hatimaye tovuti halisi ya jeshi la polisi imepatikana nayo ni:

http://www.policeforce.go.tz/index.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Habari Michuzi, Ahsante kwa mtandao wa jeshi la polisi. Lakini nao bado unaudhaifu ule ule ambao wadau wamekuwa wakijadili kwenye blog hii. Mtandao nafikiri bado hawajaumudu vuzuri maana uko taratibu sana kufunguka. Lakini kubwa zaidi ni takwimu ambazo wameziweka, ukiangalia makosa mengi ni ya mwaka 2005 na 2004, unataka kuniambia kwamba mwaka jana na mwaka huu hakuna makosa au hawajandaa tawimu mpya ya makosa hasa ya ujambazi. Hata hao watuhumiwa ambao ni wanted ni majina ya zamani sana, hata ukienda makao makuu ya jeshi la polisi utakuta hayo majina yamebandikwa tangu 2002 na 2003. Katika jeshi la polisi kuna waandishi wa habari wa jeshi la polisi, hivi hawa wanafanya nini?, Tanzania kunamatukio mengi sana kwa nini wasi-punch kwenye mtandao wao, kama hawana habari basi wawe wanachukua toka magazetini. Mtandao mzuri lakini una habari za zamani sana hausaidii kitu. Zumba's

    ReplyDelete
  2. Hii nio moja ya Tovuti ambazo zimekaa Kitanzania haswa.Zinaelewekwa vilivyo kwa kila mtanzania,lugha waliyotumia inaeleweka kwa karibu asilimia kubwa ya watanzania.

    Na zile Tovuti za "Wazungu" zijitahidi kuiga hii ya polisi.

    ReplyDelete
  3. Kura za kishindo zimewapa watawala kiburi

    Kitila Mkumbo



    WANASIASA na wafanyabiashara wana udhaifu mmoja mkubwa unaofanana; wote hupatwa na kiburi pale wanapotambua hawana mshindani.


    Mfanyabiashara anapogundua kuna mfanyabiashara mwenzake anafanya biashara kama yake, tena katika maeneo hayohayo, hujitahidi kutoa huduma nzuri kwa wateja wake, ili kuhakikisha kuwa hawamkimbii na kwamba anaongeza wateja zaidi.


    Kwa mfano, hapa nyumbani tunajua jinsi ambavyo kampuni za simu za mkononi zinavyojitahidi kutoa huduma nzuri kwa wateja wao, ili zisikimbiwe.


    Sote tunakumbuka pia adha ya maduka ya RTC. Waliokuwa na dhamana ya kuendesha haya maduka walifungua na kufunga kwa wakati waliotaka wao bila kujali mahitaji ya wateja wao.


    Na ulikuwa ukifika dukani, ilibidi ubishe hodi na ilibidi ukabiliane na maswali na majibu ya wafanyakazi waliokuwa na kiburi na dharau ya ajabu!


    Tena kuna bidhaa ilibidi uweke oda siku kadhaa ndipo uipate. Baada ya kuruhusiwa ushindani wa kibiashara, Watanzania waliyatelekeleza maduka ya RTC kote nchini, hatua iliyoyafanya maduka haya yapukutike kama majani yasiyoweza kuhimili jua la kiangazi.


    Bado tunaendelea kukabiliana na mateso ya TANESCO kutokana na shirika hili kukosa mshindani katika medani ya kutoa huduma ya umeme.


    Kila mtumiaji wa umeme hapa nchini anayajua majivuno, kiburi na dharau ya wafanyakazi wa TANESCO, kuanzia katika kuomba kuwekewa umeme hadi katika kulipa bili.


    Matatizo mengi ya TANESCO yanasababishwa na shirika hili kutokuwa na ushindani wowote. TANESCO wanajua tupende tusipende hatuna ujanja, lazima tuwategemee wao tu kwa umeme.


    Siku TANESCO wakikabiliwa na ushindani, itabidi ama waamke usingizini ama wakabiliane na madhila yaliyoikumba yaliyokuwa maduka ya RTC.


