mdau f mtimkubwa wa ufini leo katutumia ujumbe huu ambao anaomba uusome kwa makini
Watu wa pwani wakifikwa na jambo kama misiba ya mfululizo, mfumuko wa maradhi, uzazi wa mfululizo na kadhalika ulisawirisha jambo hilo na msimu wa hali ya hewa ya wakati huo linapotokea jambo. Kwa mfano, utawasikia wazee wa Kiswahili wakisema "..Kaskazi na joto..Maanake limekuwa joto kama tunafanya masaili ya kuingia jehanamu.." Kaskazi ni msimu ulio kati ya mwezi kumi na mbili (Desemba) na mwezi wa tatu (Machi). Kipindi hiki maeneo ya pwani ya Dar es Salaam, Tanga, Unguja, Pemba, na Mombasa huwa na joto kali sana na kadri unavyoenda kaskazini joto hilo huzidi!
Kusi ni msimu unaoanza mwezi wa tano (Mei) hadi Mwezi wa kumi (Oktoba). Miezi hii kwa kawaida ni miezi ya mavuno na biashara ya mazao ya misimu shambani. Kipindi hiki utawasikia wazee wa Kiswahili wakisema "..Kusi akiisha bila matamasha siyo kusi.." Kwa kuwa wakulima wanakuwa wanauza mazao yao basi ndiyo kipindi cha kuwatoa jandoni vijana wa kiume na kuwanema wanawali, hali kadhalika kufunga ndoa kwa wachumba wapya na wale wenye kufunga za mitaala. Kipindi hiki hali ya hewa huwa siyo ya joto. La hasha siwezi kusema kwamba huwa ni baridi aidha.
Zama za kale pepo za kusi na kaskazi zilikuwa zikitumiwa na wafanyabiashara. Madau yaliyosheheni bidhaa mbali mbali toka Uarabuni hususani yale ya Washihiri toka Hadhramauti (Yemen), madau ya Wahindi na mengine toka Uajemi yalikuwa yanakuja msimu wa Kaskazi na kutia nanga kwenye bandari za Unguja, Pemba, Dar es Salaam, Bagamoyo, Saadani, Tanga, Kilwa, Mafia na Mtwara. Kusi ikianza madau hayo yalikuwa yanaondoka na bidhaa mbali mbali toka kwetu na kuzipeleka nchi za mbali kuziuza. Hadi leo hii ukiwa Dar es Salaam, Bagamoyo, Unguja, Pemba, Dar es Salaam, Kilwa na Mtwara bado unaweza kuyaona madau lakini siku hizi si mengi yanayotoka nchi mbali zaidi ya Visiwa vya Komoro na Kenya.
Kusi na Kaskazi ya miaka karibuni imekuja na mageuzi ya itikadi za kisiasa za nchi nyingi za Ulaya. Februari 2005 huko Denmark wanasiasa vijana wa vyama vya The Danish people have voted to keep the current centre-right political coalition of the Venstre (The Liberal Party), Det Konservative Folkeparti (Conservative People's Party) na Dansk Folkeparti (Danish People's Party) wenye kufuata itikadi za mrengo kulia walinyakua uongozi wa kisiasa toka kwa wanasiasa wazee wa itikadi za mrengo wa kushoto. Nayo kusi ya mwezi Septemba 2006 ikakileta chama cha Moderate madarakani nchini Sweden na kuwaangusha Social democrates baada ya kuwa usukanini kwa miaka 12. Jana tarehe 19 Machi, nchini Finland vyama vya mrengo wa kulia vya Centre na Conservative vimechukuwa ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa wabunge hivyo kutakiwa kuunda serikali mpya ya mseto yenye itikadi za mrengo wa kulia.
Azima ya insha hii ni kutaka tukumbuke kwamba zile zama za kukinga mkono SIDA, DANIDA, na FINIDA ndiyo zinagota. Tukipanda ndege kuja kaskazini tuje na mikataba ya biashara tusije na mabakuli yetu ya michango au makabrasha ya ombaomba. Jinginewe, ningekuwa karibu na viongozi wetu ningewashauri wakae na kutafakari upya mahusiano na wanordic kwa sababu kusi na kaskazi zimewasogeza kwingine hawapo tena kule kwa mwanzo kwa wafadhili/wahisani na wafadhiliwa/wahisaniwa!

I like the language man ! Anza kuandika vitabu ,mtiririko mzuri
ReplyDeleteHakuna tofauti yoyote kwani ni nchi ngapi zina itikadi za mlengo wa kulia na bado zinaendelea kutoa misaada, kibao tu, tena nadhani hao ndio watatoa misaada zaidi maana hii misaada wanayotoa karibi asilimia 80 inarudi kwao tena kwa faida zaidi,tena hawa wa mlengo wa kulia ndio wanaopenda kuimarisha sera zao sehemue zingine basi wataziimarisha kwa misaada yao yenye masharti. Jamaa hawa hawasaidii sema wanatumia neno msaada wakusaidie ili iweje. Mie naona hakuna jipya hapa
ReplyDeleteHii ni falsafa hai kabisa, kaka wewe ni mwanamapinduzi wa kweli, umenikumbusha maandiko ya Ndesanjo Macha babu wa blogu za kiswahili. Safi sana kaka
ReplyDeleteKaka mkubwa hapa
Kwa Siasa za Finland hakuna tofauti yoyote itakayo tokea, Hivi vyama vilivyoshinda sio ndio mara yake ya kwanza historia inaonyesha chama cha center na national coalition vimeishakuwa viongozi wa serikali ya ufini miaka ya 80. Uchaguzi wa mwaka 95 chama cha national coalition ambacho kina mlengo wa Kulia kilikuwa madarakani (pamoja na vyama 3 vingine) na miaka hiyo yote misaada ilikuwepo hiyo natofautiana na uchambuzi huo. Kuwa mlengo wa kulia au kushoto sio sababu ya kuototoa misaada (mbona nchi nyingi zenye mlengo wa kulia ndio zinazoongoza kutoa misaada) cha muhimu ni kujitegemea wenyewe.
