hahaha! sikujua kwamba mdau maabadi wa bisengo musika ya columbus, ohio, ni lunyasi damu hadi aliponiletea snepu hii anayoitunza tokea miaka hiyo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. kumbukumbu nzuri sana,jamani wale washabki damu wa wekundu wa msimbazi tutajieni orodha hiyo!especial ww ulituma picha hii!!

    ReplyDelete
  2. simba hovyoooo,ndo mana 1993 walibamizwa na stella fainali CAF.

    ReplyDelete
  3. wachovu kweli hawa jamaa wametukimbia kwenye kombe la Taska.
    Leo tunao kigoma huku na timu ya mkoa, na watakandamizwa tu

    ReplyDelete
  4. Ebwanaeee si mchezooooooooo...kwa mbali namuona tanzania one "mwamedi mwameja" pia yuko george magele masatu na kuna mtu mmoja ambaye mpaka sasa sijaona mtu mwenye kipaje kama yeye.huyu ni HUSSEIN AMAN MASHA,nakumbuka masha alikuwa anacheza dakika tisini bila kuchafuka wakati kuna mvua na matope mengi uwanjani,jamaa alikuwa na kipaji na control ya ajabu sana.jamaaa alikuwa anakwenda mazoezi kwa nadla sana,lakini kwenye mechi vitu vyake vilkuwa si vywa mchezo.kwa wale wenye kumbukumbu ndani ya uwanja wa taifa mechi kati ya tanzania na liberia,MASHA alibaki kwenye penalty box yeye,mwameja na george weah,kwa kuonyesha yeye ni hatari alimpiga kanzu george weah alafu akaosha mbele.ilikuwa ni burudani ya kutosha sana.nakuomba kaka mchuzi ucheki huyu masha yuko wapi sasa na anafanya shughuli gani.simba hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee......................

    ReplyDelete
  5. Hi, wengi wa wachezaji hao ngoma imeisha wapeleka and wengine sasa hivi hawana kitu, nilikutana na Kipese last year nilipokuwa likizo, amepigika kinoma, sasa ni kocha wa timu ya wanawake

    ReplyDelete
  6. Simba walifungwa kimpira lakini hawajawahi kufungwa goli sita.Na fainali ya kombe lolote la CAF nyie mdembwedo mtasikia tu redioni.Rekodi ya Simba kwenye mechi za kimataifa hamtaifikia katu.Wamechukua CECAFA mara 6 nyie mmechukua mara ngapi???Waarabu wamewageuza wake kila timu kutoka arabuni inajifundishia kufunga magoli kwenu.Kazi kujitapa na mpira wa magazetini na vijiwe vya kahawa.

    ReplyDelete
  7. Simba wanaitwaga taifa kubwa kwa maana, Mataji kedekede kuanzia haya ya Bongo, ya Afrika Mashariki na Kati, ya Taska na mengineyo. Yanga nyie hamna kitu kazi mikelele tu haya sasa mbona kila siku tukikutana na nyie ni lazima muushie kulizwa tu?. Nako katika ngazi za kimataifa tuna mafanikio makubwa kushinda nyie. Sisi bado nusu tuingie nusu fainali ya mabingwa 2003, nyie enzi zile mlivyo iingia katika ligi ya mabingwa mlikuwa ni vibonde tu. Mara leo Raja kakupigeni 6 mara kesho Raja kakupigeni 3 tena nunge halafu tena nyumbani.Aibu tu nyinyi

    ReplyDelete
  8. kweli sisi Yanga tuna kigeu kigeu sana .Leo tumeshinda kwa matuta tumeshangilia tulipofungwa tulisema bahati.Madega alisema tunakwenda kucheza mpira Mwanza sio kushinda kwa matuta leo atatuambiaje wanayanga?Tumecheza mpira mbovu bila refa tungeondoka.

    ReplyDelete
  9. Anonymous wa hapo juu u just made my day, hizo story za Hussein Marsha na Joji Masatu nimezisikia sana mzee. Ila for real, Husein Marsha will go down as one of best midfielder bongo had to offer, yuko level moja na Marehemu Ramadhan Lenny, pamoja na Marehemu Method Mogella "fundi".

    Hiyo story ya kumpiga kanzu Joji Weah ndani ya 18 sikuwahi kuisikia but it sure hell entertaining to think about it.

    As far as hicho kikosi naona kuna mdhamini Azim Dewji, Mwameja, namuona Malota Soma "Ball Jugler", marehemu Edward Cyril Chumilla, Kocha King Kibaden Mputa, msaidizi Salu Madadi, Godwin Aswile "Scania", namuona Kasongo Athuman, Umecheki Joji Masatu with his signature panki.

