe kali, watu waadhibiwe na waache tupo katika ulimwengu wa maendeleo,lakini sasa tunapoitumia tofauti mitandao inakatisha tamaa,mtu anapoitumia mitandao kutoa lugha chafu haipendezi,utu wa mtu ni kuheshimiana,"Bi.Emmy alieleza.

Mafunzo hayo,yamejuimuisha wanawake viongozi na vijana wanasiasa katika ukanda wa Mkoa wa pwani,Dar es Salaam pamoja na Morogoro yamejikita hasa kuwainua wanawake katika nyanja ya Uchumi,kisiasa na kiteknolojia kwa kuwajengea uwezo katika masuala hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Youth Environmental Justice and Gender equality Bi.Philomena Mwalongo akizungumza wakati wa mafunzo ya ulinzi wa taarifa na usalama yaliyoandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE) kwa kushirikiana na Taasisi ya YOGE pamoja na Article 19. Mafunzo hayo ya siku moja yamegfanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kingsway mkoani Morogoro.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro Ruth John akifungua mafunzo ya ulinzi wa taarifa na usalama yaliyoandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE) kwa kushirikiana na Taasisi ya YOGE pamoja na Article 19. Mafunzo hayo ya siku moja yamegfanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kingsway mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Youth Environmental Justice and Gender equality Bi.Philomena Mwalongo akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya ulinzi wa taarifa na usalama yaliyoandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE) kwa kushirikiana na Taasisi ya YOGE pamoja na Article 19. Mafunzo hayo ya siku moja yamegfanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kingsway mkoani Morogoro.
Mwanzilishi wa Shirika la (TAMCODE) Bi.Rose Ngunangwa akizungumza wakati wa mafunzo ya ulinzi wa taarifa na usalama yaliyoandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE) kwa kushirikiana na Taasisi ya YOGE pamoja na Article 19. Mafunzo hayo ya siku moja yamegfanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kingsway mkoani Morogoro.


Matukio ya picha mbalimbali wakati wa mafunzo ya ulinzi wa taarifa na usalama yaliyoandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE) kwa kushirikiana na Taasisi ya YOGE pamoja na Article 19. Mafunzo hayo ya siku moja yamegfanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kingsway mkoani Morogoro.


Matukio ya picha mbalimbali wakati wa mafunzo ya ulinzi wa taarifa na usalama yaliyoandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE) kwa kushirikiana na Taasisi ya YOGE pamoja na Article 19. Mafunzo hayo ya siku moja yamegfanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kingsway mkoani Morogoro.





Matukio ya picha mbalimbali wakati wa mafunzo ya ulinzi wa taarifa na usalama yaliyoandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE) kwa kushirikiana na Taasisi ya YOGE pamoja na Article 19. Mafunzo hayo ya siku moja yamegfanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kingsway mkoani Morogoro.



 Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro Ruth John akiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa mafunzo ya ulinzi wa taarifa na usalama yaliyoandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE) kwa kushirikiana na Taasisi ya YOGE pamoja na Article 19. Mafunzo hayo ya siku moja yamegfanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kingsway mkoani Morogoro.

  (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Top News