ReplyDeleteNi kweli Mtimkubwa,na wanaotegemea kela siku zao zinahesabika...
ReplyDeleteyour damn genius man,pamoja na kuwashtua au kuwaibia sili,unafikili hayo wayaona?wao kazi hujaza mifuko yao baada ya hapo kwenda ughaibuni kuanza ombaomba,kwa lugha unanikumbusha shaban robert.
ReplyDeleteTrade not aid
ReplyDeleteBusiness people are keen to tell the G8 leaders that the way to help Africa is to allow it to help itself.
The G8 Business Action for Africa summit says trade is the answer
"It is very important that business keeps reminding (them) that aid is not a long-term solution," Sir Mark insists.
For Andrew Rugasira, chief executive of Rwenzori Coffee, a Ugandan coffee company about to start shipping its produce to the Waitrose supermarket chain in the UK, it is obvious that there is a better way.
Mr Rugasira is scathing about the way aid creates a chronic dependence which he believes stifles creativity.
Although aid and debt forgiveness is necessary in the short term, the only way to secure economic prosperity in Africa is to open up western markets to African companies eager to compete, he insists.
"Trade is the engine for growth," he declares.
Africa's income could grow quickly if trade barriers were lifted
"If Africa increased its proportion of world trade by 2%, it would bring in $150bn in extra revenue.
"That's four times the debt relief offered by the G8."
Key to this would be the removal of tariffs and agricultural subsidies in the West, which make it difficult for African exporters to compete, observes Sir Mark.
And he believes there is a chance the G8 leaders will listen.
"They will reflect and react to the will of their people," says Sir Mark.
"The subsidies are there because the governments at the time perceived that it was what their people wanted."
African efforts
But providing access to the West's cash rich markets is not enough to ensure prosperity in Africa, where there is a pronounced shortage of entrepreneurs, says Mr Dozie.
WHAT IS THE G8?
Name
Group of eight major industrialised states, inc Russia
Members
Canada, France, Germany, Italy, Japan, Russia, UK, US
Aims
Originally set up to discuss trade and economic issues
Now leaders discuss global issues of the day
2005 Summit agenda
Africa
Climate change
Read the full profile
"African governments must develop their private sector," he says. "Foreign investment is necessary, but it is not sufficient to do the magic."
And the international community should also play a part, he says.
"It is necessary for the G8 to help Africa create a critical mass of entrepreneurs."
Getting to that point has proved difficult, Mr Rugasira argues, not least because small and medium-sized enterprises find it hard to get off the ground.
"You've got to recognise the need for some government intervention" similar to that received by companies in many industries in the West, he says.
Returns
The message from many at the conference is simple.
Helping Africa to help itself is not an act of generosity or altruism, they argue, but a pragmatic strategy which offers attractive returns.
They argue that if Africa prospers, the world will prosper too - in part since poverty reduction is a powerful fillip to reduce resentment and hence the risk of terrorism.
For foreign investors, the rewards could be even more obvious.
"The returns in Africa are among the highest in the world," observes Mr Rugasira. "We need to say that
ama Mtimkubwa lugha na misamiati unayoitumia kweli Mwl wetu Betello enzi zile kumbe ulikuwa ukimsikiza kwa makini!... Uchambuzi ulioufanya ni wa kina, lakini shughuli ipo katika kuwaamsha walolala huko nyumbani Tanzania... mfano; Bado kuna Viongozi wa juu wa taifa letu bado wanatuletea stori za matatizo ya umeme na maji yanatokana na amri za mwenyezi mungu!... leo hii Mtera limejaa wameshajisahau tena! "ama chombo cha kuzama hakina rubani!" ~Mchongoma~
ReplyDeletejameni watanzania mnaijua kela annon wa hapo juu bado mwanafunzi ndio maana anaponda kela yaani msaada kwa watu wenye makaratasi ya ndoa na tunakula mpaka wastopishe tumeangaika sana bongo huku ni za bule tufanye nini eti mtimkubwa mtelemko tu
ReplyDeleteWatu wengine humu ndani BABA ZETU walipgwa chini enzi za Nyerere kwa sababu mbalmbali,mna gharabu fulani.... sasa siku hizi kazi ni kujidai mnachambua Siasa ya Tanzania na Ulaya na pia kujitikia vimbembele wakati Viongozi wa kibongo wakija Finland. Mnapoteza muda mwingi kubishana mambo ya siasa pale Chelsea na kwenye vilabu vingine vya pombe. Kwanini msiwe na hobbies kama za kwenda Gym? Na kujiweka fit ? Matumbo yanu yamevimbiana kama NDUMILAKUWILI
ReplyDelete