    Hata hivyo, TANESCO si mada yangu ya leo. Najaribu tu kuonyesha faida za ushindani katika biashara na katika maisha kwa ujumla.


    Katika jamii ambako demokrasia ya vyama vingi imeshamiri, vyama vya siasa navyo hushindana kutoa uongozi makini kwa wananchi kama ambavyo kampuni za kibiashara zinavyoshindana kutoa huduma bora kwa wateja wao.


    Chama kinachopata bahati ya kuchaguliwa kuunda serikali, hujitahidi kutekeleza yale kilichoahidi katika kampeni huku vyama vya upinzani navyo hujitahidi kuonyesha mapungufu ya chama kinachotawala huku vikitoa majibu mbadala kwa matatizo yanayoikabili jamii.


    Pale ambapo chama tawala hutokea kikaendekeza maslahi ya viongozi badala ya kukidhi matakwa ya jamii, huwa kinapata kipigo cha kushindwa, tena mara nyingi hushindwa kwa aibu.


    Nakumbuka, kwa mfano, katika uchaguzi mkuu wa Uingereza mwaka 1997, Chama cha Conservatives kilishindwa vibaya katika uchaguzi huo kwa sababu nyingi; lakini sababu kubwa kabisa ni kuwa Waingereza walikuwa wamechoshwa na majivuno na dharau ya viongozi wa chama hicho.


    Ilifika mahala chama cha Conservatives kilijiona ndio pekee kinachoweza kuongoza Uingereza na kwamba kama haupo katika chama hiki, basi mawazo yako yalikuwa hayana nafasi ya kusikilizwa.


    Nchi jirani ya Kenya pia baada ya mateso ya miaka mingi chini ya utawala wa kiimla, majivuno na dharau za chama cha KANU, wananchi waliamua, wakasema sasa inatosha, maisha yanawezekana bila KANU. Inawezekana Wakenya hawajapata mafanikio makubwa baada ya KANU, lakini tusijidanganye kuwa kuna siku watatamani kurudi katika enzi za utawala wa KANU.


    Hakuna shaka kwamba Watanzania walichoswa na ukiritimba katika biashara. Ushahidi ni ukweli kwamba Watanzania walichangamkia sana huduma za kampuni mbalimbali binafsi zilizoanza kutoa huduma baada ya mfumo wa soko huria kuruhusiwa wakati wa Mzee Ruksa na jinsi kampuni za zamani kama RTC zilivyotelekezwa bila huruma.


    Hata hivyo, sina uhakika kama Watanzania walichoshwa pia na ukiritimba katika nyanja ya siasa. Kwamba leo hii tunaye rais aliyepata ushindi wa asilimia 80 na tuna Bunge lenye kuundwa na wabunge zaidi ya asilimia 80 kutoka chama kimoja, ni dhahiri kuwa tumeendelea kukumbatia ukiritimba wa chama kimoja hadi sasa.


    Kwa kuendelea kukumbatia ukiritimba wa chama kimoja, tumeendelea kukumbatia madhila ya maduka ya RTC; tumeendelea kukumbatia watawala wenye majivuno, kiburi na dharau ya kutisha.


    Naamini wengi bado tunakumbuka majibu ya Waziri wa Fedha katika Serikali ya Mkapa kuhusu malalamiko yaliyohusu uamuzi wa serikali wa kununua ndege ya rais, iliyokuwa ghali na ya anasa kabisa kwa nchi maskini kama Tanzania.


    Wakati Serikali ya CCM chini ya Rais Mkapa ikipitisha maamuzi ya kununua ndege, kulikuwa na wananchi mamilioni wakikabiliwa na njaa. Ndipo wanaharakati na vyama vya upinzani wakaishauri serikali kuwa ingekuwa ni vizuri kununua ndege ya bei nafuu, ili fedha nyingine zielekezwe kwenye kuwaokoa wananchi waliokuwa wanakabiliwa na njaa na kutatua matatizo mengine ya kijamii.


