januari 26, 1965: dk. louis leaky akitoa hotuba mbele ya mwalimu, mkewe dk. mary leaky na chifu erasto mang'enya kabla ya kukabidhi fuvu la mtu wa kale 'zinjathropus bosei' makumbusho ya taifa dar. fuvu hilon ambalo linasadikiwa lina umri wa miaka 1.7 limehifadhiwa hapo makumbusho ya taifa (sasa panajulikana kama makumbusho na nyumba ya utamaduni) na lilivumbuliwa mwaka 1959 na dk. mary leaky huko bonde la olduvai na kabla ya kukabidhiwa lilikuwa ughaibuni kwa miaka kadhaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Rekebisha umri wa fuvu iwe miaka 1.7 million badala ya miaka 1.7.
    Shukrani kwa kutuwekea kumbukumbu hii.

    ReplyDelete
  2. Hiyo uliyofunikwa hapo ni lcd/tft monitor?? nadhani kutokana na vumbi la bongo huyo mama wa kizungu akaamua kuitia kitambaa.Kumbe bongo tuliendelea zamani.

    ReplyDelete
  3. Wengine wanaamini kuwa tulitokana na Bustani ya Eden. Wengine wanaamini kuwa tu wajukuu wa "mtu huyo wa kale 'zinjathropus bosei'."

    Sijui ukweli ni upi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...