leo kwenye mida ya saa sita hivi za mchana nilipata bahati ya kutembelewa ofisini daily news na mzee Juma a.s. ngotyagay ambaye ni mlemavu anaeishi tandika azimio, dar.
alikuja ofisini kunifuata baada ya kusikiliza idhaa ya kiswahili ya bbc majuma kadhaa yalopita kuhusu teknolojia ya blogu ambapo pamoja na kuisimulia mafanikio ya blogu ya issamichuzi.blogspot.com katika kupata wageni wengi, pia nilihojiwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na nilianzaje-anzaje kublogu.
mzee saidi, ambaye ni msikilizaji mkubwa wa bbc aliamua kujaribu kuomba msaada toka kwa wasamaria wema duniani kote wanaosoma blogu hii, huku akiwa na kicheko cha imani kubwa kwamba kilo chake kitaweza kusikika endapo atatumia njia ya blogu yetu hii.
aliniambia yeye alizaliwa tarehe 09/02/1940 huko muhoro, rufiji, akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto watatu. anasema alizaliwa kawaida tu lakini alipofikisha umri wa miaka 3 ugonjwa wa ajabu (anahisi ni polio) ulimkumba na kujikuta analemaa na kuwa kiwete.
pamoja na hayo, alijiunga na shule ya msingi ya kilindi na kisha shule ya kati ya utete kabla ya kufaulu na kuelekea uganda alikosoma elimu ya sekondari katika shule ya kabale-busega eneo la mkono, njia ya kuelekea masaka, ambako alihitimu kidato cha nne mwaka 1965.
baada ya hapo alirejea nyumbani bongo alikobahatika kupata kazi katika shirika la maji akiwa kama karani wa masijala (registry clerk) ambako alitumikia kwa miaka 22 kabla ya kustaafu. yeye ni mmoja wa wafanyakazi waanzilishi wa 'nuwa' .
anakumbuka alifunga ndoa tarehe 18/12/1976 na bibie habiba shaaban ambaye alijaaliwa kuzaa naye watoto wanne ambao ni jafari (18) ambaye kwa bahati mbaya anasumbuliwa na ugonjwa wa akili. wa pili ni salumu (12) anayesoma, na kufuatiwa na Nazira (6) na kisha muzna (4) ambao wote wako shule.
Anasema muda wote huo ameweza kuishi na kuilea familia yake kwa kiwango cha kawida hadi pesa za pensheni alizopata kazini kumuishia na malipo ya kila mwezi kuwa madogo kukidhi mahitaji, na kujikuta hana jinsi ila kuomba msaada wa pesa, hata kama kwa mkopo, ili aendelee kuilea familia yake.
jitahada za kutafuta na kupata pesa za kuanzisha mradi zimegonga ukuta na aliposikia kuhusu blogu yetu hii akapata wazo la kuomba msaada kwa wadau kumuwezesha kutimiza malengo yake. na mradi alioubuni na ambao anahisi unaweza kumuondolea umasikini kiasi cha kumzuia asiende kuwa omba omba mitaani kama wafanyavyo watu kama yeye, ni mradi wa kufuga kuku wa mayai na nyama.
kwa elimu kiasi aliyonayo ameweza kuandika propoza ya mradi na thamani yake ambao aliniletea leo ofisini ili niweze kuutangaza na kumsaidia kupata wafadhili. ana imani kubwa kuwa wadau wa blogu hii pamoja na redio ya bbc watamsaidia na tayari ameshatanguliza shukurani zake kwa msamaria mwema yeyote ataejitokeza.
pamoja na kuwa msikilizaji mzuri wa idhaa ya kiswahili ya bbc, pia hobi zake zingine ni kusoma novo, akimtaja ian flemming mtunzi wa riwaya za james bond kuwa kipenzi chake, akifuatiwa na mtunzi aliemtaja kama peter cheyney.
kwa kusema kweli niliguswa sana na ugeni wa mzee said ambaye anasema nyumbani anaitwa 'baba gay' kama kifupisho cha jina lake la mwisho. chozi lilinitoka kuona mzee ambaye ni mlemavu amefunga safari toka tandika azimio (kiasi cha kilomita 17) kuja kwangu sio kuomba msaada wa pesa bali wa kutangaziwa shida zake kupitia blogu yetu hii.