    Waziri wa Fedha wakati huo, Basil Pesambili Mramba, aliwajibu Watanzania kwa kiburi na kejeli tena ndani ya Bunge tukufu la Jamhuri ya Tanzania kuwa, “ndege ya Rais lazima inunuliwe, tena kwa bei hiyohiyo ghali, hata kama ilimaanisha wananchi wenye njaa kula nyasi.”


    Kwa hakika kauli ya Mramba ilizidi kutia doa jeusi katika utawala uliochokwa wa Rais Benjamin Mkapa. Lakini ilikuwa ni aibu zaidi kwa Rais Jakaya Kikwete kumteua Mramba kuwemo katika baraza lake la mawaziri.


    Kwa Mramba kuwepo katika Baraza la Mawaziri la Kikwete ilinifanya nianze kuutazama upya msemo unaosema ‘adui mkubwa wa mwanasiasa ni maneno yake mwenyewe’. Kama msemo huu ungekuwa ni sahihi, basi isingewezekana leo Mramba awe mbunge wa Rombo.


    Hata kama angepenya katika ubunge wa Rombo, isingewezekana awe waziri, tena waziri katika serikali iliyoahidi kumletea kila Mtanzania maisha bora kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya! Ndio nikasema katika makala yangu ya wiki iliyopita kuwa, CCM wanafanana.


    Hiki ni chama kilichosheheni kiburi na dharau ya kutisha. Hawana masikio ya kusikiliza wananchi isipokuwa ya kusikia sauti zao wenyewe.


    Ukiburi wa Serikali ya CCM umeendelea katika awamu ya nne chini ya Rais Kikwete. Ishara pekee aliyoitoa Kikwete kwamba angekuwa ni rais mwenye masikio mapana ya kusikia hata nje ya CCM, ni pale alipotoa hotuba ya kufungua Bunge.


    Baada ya hapo, Kikwete ameendeleza uCCM na pengine u-ZANU-PF; kiburi na dharau kinachoonyeshwa kwa kufanya kila jambo bila kujali hisia na matakwa ya jamii.


    Kwanza, Kikwete akaibuka na baraza kubwa la mawaziri ambalo halijawahi kutokea tangu nchi hii ipate uhuru. Wananchi wengi wakalalamika na wanaendelea kulalamika juu ya gharama kubwa alizotubebesha rais wetu kwa kuwa na mawaziri lundo.


    Wengi wetu tulitarajia Rais Kikwete angesikia kilio cha wananchi pale alipopata nafasi ya kubadilisha Baraza la Mawaziri. Lakini wapi. Rais Kikwete akafanya kama wezi wafanyavyo wanapokosa mtu wa kumwibia; kuhamisha pesa kutoka mfuko mmoja kwenda mwingine, ili kujiridhisha kwamba siku haijapita bure.


    Akaacha baraza lake kama lilivyo, isipokuwa kawabadilisha baadhi ya mawaziri kutoka jengo moja kwenda lingine na magari yao yakawa na nembo yenye jina tofauti la wizara.


    Hakuishia hapo. Siku chache baada ya kuchaguliwa, Rais Kikwete akaibuka na mtindo mpya wa kutuletea maendeleo; kuzunguka kila kona ya dunia hii akiomba misaada na mikopo kwa ajili ya kumaliza umaskini wetu.


    Serikali ya Rais Kikwete imegundua kuwa, Nyerere alikosea sana kusema eti Tanzania haina mjomba huko nje. Ghafla serikali hii sasa imepata wajomba, tena wenye roho nzuri sana kuanzia George Bush wa Marekani, Tony Blair wa Uingereza hadi Jens Stoltenberg wa Norway.


    Kwa hiyo tunaolalamika kuwa safari nyingi za nje anazofanya rais ni mzigo mkubwa kwa wapiga kura, tunaonekana hatujui tunachokiongea maana ziara za rais zimekuwa za mafanikio makubwa - misaada na mikopo ya wajomba!