    Long live Mnyama Mkali "Simba"

    ReplyDelete
  10. Hiyo timu ilikuwa kali sana lakini ngoja nijaribu kukumbuka hi list,kutoka chini waliochuchumaa G olikipa namba mbili OFFERN MARTIN,huyo anayefuata nimemsahau,ABDUL MACHINE,TOBIAS KIPESE,Sina uhakika na huyu kama JAMHURI KIHWELU,MALOTA SOMA,EDWARD CHUMILA,LENNY RAMADHANI,FIKIRI MAGOSO NA MOHAMED MWAMEJA.Kutaka juu ni Ass coach,eshete(mwithiopia)AZIM DEWJI,DEO MKUKI,GEORGE MASATU,GEORGE LUKAS,RAPHAEL PAUL(Nylon)IDD SELEMAN,KIBADENI NA KASSIM DEWJI.

    ReplyDelete
  11. Hili chama lilikuwa kama hivi.. Waliopiga magoti toka kushoto kwenda kulia. Often Martin, Rashid Abdallah, Abdul Mashine, Thomas Kipese, Kasongo Athumani, Malota Soma "Ball Juggler", Edward Chumila "Edo boy", Ramadhan Lenny "Abega", Fikiri Magoso na Mohamed Mwameja "Tanzania One". Waliosimama ni Eshete (kocha msaidizi), Azima Dewji, Godwin Aswile "Mlimba", Deo Mkuki, George Masatu, George Lucas, Michael Paul "Nylon", Iddi Selemani, King Kibaden "Mputa", Kassim Dewji.

    Lunyasi for life...

    ReplyDelete
  12. UJANJA WA SIMBA IKICHEZA NDANI YA TANZANIA TUU. YANGA INA MAFANIKIO ZAIDI IKICHEZA NJE YA TANZANIA KWA TAARIFA YENU.

    ReplyDelete
  13. WOTE MMEANDIKA MNACHOKIJUA NYINYI LAKINI NIMEONA ASILIMIA 2 TU NDIO WALIANDIKA UKWELI KUHUSU KIKOSI CHA WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA, NINA IMANI WALIOIPONDA SIMBA WOTE NI YANGA.

    TUELEWE KWAMBA SIKU ZOTE JIRANI AKIPATA MAENDELEAO ILI HALI WEWE HUNA KITU LAZIMA UCHUKIE KWA SABABU ZA CHUKI BINAFSI.

    SASA NAWAAMBIA HIVI SIMBA NDIO TIMU YA UKWELI TANZANIA, KUFUNGWA NYUMBANI KATIKA HATUA YA FAINALI MWAKA 1993 SIMBA SIO WA KWANZA KUFUNGWA ULIMWENGUNI NA WALIKUBALI KWA SABABU NDIO MATOKEO YA MCHEZO.

    NYINYI YANGA YAJKWENU YANAFAHAMIKA UZURI LAKINI HATUYATOI HADHARANI, SASA IWEJE HI LEO SIMBA WAMEWEKWA KATIKA BLOG HII MNAANZA KUSEMA OVYO TENA BILA KUTAMBUA MLISEMALO.

    NAKUOMBA SANA MICHUZI LEO HII WEKA PICHA YA YANGA ALAFU UONE YATAKAYOSEMWA YOTE YATAKUWA YA KWELI.

    KAKA NA WEWE DADA, ULIEANDIKA HAPO JUU MWASTAHILI KUKUBALIA TIMU YA SIMBA NDIO TIMU BORA TANZANIA HAKUNA NYINGINE KAMA HIYO JAMANI!!!! HAO HUWA HAWACHUKUWI UBINGWA KWA KUHONGA KAMA ILIVYOKUWA KWA WENZETU, HAO ( SIMBA) WANACHUKUWA UBINGWA KIHALALI NA NDIO MAANA WAKIENDA KUCHEZA MASHINDANO MAKUBWA AFRIKA HUWA WANAFANYA KWELI SASA WENNZETU MKIENDA HUKO MNAFIKIRIA NJIA YA MKATO ALAFU MNAJIKUTA MNATIA AIBU HADI MKIRUDI HAPA MNAOGOPA HATA KUTUTAZAMA MACHONI.

    MIMI NAPENDA SANA SOKA LA NJE LAKINI NIMECHUKIZWA NA KAULI ZENU SASA KWA NINI MSIANDIKE UKWELI JAMANI.

    HUU WAENDA MWAKA WA SABA SASA LADHA YA USHINDI WA KUMFUNGA SIMBA YANGA HAWAIJUI SASA HAMUONI HAPO KUNA WALAKINI??????