"nimepata imani kubwa na blogu yako baada ya bbc kutangaza umefikisha zaidi ya wasomaji milioni moja", aliniambia mzee huyu mlemavu ambaye anatumia baisikeli ya kiti kutembelea.
kunradhi wadau kama nitakuwa nimewakwaza kwa hili 'gazeti' lakini kama usemi wa wahenga wetu wanavyosema, 'tarishi hauwawi'. hivyo niko chini ya miguu yenu kuomba wasamaria wema tumsaidie mdau mwenzetu huyu. anuani yake na akaunti yake ya benki nimebandika huko chini.
tafadhali naomba mdau usisite kunipitishia ujumbe humu bloguni kama uko tayari kumsaidia mzee saidi na kama utapenda taja kiwango ulichotuma kwenye akaunti yake. kumbuka kutoa ni moyo...
unaweza kuwasiliana na mzee saidi kwa namba ya simu yake ya mkononi +255 756 003 156 moja kwa moja.
naomba kuwasilisha huku nikiwa na imani wadau mtasikiliza kilio cha huyu mdau mwenzetu.



Michuzi mi nitamchangia ngoja nitafakari njia nzuri ya kumtumia hizo hela maana bank transfer ni expensive kuliko money gram, anyways i will come back with any input i come accross
ReplyDeleteMichuzi huyo mzee anaonekana ana draft proposal nzuri ya kutaka kufanya biashara, hivyo mimi ninaamini kabisa anaweza ku-qualify kuomba mkopo bank kutoka katika mfuko wa ujasiliamali uliotolewa na rais JK. Pamojana wadau wengine kumsaidia lakini pia jaribu kumshauri juu hiyo mikopo.
ReplyDeleteMichuzi.
ReplyDeleteHongera kwa kazi nzuri. Mie sina uwezo wa kumsaidia ila nakuomba tu usiupdate blog yako kama kwa siku mbili tatu hivi ili watu wengi waweze kuona hii habari. Ni habari inayogusa saana na Ishallah atapata msaada
wewe annon hapo juu wa April 14 saa 1:02:00AM. Kwanza nimefurahishwa na moyo wako wa upendo kuwasaidia watu wengine wenye matatizo.
ReplyDeleteNjia nzuri ni Western union money transfer , kama upo USA ni bora zaidi njia hiyo. Sijui kwa nchi nyingine gharama zake zikoje. Ila waweza kucheck through www.westernunion.com utaweza ona gharama za kusafirisha pesa.
Ask me, if I could be of any help again kupitia blogu letu hili. I'm a big fan
MICHUZI NI JAMBO LA BUSARA LAKINI NINGESHAURI MZEE GAY ANUNULIWE BAJAJ ILI ASANYE NA APATE ANGALAU SENTI YA KULISHA NYUMBA.
ReplyDeleteNUWA NA SERIKALI SIKU HIZI HAZIANGALII WALIOSAIDIA. WAMESHINDWA KUMSAIDIA HATA BAJAJ ALIPOSTAAFU.
VIPI WANA CHOO KIKUU NAO WANA MPANGO GANI. WENYE URAIA MMBILI TUPO TAYARI KUMSAIDIA...UDSM VIPI WAMETOA CHOCHOTE?
Asante Michuzi kwa hili. Mimi ni kama mmoja wa wasomi wa hii blog yako ninashukuru kwa haya. lakini nina maswali kadhaa?
