hakuna kitu kinachokera bongo kama pale kila dereva anataka kuwahi hivyo kazi ni kuchomekea tu. hapa ni barabarani karibu na sea view

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. sasaa michuzi wote mnaendesha mumo humo??

    ReplyDelete
  2. Maskini akipata matako hulia mbwata.

    Kila maskini wa kitanzania akipata pesa anafikiria kutafuta gari bovu toka jalalani Dubai au Japan Kule wanakosingizia kuwa ni magari yaliyotumika wakati ukweli ni kuwa ni takataka ambazo wanatafuta pa kuzitupa.

    Matokeo yake tuna takataka kibao za magari haya yaliyo kwenye mawe na yanayosababisha msongamano barabarani.

    Kila mtu Maskini anataka aandike historia kuwa aliwahi kumiliki gari bila kujali hilo gari lina breki au halina.Ona sasa foleni zinavyotisha!

    ReplyDelete
  3. Hey wee annoy hapo juu. Hivi unafikiri kuwa na gari Dar ni leisure au ni luxury kama ulivyoiacha miaka ya zamani? Mji umepanuka na kuwa na gari ni necessity siku hizi. Kuna sehemu nyingi mabasi hayafiki.

    Unavyosema masikini akipata matako hulia mbwata sijui una maana gani if one can afford a car why not. And just so you know TZ kuna sheria huwezi kuingiza gari ambalo ni more than 10 yrs. Na usitudanganye kwasababu hata Europe na America ni wachache sana wanao weza kunua magari brand new. Wengi wananunua used cars tu kama bongo. Na kama ni foleni ziko kila mahali ulimwengu huu labda kama unaishi kwenye small towns na huoni hay mambo. Rush hours kila miji iko jam-packed iwe Dar, Toronto, London, Sidney or NY City

    Kumbuka miaka ya sasa hivi ni wengi tunajua maisha ya huko ughaibuni. Tumeishi huko pia na tumerudi nyumbani.

    ReplyDelete
  4. namkubaliana na anoy wa Wednesday, March 21, 2007 1:02:00 PM
    maana hao watu waliojilipua huko UK au US wanadharau sana watu wa bongo
    foleni ya magari ipo kila mahali tena paris-france it is worse
    mimi nawashauri hao jamaa waliojilipua huko wawe wanarudi home na kujionea kwa macho zaidi ya kulopokatu baada ya kuona hapa kwenye blog ya michuzi

    ReplyDelete
  5. Sio kweli kuwa takataka zilizotoka Dubai ndio zinasababisha msongamano bali ni mipango mibaya ya serikali yetu kwani nchi za wenzetu ndani baba, mama na watoto kila mtu ana gari kwani wanaendeshea wapi? nyie ndio washamba eti ushuru wa magari upandishwe ili watu washindwe kununua magari, hayo maendeleo yatatoka wapi?

    ReplyDelete
  6. Wewe ulitoa anonymous said ya Thursday, March 22, 2007 2:01:00 AM ni mshamba kama unamatatizo na watu waliojilibua sema mmoja kwa mmoja sio kujibu hoja ya magari bomgo na mambo ya wakimbizi... Hoja ya hapo juu ni wingi wa magari na sio kama mtu anauwezi wa kununua gari , thanx hiyo ni maendeleo maana nyumba, elimu , chakula bora na vingine kama mtu anaweza kununua basi mwacheni wanunua. sio mpka awe mtoto wa mkubwa , mhindi, tajiri ... je unaogoapa nini watu waki na magari ni swala ya serekali yetu kutatua matatizo kama hayo sio kusafiri safiri na kusema kuwa ndio nimeingia madarakani muda mfupi.. damnnn...

    ReplyDelete
  7. Mimi nafikiri tatizo si ubovu wa magari bali ni madereva wenyewe. Hii hali inakera maana madereva wanapoona foleni, wao huchepuka na kupita pembezoni mwa barabara mpaka wanapofika mahala kuwa hawawezi kuendelea kupita pembeni, ndio hapo wanapoanda kuchomeka ili kurudi kwenye mstari. Kinachotokea ni kwamba wanazuia magari tanayotoka upande mwingine kupita, magari yote yanasimama, hamna linalokwenda. Na hapo ndio 'foleni' inapoanza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...