    EBWANAA NAWEZA KUANDIKA HADI KESHO SASA HICHO KIDOGO KINAWATOSHA NA NINA HAKIKA SIMBA ATAENDELEA KUWADOBODESHA KATIKA LIGI KUU MSIMU WA MWAKA 2007-08.

    KAZI NJEMA KWA WOTE.

    ReplyDelete
  14. Huyo aliyesema Mwameja alidaka siku Taifa Stars ilivyocheza na Liberia ni muongo mkubwa na aogopwe kama "UKOMA". Kuweka mambo sawa Steven Nemes ndiye alidaka siku ile na alipangua kiki ya George Weah aliyekuwa wamewalamba chenga mabeki wetu na kubakia ana kwa ana na Nemes. Hayo ya Masha kumpiga kanzu Weah ni uongo vile vile, yaelekea wewe wakati huo ulikua unaishi Namanyere na mpira uliusikilizia redioni.

    ReplyDelete
  15. Hoja moja ya msingi ambayo wana yebo yebo (Yanga) au siku hizi mdebwedo hawawezi kuijibu ni kwa vipi timu inayojua na kucheza mpira wa haki, inashinda nyumbani tu? na wakati mwingine inafukuza wachezaji na benchi la ufundi mara tu baada ya kuchukua ubingwa? inaingia akilini kweli? kwa mambo kama haya bila shaka kuna jambo zaidi ya mpira uwanjani.

    ReplyDelete
  16. Huo ndiyo ushabiki wa vijiweni. Watu mnaambiwa tajeni majina ya hao wachezaji, mnaanza kubishana Mwameja na Nemes nani alidaka mechi na Liberia. Kama mmeishiwa mkae kimya ebooooo

    Mzee wa TBS

    ReplyDelete
  17. SIMBA MIAKA YOTE HAINA MSHINDANI IWE KWENYE KUTOA ZAWADI KWA WACHEZAJI WAKE AU KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA INAYOSHIRIKI.
    KIKOSI HIKI KAMA SIYO NJAMA ZA ALIYEKUWA RAFIKI WA MUHIDINI ISSA MICHUZI (DEWJI), KINGETWAA UBINGWA WA STELLA BILA MATATIZO.
    HATA HIVYO, JAMAA ALIJIRUDI NA BAADA YA KUSHINDWA KUTOA ZAWADI YA MAGARI AINA YA KIA, ALIJITAHIDI NA KUWANUNULIA TOYOTA COROLLA WACHEZAJI WOTE WALIOSHIRIKI MASHINDANO HAYO YA KOMBE LA CUF.
    HIYO NI ZAWADI KUBWA, YA KWANZA NA AINA YAKE AMBAYO ILIWAHI KUTOLEWA KWA WACHEZAJI MPIRA SIYO TU TANZANIA, BALI AFRIKA MASHARIKI, KATI NA KUSINI KWA TIMU KUWEZA KUFIKA FAINALI NA KUPEWA ZAWADI YA MAGARI INGAWA HAWAKUCHUKUA KOMBE.
    NAJUA WADAU WATADAI FEDHA ZA ZAWADI ZILITOKANA NA MAKATO YA WACHEZAJI WENYEWE, LAKINI HATA HIYO AKILI YA KUFANYA HIVYO NAYO INAHITAJI FIKIRA MBIVU ZA BUSARA KAMA WALIZONAZO SIMBA!
    KAMA KUNA SHABIKI YEYOTE WA YANGA ANABISHA JUU HILO, AJITOKEZE HAPA NA ATOE MAFANIKIO YOYOTE YA MDEBWEDO WAO TANGU ILIPOANZISHWA HADI KUGEUZWA KAMPUNI HUKU VIONGOZI WAO WAKIWA WEUPEEEE. SI BORA INGEBAKI VILE VILE KANDAMBILI!