ReplyDelete1.Jee kuna njia nyingine atakayoweza kupokea hela? Kama huyo aliyetangulia kuandika hapo juu ni kweli kufanya international wire transfer through banks wao wana charge per transaction ni hussle free kwa anayepokea bongo lakini amount akayepokea ni ndogo sana. Lets say nikitaka kumpa $50. itani cost mimi kwa moja ya bank account yangu either $20 or $35 au ndio hivyo nimtumie $50 apokee $20. Western Union or Money gram is at least a little reasonable
2.Tumeona hii proposal je anayo back up plan nyingine? Ninauliza hivi kwakua hapa kam sikosei haombi mkopo ila anaomba msaada. Mkopo mtu akiomba ni 50/50 chance either apate au asipate. Lakini kama ni msaada labda wabongo tukijikang’ata na kumtumia hela na labda zifike tu 10 million. sasa huo mradi atafanya au hatafanya?
3.How kama hapa akikubali kuomba watu mikopo instead of msaada. Kuna watu tunaweza kuinverts kupitia yeye. Japo sitahitaji any interest lakini hii ni njia mojawapo ya kumsaidia. Watu wanaweza kupata contract na yeye na kumpa from $500 - $2000 lakini kama guarantee baada ya miezi fulani ataarudisha hiyo hela. Watu wanaweza ku sacrifice any interest wangepata kwa a certain amount of money in their accounts for a certain period of time for a good course.
I hope you will take into consideration and update more about those issues.
Thanks
Michuzi,
ReplyDeletekuna mahali ktk hiyo article umetumia neno KIWETE..
Hilo sio neno sahihi mtu wangu. libadili na "alipopata ulemavu".
maneno yenye kuanza na 'Ki' ktk lugha ya kiswahili hayana tafsiri nzuri ktk jamii..
Nitachanga, thanks!
ReplyDeleteMimi niko UK na inshaalah panapo uhai nitajitahidi kuangalia jinsio gani ya kuweza kumsaidia huyo mzeee....si lazima iwe pesa lakini chochote kitakachoweza kumfanyia wepesi wa kimaisha ntajitahidi kumfanyia lililo mkononi mwangu
ReplyDeletenaunga mkono Michuzi najua unataka kubandika mapicha ya miss universe lakini hebu vuta subra kidogo kwani issue ya huyu mzee ni muhimu zaidi na inahitaji kufanyiwa kazi asap
wasalaam
Mambo ya kuchnagishana ni kizamani. Kumsadia huyu mzee ni kumtafutia kazi ili apate hizo hel. Michuzi vipi hapo daily News mzee si alikuwa registry clerk...kazi hizo zipo hapo nauhakika. Kumchangia sio ufumbuzi wa kudumu kesho tena atakuja kuomba tumchangie mtoto aende shule. MTAFUTIENI KAZI TAFADHALI!
ReplyDeleteHebu kwa dakika moja tusimuangalie huyu mzee kama mwenye upungufu wa wa kutembea bali tumwangalie kama binadamu yeyote.
ReplyDeleteUmri wake na hao watoto mbona haviendani. Jamani msinielewe vibaya lakini hata kama una hela nyingi kuzaa uzeeni guarantee ya kuwatunza watoto au kuwaona hao watoto wakikua ni ndogo.
Hili ni jambo la kuanza kulijadili sana Tanzania especially mitaa ya pwani. Tuanze kuweka awareness ya matatizo ya kuzaa watoto ukiwa mdogo sana au mzee sana.
Mimi niko Holland, kazi ya kuku nimeifanya ni ngumu sana,kwa kuwa mzee wetu ni mlemavu, na mama anavyo onekana ni mtu mzima pia,ushauri wangu ni kwamba watu wamsaidie kadri watakavyo jaaliwa, lakini wewe mchuzi jaribu kumpeleka bank apate mikopo kama ya kuchimbiwa kisima, ili afanye biashara ya kuuza maji, maana tandika maji ni taabu, hiyo ni biashara rahisi kwake na hata mama hapo ataweza kumsaidia, kuliko hao kuku, ni wagumu sana ushauri tu.
ReplyDelete