    Kama vile kiburi katika Serikali ya CCM, imekuwa ni ugonjwa wa kansa unaosambaa kila kona ya mwili mara uingiapo, kimewakumba hata maoafisa katika Wizara ya Fedha.


    Wiki iliyopita, Profesa maarufu wa uchumi Ibrahim Haruna Lipumba alichambua kwa kina, pamoja na mambo mengine, hali ya uchumi hapa nchini.


    Pamoja na mambo mengine, Profesa Lipumba akachambua na kuonyesha kwa takwimu rahisi kabisa jinsi matumizi ya ofisi ya rais yalivyozidi kwa kiwango cha ajabu bajeti iliyopangiwa.


    Badala ya kukabili hoja za Lipumba kwa uchambuzi yakinifu wa kitakwimu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja anatoa majibu rahisi kwa maswali magumu kuwa “si kweli nina uhakika hazijafika hapo”! Sasa kama sio kiburi hiki ni nini?


    Na tukumbuke kuwa, Profesa Lipumba halipwi kwa kufanya kazi ya uchambuzi alioutoa; Mgonja tunayemlipa sisi kwa kodi zetu, hawezi kutueleza bayana kwa nini rais wetu ametumia pesa nyingi zaidi kuliko alizopangiwa katika bajeti!


    Matumizi makubwa ya Ofisi ya Rais Kikwete yameonyesha kwa mara nyingine tena kuwa, matatizo yetu ya umaskini yanasababishwa na siasa zaidi kuliko hali yetu ya uchumi. Serikali yetu haijawahi kukosa uwezo wa kifedha wa kutoa huduma bora za jamii.


    Hela ilipatikana kwa ajili ya kununua ndege na rada ya anasa. Yakapatikana mabilioni ya kujenga jengo la anasa la Benki Kuu. Kuna hela ya kumuwezesha rais wetu kuzunguka kila kona ya dunia hii. Tuna hela ya kuwahudumia mawaziri 60 na magari yao 120.


    Lakini hatuna hela ya kuwalipia ada na chakula wanafunzi wanaosoma katika vyuo vyetu vikuu. Tena hatuna hela ya kununua dawa katika hospitali yetu wala ya kujenga shule, inabidi wananchi tuchangie kwa mara ya pili baada ya kulipa kodi zetu.


    Kinachokosekana katika serikali yetu ni kipaumbele kinachosababishwa na viongozi wa CCM kufanya mambo bila kujali hisia na matakwa ya jamii, ambayo tafsiri yake ni kiburi na dharau.


    Lakini cha kujiuliza, Serikali ya CCM inapata wapi kiburi na dharau walizo nazo? Ni wazi kuwa kiburi cha serikali ya CCM tumekilea sisi wenyewe wananchi. Ni kura zetu za kishindo tunazoendelea kuwapa CCM.


    Kwa kuwapa ushindi wa asilimia 80, CCM wanaamini hawana mshindani katika biashara ya siasa. Kwa hiyo hawajali, maana wanajua tupende tusipende lazima tukanunue bidhaa dukani kwao.


    Sasa ifike mahala tuwaonyeshe CCM kuwa sasa tupo katika mfumo si tu wa soko huria la biashara za bidhaa, bali pia biashara ya siasa. Tuzikatae propaganda za CCM kwamba vyama vya upinzani bado ni vichanga.


    Kwa kigezo cha sera, ni wazi kuwa sasa tuna vyama makini vya upinzani kiasi hata serikali ya Kikwete imeamua kutekeleza baadhi ya sera za baadhi ya vyama vya upinzani tena bila hata ruhusa ya hati miliki.


    Bila wananchi kuipiga kikumbo CCM kama tulivyofanya kwa maduka ya RTC, tutaendelea kukabiliana na kiburi na dharau za viongozi wetu.

    ReplyDelete
  4. michu naona kulikuwa na bifu ktk tenda ya web ya Polisi ndio maana kuna ile web feki (kama prototype ya proposal) - yaani www.cjo.co.tz, then hii ambayo inaonekana ya kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...