    ReplyDelete
  18. UKISIKIA MAMBO YA 'BORA' ZAWADI NDIO HAYO SASA ALLIYOFANYA DEWJI.. WE UNAONA GARI LA JABA LA LAKI SABA TENA RECONDITIONED NDIO ZAWADI YA MAANA.??? SANSAN ALIWATIA UMASKINI TUU WACHEZAJI KWANI HAKUNA HATA MMOJA ALIYEWEZA KUKAA NA GARI KWA MIAKA MIWILI WOOTE YALIWASHINDA NA YAKAJIFILIA MBALI. NI BORA ANGEWAPA HIZO PESA AU KUWANUNULIA VIWANJA WAJENGE.
    PILI WEWE MSHAMBA WA HAPO JUU NI KUWA, KAMA UKIWA HAUNA UHAKIKA WA MAMBO KAA KIMYA TUU. UNAPOSEMA SIMBA NDIO INATOA ZAWADI KUBWA KWA WACHEZAJI WAKE AFRIKA MASHARIKI NA KATI UNA UHAKIKA ? WEWE UNAJUA RWANDA WANAWALIPA VIZURI WACHEZAJI WAO ANGALIA TEAM KAMA APR, VILLA YA UGANDA PIA . KWANZA WACHEZAJI WA SIMBA MISHAHARA YAO NI LAKI MOJA, AMBAYO HATA DOLA MIA HAIJAFIKA!!TANGU LINI MUHINDI AU MWARABU AKATOA OVYO PESA YAKE. HALAFU WEWE UNASIFIA? KALAGHABHALOOOO..

    ReplyDelete
  19. SIMBA KWANZA KAMA MNA MAFANIKIO KWANINI MPAKA LEO HAMJAWAHI KUTOA MCHEZAJI YEYOTE AKAWIKA KIMATAIFA MPAKA KUCHEZA KLABU KUBWA PROFFESIONALLY? WACHEZAJI WAKICHEZEA SIMBA BASI NDIO MWISHO WA MAENDELEO YAO, HAWAENDI ZAIDI YA HAPO KWA VIONGOZI HUWA WANAZIBIA WAKITAKA KWENDA NJE KUCHEZA. HUU NI USHAMBA WA KUTUPWA, HALAFU MNAJIONA WAJANJA KUIFUNGA YANGA TUU. TENA NGOJA LIGI YA KWELI IANZE YANGA TURUDISHE KOMBE LETU. MNYAMA HAPATI KITU LIGI KUU KWANI MWAKA HUU MNA VIPINGAMIZI VINGI SANA; YANGA, PAN AFRICAN, TOTO AFRICA NA PRISONS HAPO MTAISHIA KUPATA POINTI ZA DROO KAMA MKIJITAHIDI TENA MKUMBUKE HAMNA MATUTAAAAAAAAAA..

    ReplyDelete
  20. Wewe anon; wa 10:01 (shabiki wa mdebwedo) nadhani hujamuelewa vizuri Lunyasi mwenzangu.
    Au pengine kiswahili kinakupiga chenga hasa wale wanaojilipua huko majuu kama wewe.
    Nadhani ukisoma vizuri, jamaa anadai kuwa hiyo ILIKUWA (ilikuwa narudia...sentensi iliyopita) moja kati ya zawadi kubwa ZILIZOWAHI (zilizo) kutolewa kwa timu kufika fainali BILA kutwaa KOMBE na kupewa zawadi ya GARI!
    Mtu ukipewa zawadi iwe BORA zawadi au ZAWADI bora, ni zawadi tu. Kwa hiyo kama magari yalikuwa "nyanya", BADO ni ZAWADI.Au siyo wan LUNYASI wenzangu.
    Yanga (mdebwedo) pamoja na kupata zaidi ya $30,000 toka CAF, lakini wachezaji wao waliambulia mikono mifupi huku viongozi wakitumbua mabaki.
    Tatizo MDEBWEDO wengi wanajifanya wasomi lakini ELIMU yenyewe imeshikwa katika MAKABURI ya KINONDONI kuiloga SIMBA. WAPI BABA.
    UBINGWA wenu mwaka jana mmepewa baada SIMBA kunyang'anywa pointi dhidi Kagera huku MKIBEBWA na TFF yenu ya PAN NA YANGA. KATAENI!
    NA NDIYO MAANA RAMESHA PATWA nusura afungiwe kwa kutaka kumpa rushwa mwamuzi wa mechi ya kimataifa dhidi yenu ili mpate ushindi. Unakumbuka enzi hizo. RUhswa mpaka kwenye mechi za KIMATAIFA!
    SIMBA STILL THE BEST NOT HERE IN TANZANIA, BUT IN AFRICA!

    ReplyDelete
  21. Issa Makongoro alifungiwa maisha na CAF wa kujaribu kuwahonga waamuzi wa kutoka Ethipia na hivi karibuni Ivo Mapunda alikaririwa akisema kwamba Yanga hawawezi kushinda kama wasipomhonga mwamuzi.Kwa wale wasiomkumbuka Issa Makongoro alikuwa katibu mkuu wa Yanga.Hivyo Mdebwedo wana historia ya kuwa timu ya kwanza na ya pekee Tanzania kiongozi wake kufungiwa kwa kutaka kuhonga waamuzi.Mambo hayo fanyeni kwa TFF lakini nje ndio maana mnafungwa magoli sita.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...